Ukweli kuhusu kauli ya Papa huu hapa, vyombo vya habari vinapotosha

Umeelewa vizuri kama mimi.
Tatizo kubwa kwa sasa ni uelewa mdogo kwa lugha na utambuzi/maarifa.
Yan mtu hajishughulishi na ufafanuzi kwa sabab uelewa wake unapokea vitu lain na hauzid hapo.
Manake hata hajui misingi ya iman yake. Ni muumin tu.
Tatizo la pili ni Uadui/upinzan wa kiiman na kiitikad. Kuna anayebisha ilimrad papa na kanisa kwa pamoja ionekane ovyo na upotofu.
HItimisho: TUJITAHIDI KUSHIKAMANISHA IMANI NA AKILI!
Wadhambi kama wezi, wazinzi, waongo wauaji, makahaba, walevi n.k

Kulingana na mafundisho yenu ya ukatoliki hupewa baraka baada ya kutubu dhambi zao na kukiri kuachana na matendo yao maovu kwa kuyaungama na kuyajutia.

Kwamba kama mtu alikuwa mwizi, mwongo, mlevi hatorudi kuendelea na matendo yake ya uwizi, uongo na ulevi.

Sasa je wapenzi wa jinsia moja wakisha barikiwa wata achana na kutengana?

Au wata endelea kupokea baraka katika hali hiyo hiyo ya ushoga wao, ilhali ni dhambi kwa mujibu wa mafundisho ya ukatoliki wenu?
 
Hivi akili zako zina akili? Unawajuwa Illuminati? Nani anacontrol media na world market?

Vitu vingine vipo nje ya level yako ya ufahamu.

Mimi nikitaka habari za Simba nitaingia kwenye App ya Simba siwezi kwenda kuzitafuta kwenye App ya Yanga.

Habari za Papa zitafute Vatican Wana media zao.
Vatican wanasema mashoga wabarikiwe. Thibitisha vinginevyo.
 
Papa kakosea sana, mleta mada usitetee ujinga kama huo ata siku moja.
Mimi ni mkristo, nampenda Kristo.

Kazi ya kanisa ni kukemea maovu/ dhambi. Ushoga ni Dhambi, hivyo papa alipaswa akemee ndoa za jinsia moja, akemee ushoga na sio vinginevyo.

Kanisa linapotea, na watakaolipoteza zaidi ni sisi ambao tinashindwa kuusema ukweli
 
Icho ndio kilichokatazwa ,ata papa kapinga kwa watu wawili hao kwenda kuomba baraka ,kisha wapewe,imekatazwa kabisa kwa herufi kubwa,lakini akienda mmoja akiomba baraka,padri hatomuuliza kama yeye ni gasho au lah,atapatiwa baraka,apate neema ,Kama kujirudi aweze kujirudi
Kwa hiyo shoga mmoja akipewa baraka itamfanya aachane na shoga mwenzake?

Au baada ya yeye shoga mmoja kupewa baraka,ata endelea na ushoga huku akijua baraka si zipo tu muda wowote.

Kwamba itakuwa ni kufukuana mitaro kisha shoga mmoja anabaki nyumbani, Shoga mwingine anaenda kwa baba paroko kupokea baraka....

Kwamba sasa ruksa kufukuana mitaro huku unapata baraka, Cha msingi tu aende shoga mmoja.

Hivi huyo Papa wenu ana jielewa kweli?
 
Papa kakosea sana, mleta mada usitetee ujinga kama huo ata siku moja.
Mimi ni mkristo, nampenda Kristo.

Kazi ya kanisa ni kukemea maovu/ dhambi. Ushoga ni Dhambi, hivyo papa alipaswa akemee ndoa za jinsia moja, akemee ushoga na sio vinginevyo.

Kanisa linapotea, na watakaolipoteza zaidi ni sisi ambao tinashindwa kuusema ukweli
Wewe ni mkatoliki?
 
Kristo.

Kuhusu wapenzi wa jinsia Moja Papa anasemaje?

Ukweli uko hapa!

"Fiducia suplicans". Ni barua alioandika papa juu ya maana ya Baraka katika uchungaji.

"On the pastoral meaning of blessings"

Katika barua hiyo papa aliandika kujibu maswali ambayo watu wanauliza Sana Kanisa sasa, juu ya msimamo wa kanisa juu ya wapenzi wa jinsia Moja na ndoa za Jinsia Moja. Maana Kila papa katika kipindi chake analazimika kujibu maswali ya kijamii yanayogusa Imani.

Fiducia suplicans n kilatini maanake " n kwamba tusimamie wapi? "On the pastoral meaning of blessing"

Makuhani tusimamie wapi katika maana ya kichungaji ya kutoa Baraka? Papa hazungumzii katika hii barua habari za ndoa ya jinsia Moja, bali Kwa ujumla barua yote anaelezea hasa maana ya Baraka na mapadre watoeje Baraka katika kipindi hiki chenye mchanganyiko wa watu "wema" wenye bidii na pia kipindi chenye maovu yake mchanganyiko.

ANGALIZO
Kwenye hiyo barua papa anatatua changamoto Moja kwamba je mtu huyo mdhambi anaeishi ndoa ya jinsia Moja je anahaki yakubarikiwa?

Hapo hashughuliki hasa na swali eti kubariki ndoa ya jinsia Moja, ameweka wazi kabisa kuwa haifai na haiwezekani.

Kwenye barua anajibu swali kwamba je mtu Mmoja anastahili kubarikiwa? Haisemi abarikiwe kwasabab yeye ni shoga hapana ila kwasabab yeye n mtu.

Kwa maana nyingine je Kanisa liwatenge watu ambao ni mashoga?

Swali hilo limetokea wapi? Huku ulaya nduguzanguni watu hupenda mtu Mmoja Mmoja anakwenda Kwa Padre anamwambia Padre nibariki. Sisi pia huwa mtu unakuta anasafiri anakwenda Kwa Padre, "baba naomba Baraka nasafiri". Padre anambariki. Mtu anapeleka mbegu za kupanda baba naomba Baraka, mwanafunzi anakwenda Kwa Padre baba nimeleta vifaa vyangu vya shule naomba baraka, Padre anabariki.

Watu wakamuuliza papa je mtu mdhambi akimwambia Padre baba naomba Baraka je padre akatae? Aseme Baraka ni Kwa ajili ya watu wema?

Papa akasema Kama akija mtu yoyote akaomba kubarikiwa basi Padre anaweza kumbariki hata kama anaishi dhambi zake kama huyo wa jinsia Moja. Wasibaguliwe kwamba Baraka n ya watu fulan wema

Lakini wasibarikiwe wakiwa wawili kama vile ni wanandoa! Ametoa tahadhari kubwa kuzuia fikra zozote kwamba tunawabariki kama vile Kanisa linaruhusu maisha yao hapana! Ndugu zanguni Baraka sio sakramenti. Ndio maana Padre baada ya Misa anabariki wote hatengi wema zaidi na wakosefu Zaidi. Ila sakramenti sio Kila Mmoja anaruhusiwa. Watu wa ndoa ya jinsia Moja wao pia wamejifungia masakramenti.

Kwa waraka huo Padre anaweza kubariki watu wakiwa katika kundi kama kanisani au kikundi Cha Sala au wasafiri, pia mtu Mmoja Mmoja Padre anaweza kumbariki bila kumuuliza hali yake ya dhambi, hata kama anajua huyo mtu anaishi hali yake ya dhambi Padre ambariki tu. Kwanini maana kupitia Neema za Mungu mtu huweza kubadilishwa pia.

Luka 15:1. Siku moja, watozaushuru na wenye dhambi wengi walikwenda kumsikiliza Yesu. Mafarisayo na waalimu wa sheria wakaanza kunungunika: “Mtazameni mtu huyu! Anawakaribisha wenye dhambi, na tena anakula nao.....

Ngoja tuone baadhi ya nukuu kwenye barua hiyo.

Maelezo hayo yapo kwenye barua hiyo "Fiducia suplicans". Sura ya III

"Blessings of Couples in Irregular Situations and of Couples of the same sex". Kiswahili. Baraka Kwa wanaoishi wawili/kama mume na mke katika mazingira yasiyokuwa ya kiutaratib (utaratib kulingana na Kanisa) na ya watu wanaoishi pamoja wa jinsia Moja kama vile ni mume na mke.

Sasa Kwa kichwa hicho Cha habari anasemea sio tu watu wa jinsia Moja bali hata wale ambao hawapo katika ndoa inayotambuliwa kikanisa. Mfano wachumba wasibariki ndoa, wengine wameolewa mitara wote wanahusishwa kwenye kundi hilo. Papa anasema wote Padre anaweza kumbariki tu mtu huyo mkosefu akija Padre ambariki lakin anatoa mkazo isifanyike Baraka rasmi kama vile n sakramenti. Wala wasijisikie kuwa wanahalalishwa hapana.

Nanakuu hiyo barua
No 31. Uwezekano wa kutoa Baraka Kwa watu kama hao......

32. "Indeed the grace of God works in the lives of those who do not claim to be righteous but who acknowledge themselves humbly as sinners, like everyone else.".

"Hakika Neema ya Mungu hufanya kazi katika maisha ya wale ambao hawajidai kuwa wenye haki, lakini wanaojikubali Kwa unyenyekevu wakosefu "

Papa anasema Baraka hiyo ni Neema ambayo Mungu ataitumia kuwaongoa lakini Neema ya Mungu hufanya kazi ndani ya mtu anaekubali Kwa unyenyekev kuwa yeye ni mdhambi. Watu hao wakubali kuwa wao n wakosefu wampe Mungu ushirikiano.
No 33 "This is a blessing that, although not included in any liturgical rite........, "Hii ni baraka ambayo, ingawa haijajumuishwa katika ibada yoyote ya kiliturujia,

No 36 In this sense, it is essential to grasp the Holy Father’s concern that these non-ritualized blessings "kwa maana hii ni muhimu kutambua mtazamo wa baba mtakatifu kwamba hizi baraka ambazo sio rasmi kama zingine za kwenye ibada........ hapa anaonyesha ni za kawaida sio rasmi kama za kwenye liturjia

39. In any case, precisely to avoid any form of confusion or scandal, when the prayer of blessing is requested by a couple in an irregular situation, even though it is expressed outside the rites prescribed by the liturgical books, this blessing should never be imparted in concurrence with the ceremonies of a civil union, and not even in connection with them. Nor can it be performed with any clothing, gestures, or words that are proper to a wedding

39. .......this blessing should never be imparted in concurrence with the ceremonies of a civil union, and not even in connection with them. Nor can it be performed with any clothing, gestures, or words that are proper to a wedding

Baraka hizi zisitolewe Kwa namna yoyote inayoendana na muunganiko kama ule wa ndoa na Wala hata Kwa mfanano zisiendane, Wala zisifanywe kama Kwa mavaz ya ndoa ama ishara au maneno ya kubariki ndoa.

Civil union n msamiati wanaotumia zaidi Kwa watu wa jinsia moja anasema Baraka hizo zisielekee Wala Kwa namna yoyote inayoashiria kitu kama hicho.

Anaependa uisome mwenyewe kwenye mtandao "Fiducia suplicans" kuanzia no 31. Itajitokeza Kwa kiitalianoa lakin mwanzo wa document kushoto kabisa wameorodhesha lugha ya kuchagua bofya " Testo in lingua linglese" itabadilika kuwa Kwa kiingereza.
Shetani huwa anakuja kama malaika wa nuru kumbe anakupoteza. "Eti wabarikiwe kwa Kuwa ni watu" Mungu alishawahi Choma moto mataifa mawili kwa sababu ya hii dhambi. Papa kwa Kuwa ni kiongozi wa dini angesimamia biblia inavyosema maana biblia ndio katiba ya wakristo. Neno la Mungu linasema mwanaume usilale na mtu mume kama vile mke. Over
 
Wapenzi wa jinsia moja (Mashoga) wakisha barikiwa na kuungama, Je wata tengana na kuachana?

Au wataendelea kupewa baraka huku wakiendelea kufukuana mitaro?
Hao imekatwazwa ,wapi imehalalishwa kwao kupewa baraka,naona haujaelewa bado
 
Binafsi maelezo yako nimeyaelewa vizuri,suala la kuyakubali ni jambo lingine,ila kuelewa nimeyaelewa.

Kama nimeelewa vizuri ni kwamba papa ameruhusu mashoga wabarikiwe sio kwa sababu ya ushoga wao bali ni kwa sababu ya kuwa wao ni binadamu kama binadamu wengine.

Kwa maana kama ambavyo mwizi akienda kanisani anataka baraka kwa jambo lake ambalo halihusiani na wizi basi padre atambariki na baraka hizo haziendi kwenye kubariki wizi wake huo.

nimeelewa vyema kwamba ushoga ni dhambi kama zilivyo dhambi zingine za wizi,uzinifu,ufisadi n.k

Hivyo kama mwizi,mzinifu,fisadi,mla rushwa huwa wanaenda kanisani kupata baraka tena sio baraka za kubariki dhambi hizo basi na shoga nae pia anayo haki hiyo kupata baraka hizo ambazo hazihusiani na kubariki ushoga.

HOja hizi zina make sense kwa kila mtu lakini nadhani wapo watu ambao watachukuahii kama fimbo ya kuchapa watu fulani.

Baadhi yetu wa dini isiyokuwa ukristo tutatumia fimbo hii kuwachapia wakristo.

Na hata wasioamini dini watatukia hii kama fimbo kuwachapa watu wa dini.

NA pengine hata wakristo ambao sio wa dhehebu hilo watatumia hiyo kama fimbo kuwachapa watu wa dhehebu hili.
Uko sahihi
 
Thibitisha wewe Kwa kuweka hapa source ya Vatican na siyo source ya Illuminati na Freemason.
Mm nimekupa source unayoiita ya illuminati kuwa vatican wanasema mashoga yabarikiwe. Wewe unapinga kwa source ipi uliyoileta?
 
sasa unapaswa kuonyesha maneno ya kumbariki gaidi na mwizi yametoka wapu?
Papa kabriki usenge na usagaji ama hajabariki[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Yaani wakristo mnatetea nini hapo haya kaoaneni huko papa lishatoa baraka
Usikute papa nae ana mmewe ila anamficha ficha
 
Hao imekatwazwa
Hizo baraka wanazo takiwa kupewa ni zipi haswa?
,wapi imehalalishwa kwao kupewa baraka,
Wanapewa nini?

Hebu fafanua vizuri hii statement.

"Blessings to same sex couples"
naona haujaelewa bado
Iko hivi [emoji116]

shoga mmoja anaweza kwenda kuomba baraka, Huku shoga mwenzake akibaki nyumbani.

Cha msingi ameenda kama wadhambi wengine na anastahili kupewa baraka.

Then baada ya hapo, Business as usual kufukuana mitaro.

Cha msingi wasiende wote wakajulikana wao ni mashoga.

Baraka si zipo kwa wadhambi wote muda wowote tu, kwa hiyo hata shoga akitaka baraka ni kumcheki baba paroko tu anytime

Yani huo waraka alio utoa papa ni sawa na kusema unaweza kufanya dhambi na kuhurumiwa kwa vile Mungu anasamehe tu muda wowote.

Kuna sehemu kwenye huo waraka unasema God's love is infinite.

kwamba unaweza kufanya dhambi, ukichoka anytime unatubu na Mungu huyo ata kupenda tu..

Kwanza wadhambi wengine kulingana na mafundisho ya ukatoliki hukiri na ku ungama dhambi zao kisha huomba baraka wasitende tena dhambi zao.

Je mashoga wakisha ombewa na kupewa baraka wata tengana na kuachana?
 
Papa kabriki usenge na usagaji ama hajabariki[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Yaani wakristo mnatetea nini hapo haya kaoaneni huko papa lishatoa baraka
Usikute papa nae ana mmewe ila anamficha ficha
Mkuu bwana utam,
Kwanza hapana sehemu nimesema mimi ni mkristo hilo linaonyesha wewe ni muongo.

Pili, onyesha mahala pope anasema waoane?

Neno usikute ni dhahania tu, kama mimi nikiamua kusema bwana utam usikute ni malaya, wala halina uhalisia mpaka nitapothibitisha.

Pointi yako ni ipi?
 
Kristo.

Kuhusu wapenzi wa jinsia Moja Papa anasemaje?

Ukweli uko hapa!

"Fiducia suplicans". Ni barua alioandika papa juu ya maana ya Baraka katika uchungaji.

"On the pastoral meaning of blessings"

Katika barua hiyo papa aliandika kujibu maswali ambayo watu wanauliza Sana Kanisa sasa, juu ya msimamo wa kanisa juu ya wapenzi wa jinsia Moja na ndoa za Jinsia Moja. Maana Kila papa katika kipindi chake analazimika kujibu maswali ya kijamii yanayogusa Imani.

Fiducia suplicans n kilatini maanake " n kwamba tusimamie wapi? "On the pastoral meaning of blessing"

Makuhani tusimamie wapi katika maana ya kichungaji ya kutoa Baraka? Papa hazungumzii katika hii barua habari za ndoa ya jinsia Moja, bali Kwa ujumla barua yote anaelezea hasa maana ya Baraka na mapadre watoeje Baraka katika kipindi hiki chenye mchanganyiko wa watu "wema" wenye bidii na pia kipindi chenye maovu yake mchanganyiko.

ANGALIZO
Kwenye hiyo barua papa anatatua changamoto Moja kwamba je mtu huyo mdhambi anaeishi ndoa ya jinsia Moja je anahaki yakubarikiwa?

Hapo hashughuliki hasa na swali eti kubariki ndoa ya jinsia Moja, ameweka wazi kabisa kuwa haifai na haiwezekani.

Kwenye barua anajibu swali kwamba je mtu Mmoja anastahili kubarikiwa? Haisemi abarikiwe kwasabab yeye ni shoga hapana ila kwasabab yeye n mtu.

Kwa maana nyingine je Kanisa liwatenge watu ambao ni mashoga?

Swali hilo limetokea wapi? Huku ulaya nduguzanguni watu hupenda mtu Mmoja Mmoja anakwenda Kwa Padre anamwambia Padre nibariki. Sisi pia huwa mtu unakuta anasafiri anakwenda Kwa Padre, "baba naomba Baraka nasafiri". Padre anambariki. Mtu anapeleka mbegu za kupanda baba naomba Baraka, mwanafunzi anakwenda Kwa Padre baba nimeleta vifaa vyangu vya shule naomba baraka, Padre anabariki.

Watu wakamuuliza papa je mtu mdhambi akimwambia Padre baba naomba Baraka je padre akatae? Aseme Baraka ni Kwa ajili ya watu wema?

Papa akasema Kama akija mtu yoyote akaomba kubarikiwa basi Padre anaweza kumbariki hata kama anaishi dhambi zake kama huyo wa jinsia Moja. Wasibaguliwe kwamba Baraka n ya watu fulan wema

Lakini wasibarikiwe wakiwa wawili kama vile ni wanandoa! Ametoa tahadhari kubwa kuzuia fikra zozote kwamba tunawabariki kama vile Kanisa linaruhusu maisha yao hapana! Ndugu zanguni Baraka sio sakramenti. Ndio maana Padre baada ya Misa anabariki wote hatengi wema zaidi na wakosefu Zaidi. Ila sakramenti sio Kila Mmoja anaruhusiwa. Watu wa ndoa ya jinsia Moja wao pia wamejifungia masakramenti.

Kwa waraka huo Padre anaweza kubariki watu wakiwa katika kundi kama kanisani au kikundi Cha Sala au wasafiri, pia mtu Mmoja Mmoja Padre anaweza kumbariki bila kumuuliza hali yake ya dhambi, hata kama anajua huyo mtu anaishi hali yake ya dhambi Padre ambariki tu. Kwanini maana kupitia Neema za Mungu mtu huweza kubadilishwa pia.

Luka 15:1. Siku moja, watozaushuru na wenye dhambi wengi walikwenda kumsikiliza Yesu. Mafarisayo na waalimu wa sheria wakaanza kunungunika: “Mtazameni mtu huyu! Anawakaribisha wenye dhambi, na tena anakula nao.....

Ngoja tuone baadhi ya nukuu kwenye barua hiyo.

Maelezo hayo yapo kwenye barua hiyo "Fiducia suplicans". Sura ya III

"Blessings of Couples in Irregular Situations and of Couples of the same sex". Kiswahili. Baraka Kwa wanaoishi wawili/kama mume na mke katika mazingira yasiyokuwa ya kiutaratib (utaratib kulingana na Kanisa) na ya watu wanaoishi pamoja wa jinsia Moja kama vile ni mume na mke.

Sasa Kwa kichwa hicho Cha habari anasemea sio tu watu wa jinsia Moja bali hata wale ambao hawapo katika ndoa inayotambuliwa kikanisa. Mfano wachumba wasibariki ndoa, wengine wameolewa mitara wote wanahusishwa kwenye kundi hilo. Papa anasema wote Padre anaweza kumbariki tu mtu huyo mkosefu akija Padre ambariki lakin anatoa mkazo isifanyike Baraka rasmi kama vile n sakramenti. Wala wasijisikie kuwa wanahalalishwa hapana.

Nanakuu hiyo barua
No 31. Uwezekano wa kutoa Baraka Kwa watu kama hao......

32. "Indeed the grace of God works in the lives of those who do not claim to be righteous but who acknowledge themselves humbly as sinners, like everyone else.".

"Hakika Neema ya Mungu hufanya kazi katika maisha ya wale ambao hawajidai kuwa wenye haki, lakini wanaojikubali Kwa unyenyekevu wakosefu "

Papa anasema Baraka hiyo ni Neema ambayo Mungu ataitumia kuwaongoa lakini Neema ya Mungu hufanya kazi ndani ya mtu anaekubali Kwa unyenyekev kuwa yeye ni mdhambi. Watu hao wakubali kuwa wao n wakosefu wampe Mungu ushirikiano.
No 33 "This is a blessing that, although not included in any liturgical rite........, "Hii ni baraka ambayo, ingawa haijajumuishwa katika ibada yoyote ya kiliturujia,

No 36 In this sense, it is essential to grasp the Holy Father’s concern that these non-ritualized blessings "kwa maana hii ni muhimu kutambua mtazamo wa baba mtakatifu kwamba hizi baraka ambazo sio rasmi kama zingine za kwenye ibada........ hapa anaonyesha ni za kawaida sio rasmi kama za kwenye liturjia

39. In any case, precisely to avoid any form of confusion or scandal, when the prayer of blessing is requested by a couple in an irregular situation, even though it is expressed outside the rites prescribed by the liturgical books, this blessing should never be imparted in concurrence with the ceremonies of a civil union, and not even in connection with them. Nor can it be performed with any clothing, gestures, or words that are proper to a wedding

39. .......this blessing should never be imparted in concurrence with the ceremonies of a civil union, and not even in connection with them. Nor can it be performed with any clothing, gestures, or words that are proper to a wedding

Baraka hizi zisitolewe Kwa namna yoyote inayoendana na muunganiko kama ule wa ndoa na Wala hata Kwa mfanano zisiendane, Wala zisifanywe kama Kwa mavaz ya ndoa ama ishara au maneno ya kubariki ndoa.

Civil union n msamiati wanaotumia zaidi Kwa watu wa jinsia moja anasema Baraka hizo zisielekee Wala Kwa namna yoyote inayoashiria kitu kama hicho.

Anaependa uisome mwenyewe kwenye mtandao "Fiducia suplicans" kuanzia no 31. Itajitokeza Kwa kiitalianoa lakin mwanzo wa document kushoto kabisa wameorodhesha lugha ya kuchagua bofya " Testo in lingua linglese" itabadilika kuwa Kwa kiingereza.
Marekebisho
Mkuu civil union sio Ndoa ya Jinsia moja
 
Hapa umekuwa mwongo, Ukristo maana yake ni matendo safi, unapoingia tu kwenye nyumba ya MUNGU unatubu kuanguka kwako na kuomba utakaso kabla ya mengine yote. Hata KRISTO mwenyewe alisamehe kwanza ndipo akabariki. Hakuna sehemu ambapo alibarikiwa mtu mwenye nia ya kuendelea na dhambi iliyomfanya kuwa mchafu. Kuanguka kupo na ndio maana tukaletewa toba na neema.

Wewe unachosema ni tafauti kabisa na dhana nzima ya kuwa mkristo.
kanisa katoliki limefanya wakristo wote tumeaonekana wa hovyo, tunajua haya mambo yapo kwa dini zote ila kutolewa tamko na kiongozi mkubwa tumeingia chaka, angekaa kimya tu mambo yaendelee kimya kimya kama zamani.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Back
Top Bottom