Ukweli kuhusu kauli ya Papa huu hapa, vyombo vya habari vinapotosha

Sio kweli kabla ya baraka unatubu na kua msafi,baraka sio sacramenti
Hapa umekuwa mwongo, Ukristo maana yake ni matendo safi, unapoingia tu kwenye nyumba ya MUNGU unatubu kuanguka kwako na kuomba utakaso kabla ya mengine yote. Hata KRISTO mwenyewe alisamehe kwanza ndipo akabariki. Hakuna sehemu ambapo alibarikiwa mtu mwenye nia ya kuendelea na dhambi iliyomfanya kuwa mchafu. Kuanguka kupo na ndio maana tukaletewa toba na neema.

Wewe unachosema ni tafauti kabisa na dhana nzima ya kuwa mkristo.
 
Wadhambi kama wezi, wazinzi, waongo, wauaji, makahaba n.k hubarikiwa ili waachane na matendo yao maovu na waenende katika kufanya mema.

Je mashoga wakisha barikiwa wata tengana na kuachana na mapenzi yao ya jinsia moja?

Kwanza hao wadhambi wengine kulingana na kanisa katoliki hupewa baraka pale ambapo hutubu makosa yao kwa kuya ungama kuyajutia na kukiri kuachana nayo.

Je mashoga wakisha barikiwa wata achana?

Au wata endelea kupokea baraka kwenye hali yao hiyo hiyo ya ushoga siku zote?

Lengo kuu na dhumuni la kuwabariki ni nini haswa?

Waachane au waendelee na mapenzi yao ya jinsia moja huku wakipata baraka?
 
Kabla sijakujibu,unajua maana ya sacrament ya kitubio?,unajua baraka inatolewaje?unachanganya vitu viwili kwa pamoja ,baraka haitolewi kwa mtu pekee ,bali ata vitu,umejenga nyumba ,ukaomba ibarikiwe,je hiyo nyumba ikibarikiwa ,uliyejenga utaulizwa umejenga kwa pesa Halali au ya wizi?
Unapeleka mbegu kanisani,zinaombewa kabla ya kwenda kupanda.je padri unataka apeleleze shamba ni lako au lina migogoro
 
Mkuu, hapa ni kujiongeza tu sababu kinachoendelea kipo wazi haihitaji nguvu kuelewa.

Kaburi hata ulirembe vipi juu ndani kuna maiti. Hapa kinachofanywa na kondoo wa bwana ni kuliremba kaburi ila ukifungua maiti ipo.

Njia sahihi ni kumpinga papa maana ni binadamu sio kuremba remba kinachoripotiwa kuwa kimetoka kwake.
 
Kulikuwa na sababu gani ya kutolea tamko ushoga kama dhambi hazina uhusiano na kutolewa baraka? Kanisa lina nia ya kurahisisha ushoga kwenye akili za waumini. Ni suala la muda tu.
 
Hiki ndio maana yake, ila watu wanapotosha kwa makusudi.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
Wapenzi wa jinsia moja wanapewa baraka kwa lengo gani haswa?

Waachane au waendelee na mapenzi yao ya jinsia moja?

Wakati wanapewa baraka watahimizwa waachane au waendelee na mapenzi yao ya jinsia moja?

Wadhambi wengine katika kanisa katoliki hupewa baraka pale ambapo hutubu makosa yao kwa kuyaungama, kuyajutia na kukiri kuachana nayo.

Je mashoga wakisha barikiwa wata tengana?

Au wata endelea kupokea baraka ilhali ushoga ni dhambi kwa mujibu wa ukatoliki?
 
Je mashoga wakisha barikiwa itawafanya waachane na watengane?

Kwamba baraka itawasaidia wasiendelee kuwa wapenzi wa jinsia moja?
 
Ww mwenyewe kwa bandiko hili umeshahalalisha ushoga ndani ya kanisa
 
Umefafanua vyema.
 
Hilo si linafanyika kila siku, kwani lilikua linahitaji tamko kwani?
 
Waumini wa kanisa katoliki kazi mnayo, mnataka kufafanua kitu ambacho kimsingi kukifafanua inabidi kujizima data, tunawaangalia tu, ila papa kasema, nyie akina nani mnatolea ufafanuzi tamko la papa?
 
Je mashoga wakisha barikiwa itawafanya waachane na watengane?

Kwamba baraka itawasaidia wasiendelee kuwa wapenzi wa jinsia moja?
Swali lako ilitakiwa liwe je mtu akipata baraka,anapata Nini rohoni?mtu yeyote anapata neema ya Mungu,neema ya Mungu ukiipata unapatwa na hofu ya Mungu,na kuzikataa dhambi,uikshakua na ukaribu Mungu ,roho mtakatifu anakuongoza muda wote,kwa hiyo ata Kama ni shoga,huenda akajirudi ,na kupiga magoti kwa Mungu,yeye anasema japokua dhambi zenu ni nyekundu Kama damu,nitazibadili zitakua nyeuoe kama theluji
 
Hilo si linafanyika kila siku, kwani lilikua linahitaji tamko kwani?
Kabisa. Sasa sijui kwanini kuna watu hawaoni kinachoendelea? Kinachoendelea ni maandalizi ya kuupokea ushoga kwa vizazi vijavyo ndani ya imani. Na hili linafanywa na mashoga wazungu.

Kwenye filamu wamepokelewa, kwenye michezo wamepokelewa, kwenye siasa wamepokelewa kilichobaki ni kanisani na msikitini. Hapa wakiweza basi zoezi limefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana.
 
Aisee. Mkuu, we unaona kila kitu kipo sawa?
 
Hivi akili zako zina akili? Unawajuwa Illuminati? Nani anacontrol media na world market?

Vitu vingine vipo nje ya level yako ya ufahamu.

Mimi nikitaka habari za Simba nitaingia kwenye App ya Simba siwezi kwenda kuzitafuta kwenye App ya Yanga.

Habari za Papa zitafute Vatican Wana media zao.
 
Baraka hizo hutolewa baada ya ungamo la dhambi ambalo hufanyika wakati ibada ina anza.

Kwenye ibada za wakatoliki kuna kipengele cha "Kukiri dhambi" ambapo Padri husema tukiri makosa yetu, waumini hukiri kwa kusema...[emoji116]

"Namuungamia Mungu mwenyezi nanyi ndugu zangu kwani nimekosa mno kwa mawazo, kwa maneno, kwa vitendo na kwa kutotimiza wajibu nimekosa mimi, nimekosa mimi, nimekosa sana ndio maana namuomba Maria mwenye heri bikira daima malaika na watakatifu wote nanyi ndugu zangu niombeeni kwa bwana Mungu wetu"

Kisha padri husema...[emoji116]

" Mungu mwenyezi atuhurumie, atusamehe dhambi zetu atufikishe kwenye uzima wa milele"

Waumini huitika Amina.

Hapo baraka imetolewa kusafisha matendo yao maovu kulingana na mafundisho yenu ya ukatoliki kwamba kama mtu alikuwa mwizi ame ungama na ataacha wizi wake, kama mtu alikuwa muongo ame ungama na ataacha uongo wake, Kama mtu alikuwa mzinzi ataacha uzinzi wake na kukiri kuachana na matendo hayo.

Sasa je wapenzi wa jinsia moja (mashoga) wakisha barikiwa na kuungama wata achana na kutengana?

Kwamba hawata endelea tena kuwa wapenzi wa jinsia moja?

Au wata endelea kubarikiwa hivyo hivyo kila siku, Huku wakiendelea kufukuana mitaro?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…