Kigamboni kipindi huu ubia wa kishetani unafanyika bei ya ardhi iliyokuwa sokoni ni kati ya 1,500,000/= na 4,500,000/= kwa eka kutegemea na sehemu husika! na ardhi ilikuwa inapatikana sana! Sasa katika mazingira hayo ni mwekezaji ibilisi tu ambaye ataamua kutokununua ardhi mwenyewe halafu aingie ubia na mtu au kampuni inayothaminisha ardhi yake kwa sh 775,000,000/= kwa eka badala ya kuinunua mwenyewe kwa sh 5,000,000/= kwa eka!.
Hiyo ni tisa lakini kumi huyo mbia aliyethaminisha ardhi yake kwa sh 775,000,000/= bado anakutaka wewe umkopeshe pesa na ndiye anayemiliki share nyingi zaidi!
Ninachokiona hapa ni ufisadi uliokubuhu! Yaani nakopa pesa kwako halafu nanunua ardhi kwa bei chee halafu naingia ubia na wewe na kuithàminisha ardhi niliyonunua kwa hela niliyokopa kwako kwa bei mbaya kisha mimi ndo nakuwa mmiliki wa mradi mwenye hisa nyingi wakati kimsingi pesa yote ya mradi imetoka kwako!