kijana wa leo ngoja nikupe explanation for dumb ,
imagine wewe una kiwanja cha heka moja hapo kibaha ambacho tusema thamani yake waweza muuzia mtu kwa milion 10,
wanakuja wawekezaji wanataka kuweka mradi wa kujenga maghorofa ya kupangisha na wanataka wakupe milion 10 uwaachie kiwanja,
unapiga hesabu ya mradi utakaowekwa hapo na kuona utakuwa na thamani ya bilion 100,unaona kuuza kiwanja kwa milion 10 utakuwa umewapa watu ulaji,
unakataa kuuza,wanakubembeleza hatmaye unakubali kuingia nao ubia na mnapanga katika mradi huo upewe hisa 20%,ambayo kama sikosei ni thamani kama milion 200.
Kumbuka mwanzo thamani halisi ya hiyo heka yako moja ni sh milion 10,
lakini kwasababu umeingia mkataba wa land for equit sasa thamani yako katika mradi huo ni milioni 200.
Ndicho kilichotokea,halafu watu wanatumia umbumbu wa watu kutojua haya mambo kwa kuwapaka watu matope kuwa kuna ufisadi,
sasa swali ukipeleka mahakamani hii kesi utashinda au ndo yaleyale ya Dowans