MR MAJANGA
JF-Expert Member
- Oct 4, 2014
- 3,444
- 10,687
Land for Equity (Ardhi Kwa Hisa) na Mradi wa NSSF Dege Beach Kigamboni
Leo Magazeti mengi yameandika kuwa kuna ufisadi mkubwa kwenye miradi ya Shirika la Hifadhi ya Jamii(NSSF), Hasa Mradi wa Dege Beach Huko Kigamboni ambapo imeelezwa Kuwa Katika Kila Kiwanja Kimoja kati ya Viwanja 300 vilivyoko Katika hatua ya kwanza ya Mradi thamani ya Kiwanja imezidishwa Kwa zaidi ya Shilingi Milioni 775. Ikielezwa Kuwa thamani ya Kila Kiwanja Ni Shilingi Milioni 25 Tofauti na Milioni 800 ambazo NSSF imenunua Kwa Kila Kiwanja Kimoja Kwa Mujibu wa Mkataba kati yake Na Kampuni ya Azimio.
Taarifa Hizi ni za Uongo. Ukweli ni Kuwa NSSF haikununua Ardhi eneo la Dege Beach, Kigamboni Kwa thamani ya Milioni 800 Kwa Kiwanja, imepewa Ardhi Bure Ili iwekeze Kwa kuingia Ushirika wa Mradi Katika Ardhi ya Mtu Binafsi (Kampuni ya Azimio).
Aina hiyo ya Ushirika hujulikana Kwa wataalam wa Sekta ya Majengo (Real Estate) Kama Utaratibu wa "Land for Equity" (Yaani Ardhi Kwa Hisa). Ambapo Katika Makubaliano ya Mradi, Mbia Mmoja wa Mradi anatoa Ardhi Na Mbia mwengine anatoa Fedha za Uwekezaji. Na kisha Hisa za Mradi hugawanywa kulingana Na mtaji wa Kila Mmoja (Ardhi Kwa Mbia wa kwanza, Na Fedha Kwa Mbia mwengine).
Na hili si Jambo jipya nchini. Uchunguzi unathibitisha kuwa kilichofanywa na NSSF (Katika Mradi wa Dege Beach Kigamboni) ndicho kinachofanywa na taasisi mbalimbali nchini (wakiwemo NSSF wenyewe), katika Miradi mbalimbali ya Uwekezaji wa Ushirikiano kati sekta ya Majengo.
Baadhi ya mifano ya Miradi ya namna hiyo ni kama ifuatavyo:
• Miaka ya 90 Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) liliingia makubaliano na Shirika la Mafuta la Taifa (TPDC) kujenga Jengo la Mafuta House kwenye ardhi inayomilikiwa na NHC katika eneo ambalo sasa pamejengwa Jengo la Banjamin Mkapa Towers. Katika Ujenzi Huo NHC walipewa asilimia 25 ya thamani ya mradi kwa kutoa ardhi (Land for Equity) ambayo mwaka 1995 ilikuwa ni Shilingi bilioni 19 bilioni. Kwa mujibu wa mkataba huo thamani ya ardhi ile mwaka huo ilikuwa shs 4.75 bilioni.
Mwaka 1995 thamani ya ardhi katikati ya jiji la Dar es salaam ilikuwa ni shilingi 62,500 kwa kila mita ya mraba na kiwanja kile kina mita za mraba 6,221 sawa na ekari moja na nusu. Kwa kutumia mahesabu ya kawaida thamani ya ardhi ya NHC ingekuwa shilingi 388 milioni Na si hiyo 4.75 Bilioni ambayo inaonyesha bei kukuzwa Kwa nyongeza ya shilingi 4.35 bilioni.
• NSSF ni mfaidika wa Utaratibu wa "Land for Equity" Katika mradi Mpya wa Umeme Mkuranga. Mwaka 2014 NSSF ilinunua ardhi kwa thamani ya shilingi 100 milioni, ardhi hiyo ilikuwa Ni jumla ya ekari 100.
Mwaka 2015 Wawekezaji waliingia ubia na Shirika la NSSF Ili kujenga Mtambo wa Umeme Katika ardhi Husika. Mchango wa NSSF Katika Mradi Huo ulikuwa ni ardhi yake ya Ekari 100 ambayo iliinunua Kwa Shilingi Milioni 100 Tu Mwaka Mmoja nyuma. Lakini Katika Mkataba wa Mradi Huo NSSF imepata asilimia 10 ya thamani ya Mradi Mzima wa Uwekezaji ambayo ni Dola za Kimarekani 450 Milioni Sawa na zaidi ya Shilingi 900 Bilioni.
Katika Mradi huu wa Mkuranga NSSF ndani ya mwaka mmoja iliweza kupandisha thamani ya ardhi ile kutoka shilingi 100 milioni mpaka shilingi 90 Bilioni ambayo ni Asilimia 10 ya thamani ya Mradi Wote. Kama zingetumika Hesabu Za kawaida Tu thamani ya Uwekezaji wa NSSF kwenye Mradi Husika ilipaswa Kuwa Asilia 0.06 Tu Na Sio Asilimia 10 walizopewa.
• Mradi mwengine uliofuata Utaratibu wa "Land for Equity" (Ardhi Kwa Hisa) ni Taarifa Juu ya makubaliano kati ya NHC na PPF Katika Ujenzi wa Jengo la PPF Tower Mwanza, ambapo NHC walitoa ardhi na kupewa Aslimia 25 ya hisa za mradi husika. Mradi huo una thamani ya Shilingi bilioni 258, Lakini Ukubwa wa ardhi waliyotoa NHC ni Kiwanja cha ekari moja tu.
Kamwe huwezi kusikia ikisemwa kuwa PPF wamenunua Kiwanja Cha Ekari Moja Kwa thamani ya Shilingi Bilioni 64 Kwa Kuwa Ni Ushirika wa Pamoja.
• NSSF imejenga jengo RITA, eneo la Posta jirani Kabisa na Jengo la Klabu ya Billicanas Jijini Dar es salaam. Katika Mradi Huo RITA iliyojengewa Jengo Husika, Na Kwa Kutoa ardhi hiyo wamepata hisa Asilimia 25 ya thamani ya mradi mzima wa Jengo Hilo, ambayo ni hilingi Bilioni 198.
Lakini Ukubwa wa Kiwanja cha RITA ni nusu ekari tu. Kamwe huwezi kusikia NSSF wamenunua nusu ekari kwa Shilingi bilioni 49 Katika Mradi wa Jengo la RITA.
• Miradi mengine iliyofuata Utaratibu huu wa "Land for Equity"
* Mradi kati ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) na Fida-Hussein Katika Jengo lililoko Maeneo ya Jirani Na Hospitali ya Ocean Road.
* Mradi wa Jengo la UVCCM eneo la Fire Jijini Dar es salaam.
* Mradi wa Jengo la Mwalimu Nyerere Foundation eneo la Posta.
* Mradi wa Jengo la UWT (Makao makuu ya Airtel) eneo la Morocco nk.
• Hitimisho:
NSSF iliingia ubia na kampuni ya Azimio Kwaajili ya Uendelezwaji wa Ardhi Katika Mradi wa Dege Beach Kule Kigamboni. Kampuni ya Azimio Kwa Kutoa Ardhi ya Mradi Husika ilipewa asilimia 20 ya thamani ya mradi wa Dege Eco Village.
Lakini Pia kwenye Mkataba wa Mradi Azimio wanapaswa Kutoa 35% ya Fedha za thamani ya Mradi, Hivyo kuwafanya wawe na 55% ya Mradi Husika Huku NSSF wakiwa na 45 ya Mradi Kwa Fedha watakazotoa.
Naona mbinu ya maghufuli inafanikiwa anajua akimtumbua dau zitatoka nyaraka za makampuni mengine itakuwa rahisi kuwatumbua wote kwa wakati mmoja maana kuna watu wameficha mafaili ya ushahidi