Mkuu
Samvulachole,
Mie naona huna hoja hapa, kama NSSF haijanunua hiyo ardhi sawa lakini huwezi kusema imepewa bure.
Ngoja nikupe mfano mdogo tu, tunataka kujenga Nyumba ya Biashara mimi
Shark na wewe
Samvulachole. Gharama za ujenzi wa nyumba hiyo ambazo mimi nitazitumia labda ni 60mil. Wewe unatoa kiwanja (unachokiita cha bure) unasema kina value ya 40mil. Hivyo gharama za ujenzi za Jumla hapa zitakua 100mil hivyo mimi nitakua nimetumia 60% ya ujenzi wote huku wewe ukidai umetumia 40% ya ujenzi wote (Capital invested). Na makubaliano ni kugawana faida kulingana na % ya uwekezaji (60:40)
Ukute kumbe wewe kiwanja chako market value yake ni labda 10mil tu na sio 40mil kama ulivyotaja awali, hivyo umewekeza 10mil/(60mil +10mil) = 14.3% ambayo ungestahili kama mgawo/hisa zako na sio 40% za awali, huoni kama hapa wewe
Samvulachole /Azimio unanidhulumu mimi
Shark /NSSF??
Sawa, mimi sijanunua kiwanja kwako kwa hiyo 40mil lakini ndio mtaji ulioutaja, na kwenye mgawo nawe utakuwepo sababu umetoa mtaji wa kiwanja. Lakini huoni kama kwa wewe kutaja value kubwa ya mtaji wako wakati sio itakupelekea wewe kupata mgawo mkubwa zaidi ya unaostahili??