Ukweli kuhusu Mradi wa NSSF wa Dege Beach Kigamboni

Looks like Gazeti la mwananchi wana ajenda zao na Nssf na Dr Dau...kwann hawaelezi ukweli?
 
Land for Equity (Ardhi Kwa Hisa) na Mradi wa NSSF Dege Beach Kigamboni.
Mkuu Bishoo Likubwa, next time uki copy na ku paste, toa haki kwa aliyeandika ambako umenyofoa hivyo hivyo ilivyo, huu mtindo wa vichwa maji,au madebe matupu kupiga kelele nyingi kwa ku copy na ku paste madini ya watu wengine ili nao waonekana ni vichwa, ni wizi tuu, hivyo hayo ni majizi tuu kama majizi mengine yoyote hata kama wizi huo umefanywa humu humu jf!.

Mwenye haki na bandiko hili ni
Ukweli kuhusu Mradi wa NSSF wa Dege Beach Kigamboni | Page 4 ...

Lijitu likubwa zima, lina kwiba kwa kucopy na kupaste kila kitu vile vile kilivyo kutoka humu humu jf, bila aibu, tena mchana kweupe, huu sio just wizi wa kawaida, nadhani kuna elements za sanity!.

NB. Naunga mkono headline.

Paskali
 
Hatuwez kuwaacha mkipotosha sasa

Ukweli uelezwe jamii ijue
Hapana, Mimi sijapotosha ila Mimi ni mtazamaji tu, kama unataka ukweli uelezwe Jamii ijue sidhani kama Wewe ndio the right person wa kueleza huo ukweli, nimesema sidhani! Kwahio kwa kuwa Huna hata Legal Authority ya kuuleza ukweli ndio maana nikasema asante kwa taarifa ndefu na nzuri nani nimejifunza jambo ila tusubiri kwenye Legal Authority wakishafanya uchunguzi si ukweli utajulikana?

Usitumie nguvu nyingi namna hii Mpwa. Kweli itatuweka guru, itachelewa tu lakini itafika.
 
Land for Equity (Ardhi Kwa Hisa) na Mradi wa NSSF Dege Beach Kigamboni

Leo Magazeti mengi yameandika kuwa kuna ufisadi mkubwa kwenye miradi ya Shirika la Hifadhi ya Jamii(NSSF), Hasa Mradi wa Dege Beach Huko Kigamboni ambapo imeelezwa Kuwa Katika Kila Kiwanja Kimoja kati ya Viwanja 300 vilivyoko Katika hatua ya kwanza ya Mradi thamani ya Kiwanja imezidishwa Kwa zaidi ya Shilingi Milioni 775. Ikielezwa Kuwa thamani ya Kila Kiwanja Ni Shilingi Milioni 25 Tofauti na Milioni 800 ambazo NSSF imenunua Kwa Kila Kiwanja Kimoja Kwa Mujibu wa Mkataba kati yake Na Kampuni ya Azimio.

Taarifa Hizi ni za Uongo. Ukweli ni Kuwa NSSF haikununua Ardhi eneo la Dege Beach, Kigamboni Kwa thamani ya Milioni 800 Kwa Kiwanja, imepewa Ardhi Bure Ili iwekeze Kwa kuingia Ushirika wa Mradi Katika Ardhi ya Mtu Binafsi (Kampuni ya Azimio).

Aina hiyo ya Ushirika hujulikana Kwa wataalam wa Sekta ya Majengo (Real Estate) Kama Utaratibu wa "Land for Equity" (Yaani Ardhi Kwa Hisa). Ambapo Katika Makubaliano ya Mradi, Mbia Mmoja wa Mradi anatoa Ardhi Na Mbia mwengine anatoa Fedha za Uwekezaji. Na kisha Hisa za Mradi hugawanywa kulingana Na mtaji wa Kila Mmoja (Ardhi Kwa Mbia wa kwanza, Na Fedha Kwa Mbia mwengine).

Na hili si Jambo jipya nchini. Uchunguzi unathibitisha kuwa kilichofanywa na NSSF (Katika Mradi wa Dege Beach Kigamboni) ndicho kinachofanywa na taasisi mbalimbali nchini (wakiwemo NSSF wenyewe), katika Miradi mbalimbali ya Uwekezaji wa Ushirikiano kati sekta ya Majengo.

Baadhi ya mifano ya Miradi ya namna hiyo ni kama ifuatavyo:

• Miaka ya 90 Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) liliingia makubaliano na Shirika la Mafuta la Taifa (TPDC) kujenga Jengo la Mafuta House kwenye ardhi inayomilikiwa na NHC katika eneo ambalo sasa pamejengwa Jengo la Banjamin Mkapa Towers. Katika Ujenzi Huo NHC walipewa asilimia 25 ya thamani ya mradi kwa kutoa ardhi (Land for Equity) ambayo mwaka 1995 ilikuwa ni Shilingi bilioni 19 bilioni. Kwa mujibu wa mkataba huo thamani ya ardhi ile mwaka huo ilikuwa shs 4.75 bilioni.

Mwaka 1995 thamani ya ardhi katikati ya jiji la Dar es salaam ilikuwa ni shilingi 62,500 kwa kila mita ya mraba na kiwanja kile kina mita za mraba 6,221 sawa na ekari moja na nusu. Kwa kutumia mahesabu ya kawaida thamani ya ardhi ya NHC ingekuwa shilingi 388 milioni Na si hiyo 4.75 Bilioni ambayo inaonyesha bei kukuzwa Kwa nyongeza ya shilingi 4.35 bilioni.

• NSSF ni mfaidika wa Utaratibu wa "Land for Equity" Katika mradi Mpya wa Umeme Mkuranga. Mwaka 2014 NSSF ilinunua ardhi kwa thamani ya shilingi 100 milioni, ardhi hiyo ilikuwa Ni jumla ya ekari 100.

Mwaka 2015 Wawekezaji waliingia ubia na Shirika la NSSF Ili kujenga Mtambo wa Umeme Katika ardhi Husika. Mchango wa NSSF Katika Mradi Huo ulikuwa ni ardhi yake ya Ekari 100 ambayo iliinunua Kwa Shilingi Milioni 100 Tu Mwaka Mmoja nyuma. Lakini Katika Mkataba wa Mradi Huo NSSF imepata asilimia 10 ya thamani ya Mradi Mzima wa Uwekezaji ambayo ni Dola za Kimarekani 450 Milioni Sawa na zaidi ya Shilingi 900 Bilioni.

Katika Mradi huu wa Mkuranga NSSF ndani ya mwaka mmoja iliweza kupandisha thamani ya ardhi ile kutoka shilingi 100 milioni mpaka shilingi 90 Bilioni ambayo ni Asilimia 10 ya thamani ya Mradi Wote. Kama zingetumika Hesabu Za kawaida Tu thamani ya Uwekezaji wa NSSF kwenye Mradi Husika ilipaswa Kuwa Asilia 0.06 Tu Na Sio Asilimia 10 walizopewa.

• Mradi mwengine uliofuata Utaratibu wa "Land for Equity" (Ardhi Kwa Hisa) ni Taarifa Juu ya makubaliano kati ya NHC na PPF Katika Ujenzi wa Jengo la PPF Tower Mwanza, ambapo NHC walitoa ardhi na kupewa Aslimia 25 ya hisa za mradi husika. Mradi huo una thamani ya Shilingi bilioni 258, Lakini Ukubwa wa ardhi waliyotoa NHC ni Kiwanja cha ekari moja tu.

Kamwe huwezi kusikia ikisemwa kuwa PPF wamenunua Kiwanja Cha Ekari Moja Kwa thamani ya Shilingi Bilioni 64 Kwa Kuwa Ni Ushirika wa Pamoja.

• NSSF imejenga jengo RITA, eneo la Posta jirani Kabisa na Jengo la Klabu ya Billicanas Jijini Dar es salaam. Katika Mradi Huo RITA iliyojengewa Jengo Husika, Na Kwa Kutoa ardhi hiyo wamepata hisa Asilimia 25 ya thamani ya mradi mzima wa Jengo Hilo, ambayo ni hilingi Bilioni 198.

Lakini Ukubwa wa Kiwanja cha RITA ni nusu ekari tu. Kamwe huwezi kusikia NSSF wamenunua nusu ekari kwa Shilingi bilioni 49 Katika Mradi wa Jengo la RITA.

• Miradi mengine iliyofuata Utaratibu huu wa "Land for Equity"
* Mradi kati ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) na Fida-Hussein Katika Jengo lililoko Maeneo ya Jirani Na Hospitali ya Ocean Road.
* Mradi wa Jengo la UVCCM eneo la Fire Jijini Dar es salaam.
* Mradi wa Jengo la Mwalimu Nyerere Foundation eneo la Posta.
* Mradi wa Jengo la UWT (Makao makuu ya Airtel) eneo la Morocco nk.

• Hitimisho:

NSSF iliingia ubia na kampuni ya Azimio Kwaajili ya Uendelezwaji wa Ardhi Katika Mradi wa Dege Beach Kule Kigamboni. Kampuni ya Azimio Kwa Kutoa Ardhi ya Mradi Husika ilipewa asilimia 20 ya thamani ya mradi wa Dege Eco Village.

Lakini Pia kwenye Mkataba wa Mradi Azimio wanapaswa Kutoa 35% ya Fedha za thamani ya Mradi, Hivyo kuwafanya wawe na 55% ya Mradi Husika Huku NSSF wakiwa na 45 ya Mradi Kwa Fedha watakazotoa.
20161030_043452.jpg
 
wewe unakanusha hiyo ripoti ukiwa kama nani labda?
 
Watu wamepiga pesa kirahisi rahisi tu,
800 * 3500 = 2.3tr wakati thamani ya ardhi ya soko ni
25 * 3500= 87bn, huu ni wizi mkubwa zaidi ya Escrow, Richmond na takataka nyingine. Ona aibu THE BIG SHOW hata Allah haruhusu huu utapeli.
 
Nasubiri kwa ham kusoma Jinsi Paskal Mayala atakavyokuja kumjibia na kumtetea huyu Mkurugezi mpya
Mkuu Samvu, kwanza asante kwa hii, kwa vile mimi sio insider wa NSSF, then utasubiri sana!.

Sifa Kuu ya JF ni kwa watu kusema ukweli daima no matter what, ombi langu kwako, kwa vile umekuja humu na facts, lets keep more facts to an open tukianzia na hii hoja ya kuna mtu yuko very desperate, ndipo tuje kwenye justification ya NSSF kufanya land acquisition kwa ubia katika eneo ambalo sio too demanding. Hiyo mifano mingine yote ni maeneo ya mjini kati, very prime na very demanding. Huko tutafika, tuanze na hii ya desperation.

Kwa vile kwenye hitimisho lako umesema nakuku quote
"Out of desperation Huyu Mkurugenzi mpya wa NSSF fed the reporters with all lies (Tariff za uwongo)", ili bandiko lako hili lisiwe ni kampeni maalum ya trying ya "saving the faces", utakuwa umelitendea haki jukwaa hili kama utaeleza huyo Mkurugenzi wa NSSF who fed the reporters with all lies out of desperation, yuko desperate for what? .

Tuanzie hapo.

Paskali
Mkuu,
Samvulachole
bado nakusubiria kwenye haya, ile twende kidogo kidogo.

Paskali
 
Eti NSSF wamepewa bure, hakuna ardhi ya bure wadanganyeni mtakaowapata.
 
Magazeti yafanye utafiti wa kutosha kabla ya kuandika kwenye magazeti yao.
 
Land for Equity (Ardhi Kwa Hisa) na Mradi wa NSSF Dege Beach Kigamboni

Leo Magazeti mengi yameandika kuwa kuna ufisadi mkubwa kwenye miradi ya Shirika la Hifadhi ya Jamii(NSSF), Hasa Mradi wa Dege Beach Huko Kigamboni ambapo imeelezwa Kuwa Katika Kila Kiwanja Kimoja kati ya Viwanja 300 vilivyoko Katika hatua ya kwanza ya Mradi thamani ya Kiwanja imezidishwa Kwa zaidi ya Shilingi Milioni 775. Ikielezwa Kuwa thamani ya Kila Kiwanja Ni Shilingi Milioni 25 Tofauti na Milioni 800 ambazo NSSF imenunua Kwa Kila Kiwanja Kimoja Kwa Mujibu wa Mkataba kati yake Na Kampuni ya Azimio.

Taarifa Hizi ni za Uongo. Ukweli ni Kuwa NSSF haikununua Ardhi eneo la Dege Beach, Kigamboni Kwa thamani ya Milioni 800 Kwa Kiwanja, imepewa Ardhi Bure Ili iwekeze Kwa kuingia Ushirika wa Mradi Katika Ardhi ya Mtu Binafsi (Kampuni ya Azimio).

Aina hiyo ya Ushirika hujulikana Kwa wataalam wa Sekta ya Majengo (Real Estate) Kama Utaratibu wa "Land for Equity" (Yaani Ardhi Kwa Hisa). Ambapo Katika Makubaliano ya Mradi, Mbia Mmoja wa Mradi anatoa Ardhi Na Mbia mwengine anatoa Fedha za Uwekezaji. Na kisha Hisa za Mradi hugawanywa kulingana Na mtaji wa Kila Mmoja (Ardhi Kwa Mbia wa kwanza, Na Fedha Kwa Mbia mwengine).

Na hili si Jambo jipya nchini. Uchunguzi unathibitisha kuwa kilichofanywa na NSSF (Katika Mradi wa Dege Beach Kigamboni) ndicho kinachofanywa na taasisi mbalimbali nchini (wakiwemo NSSF wenyewe), katika Miradi mbalimbali ya Uwekezaji wa Ushirikiano kati sekta ya Majengo.

Baadhi ya mifano ya Miradi ya namna hiyo ni kama ifuatavyo:

• Miaka ya 90 Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) liliingia makubaliano na Shirika la Mafuta la Taifa (TPDC) kujenga Jengo la Mafuta House kwenye ardhi inayomilikiwa na NHC katika eneo ambalo sasa pamejengwa Jengo la Banjamin Mkapa Towers. Katika Ujenzi Huo NHC walipewa asilimia 25 ya thamani ya mradi kwa kutoa ardhi (Land for Equity) ambayo mwaka 1995 ilikuwa ni Shilingi bilioni 19 bilioni. Kwa mujibu wa mkataba huo thamani ya ardhi ile mwaka huo ilikuwa shs 4.75 bilioni.

Mwaka 1995 thamani ya ardhi katikati ya jiji la Dar es salaam ilikuwa ni shilingi 62,500 kwa kila mita ya mraba na kiwanja kile kina mita za mraba 6,221 sawa na ekari moja na nusu. Kwa kutumia mahesabu ya kawaida thamani ya ardhi ya NHC ingekuwa shilingi 388 milioni Na si hiyo 4.75 Bilioni ambayo inaonyesha bei kukuzwa Kwa nyongeza ya shilingi 4.35 bilioni.

• NSSF ni mfaidika wa Utaratibu wa "Land for Equity" Katika mradi Mpya wa Umeme Mkuranga. Mwaka 2014 NSSF ilinunua ardhi kwa thamani ya shilingi 100 milioni, ardhi hiyo ilikuwa Ni jumla ya ekari 100.

Mwaka 2015 Wawekezaji waliingia ubia na Shirika la NSSF Ili kujenga Mtambo wa Umeme Katika ardhi Husika. Mchango wa NSSF Katika Mradi Huo ulikuwa ni ardhi yake ya Ekari 100 ambayo iliinunua Kwa Shilingi Milioni 100 Tu Mwaka Mmoja nyuma. Lakini Katika Mkataba wa Mradi Huo NSSF imepata asilimia 10 ya thamani ya Mradi Mzima wa Uwekezaji ambayo ni Dola za Kimarekani 450 Milioni Sawa na zaidi ya Shilingi 900 Bilioni.

Katika Mradi huu wa Mkuranga NSSF ndani ya mwaka mmoja iliweza kupandisha thamani ya ardhi ile kutoka shilingi 100 milioni mpaka shilingi 90 Bilioni ambayo ni Asilimia 10 ya thamani ya Mradi Wote. Kama zingetumika Hesabu Za kawaida Tu thamani ya Uwekezaji wa NSSF kwenye Mradi Husika ilipaswa Kuwa Asilia 0.06 Tu Na Sio Asilimia 10 walizopewa.

• Mradi mwengine uliofuata Utaratibu wa "Land for Equity" (Ardhi Kwa Hisa) ni Taarifa Juu ya makubaliano kati ya NHC na PPF Katika Ujenzi wa Jengo la PPF Tower Mwanza, ambapo NHC walitoa ardhi na kupewa Aslimia 25 ya hisa za mradi husika. Mradi huo una thamani ya Shilingi bilioni 258, Lakini Ukubwa wa ardhi waliyotoa NHC ni Kiwanja cha ekari moja tu.

Kamwe huwezi kusikia ikisemwa kuwa PPF wamenunua Kiwanja Cha Ekari Moja Kwa thamani ya Shilingi Bilioni 64 Kwa Kuwa Ni Ushirika wa Pamoja.

• NSSF imejenga jengo RITA, eneo la Posta jirani Kabisa na Jengo la Klabu ya Billicanas Jijini Dar es salaam. Katika Mradi Huo RITA iliyojengewa Jengo Husika, Na Kwa Kutoa ardhi hiyo wamepata hisa Asilimia 25 ya thamani ya mradi mzima wa Jengo Hilo, ambayo ni hilingi Bilioni 198.

Lakini Ukubwa wa Kiwanja cha RITA ni nusu ekari tu. Kamwe huwezi kusikia NSSF wamenunua nusu ekari kwa Shilingi bilioni 49 Katika Mradi wa Jengo la RITA.

• Miradi mengine iliyofuata Utaratibu huu wa "Land for Equity"
* Mradi kati ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) na Fida-Hussein Katika Jengo lililoko Maeneo ya Jirani Na Hospitali ya Ocean Road.
* Mradi wa Jengo la UVCCM eneo la Fire Jijini Dar es salaam.
* Mradi wa Jengo la Mwalimu Nyerere Foundation eneo la Posta.
* Mradi wa Jengo la UWT (Makao makuu ya Airtel) eneo la Morocco nk.

• Hitimisho:

NSSF iliingia ubia na kampuni ya Azimio Kwaajili ya Uendelezwaji wa Ardhi Katika Mradi wa Dege Beach Kule Kigamboni. Kampuni ya Azimio Kwa Kutoa Ardhi ya Mradi Husika ilipewa asilimia 20 ya thamani ya mradi wa Dege Eco Village.

Lakini Pia kwenye Mkataba wa Mradi Azimio wanapaswa Kutoa 35% ya Fedha za thamani ya Mradi, Hivyo kuwafanya wawe na 55% ya Mradi Husika Huku NSSF wakiwa na 45 ya Mradi Kwa Fedha watakazotoa.
Wamiliki wa Azimio ni Nani? Je hakuna inside dealings hapo kweli
 
Dah....Mkuu umekuja thread mbili yote sababu umesikia Nssf inawezekana Dau hajui utamu wa pesa au alikuwa anakushilikisha kazi zote za Nssf
 
Hizo projects ulizotaja UVCCM, Rita, PPF, Benjamin tower ukiangalia utaona kuwa maeneo hayo yapo strategic na kutokana na location yake mwekezaji anakuwa hana option zaidi ya kukubaliana na mwenye ardhi. Unaweza ukaona kwa sasa Kariakoo wachaga na wakinga wanachukua ardhi na kujenga magorofa kisha jengo linakuwa jointly owned.

Pia taasisi za umma zikiingia mikataba zenyewe kwa zenyewe hata kama mmoja anagain zaidi hamna tatizo cuz zote ni public money na ni sawa na kuhamishia fedha zako toka mfuko huu na kupeleka kwenye mfuko mwingine.

Najiuliza bado kwanini NSSF hawakununua ardhi Kigamboni kisha waiendeleze wenyewe wakati maeneo kigamboni yapo wazi mengi tu? Kwanini waingie ubia na kampuni binafsi tena yeye ndio awe main shareholder? Mpaka hapo project ilipofikia, Azimio wameshatoa cash kiasi gani?
Hiyo Azimio ni ya nani? Who are the shareholders?
UNAMJUA AKBAR?
 
Looks like Gazeti la mwananchi wana ajenda zao na Nssf na Dr Dau...kwann hawaelezi ukweli?
Gazeti haliandiki habari zake kwa kusakura Bali toka ktk source ambazo ni purified,sasa kulauimu gazeti badala ya CAG ni upunguani
 
Watu wamepiga pesa kirahisi rahisi tu,
800 * 3500 = 2.3tr wakati thamani ya ardhi ya soko ni
25 * 3500= 87bn, huu ni wizi mkubwa zaidi ya Escrow, Richmond na takataka nyingine. Ona aibu THE BIG SHOW hata Allah haruhusu huu utapeli.
Unahitaji roho ngumu sana kuiba namna hii, sidhani kama hii ni kweli
 
Magazeti yafanye utafiti wa kutosha kabla ya kuandika kwenye magazeti yao.
Utafiti uliofanywa na Ernst and Young's kwa makubaliano na CAG,na taarifa zinazosambaa ni za CAG magazeti ni WAKALA tu wa kutuhabarisha,hii kitu ishatua bungeni syo siri tena,itajadiliwa at the same time vijana wa kazi wakifukunyua zaidi ili balozi awajibishwe,sasa kulaumu magazeti ni utaahira
 
Hatuwez kuwaacha mkipotosha sasa

Ukweli uelezwe jamii ijue
Ni kitu gani kimepotoshwa mkuu , usipindishe ukweli , hiyo ndo hali halisi na kumbuka kuwa kwa sababu ya ufisadi huo kuna wakati mlishindwa kulipa mafao hadi wanachama wakawaita watu wa ITV I think 2014 habari ilitoka ktk jiji letu saa 12 jioni,sasa we jipumzikie dau ashughulikiwe wewe hatakuhusu maada wewe ni sawa na chawa tu.
 
Back
Top Bottom