Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Mkuu Fundi Mchundo , hayo ni makombora ya uhakika kabisa.
Ningekua Mohammed Said ningeandika kitabu kingine cha kujisahihisa.
Sasa hebu tukae chonjo, tungojee hadithi nyingine ya Mohammed Said, nusu page ya "alisema hivi", "akamjibu hivi", "inaaminika hivi" nk
Asije sema tunamdharau, tumeshazoea modus operandi yake muungwana huyu, endelea.
LG: Hilo la kuandika kitabu cha kujisahihisha hakitakuwa na maana sana kama nitakiandika mimi. Mimi tayari nina vitabu kadhaa na papers. Nakushaurini mjikusanye msaidiane kuandika ili nami mnipe fursa ya kuwasoma wazee wenu katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.
Hapa afadhali sheikh Mohammed umefuata suna kwa kuonesha ukali wako kidogo.Hayo maroketi uliyotupa si ya kawaida.Mimi nimefurahishwa hasa na kombora la nne,kuhusu Japhet Kirilo.FM: Kwanza. hilo la title ni kweli yaliyomo ndani hayafanani sana na anuani na ntakupa sababu. Mwalimu wangu Maalim Haruna akisema, "Kila binadamu umuonae katika mgongo wa ardhi jua ana kitu kinamtisha hata akiwa na nguvu kiasi gani. Mimi nilkuwa kwa muda mrefu natafuta kitu kinachomtia hofu Nyerere. Nikakipata. Kwanza hakuwa anapenda kunasibishwa na waasisi waliomtangulia katika kupigania uhuru wa Tanganyika. Pili alikuwa akiuhofia sana Uislam. Ushahidi nimetoa ukumbini jinsi alivyowapa Kivukoni kazi ya kuandika historia ya TANU na ikaandikwa kwa sampuli ya kumpendeza yeye. Nilipoandika ile makala katika Africa Events (March/April 1988) magazeti yakakusanywa na kuchomwa moto. Hapo ndipo nilipojua kinachomtisha na ndiyo nikatoa anuani hii kwa kitabu changu: The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Utold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika.
Swali ulouliza wewe nilishaulizwa sana lakini sikuwa natoa jibu. Nilikuwa nasubiri mtu kama wewe ndiyo nilitoe maana kwako wewe jibu lina maana kuliko kwengineko.
Pili: Kuhusu kuwa mimi sielewi maana ya "definite article" nakuibia siri. Cambridge English Language Oral Examination - Merit Pass (1st Class).
Tatu: Kusisitiza usome kitabu ni kukurahisishia kazi kwani ni dhahir kuwa endapo ungelichukua tabu ya kusoma kitabu changu kuna maswali usingeliuliza hivyo tungeokoa muda. Huwezi kujadili kitu usichokifahamu.
Nne: Hili la Japhet Kirilo usiongelileta kama ungesoma kitabu. Kamati ya Meru Land Case ilikuwa - Abbas Sykes, Abdu Kandoro na Japhet Kirilo. Fedha za Kirilo za safari alizituma Ally Sykes (Mweka Hazina wa TAA) kwa Money Order kwenda USA River bahati mbaya hapo hapakuwa na Posta hivyo Kirilo hakuzipata fedha zile. Kamati ilitembea takriban nchi nzima. Serikali ilimnyima Kirilo pasi ya kusafiri ikabidi Abdu Sykes Rais wa TAA aingilie kati na pasi ikatolewa.
Tano: Hili la umaarufu hujibu mimi maarufu toka azal pale ninaposhutumiwa kuwa natafuta umaarufu. Wala sishangai kuwa hunijui. Mtu hata akiwa maarufu vipi si wote watamfahamu. Lakini sasa bado tu hunijui?
Sita: Kujuana na watu maarufu siyo ujanja wangu ni kutokana na kuzaliwa katika jamii hiyo na kwa wakati ule na sehemu ile vinginevyo ningelikuwa kama mtu mwingine yeyote.
Saba: Hilo la kujifanya mnyenyekevu hilo kwa watu wengine kusema.
Nane: Hizo takwimu za Waislam Bungeni sijaziona tafadhali nitumie tena.
Tisa: Simlazimishi mtu kuamini nisemayo hata kama nitataka uwezo huo sina.
Sheikh mohammed said, nadhani wewe ni moja ya hazina la taifa letu, nimesoma vyuo tofauti , nimesomeshwa na maprofesa lkn mimi ni mmoja wa watu ninaesoma sana makala kupitia magazeti yetu.naadinka makala pia hata siku moja sikuwahi kuona makala yako ikijibwa kwenye magazeti yetu. Kwa mfano makala unazotuma katika gazeti la rai na annur na magazeti mengine mimi niliwahi kuandika makala kupitia gazeti moja nchini kuhusu historia hii kwa kunukuu maneno yako. Lkn hadi leo hii miaka 3 sasa sikuwahi kuona majibu au kuikosoa historia hii. Licha ya hayo magazeti yanasomwa na magwiji wa historia nchini.
Endelea kutoa darsa
Mohammed,Jasusi: Ahsante kwa mchango wako. Naomba nifafanulie sentensi yako ya mwisho sijaelewa "sijamwona hata kiduchu...." Je, una maana sijamsifia Nyerere? Kama ni kuwa sijamsifia nifahamishe tafadhali. Huko "Nimemaliza" ndiyo hutaki tena mjadala na mimi?
Mohammed,Jasusi: Labda unifahamishe kwa hiyo TAWA na katiba kuweka hapa kwa kuwa unahisi ni kitu kikubwa? Kama ni hivyo jibu ni kuwa Kleist Sykes kaasisi African Association 1929 akiwa katibu na alikuwa kijana wa miaka 25. African Association ndiyo hii iliyokuja kuzaa TAA na TANU. Hivi unataka kuita TAWA harakati? Au unataka kufananisha TAWA na TAA? Labda nikuulize hiyo TAWA ilifanya nini? Sidhani kama unahitaji mimi nieleze yale yaliyofanywa na AA na TAA. Najua yote umeshasoma katika kitabu changu. La kama utapenda niyaweke ukumbini kwa ajili ya faida ya wanaukumbi ahlan wasahlan.
Mohammed,
Ninachosema ni kwamba Nyerere unayetuelezea wewe ni Nyerere aliyekuja Dar-es-Salaam akivaa kaptura, na kukaribishwa na kina Sykes hatimaye akawa kiongozi wa TAA. Hujasema kuwa Nyerere huyo, alipokuwa Makerere, tayari alikuwa anajishughuliksha na harakati za TAA. Nyerere huyo, ambaye Abbas Sykes alimwita "mtu aliyekuja kutukomboa" simwoni kitabuni mwako. Namwona Nyerere aliyekarimiwa na Waislamu, akapewa uongozi wa TAA na kushiriki kwenye uanzilishaji wa TANU kana kwamba yeye hakuwa na mchango wowote muhimu kwenye harakati hizo. Hicho ndicho ninachokisema na hicho ndicho kinachokosekana kwenye portrayal yako ya Julius Nyerere. Si jambo la kumsifia, lakini kumpa mnyonge haki yake. Mjadala uendelee lakini nimemaliza hii ya portrayal ya Nyerere kama passive participant.
Mohammed,Jasusi: Hebu ngoja nikupe habari za Lady Judith Listowel. Huyu mama mume wake alikuwa Gavana Ghana. Alikuja Dar es Salaam na kupokelewa na Ally Sykes baada ya Listowel kujulishwa kwake na Peter Colmore. Colmore ndiyo alikuwa Mr Fix pale Nairobi. Wazungu wote wakiwa na jambo lao kuanzia kufungua biashara hadi kwenda Mombasa kwa mapumziko Colmore ndiyo alikuwa mtu wao. Mimi nilikuwa nikimuona Colmore toka utoto wangu na nikakutananae nyumbani kwake Muthaiga mwaka 1995. Nilikwenda kumhoji nilikuwa naandika kitabu "Under the Shadow of British Colonialism in Tanganyika." Yeye ndiye aliyenipa habari za Judith Listowel. Ikawa kila nikenda Nairobi nitampigia simu na yeye atanikaribsisha Muthaiga Club na hapo atanipa stori nyingi sana za Dar es Salaam, Kampala na Nairobi ya 1950s huko akiwa na akina Kabaka Freddy Mutesa, Frank Humplink, Eduardo Masengo, Ally Sykes na jamaa wengine. Niliokota mengi sana kwake. Yeye ndiye mtu wa kwanza kuwa na tape recorder East Africa na wa kwanza kurekodi muziki HMV. Yeye ndiye aliyewakuza wanamuziki kama Msafiri Morimori, Masengo Eduardo na yeye ndiye aliyemleta Jean Mwenda Bosco Nairobi mwaka 1960. Nilijitahidi sana kumshawishi niandike biography yake lakini alikataa. Alipokufa nilishtushwa na taazia nyepesi zilizoandikwa na magazeti ya Kenya. Nilipoandika yangu Mhariri wa The East African alinipigia simu akaniuliza nilimjuaje kiasi cha kuweza kuandika taazia kama ile. Nilimjibu, "Colmore alikuwa baba yangu." Lakini ninachotaka kukuambia khasa ni kuwa Peter Colmore akimchukia sana Nyerere na kisa ni kuwa alihujumu biashara zake na kutaifisha nyumba yake iliyokuwa Moshi. Insha Allah siku nyingine nitakupa kisa cha Ally Sykes alipowapeleka Colmore na Masengo kuonana na Nyerere nyumbani kwake Magomeni Majumba Sita.