Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

Status
Not open for further replies.
Mkuu Fundi Mchundo , hayo ni makombora ya uhakika kabisa.
Ningekua Mohammed Said ningeandika kitabu kingine cha kujisahihisa.
Sasa hebu tukae chonjo, tungojee hadithi nyingine ya Mohammed Said, nusu page ya "alisema hivi", "akamjibu hivi", "inaaminika hivi" nk
Asije sema tunamdharau, tumeshazoea modus operandi yake muungwana huyu, endelea.

LG: Hilo la kuandika kitabu cha kujisahihisha hakitakuwa na maana sana kama nitakiandika mimi. Mimi tayari nina vitabu kadhaa na papers. Nakushaurini mjikusanye msaidiane kuandika ili nami mnipe fursa ya kuwasoma wazee wenu katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.
 
Mkuu Mohammed Said, umechagua mada isiyo kufaa kwa kuandika kitabu kwa ajili ya jamii ya Kitanzania.Hicho kitabu ungetoa angalizo -"For Muslim Eyes Only", kisingeleta mtafaruku.
Kwa vyovyote vile kutokana na utangulizi wako tuliouona hapa jamvini, sitakinunua as I will be wasting my money.Hivo basi acha kukipigia chapuo jamvini for a book that is both controversial and full of half truths
 
Mohammed,
Nyerere hakuacha kazi ya ualimu kwa kushinikizwa na wamishenari. Ulikuwa ni uamuzi wake mwenyewe akitaka kutumia muda wake katika harakati za TANU. Niambie ni mmishenari gani uliyezungumza naye akakuhakikishia kuwa ndio wao waliomlazimisha Mwalimu kuacha kazi. Ni vitu vidogo kama hivi vinavyopaka tope kazi yako, lakini kwako naona ni muhimu kwa sababu unataka kuonyesha jinsi Nyerere alivyokuwa "controlled" na hao wamishenari.
 
Jasusi: Ahsante kwa angalizo lako. Baada ya Nyerere kurudi kutoka UNO na yale mapokezi makubwa aliyopata mambo yakawa moto sasa Wamishionari wakamwambia achague moja kati ya mawili siasa au kazi ya ualimu. Ikiwa una taarifa nyingine nifahamishe siwezi kukataa kusahihishwa. Lakini nilivyopokea mimi kwa wazee wangu ni kuwa baada ya Nyerere kupata ile barua aliileta kwa Mzee Clement Mtamila ambae kwa wakati ule ndiye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya TANU. Mzee Mtamila akaitisha mkutano wa Kamati Kuu nyumbani kwake Mtaa wa Kipata/Sikukuu. Kamati iliamua kumshauri aache kazi. Kisa hiki nimekieleza kwa kirefu katika kitabu changu. Juu ya hayo kama una taarifa kinyume ya haya niliyoeleza ueleze ukumbi. Sijataka hata kidogo kuonyesha jambo kinyume cha ukweli. Niamini.

Nyumba ya Mzee Mtamila haikuwa mbali na kwetu. Mzee Mtamila alikuwa hakimu mahakama ya Temeke. Basi watoto tukipita nje ya nyumba yake tulikuwa tukichungulia kwenye sitting room yake. Kulikuwa na picha nyingi sana za black and white katundika ukutani zikionyesha mikutano ya mwanzo ya TANU iliyokuwa ikifanyika Mnazi Mmoja mbele ya sasa lilipo jengo la Elimu ya Watu Wazima. Kwa kweli mimi sijui kwa nini zile picha nikizipenda ilikuwa lazima nisimame pale mlangoni na kuzichungulia.

Nyumba hii imevunjwa kuna gorofa hivi sasa. Mara ya mwisho kuingia mle nilikwenda kwa Mzee Baharoon ambae ni baba mkwe wa rafiki yangu. Hii ni kama zaidi ya miaka kumi na kitu iliyopita.

Kuna makala nimeandika kuhusu kuvunjwa kwa nyumba za historia ya uhuru wa Tanganyika naingia archive nikiipata Insha Allah nitaiweka ukumbini.
 
LG: Sijamfunga mtu minyororo. Una uhuru wa kufanya upendavyo. Tuendelee na mjadala. Hilo la kujikusanyana na nyie mkaandika habari mathalan za wazee wenu unaliona zito? Nimemshauri kijana mmoja anosomesha historia katika moja ya vyuo vikuu vyetu atoe assignment kwa wanfunzi wake wakati wa likizo wafanye utafiti na waandike kuhusu siasa za utaifa na kupigania uhuru wa Tanganyika. Insha Allah huenda tukapata mengi kutoka mikoani.
 
FM: Kwanza. hilo la title ni kweli yaliyomo ndani hayafanani sana na anuani na ntakupa sababu. Mwalimu wangu Maalim Haruna akisema, "Kila binadamu umuonae katika mgongo wa ardhi jua ana kitu kinamtisha hata akiwa na nguvu kiasi gani. Mimi nilkuwa kwa muda mrefu natafuta kitu kinachomtia hofu Nyerere. Nikakipata. Kwanza hakuwa anapenda kunasibishwa na waasisi waliomtangulia katika kupigania uhuru wa Tanganyika. Pili alikuwa akiuhofia sana Uislam. Ushahidi nimetoa ukumbini jinsi alivyowapa Kivukoni kazi ya kuandika historia ya TANU na ikaandikwa kwa sampuli ya kumpendeza yeye. Nilipoandika ile makala katika Africa Events (March/April 1988) magazeti yakakusanywa na kuchomwa moto. Hapo ndipo nilipojua kinachomtisha na ndiyo nikatoa anuani hii kwa kitabu changu: The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Utold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika.

Swali ulouliza wewe nilishaulizwa sana lakini sikuwa natoa jibu. Nilikuwa nasubiri mtu kama wewe ndiyo nilitoe maana kwako wewe jibu lina maana kuliko kwengineko.

Pili: Kuhusu kuwa mimi sielewi maana ya "definite article" nakuibia siri. Cambridge English Language Oral Examination - Merit Pass (1st Class).

Tatu: Kusisitiza usome kitabu ni kukurahisishia kazi kwani ni dhahir kuwa endapo ungelichukua tabu ya kusoma kitabu changu kuna maswali usingeliuliza hivyo tungeokoa muda. Huwezi kujadili kitu usichokifahamu.

Nne: Hili la Japhet Kirilo usiongelileta kama ungesoma kitabu. Kamati ya Meru Land Case ilikuwa - Abbas Sykes, Abdu Kandoro na Japhet Kirilo. Fedha za Kirilo za safari alizituma Ally Sykes (Mweka Hazina wa TAA) kwa Money Order kwenda USA River bahati mbaya hapo hapakuwa na Posta hivyo Kirilo hakuzipata fedha zile. Kamati ilitembea takriban nchi nzima. Serikali ilimnyima Kirilo pasi ya kusafiri ikabidi Abdu Sykes Rais wa TAA aingilie kati na pasi ikatolewa.

Tano: Hili la umaarufu hujibu mimi maarufu toka azal pale ninaposhutumiwa kuwa natafuta umaarufu. Wala sishangai kuwa hunijui. Mtu hata akiwa maarufu vipi si wote watamfahamu. Lakini sasa bado tu hunijui?

Sita: Kujuana na watu maarufu siyo ujanja wangu ni kutokana na kuzaliwa katika jamii hiyo na kwa wakati ule na sehemu ile vinginevyo ningelikuwa kama mtu mwingine yeyote.

Saba: Hilo la kujifanya mnyenyekevu hilo kwa watu wengine kusema.

Nane: Hizo takwimu za Waislam Bungeni sijaziona tafadhali nitumie tena.

Tisa: Simlazimishi mtu kuamini nisemayo hata kama nitataka uwezo huo sina.
Hapa afadhali sheikh Mohammed umefuata suna kwa kuonesha ukali wako kidogo.Hayo maroketi uliyotupa si ya kawaida.Mimi nimefurahishwa hasa na kombora la nne,kuhusu Japhet Kirilo.
Lakini usishangae hawa jamaa hawana haya na ni wapiganaji hodari wa Tume ya majeshi aliyojisifia kardinali Pengo kwa Papa.
Hapa hawawezi kuondoka hata wakijeruhiwa na maroketi yako.Ukiangalia hapo umejibu na kuweka wazi kuliko kawaida lakini hizo watasema ni hadithi wanazozipenda!
Kumbuka hii tume ya majeshi ipo kazini ndani ya jeshi lenyewe,ndani ya bunge,mawizara na hata kwenye mitandao.Hawa walijipenyeza mwaka 1998 ndani ya jeshi la polisi na kuuwa vijana msikitini Mwembechai.Wale wapiganaji wao bungeni wakasema serikali haina fedha kuunda tume kuchunguza kadhia ile,lakini pesa hazikukosekana kuunda tume kuchunguza mbwa aliyeitwa Immigration
Hawapo kukuvunjia heshima wewe tu bali uislamu wote kwa ujumla kama alivyowahi kugusia Lole kwenye 796.

" Jamaa huyu anaweka mjadala kwa nia ya kuudhibiti ukristo ili uislamu uneemeke kwa sababu yoyote ile. Na vile vile basi anatazamia watu wakae doro na kukubali yale yanayotolewa na kuelezewa as if mipango yote ya kuleta uhuru ilifanyika na kina Sykes na waislamu wengine, na Mwalimu akakaribishwa tu ku-officiate the occassion.
History cannot be so simple and cheap."

Kwa hali hiyo usitarajie akina Fundi,Lole na wenzao kukaa doro wanapoona uislamu utaneemeka kutokana na ukweli wa historia ya Tanganyika,ni lazima waivuruge tu iende kwa matakwa ya dini yao ambayo dhulma kwao si tatizo.
 
Mohammed,
Kabla sijaongezea hili la Nyerere kuacha kazi nakuletea na wewe dondoo hii kutoka kitabu cha Judith Listowell:
"In his second year, (at Makerere) young Nyerere began to grope for a political organisation, something that could, eventually
be transformed into a political party and help the Tanganyikans to work for self government. He and Hamza Mwapachu,
his closest friend, founded the Tanganyika African Welfare Association, known as TAWA.
I drafted TAWA's constitution [Julius Nyerere has told the author]. It was frankly political. Then I sent it to a number
of friends and to people who I thought might sympathise and join. One of them wrote back saying that there existed an organisation
in Tanganyika which would be excellent for my purposes, the Tanganyika African Association. It had quite a past, Sir Donald
Cameron having founded it to provide Africans in towns with a sounding board and a place where they could discuss their views.
It had the further advantage, he said, of having branches in all sizable towns. Cameron had not intended it as a political organisation
although he had not forbidden political discussion." page 184.

Huyo ndiye Nyerere aliyekuwa Makerere, aliyekwenda Dar-es-Salaam na kukaribishwa na akina Sykes na kujiunga na TAA. Kumbe alishashiriki katika harakati tangu akiwa Makerere. Hilo hujasema kwenye kitabu chako. Nitarudi baadaye
 
one of the sykes nadhani badomzima namfahamu kama mze ambae hupenda kutoa story mbalimbali hasa kuhusu TANU.
Hana makuu sana

hizo hadithi za namba za mitihani kuletwa na kighoma malima zinakuzwa pia na Basalehe wasikwepeukweli wakati wakristo wakijenga mashule
wao madrasa. Mtihani hauulizi juzuu elimu dunia tuu
mzee said chonde chonde usituletee uchochezi
 
Sheikh mohammed said, nadhani wewe ni moja ya hazina la taifa letu, nimesoma vyuo tofauti , nimesomeshwa na maprofesa lkn mimi ni mmoja wa watu ninaesoma sana makala kupitia magazeti yetu.naadinka makala pia hata siku moja sikuwahi kuona makala yako ikijibwa kwenye magazeti yetu. Kwa mfano makala unazotuma katika gazeti la rai na annur na magazeti mengine mimi niliwahi kuandika makala kupitia gazeti moja nchini kuhusu historia hii kwa kunukuu maneno yako. Lkn hadi leo hii miaka 3 sasa sikuwahi kuona majibu au kuikosoa historia hii. Licha ya hayo magazeti yanasomwa na magwiji wa historia nchini.
Endelea kutoa darsa

Mkuu Malaria S. ,makala za MS katika magazeti uliyoyataja hazipati majibu kwa vile, moja, nobody is interested , two magazeti uliyo taja ni kioo tosha cha kile tunacho mshauri MS afanye.Vitabu vyake avipeleke kule kuliko na wenye interest ya kuvisoma na atapata wafuasi wasio jua kuchambua pumba na mchele.
Hapa JF hata nukta na alama ya kuuliza inachambuliwa , hapa ni hadharani.

Akitaka isichambuliwe kabisa aipeleke msikitini.
 
Nyerere kushinikizwa na wamishenari kuacha kazi:
Kutoka kitabu "We Must Run While They Walk," A Portrait of Africa's Julius Nyerere, William Edgett Smith anaandika:
Nyerere had been hired to teach history at St Francis College in Pugu, 12 miles from Dar-es-Salaam. At first he was paid 300 pounds a year. "But after a little noise," he has said, "they raised it to 450. I knew this was only 3/5 of what I would receive if I were an expatriate. But I also knew it was more was more than I would have been paid for the same kind of work in England. pg. 62-63
......Later, when Nyerere was forced to resign his teaching job because of his political activities, his friends were even more impressed. "He showed he was prepared to sacrifice," Sykes (Abbas) said. "We said, 'Here is a man who has come to save us." pg 66
In addition, Nyerere, as a mission school teacher, was relatively free of government control, whereas most of the TAA leaders were civil servants.
Kwanza, unaona hata kina Sykes walimshabikia, kwa tabia yake, kuwa huyu kaja kutukomboa. Pili. Aliacha kufundisha shule za serikali na kujiunga na shule ya misheni kwa sababu kule hawakumwekea misukule katika kuendelea na harakati zake za TANU. Hakuna mkono wa mmishenari hapo. Huyu Nyerere aliyesifiwa na akina Abbas Sykes kuwa kaja kutokomboa sijamwona hata kiduchu katika kitabu chako. Nimemaliza.
 
Jasusi: Ahsante kwa mchango wako. Naomba nifafanulie sentensi yako ya mwisho sijaelewa "sijamwona hata kiduchu...." Je, una maana sijamsifia Nyerere? Kama ni kuwa sijamsifia nifahamishe tafadhali. Huko "Nimemaliza" ndiyo hutaki tena mjadala na mimi?
 
Jasusi: Labda unifahamishe kwa hiyo TAWA na katiba kuweka hapa kwa kuwa unahisi ni kitu kikubwa? Kama ni hivyo jibu ni kuwa Kleist Sykes kaasisi African Association 1929 akiwa katibu na alikuwa kijana wa miaka 25. African Association ndiyo hii iliyokuja kuzaa TAA na TANU. Hivi unataka kuita TAWA harakati? Au unataka kufananisha TAWA na TAA? Labda nikuulize hiyo TAWA ilifanya nini? Sidhani kama unahitaji mimi nieleze yale yaliyofanywa na AA na TAA. Najua yote umeshasoma katika kitabu changu. La kama utapenda niyaweke ukumbini kwa ajili ya faida ya wanaukumbi ahlan wasahlan.
 
Ninachosema ni kwamba Nyerere unayetuelezea wewe ni Nyerere aliyekuja Dar-es-Salaam akivaa kaptura, na kukaribishwa na kina Sykes hatimaye akawa kiongozi wa TAA. Hujasema kuwa Nyerere huyo, alipokuwa Makerere, tayari alikuwa anajishughuliksha na harakati za TAA. Nyerere huyo, ambaye Abbas Sykes alimwita "mtu aliyekuja kutukomboa" simwoni kitabuni mwako. Namwona Nyerere aliyekarimiwa na Waislamu, akapewa uongozi wa TAA na kushiriki kwenye uanzilishaji wa TANU kana kwamba yeye hakuwa na mchango wowote muhimu kwenye harakati hizo. Hicho ndicho ninachokisema na hicho ndicho kinachokosekana kwenye portrayal yako ya Julius Nyerere. Si jambo la kumsifia, lakini kumpa mnyonge haki yake. Mjadala uendelee lakini nimemaliza hii ya portrayal ya Nyerere kama passive participant.
 
Kati ya 1929 na 1945 ni miaka mingi sana. Huwezi kuniambia hiyo TAA ya 1929 ndiyo hiyo hiyo iliyokuwepo 1945 au hata 1952. Lazima kulikuwepo transformation, ama ya mwundo au uongozi. Nimetaja TAWA kwa sababu ilianzishwa katika eneo ambako hakukuwepo TAA na kuonyesha kuwa Nyerere was not a docile bystander. Alikuwa mwanaharakati hata akiwa mwanafunzi Makerere unless tunatofautiana katika tafsiri yetu ya neno "harakati."
 
Jasusi: Hilo usemalo ni sawa. African Asociation na hata TAA zilikuwa wakati mwingine juu wakati mwingine zinasinzia kutokana na uongozi uliokuwepo wakati huo. Hili silisemi mimi nawanukuu Hassan Suleiman na Ali Ponda waliokuwa viongozi wa African Association Dodoma nyakati kabla ya Vita Kuu ya Pili.

Mimi sijasema kama Nyerere alikuwa kakaa tu la hasha. Ila nataka nikueleze kama unataka kumkuza Nyerere katika TAA katika miaka ya mwanzo kabisa ya 1950s utapata tabu sana.

Huo ulikuwa wakati wa Abdu Sykes. Nyerere alikuja kung'ara 1954 baada ya safari ya UNO.

Hata hivyo kama unazijua harakati za Nyerere na TAWA basi ziweke ukumbini kwa faida yetu sote.
 
Mohammed,
Ninachosema ni kwamba Nyerere unayetuelezea wewe ni Nyerere aliyekuja Dar-es-Salaam akivaa kaptura, na kukaribishwa na kina Sykes hatimaye akawa kiongozi wa TAA. Hujasema kuwa Nyerere huyo, alipokuwa Makerere, tayari alikuwa anajishughuliksha na harakati za TAA. Nyerere huyo, ambaye Abbas Sykes alimwita "mtu aliyekuja kutukomboa" simwoni kitabuni mwako. Namwona Nyerere aliyekarimiwa na Waislamu, akapewa uongozi wa TAA na kushiriki kwenye uanzilishaji wa TANU kana kwamba yeye hakuwa na mchango wowote muhimu kwenye harakati hizo. Hicho ndicho ninachokisema na hicho ndicho kinachokosekana kwenye portrayal yako ya Julius Nyerere. Si jambo la kumsifia, lakini kumpa mnyonge haki yake. Mjadala uendelee lakini nimemaliza hii ya portrayal ya Nyerere kama passive participant.

JASUSI: Kwa hisani yako hebu achana na haya maneno ya "kaptula" mimi nimeeleza hapa Ukumbini kuwa baba yagu akivaa kaptula akienda kazini. Abdu Sykes akiwa Market Master Soko la Kariakoo ofisi yake ilikuwa pale Mtaa wa Swahili nyuma Tandamti mbele Mkunguni watu wakimwona pale kavaa kaptula na shati jeupe.

Tufanye mjadala wa maana tuache lugha zisizofaa. Sawa Mkuu? Usiharibu mjadala tuna dhima kwa watu wanaotusoma hawategemei sisi tuuchafue ukumbi.
 
Mohammed,
Haja yangu si kumkuza Nyerere. Ni kuonyesha kuwa na yeye alikuwa na mchango katika harakati za TAA hata kabla ya kuja Dar-es-Salaam, kwamba it was inevitable nyota ya Nyerere ingeng'ara katika harakati za ukombozi wa Tanganyika. Siwezi kumshindanisha Nyerere na Abdu Sykes. Kila mtu alikuwa na mchango wake kwa pamoja na kila mtu kwa wakati wake.
 
LG: Mjadala ukichafuka mimi nitalia na wewe. Kwa nini unaudhika kwa mambo madogo tu. Sasa hii ya msikiti ya nini hapa?

Unadhani nani atatuunga mkono kustawisha ukumbi ikiwa michango ni hii ya kuparurana?

Hujui kuwa sisi tunajinadi kwa kauli mbiu "great thinkers?"
 
Jasusi: Hebu ngoja nikupe habari za Lady Judith Listowel. Huyu mama mume wake alikuwa Gavana Ghana. Alikuja Dar es Salaam na kupokelewa na Ally Sykes baada ya Listowel kujulishwa kwake na Peter Colmore. Colmore ndiyo alikuwa Mr Fix pale Nairobi. Wazungu wote wakiwa na jambo lao kuanzia kufungua biashara hadi kwenda Mombasa kwa mapumziko Colmore ndiyo alikuwa mtu wao. Mimi nilikuwa nikimuona Colmore toka utoto wangu na nikakutananae nyumbani kwake Muthaiga mwaka 1995. Nilikwenda kumhoji nilikuwa naandika kitabu "Under the Shadow of British Colonialism in Tanganyika." Yeye ndiye aliyenipa habari za Judith Listowel. Ikawa kila nikenda Nairobi nitampigia simu na yeye atanikaribsisha Muthaiga Club na hapo atanipa stori nyingi sana za Dar es Salaam, Kampala na Nairobi ya 1950s huko akiwa na akina Kabaka Freddy Mutesa, Frank Humplink, Eduardo Masengo, Ally Sykes na jamaa wengine. Niliokota mengi sana kwake. Yeye ndiye mtu wa kwanza kuwa na tape recorder East Africa na wa kwanza kurekodi muziki HMV. Yeye ndiye aliyewakuza wanamuziki kama Msafiri Morimori, Masengo Eduardo na yeye ndiye aliyemleta Jean Mwenda Bosco Nairobi mwaka 1960. Nilijitahidi sana kumshawishi niandike biography yake lakini alikataa. Alipokufa nilishtushwa na taazia nyepesi zilizoandikwa na magazeti ya Kenya. Nilipoandika yangu Mhariri wa The East African alinipigia simu akaniuliza nilimjuaje kiasi cha kuweza kuandika taazia kama ile. Nilimjibu, "Colmore alikuwa baba yangu." Lakini ninachotaka kukuambia khasa ni kuwa Peter Colmore akimchukia sana Nyerere na kisa ni kuwa alihujumu biashara zake na kutaifisha nyumba yake iliyokuwa Moshi. Insha Allah siku nyingine nitakupa kisa cha Ally Sykes alipowapeleka Colmore na Masengo kuonana na Nyerere nyumbani kwake Magomeni Majumba Sita.
 
Mimi sikuwahi kukutana na Peter Colmore, lakini nilipokuwa nafanya utafiti wa muziki wa Masengo kuna jamaa pale Nairobi akanipa simu yake.
Nikamwambia nafanya utafiti wa muziki wa Edward Massengo kwa kipindi cha redio, akaniambia niende kwake atanipa tapes za muziki. Kwa kuwa nilikuwa naondoka usiku huo nilituma kijana pale ofisini Nairobi akanichukulie tape na kuiweka kunitumia Marekani. Nimeipata muda tu wakati natayarisha kipindi nikapata habari kuwa Edward Massengo amefariki huko kwao Lubumbashi. Nikapiga simu Lubumbashi, nikaongea na wanae Edward Massengo nikawaambia natayarisha kipindi cha memorial ya baba yao. Nikatumia ile tape ya muziki alionipa Colmore, nikampigia Ally Sykes ( alikuwa hana habari wakati huo) nikamwambia Massengo amefariki na nafanya kipindi cha memorial. Tukazungumza, nikatayarisha kipindi na bahati nzuri kimerushwa na Radio Ngoma FM Lubumbashi siku Massengo anazikwa. Baadaye nikazungumza na wanae wakashangaa nimepata wapi ule muziki wa baba yao. Baadhi wakasema hata wenyewe hawakuwa nao. Eniwei, sikutaka kutoka nje ya mjadala lakini ulipomtaja Colmore nikashindwa kujizuia. Tape ya memorial ninayo hadi leo napanga kumpelekea Ally nitakaporejea Dar-es-Salaam. Colmore alipofariki nilipigiwa simu na ofisi yetu Nairobi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom