Ndio maana Biblia inasema kanisa hili lililoitwa "Babeli Mkuu, mama wa makahaba na machukizo ya nchi".Ufunuo 17:5.
ni kanisa mama na lina watoto wanaofuata nafundisho yake.Linaitwa babeli baada ya kubadili amri za Mungu pamoja na majira rejea Daniel 7:25. " Naye atanena maneno kinyume chake aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake aliye juu, naye ataazimu kubadili majira na sheria, nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, nyakati na nusu wakati"
Anayezungumziwa hapo ni utawala wa kipapa wa kanisa la Roman Catholic.kanisa limetesa watakatifu wa Mungu kama ilivyotabiliwa kwa siku 1260 (ufunuo 11:3: ufunuo 12:6)au miezi 42 (ufunuo 11:2), au miaka mitatu na nusu (Daniel 7:25). Hiki ndicho kipindi cha zama za giza. Biblia haikiruhusiwa kusomwa na waumini wa kawaida isipokuwa misale ya waumini ambayo tayari ilikuwa imepotishwa. Ni kipindi hiki waliibuka wana matengenezo wakiwemo Martin Luther, Jan Huss, Jerome na wengineo ambao walianza kupinga mafundisho potofu ikiwemo kutubu dhambi kwa padri na kupewa cheti cha msamaha., ibada za wafu n.k. mambo haya yaliamsha mateso kwa hawa watakatifu wa Bwana kama ilivyotabiriwa kuwa watatiwa mikononi mwa huyu mnyama, ama pembe ndogo iliyozuka katika pembe za huyu mnyama yaani Rumi ama Babeli Mkuu yule kahaba wa Ufunuo 17:5.
Haya mambo yako wazi, historia iko wazi na Biblia imetoa nuru ya kutosha kuhusu uasi wa Roman Catholic, jambo lililopelekea kuitwa "Mama wa Makahaba na machukizo ya nchi". Nawasihi turejee mafungu hayo niliyotoa kwa kupata maarifa ya kutusaidia katika wokovu wetu.