Ukweli kuhusu Wakatoliki kutokuabudu sanamu zilizopo makanisani

Tunashukuru kwa kutufafanulia kwa kina.
Tatizo la madhehebu mengine haya ni SHULE.
Kwao shule ndiyo tatizo la msingi na ndiyo maana huwa hawaelewi nini maana ya kuabudu sanamu, na pia hawaelewi kama Mungu alikataa kuziabudu na kuzitumikia sanamu au alikataa kuzichonga sanamu.
Kutokana na tatizo lao hilo la msingi usishangae bado hawajaelewa pamoja na ufafanuzi huo.
Ubarikiwe sana.
 
Hebu jisemee nafsi yako....Huko hivyo na nani...??

Pole maana una-poor catechesis....

Sikujua kuwa wewe ni mtupu kiasi hiki...ningejua parokia yako, nikikuona tu unaingia nahakikisha nakutoa nje maana wewe ni mafiki wa kiwango cha juu
huna mamlaka na kanisa mpaka umtoe mtu nje ww unauhakika ni msafi mbele za mungu acha kujiona bora
 
Amri kuu upendo tu hizo chuki muachie mwenyewe Mungu ndo atajua .....wewe hata uchukie haitabadili kitu
 
Imeandikwa usiwe na miumgu wengine ila mimi.Usijifanyie sanamu ya kuchonga mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni au kilicho chini duniani au kilicho majini chini ya nchi.Usivisujudie wala kuvitumikia.
Sasa hapa kwa wenzetu inakuwaje?
 
Kusoma tushindwe na kuona napo kuwe shida
 
math 5;17-19
17 Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.
18 Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie.
19 Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.
 
MUNGU si kigeugeu kama mwanadamu ,ukiona neno lake linajipinga ujue tatizo lipo kwako. malach 3;6
 
Kwaiyo hilo andiko lina sapoti au lina pinga?naomba kueleweshwa tafadhali
 
Imeandikwa usiwe na miumgu wengine ila mimi.Usijifanyie sanamu ya kuchonga mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni au kilicho chini duniani au kilicho majini chini ya nchi.Usivisujudie wala kuvitumikia.
Sasa hapa kwa wenzetu inakuwaje?
aisee huwa wanazipa heshima zile sanamu kama ndo watu halisi
 

rejea hotuba ya Yesu mlimani... jee Yesu kwa kuongea hivyo ni mdogo kabsaa ktk Ufalme wa mbinguni [emoji46] ona na hapa [emoji117] wapi Tora iliamrisha kihivyo [emoji15] [emoji46] usisome Biblia Takatifu kama usomavyo gazeti la udaku, sababu Imeandikwa [emoji117]
 
swali zuri, unatakiwa ujue kwamba kuna tofaut kati ya amri za mungu na amri za mussa/wazee wa israel
amri kumi za mungu zilitolewa zitumike kama kioo kwa binadamu ili kujua umetenda dhambi,lakini amri za mussa zilikuwa ni kama sheria za nchi ili kuongoza vyema
je,ni sehemu gani katika amri kumi za mungu zilizungumzia kiapo???????????
 
Na zile sanamu Mungu alizomuagiza musa kuchonga?
 
Mleta hoja atakuwa mvuta bhangi. Kwanini ukosoe imani za watu? Endelea na imani yako achana na wengine
 
Kama tukiweza kujua kuwa hata nyumba za ibada tunazojenga bado kimsingi ni kazi za mikono yetu wenyewe.

Biblia Agano la Kale limejaa maandiko kuhusu manabii na wafalme walivyo kuwa wakizivunja madhabahu za miungu ashera na mabaali na kumjengea Mungu wa Abraham, Isack na Yakobo madhabahu.

Kwa jinsi hii dhana ya kuabudu sanamu inavyo chukuliwa na baadhi yetu humu hata hizi nyumba za ibada na madhabahu zitakuwa ni sanamu.

Mpinga kristo ana nguvu ya ajabu mno kawashikia akili baadhi ya wakristo hata wakiuona msalaba wana uogopa kama ukoma.

Wakati msalabani ndipo hasa ukombozi wetu Wakristo ulipo patikana. Shetani alishindwa katika msalaba lakini yeye alivyo na hila na maujanja ujanja kawafanya baadhi ya wale wanaojiiata wakristo kindakindaki wanaukimbia msalaba. Hakika Mandiko Matakatifu haya kukosea pale yalipo sema, "Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa."

Hivi kwa nini fimbo za Musa, Haruni na Yakobo zisiwe masanamu? Ama kwa hakika wako Wakristo wamegeuka kuwa laana (yaani wamekua laana kwa maana ya laanatula) katika Ukristo badala ya kuwa baraka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…