Neema, baraka na Upendo wa MUNGU, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Ushirika wa Roho Mtakatifu viwe nanyi nyote......!!!!. Ndugu zangu kumekuwa na kelele za hapa na pale kuwa eti Wakristo Wakatoliki wanaabudu Sanamu, hoja hii SIYO YA KWELI Kabisa. Nasisitiza siyo ya Kweli,Jamani mbona mnatuwekea maneno mdomoni ???.,nasema hivi Wakatoliki hatuabudu Sanamu.Weeee !!! hebu tuliza Munkali, fuatana nami.
A:UTANGULIZI.
Katika Biblia MUNGU alikataza Ibada ya Sanamu, lkn jinsi alivyokataza, katazo hilo limewaacha Wakristo Wengi njia panda, hivyo kujikuta wakichanganyikiwa.
Kutoka 20:4-"Usijifanyie Sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu Mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia ".
Kumbukumbu la torati 5:8-"Usijifanyie Sanamu ya kuchonga, mfano wa kitu chochote kile kilicho juu Mbinguni, au kilicho chini duniani, au kilicho majini chini chini ya nchi ".
Sehemu hizi ktk Biblia zikichukuliwa jinsi zilivyo maana yake zinakuwa zimetoa katazo la kutengeneza Sanamu kitu chochote kile wala picha hata Video .Sasa Ndugu Zangu, Walioweka picha za wapendwa wao majumbani, maofisini, vyombo vya Usafiri na kwenye mabango ya Matangazo ni Wakatoliki tu ???. Hivi pesa tunazotumia si zina picha za Viongozi,Wanyama na mimea, je kwa mujibu wa Vifungu tulivyosoma si mnakosea Jamani ??, Mnaonaje km mngetuachia hayo Manoti na masarafu ya hela sisi Wakatoliki ??, Najua wako wenye Vichwa vya Panzi hao watashupaza shingo kuwa picha sio sawa na Sanamu, Nawaambia tulizeni boli, twende taratibu tuwakokote "SLOW LEARNERS ".Nakwambia hivi Kibiblia "SANAMU ni SAWA NA PICHA ni SAWA na SANAMU ".Upo hapo ???!!!. Kama unabisha soma hapa Marko 12:15-16.
15 Tumpe, tusimpe ?,naye akijua unafiki wao, Akawaambia, mbona mmenijaribu ? Nileteeni dinari niione.
16 Wakaileta. Akawaambia ,ni ya nani Sanamu hii na anwani hii ?? wakamwambia ni ya Kaisari.
-Unaona ???!!!. Picha ya Kaisari, kiongozi wa nchi ambayo ipo kwenye Fedha, hapa ktk Biblia inatajwa km Sanamu ya Kaisari na hata Yesu Mwenyewe aliitumia sarafu hiyo. Kumbe mtaona kuwa kwa kuishia ktk mstari wa "4" sura ya 20 ya Kitabu cha Kutoka na mstari wa "8" sura ya 5 ya Kitabu cha Kumbukumbu la torati, Mwenyezi MUNGU amekataza kila kitu kihusucho Sanamu na picha ,lkn ili kujua ni kwanini MUNGU aliagiza hivyo au dhamira yake nini, na kwamba lengo lake si kuzuia Sanamu km Sanamu bali Ibada kwa Sanamu, hebu sasa tusome taratibu na kwa tafakari ya kina mistari inayofuata.Kutoka 20:4-6 na Kumb. 5:8-10.
Kutoka 20:4-6.
4 Usijifanyie Sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu Mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
5 Usivisujudie wala kuvitumikia. Kwa kuwa mimi Bwana Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu :nawapatiliza wana maovu ya Baba zao,hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
6 Nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri Zangu.
Kumbukumbu la torati 5:8-10.
8 Usijifanyie Sanamu ya kuchonga, mfano wa kitu chochote kilicho juu Mbinguni, au kilicho chini duniani, au kilicho majini chini ya nchi.
9 Usivisujudie wala kuvitumikia.Kwa kuwa mimi Bwana Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, nawapatiliza wana uovu wa baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
10 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao na kuzishika amri Zangu.
Kumbe hoja ya msingi hapa ni "USIVISUJUDIE WALA KUVITUMIKIA".na Mwenyezi MUNGU ametoa sababu ya Kwanini "TUSIVISUJUDIE WALA KUVITUMIKIA ".Nayo ni kwamba -yeye ni MUNGU mwenye wivu. Kumbe anachokataza MUNGU ni kuchonga Sanamu na kisha Sanamu hizo kuanza kuabudiwa kanakwamba ni MUNGU Mwenyewe, na MUNGU anatoa katazo hilo kwasababu Waisraeli waliyafanya hayo,walichonga Sanamu na wakaziabudu. Kujua kwamba MUNGU alizuia tu Kuabudu Sanamu na si kuzitengeneza hebu tuone jinsi MUNGU Mwenyewe alivyoamuru mara kadhaa Sanamu kutengenezwa na kuwekwa Hekaluni .
B:BIBLIA TAKATIFU, INAFUNDISHA
KUWA MUNGU ALIRUHUSU SAN
AMU KUTENGENEZWA.
1.Mungu alimwamuru Musa kutengeneza Sanamu za Makerubi na kisha kuwekwa Hekaluni -Kut. 25:18-19.
18 Nawe fanya makerubi mawili ya dhahabu :uyafanye ya kazi ya kufua, katika hiyo miisho ya kiti cha rehema, huku na huku.
19 Weka kerubi Moja mwisho Mmoja, na kerubi la pili mwisho wa pili. Fanya hayo makerubi ya kitu kimoja na kiti cha rehema, mwisho huku na mwisho huku.
Mambo hayo !!!, MUNGU anamwamuru Musa kutengeneza Sanamu za makerubi, makerubi wawili hao hukaa juu ya sanduku atokeapo Bwana. Kwa hiyo Bwana amesema ktk Biblia yeye hukaa juu ya Makerubi, rejea 1Sam.4:4, 2Sam.6:2 , 2Fal.19:15 ,Zab.80:1.
Katika Kitabu hicho cha Kutoka 26:1:Mwenyezi MUNGU anaendelea kutilia msisitizo juu ya kuwekwa kwa Sanamu za makerubi ktk Hekalu .
2.MUNGU alimwamuru Musa kutengeza Sanamu ya nyoka wa Shaba -Hesabu 21:8.
8 Bwana akamwambia Musa, jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi ".
Ona sasa !, MUNGU anamimina uponyaji wake ndani ya Sanamu ya nyoka wa Shaba, kwamba mtu akiumwa na nyoka, aitazamapo Sanamu hiyo ataishi ,Hebu fikiri hapo, Kwanini asingesema kuwa labda watu wataje tu jina lake nao wataishi ? Au Musa awaguse tu nao wataishi ?. Mwinjili Yohane hueleza kuwa Sanamu hiyo ya nyoka wa Shaba ni mfano wa Kristo aliyeinuliwa msalabani. Kama vile Waisraeli walivyomtazama nyoka wa Shaba walipona, vivyo hivyo kila Mmoja anayemtazama Kristo msalabani kwa kusadiki (Jicho la IMANI) ana Uzima wa milele. rejea Yohane 3:14-15.
14 Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa,
15 Ili kila aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye.
3.Katika Kitabu cha Wafalme, Mfalme Sulemani alijenga Hekalu na Kisha kulipamba Hekalu hilo kwa Vito vya Dhahabu na SANAMU.rejea 1Wafalme 6:23-28.
23 Akafanya ndani ya chumba cha ndani makerubi mawili ya mzeituni, kwenda juu mikono Kumi.
24 Na bawa Moja la kerubi lilikuwa mikono mitano urefu wake, na bawa la pili la kerubi mikono mitano ,mikono Kumi toka mwisho wa bawa Moja hata mwisho wa bawa la pili.
25 Na kerubi la pili lilikuwa mikono Kumi :makerubi yote mawili yalikuwa ya cheo kimoja na namna Moja.
26 Kwenda juu Kwake kerubi Moja kulikuwa mikono Kumi, na kerubi la pili vivyo.
27 Akayaweka hayo makerubi katika nyumba ya ndani, na mabawa ya makerubi yakanyoshwa, bawa la moja likafika ukutani huko, na bawa la kerubi la pili likafika ukutani huko :mabawa yao yakagusana katikati ya Nyumba.
Akayafunika makerubi kwa dhahabu.
Mfalme Sulemani, hakuishia kuweka Sanamu za makerubi tu, kama tulivyoona hapo, bali aliweka hata SANAMU za Wanyama km vile Ng'ombe na Simba, rejea 1Wafalme 7:23-26,27-29.Aidha Mfalme Sulemani alilipamba Hekalu hili kwa Michoro rejea 1Wafalme 7:36.
Baada ya Ujenzi wa Hekalu kukamilika, Mwenyezi MUNGU alimtokea Mfalme Sulemani na kumwambia kuwa Nyumba hiyo, yaani Hekalu, ameitakasa na tena Macho yake MUNGU na Moyo wake utakuwapo hapo siku zote. rejea 1Wafalme 9:1-3.
1 Ikawa Sulemani alipokwisha kuijenga nyumba ya Bwana, na nyumba ya Mfalme, na mambo yote yaliyoingia moyoni mwake Sulemani, naye akataka kuyafanya,
2 basi, Bwana akamtokea Sulemani mara ya pili kama alivyomtokea huko Gibeoni.
3 Bwana akamwambia, Nimeyasikia maombi yako na dua zako, ulizotoa mbele Zangu. Nimeitakasa nyumba hii uliyoijenga ili niweke jina langu humo milele, tena macho yangu na Moyo Wangu utakuwapo hapo siku zote.
Ona sasa !!!, MUNGU anavyolitakasa na kulikubali Hekalu lililokuwa limejengwa na Mfalme Sulemani, Kama Kweli SANAMU zingekuwa ni Chukizo kwa Mungu hapo MUNGU si angelimkaripia Sulemani ??. Lkn MUNGU hakufanya hivyo kwasababu Mfalme Sulemani hakuweka Sanamu hizo kwa nia ya Kuziabudu km ambavyo Kanisa Katoliki linafanya kwa kuweka Sanamu si kwa lengo la Kuziabudu.
4.Wafilisti walipo lichukua Sanduku la Agano la Kale kwa nguvu Kutoka kwa Waisraeli na kisha kuadhibiwa na MUNGU ,Walipotaka kulirudisha waliwauliza Makuhani na Waaguzi, wafanye nini watakapokuwa wanalirudisha Sanduku hilo ili kujipatanisha na MUNGU, waliambiwa kuwa -Watoe sadaka ya kuteketezwa ya ng'ombe wawili na SANAMU TANO ZA DHAHABU ZA MAJIPU na TANO Za PANYA -Rejea 1Samweli 6:1-15.(Kutokana na urefu wa somo Naomba ujisomee Mwenyewe, maana sio vizuri kukutafunia kila kitu).
5.Katika Agano jipya, Sanamu za Viongozi wa Serikali ziliwekwa katika Fedha na kisha kutumika katika Mzunguko wa Kiuchumi. rejea Marko 12:13-17.
13 Wakatumwa Kwake baadhi ya Mafarisayo na Maherodi, ili wamnase kwa maneno.
14 Hata walipofika walimwambia, Mwalimu twajua ya kuwa wewe u mtu mkweli, wala hujali cheo cha mtu ,kwa maana hutazami sura za watu, lakini katika Kweli waifundisha njia ya Mungu. Je, ni halali kumpa kaisari kodi au siyo ?
15 Tumpe, tusimpe ? Naye, kujua unafiki wao, Akawaambia, mbona mmenijaribu ? Nileteeni dinari niione.
16 Wakaileta Akawaambia, ni ya nani Sanamu hii na anwani hii ? Wakamwambia ni ya Kaisari.
17 Yesu akajibu, Akawaambia, mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na yaliyo ya Mungu mpeni Mungu. Wakamstaajabia sana.
Mafarisayo na Maherodia wanapomjaribu Yesu juu ya kulipa kodi kwa Kaisari swali lao linajibiwa kwa kutumia sarafu yenye SANAMU ya mtawala Yaani Kaisari, Jibu la Yesu linakuwa "Mpeni Kaisari yaliyo yake Kaisari, na Mpeni MUNGU yaliyo ya MUNGU ".Fikiri hapo !, Mbona Yesu hasemi msitumie hii Dinari kwasababu ina Sanamu ya Kaisari maana kadiri ya Kumb.5:8 na Kut. 20:4,ni kosa. Lkn Yesu hawakatazi kwasababu anajua kuwa Mungu hachukii Sanamu km Sanamu, bali anachukia Ibada ya Sanamu.
C:HITIMISHO .
Wapendwa sana wanajukwaa,Bado nina mengi ya kuwaeleza Kuhusu Sanamu, lkn nahisi nitawachosha sana lkn naamini nimetoa mwanga angalau kidogo tu. Tukumbuke kuwa hata sisi Wanadamu tuliumbwa kwa Sura na mfano wa MUNGU -rejea Mwanzo 1:26 ,hivyo hata sisi ni Sanamu, maana kitu chochote kilichoumbwa au kutengezwa kwa mfano wa kitu kingine ni Sanamu. Naendelea kukazia kuwa Wakatoliki HATUABUDU SANAMU, Sanamu hutumika tu Kanisani kwaajili ya kumrahisishia muumini kuelewa IMANI yake, sawa na wewe Unapotaka Kumuelezea Mwanao juu ya Namna Babu yake aliyefariki miaka mingi kabla ya yeye kuzaliwa kwa kutumia Picha. Hata katika Elimu Walimu huwa wanatumia mbinu mbalimbali kuhakikisha kwamba Wanafunzi wanaelewa somo lake, wapo wanatumia Picha, Michoro, Sanamu na kufanya ziara za Kimasomo. Tulipokuwa Sekondari ktk Maabara ya Biolojia kulikuwa na Sanamu kubwa ya SKELETON ya binadamu iliyotumika kujifunzia na Wanafunzi wa Dini zote tuliitumia kujifunzia lkn sikuwahi kusikia mtu yeyote akikataa au kulalamika kuwa mbona Sanamu zimekatazwa.Hivyo Kanisa Katoliki haliabudu Sanamu, Tunayemwabudu ni MUNGU Mmoja, ktk Nafsi tatu Yaani MUNGU Baba, MUNGU Mwana na MUNGU Roho Mtakatifu.
Karibuni sana, kwa maswali, dukuduku, n. K. Matusi mwiko.
C. C. Edwayne