Ukweli kuhusu Wakatoliki kutokuabudu sanamu zilizopo makanisani

Ukweli kuhusu Wakatoliki kutokuabudu sanamu zilizopo makanisani

Usidhani kanisa katoliki ni mapadre tu na maaskofu na masista.

Kanisa ni pamoja na wewe yaani kila aliyebatizwa na hivyo kila mmoja ana duty ya kulilinda kanisa.

Hivyo mjibu huyo muhubiri usisubiri askofu au padre.

Nimekuwa namsikiliza mhubiri mmoja nadhani ni msabato. Kila mara anarejea juu ya makanisa, anayosema ni waabudu Sanamu na wanaosali jumapili (akiita siku ya jua) badala ya sabato. Nadhani ni wakati muafaka wa kumjibu. Uongo ukirudiwa mara kwa mara wasikilizaji wanaweza kudhani ndiyo ukweli. Wajuzi wa mafundisho ya RC ni wakati sasa wa kujibu
 
Usidhani kanisa katoliki ni mapadre tu na maaskofu na masista.

Kanisa ni pamoja na wewe yaani kila aliyebatizwa na hivyo kila mmoja ana duty ya kulilinda kanisa.

Hivyo mjibu huyo muhubiri usisubiri askofu au padre.
Pamoja na ukweli huo, kuna waliozama kwenye hiyo taaluma wanaweza kujibu kitaaluma. Vinginevyo utababaisha halafu waonekane washindi. Kuna waliosomea biblia, kuna waliosomea elimu Mungu. Wewe unafikiri Kila mmoja anaweza? Mimi Nina taaluma yangu na ukiigusa nitaijibu bila kubabaisha.
 
Pamoja na ukweli huo, kuna waliozama kwenye hiyo taaluma wanaweza kujibu kitaaluma. Vinginevyo utababaisha halafu waonekane washindi. Kuna waliosomea biblia, kuna waliosomea elimu Mungu. Wewe unafikiri Kila mmoja anaweza? Mimi Nina taaluma yangu na ukiigusa nitaijibu bila kubabaisha.

Kila mkristo ana wajibu wa kujua biblia,kila mkristo ana wajibu wa kufahamu maandiko vinginevyo unaweza unadanganywa
 
Nimekuwa namsikiliza mhubiri mmoja nadhani ni msabato. Kila mara anarejea juu ya makanisa, anayosema ni waabudu Sanamu na wanaosali jumapili (akiita siku ya jua) badala ya sabato. Nadhani ni wakati muafaka wa kumjibu. Uongo ukirudiwa mara kwa mara wasikilizaji wanaweza kudhani ndiyo ukweli. Wajuzi wa mafundisho ya RC ni wakati sasa wa kujibu
Usipoteze muda kubishana na mjinga. Kiimani unatakiwa kumwombea.

Paulo aliyekuwa kiongozi mkuu wa kulihujumu Kanisa la Kristo alikuja kuwa mtume wa Kristo aliyefanya kazi kubwa sana. Hata huyo unayemsema, usishangae siku nyingine akasimama mbele yako akikuhubira mafundishobya kweli kuliko hayo ya upotofu anayoyatoa sasa.

Ila kama wewe unayumba kwa sababu ya kutolijua neno la Mungu, jibidishe kuyajua maandiko:

Kwa ufupi kabisa, rejea hapa:

1) kwa nini Kristo aliuawa?
JIBU: Kwa sababu ya kutotii sheria.

2) Sheria gani
JIBU: Sheria ya Musa, yaani kumbukumbu la torati.

3) Sheria gani ilikuwa kuu kuliko zote kwenye kumbukumbu la torati?
JIBU: Sheria ya sabato

Yesu kutozingatia mafundisho ya mafarisayo kuhusiana na sabato, ndiyo mwanzo wa chuki za mafarisayo na makuhani dhidi ya Kristo. Tena wakasema wazi kuwa, kama angekuwa mwana wa Mungu angeitii Sabato. Naye akawaambia wazi kuwa yeye ni mkuu kuliko sabato. Yeye ni bwana wa Sabato. Kwa nini uiabudu siku ya Sabato badala ya kumwabudu yeye aliye bwana wa Sabato?

Kwa hiyo Kristo aliuawa kwa kutoitii sheria. Kwa kutoitii sheria za kumbukumbu la torati, ambako sheria kuu ni utii wa sabato. Kwa sababu kutokutii sabato lisingekuwa kosa kubwa la kuhukumiwa kifo na Pilato kiongozi mwakilishi wa mfalme wa Roma, wakamtengenezea kesi ya kubumba ya uchochezi kuwa anawachochea watu wasilipe kodi kwa mfalme Kaizari wa Roma.

Paulo anasema wazi Kristo alihukumiwa kwa sababu ya kutoitii sheria, akayashinda mauti. Baada ya ushindi wa Kristo yaani kuyashinda mauti, sisi tulioshinda na kufufuka na Kristo, tukirudi kuitumikia sheria, basi kifo cha Kristo ni bure.

Mkristo hustahili kuiabudu sabato, au kuiabudu siku, mwabudu Bwana wa Sabato katika kweli na haki.
 
Sawa yeye ameongea hivyo na akaona yuko sahihi na mimi pia nataka nijue kutoka kwake,Hiyo Jumamosi anayosema ndio sabato kaitoa kwenye kalenda ipi?ya kirumi,ya waislam au wayahudi,kalenda kutoka mbinguni au(ambayo sidhani kama ipo),kalenda ya wamisri,wahindi n.k

Hizo ibada za sanamu katika ukatoliki ni zipi? maana nachojua sisi ibada yetu imekuwa ni misa ambayo hufanyika siku zote za wiki(Jumapili ikiwa ni siku ambayo waumini ufika kwa namba kubwa kanisani).Ibada hii ya misa imegawanyika sehemu kuu mbili:Liturijia ya neno na liturijia ya ekaristi(sasa hapa sanamu ni lipi linaloabudiwa?)
 
Kuna wakati, nilipokuwa nimemaliza masomo yangu ya kidato cha 6, ikiwa ni pamoja na masomo ya biblia, nilialikwa kwenye mkutano wa wasabato. Nilienda huko nikiwa sijui kuwa ningepewa nafasi ya kuongea.

Cha ajabu, nikawekwa kama mtu wa kujibu maswali waliyokuwa wakiyaelekeza kwa Kanisa Katoliki. Nilijibu, kwa kadiri Roho alivyoniongoza.

Wote wakawa kimya kabisa. Nilishangaa mwishowe kufuatwa na viongozi wao kuwa eti wananiomba nijiunge nao na kisha niwe mchungaji wa Kanisa lao. Nilishangaa sana, nikawauliza kuwa tangu mwanzo wamelituhumu Kanisa Katoliki kuwa limepotoka, inakuwaje tena mimi Mkatoliki naweza kuwa kiongozi wao? Hawakuwa na jibu.

Nilivyomaliza masomo yangu ya shahada ya pili, nilipofika Dar, nikaalikwa na jamaa mmoja, aliwahi kuwa mtu mkubwa kwenye ngazi ya kitaifa kwenye Serikali. Yeye ni muislam. Nikaitikia mwaliko, nikaenda. Kufika huko nikashangaa walikuwa wamejaa wasomi wa dini ya Kiislam. Pekee yangu nilitengewe kiti, huku wao wote wakiwa wameketi kwenye majamvi. Nikaanza kuulizwa mambo ya Ukristo. Sikuwa nimejipanga kwa hilo. Lakini kwa utulivu niliwajibu kadiri nilivyoweza, hata wakaishiwa swali lolote.

Nilitafakari sana kwa nini niliitwa mimi, lakini baadaye nilikuja kutambua kuwa kuna ndugu zangu, nao walikuwa wasomi wazuri kwenye elimu ya Dunia, lakini hawakuwa vizuri sana kwenye mafundisho ya kiimani. Na kuna watu walitaka kuwabadilisha wale ndugu zangu kwenda uislam, na ikaelezwa kwamba kikwazo ilikuwa mimi. Hivyo wakinibadilisha mimi, basi wale wengine watanifuata.

Nashukuru mpaka leo wote tupo katika imani yetu.

Na neno la mwisho nililowaambia wale wasomi wa dini ya Kiislam ni kwamba sisi katika Ukristo tunaamini sana katika neema. Na neema hiyo inaweza kumwangukia yeyote, na ukashangaa aliyekuwa imamu au hata mpagani, siku nyingine anaweza kuja kuwa mkristo, tena kukuzidi hata wewe uliyedhania unaujua zaidi ukristo, akawa mwalimu wako.

Kwa hiyo usighadhabike Kanisa likinenewa vibaya. Kristo pamoja na ukuu wote, na mamlaka yote, alidhalilishwa, alitukanwa, alipigwa, alivuliwa nguo, alitemewa mate, hakuhangaika na waliomtendea hayo. Alipofufuka neno lake la kwanza lilikuwa Shalom, yaani muwe na amani, nimekamilisha, msiwe na mashaka. Mkristo unatakiwa kuyaiga maisha ya Kristo. Hatushindani katika kumjua au kumwabudu Mungu. Hata anayetusi, ujue Mungu ameruhusu, asipotaka, hawezi hata kuupanua mdomo wake.
 
Mimi ni mlutheran , lakini watu kupingana na taasisi ya ukatoliki yenye zaidi ya miaka 2000+ ni ujinga kwa haya madhehebu ambayo hayana hata 300 years.. ni sawasawa na kujilisha upepo halafu sijawahi bahatika kusikia kiongozi wa katolik anatoka hewani na kuanza kujibishana na Hawa wenye dini zao. Hata ibada za katolik ni nadra sana kukuta wanapondea dini za wengine.
 
Hawa hata msalaba hawautaki,sasa tunawasaihdiaje??

Mtu anayeuliza swali anatakiwa awe tayari kujibiwa.
 
Mimi ni mlutheran , lakini watu kupingana na taasisi ya ukatoliki yenye zaidi ya miaka 2000+ ni ujinga kwa haya madhehebu ambayo hayana hata 300 years.. ni sawasawa na kujilisha upepo halafu sijawahi bahatika kusikia kiongozi wa katolik anatoka hewani na kuanza kujibishana na Hawa wenye dini zao. Hata ibada za katolik ni nadra sana kukuta wanapondea dini za wengine.
Roman catholic mind your own business
 
Dini ni utapeli,
The Catholic Church played a vital role in the trans-Atlantic slave trade, according to historians and several published thesiis on the topic.

The trans-Atlantic slave trade was introduced by the coming of the Europeans who came with the Bible in the same manner that Arab raiders and traders from the Middle East and North Africa introduced Islam through the Trans-Saharan slave trade, according to AfricaW.com, a premiere informational website available throughout the continent.

“In fact, the Church was the backbone of the slave trade,” the authors wrote. “In other words, most of the slave traders and slave ship captains were very ‘good’ Christians.”

For example, Sir John Hawkins, the first slave-ship captain to bring African slaves to the Americas, was a religious man who insisted that his crew “serve God daily” and “love one another.” His ship, ironically called “The Good Ship Jesus,” left the shores of his native England for Africa in October 1562. Some historians argue that if churches had used their power, the Atlantic slave trade might have never occurred.
 
Kwanza ungeuliza kwa nini kwenye mkutano au mahakama unaonyesha heshima kwa kuinama kama wakatoliki,
Pili jiulize kwa nini kila nembo ya hospitali ina sanamu ya nyoka
Screenshot_20230409-134303.jpg
 
Back
Top Bottom