Mimi ni Roman Catholic
Sijawahi kuabudu sanamu hata siku moja. Kanisani naziona sanam kama zinatoa lugha ya picha kwa waumini.
Mfano sikujua kusulubiwa kunakuwaje mpaka nilipoiona sanamu ikinionyesha namna mtu anayesulubiwa msalabani anavyo kaa msalabani.
Bwana Yesu Kristo alifundisha mahali na kusema
" Ufalme wa mbingu upo mioyoni mwenu "
Hivyo maamuzi yako ndiyo yanayo zingatiwa kuhusu nini unaabudu.
Unaweza ukaingia kanisani iliyojaa sanamu lakini wewe moyo na akili zako ukaziongoza katika kumwabudu Mungu.
Unaweza kuingia kanisa ambalo halina sanamu hata moja na ukaabudu miungu mingine
kama kwa wanaume kuelekeza akili zao kwa wanawake warembo walioko kanisani badala ya kumwomba Mungu.
Watu wa siku hizi wanaabudu miungu mingi tu bila kujijua.
Wengine wanaabudu simu, kila wakati wana chati au kuangalia video, hawana muda wa kuenda kanisani wala kusali.
Wengine wanaabudu wanamuziki au wacheza mpira nk. mpaka wamechora tatuu zao mwilini
Mimi hata kwa bahati mbaya nikiingia kanisa la shetani nitamwabudu Mungu rohoni na sala zangu zitamfikia, na shetani hatanigusa mpaka natoka.
Je wewe moyoni unamwabudu nani ?
Ukimjua na kumwabudu Mungu kwa dhati hakuna cha sanamu wala shetani watakao kubabaisha.
Tuonane baadae