Ukweli kuhusu Wakatoliki kutokuabudu sanamu zilizopo makanisani

Ukweli kuhusu Wakatoliki kutokuabudu sanamu zilizopo makanisani

NI KWELI WAKATOLIKI WANAABUDU SANAMU ?


Utangulizi
Kati ya dhambi ambazo kwa wakatoliki ndiyo wazi kwa watu ni dhambi ya kuabudu sanamu. Dhambi hii imewafanya wakatoliki waonekane au hawasomi Biblia au wanasoma ila hawaelewi au wanasoma na kuelewa lakini wamekuwa wakipuuza maandiko Matakatifu. Ubayana wa dhambi hii kwa wakatoliki ni kile wanachokifanya siku ya Ijumaa Kuu na mambo yanayoonekana katika nyumba za kuabudia kama makanisa ambapo sanamu lukuki zinaonekana, toka zile za vitu vya duniani hadi vile za mbinguni.

Tuhuma kwa wakatoliki haitoki hewani, bali ni kutokana na mambo hayo kwenda kinyume na baadhi ya aya katika maandiko matakatifu. Law. 19:4; 1Yoh. 5:21; Zab.115:1 9)
Kifupi ni wazi kabisa kuwa kuziabudu sanamu ni kosa; na hata katika baadhi ya nukuu kuzichonga pia imeoneshwa kuwa ni kosa. (Kumb. 20:3 5 na Kumb. 5:7 10). Sisi wakatoliki tonazo sehemu nyingi tu tulikoweka hizo sanamu ndiyo maana tunatuhumiwa kuwa kinyume cha Maandiko Matakatifu.

Kwa nini wakatoliki wamechonga sanamu ingawa imekatazwa (Kumb. 20:3 5 na Kumb. 5:7 10)?
Wakatoliki wameangalia roho ya katazo la kuchonga sanamu na si katazo lenyewe tu. Roho ya katazo la kutochonga sanamu haikuwa Mungu kuamua kuzichukia tu sanamu, la hasha! Bali Mungu aliwakataza waisrael wasichonge sanamu za vitu wala vya duniani wala vya mbinguni kwa sababu alijua kuwa waisrael ambao wakati ule walizungukwa na makabila ya kipagani ambayo yalikuwa na kawaida ya kuabudu sanamu. Ili kuwaepusha Waisraeli, ambao imani yao kwa Mungu mmoja ilikuwa bado kukomaa, aliwakataza wasichonge. Kwa hiyo roho ya katazo hilo lilikuwa ni hatari ya kuanza kuziabudu kama walivyokuwa wanafanya wenzao wapagani.

Tunasema hivyo kwa sababu Mungu huyo huyo aliyewakataza Waisraeli kuchonga sanamu katika Kumb. 20:3 5, mbele kidogo anamwagiza Musa huyo huyo kuchonga sanamu ya makerubi katika sanduku la Agano (makerubi ni vitu vya mbinguni) ( Kumb. 25:18 20, Ebr. 9:5). Hapa Mungu ameonekana kutengua kile ambacho alisema pale mwanzoni kuwa wasichonge sanamu yoyote. Utenguzi huo si wakimaana; si wa kiroho ya sheria, bali ni wa kidhana ya katazo. Maana yake, Mungu anamruhusu Musa kuchonga sasa sanamu akijua kwamba Waisrael sasa wamekomaa kiimani kiasi kwamba hata wakichonga sanamu hawataweza kuiabuni ikichukua nafasi ya Mungu. Kwa hiyo roho ya katazo ilikuwa ni kutoabudu sanamu.

Kama haitoshi, ukienda mbele kidogo ya kitabu hicho cha Kumbukumbu la Torati Mungua anafanya mchezo wa hatari zaidi wa kumwambia Musa achonge nyoka wa shaba (kitu cha duniani) na kumweka kwenye mti na kila amtazamaye angepona. (Hes. 21: 8-9, Yoh. 3:14 15). Musa alitekeleza agizo hilo naye Mungu alimuhesabu kama mtiifu kwake. Hata hapa pia Mungu ameona kuwa waisraeli sasa imani yao kwa Mungu mmoja ni thabiti kiasi kwamba hata kama wakiona sanamu wasingeweza kuziabudu wakamsahamu Mungu wao. Si kwamba Mungu ana chuki na sanamu, hata kidogo. Kama Mungu angekuwa na chuki na sanamu tusingeweza kuziona nukuu zifuatazo: Kut. 29:37, 1Fal. 7:29, Hek. 16:7.
Kifupi, imani ya mwanadamu hukua kama vile akili ya mtu inavyokua kutoka utoto, ujana hadi utu uzima. Mwanzoni kabisa waisraeli walikuwa kama watoto kiimani. Kumbuka Abrahamu alitoka kwenye nchi ya kipagani baadaye taratibu Mungu anamtoa kutoka katika utamaduni huo wa kuabudu miungu hadi kwenye kumwabudu Mungu mmoja. Kilele cha kumwabudu Mungu mmoja kinafikia pale mlimani sinai wanapopewa sheria. Kukua taratibu huko kwa imani ya waisrael ndiyo sababu inayofanya kuwepo tofauti ya nukuu za Mungu kukataza au kuruhusu kutengeneza sanamu. Hii ni sawa na mtoto anayekatazwa kushika kisu na mama yake lakini anapofikia umri wa kupevuka anaruhusiwa kushika kisu. Sisi wakatoliki siyo watoto wadogo kiimani hata tuogope kuchonga sanamu tusijeziabudu. Tunazichonga tukijua kwamba hata siku moja hazitaweza kutudhuru kwa sisi kuanza kuziabudu. Wale wote wanaogopa kuzichonga sanamu, wajue kuwa wao ni wachanga kiimani.

Kama Mungu hakatazi kuchonga sanamu ila anakataza kuzifanyia ibada, je, sisi wakatoliki hatufanyi hivyo?
Kujibu swali hilo, ndiyo nitakuwa nimegusa kiini cha swali lack Sr. Gracia. Nakuomba fuatilia maelezo yangu, huu ulikuwa kama utangulazi tu.

KUABUDT MSALABA
Kama wakristo, hatuna budi kujisifu kwa vile tumekomboleva kwa fjia ya msalaba ambapo Bwana wetu Yesu Kristo alatundikwa na `kafa juu yake. Lengo la Yesu ni kutuletea wokovt. Mimi na wewe tulistahili kupata adhabu hii ambayo yeye ameipata badala yetu. Kwetu msalaba ni ukombozi, msalaba ni sehemu ya maisha yetu na msalaba ni haki yetu. Hivyo msalaba ni lazima uheshimiwe na si kuabudiwa. Anayepaswa kuabudiwa ni Mungu peke yake. Zipo heshima za viwango tofauti:
Mungu kwanza (latria) tunamwabudu.
Bikira Maria (Hyperdulia)
Watakatifu wengine na vitu wanavyohusika navyo (dulia)
Picha na sanamu pia hupewa heshima isiyoizidi ile ya watakatifu na Bikira Maria.
Hayo ndiyo madaraja ya heshima ambayo tunazitoa, 2 hadi 4 ni heshima tu.

Mpendwa Sr.Gracia,sijafikia ufundi wa kufafanua yote unayopenda kuyajua ila nataka nijaribu kadiri nitakavyoweza japo kwa kifupi kiha upitie.Yaliyo ya kizushi yafumbie macho na usiniseme nikatengwa na Kanisa. Nianze kwa kueleza maana ya neno sanamu kisha nitaendelea:

Sanamu
Ni kitu kilichochongwa au kutengenezwa kikiwakilisha kitu halisi,mtu,mnyama,mchoro au chochote kile kilicho halisi.Kwa hiyo ili kukiita sanamu,hicho ambacho kimetengenezwa,lazima kikiwakilishe kitu halisi,ndiyo maana ukitembelea sehemu za makumbusho utakuta sanamu za maraisi,nenda Butiama utaikuta sanamu ya Baba wa Taifa letu au kule Zanzibar utakuta sanamu ya mzee Karume n.k.Pamoja na hayo,kitu sanamu,kinaweza kikachukua mtindo wa picha.Mtu aliye na photo albam zile zote zilizomo iwe ni sura za watu,wanyama,miti au vitabu ni sanamu za hao au hicho kilichowakilishwa kwa njia ya hizo picha.Mtu akiandika kitabu cha historia kwa mfano,alichoandika si historia yenyewe kwa kuwa historia huwezi ukaiandika bali ataandika kiwakilishi cha historia ambacho amekiweka katika maandishi.Maandishi hayo{zile herufi} ni sanamu. Kwa maneno mengine,ukiwa huko shuleni unafundisha,herufi zote zilizomo kichwani mwako,ukiziandika tu ubaoni tayari elewa kuwa unaandika sanamu na wote watakayoyasoma hayo maandishi,wanasoma sanamu.Kwa kifupi,sanamu ya kila kitu inaanzia kichwani au akilini mwa mtu,anapoichonga au kuiandika au kuichora basi anaiumba kadili aijuavyo.Kitu halisi kinakuwepo lakini mwandishi au mchongaji amekiwakilisha kwa mtindo wake.

KUABUDU
Hiki daima ni kitendo cha kumtukuza mtu, kitu au chochote ambacho si mungu [herufi ndogo} kama vile unavyomtukuza Mungu {herufi kubwa}mwenyewe.Lazima kila mmoja atambue kuwa anayestahili kutukuzwa ni Mungu tu kama tunavyosoma katika Biblia Takatifu rej.Mdo 17:28 KWA KUWA NDIYE ANATUWEZESHA KWENDA NA KUFANYA CHOCHOTE, au rej Kumb 4:15/28,15:42ff sehemu ambazo Mungu ametukataza kuabudu kitu kingine chochote tofauti na yeye.

Je, tunapotuhumiwa kuwa tunaabudu sanamu wanatusingizia?Sanamu hutusaidiaje?
Lengo la kutumia sanamu ni pamoja na kutukumbusha kitu kilichokuwepo kwani ukufuatilia maelezo yangu juu ya neno sanamu utagundua kuwa huwezi kuitengeneza ya mtu ambaye bado hujamwona.Kwa hiyo zinatumika kama nyenzo ya kutukumbusha yaliyotokea zamani za kale. Ndivyo kwa mfano matumizi ya picha yaliyopoUkienda Nairobi kwenye malezi na huko ukaamua kupiga picha ukiwa katika barabara nzuri utaitunza kama ukumbusho wako na hiyo itakufanya ulikumbuke kwa urahisi tukio hilo kuliko kama ukisimulia tu.
Kuhusu suala la kuabudu ili mtu aambiwe kuwa ameabudu lazima awe ametimiza mambo makuu mawili yaani:
Kuwa na nia kamili ya kuabudu ile sanamu ikichukua nafasi ya Mungu
Kufanya ibaada ya dhati ya kuiabudu hiyo/hizo sanamu.
Kuna mambo kama tisa hivi ambayo mmoja anaweza kuyafanya akiwa katika ibada ya sanamu. Mambo hayo yametajwa katika Biblia Takatifu.
Utoe sadaka Hos 4:13
Uitolee sanamu yako ubani 1 Fal 11:8
Ufanye tambiko mbele ya sanamu yako Isa 57:6
Uitolee zaka Hes 2:8
Uweke sanamu yako juu ya meza au tuseme iwepo meza Isa 65:11
Usujudie sanamu yako 1Fal 19:18
Uiinulie mikono sanamu yako Isa 44:20
Uichezee ngoma sanamu yako 1Fal 18:26
Ulale kifudifudi na kuipigia makofi sanamu yako (1Fal. 18:26).

Nini wafanyacho wakatoliki?
Kwanza, wakatoliki hawaamini juu ya miungu mingi kama walivyofanya watu wa kale.Hakuna mkatoliki anayedai kuwa Maria na Watakatifu ni miungu wala hawasemi kuwa msalaba una nguvu kuliko Mungu.Haya ni mashtaka ya watu wasiojua nini wakatoliki wanakifanya.Wayahudi kwa asili waliabudu miungu mingi hadi pale Mungu alipojifunua kwao na kuwataka waache kuiabudu miungu isiyo ya kweli.Pamoja na hayo katika safari yao ya maisha hawakuonesha kutii agizo la Mungu na matokeo yake waliweza kuiabudu hata miungu ya uongo.

Pili, Wakatoliki wanatambua kuwa Mungu ajua yote na hafungwi na muda.Kwa hekima kubwa aliyonayo,hawezi kuikasirikia sanamu ambayo inaheshimiwa tu kama ukumbusho wala haichukui nafasi yake.Mungu alikuwa akiwaadhibu vikali Wayahudi kwa kuwa kila walipohisi kuwa amewaacha,waliacha kumwamini wala kumwabudu yeye bali wakajitengenezea sanamu za kuchonga na hizo wakasemezana na kukubaliana kuwa ndo Mungu mwenyewe.Mungu alichukia na kuwaadhibu kwa vile waliziabudu na zikachukua hadhi kama ya Mungu wa kweli.

Tatu, Mungu kwa kutambua kuwa si kila sanamu imetengenezwa ili ichukue nafasi yake,aliweza kumruhusu hata Musa kutengeneza sanamu kwa lengo maalumSehemu ambazo Mungu karuhusu sanamu ni nyingi sana katika Biblia rej. Hes 21:8f,Ebr 9:5, Yn 3:14f,Kut 16:31,2 Nyak 3:10, 4:4, Eze 41: 17 ff,n.k Kwanini anaruhusu?Kwa kuwa hazina madhara,zimetengenezwa kwa lengo lisilo la kuziabudu.

Je, tuseme nini juu ya kile tufanyacho Ijumaa Kuu?
Kitu cha msingi ni kusikiliza maneno ya Padre au shemasi anapowaalika watu kuja kuanza kuabudu.Padre au shemasi husema,
Huu ndio mti wa msalaba, ambao wokovu wa dunia
umetundikwa juu yake, njooni tuuabudu.
Ukifuatilia kwa makini kiswahili sanifu na bahati njema wewe mwalimu japo sijui wa somo lipi, utagundua kuwa, Padre hufanya mambo haya yafuatayo katika mwaliko huo:
Hutuonesha mti wa msalaba.
Hutuambia kuwa juu ya mti huo,wokovu umetundikwa
Kisha hutualika tukauabudu.

Ningekuwa naongea nawe,ningekuuliza hivi hutualika tukauabudu mti wa msalaba au wokovu ambao umetundikwa juu ya huo mti au tukauabudu mti na msalaba au tukauabudu nini? Hebu fikiri kisha uone kama mawazo yako ni sawa na nitakachokisema hapa chini kabla hujaangalizia!

Wakatoliki hualikwa kufanya nini?
Kwa mwaliko huo,wakatoliki hualikwa kwenda kuuabudu WOKOVU ulio juu ya msalaba.WOKOVU NI NINI? WOKOVU ni jina lililoandikwa kwa kiswahili.Jina wokovu kibiblia na kwa lugha asili ya Biblia ni sawa na jina YESHUA kwa kiebrania au YOSHUA. Mwanangu,wewe unamfahamu Yoshua katika Biblia kuwa alichukua jukumu la kuwaingiza Waisrael katika nchi ya ahadi baada ya Musa kufa kwani huyu ndiye aliyekuwa msaidizi wa Musa.Yoshua aliwachukua watu hawa wakiwa ng`ambo ya mto Yordan wakisubilia tu kuiingia nchi ya ahadi.Kumbe kwa Waisrael Yoshua ni mtu wa muhimu sana kwao kwani baada ya Musa kuwatoka,wanamtumainia Yoshua na kumwona kuwa ni Mwokozi wao kwa kitendo cha kuwafikisha salama katika nchi ya ahadi ambayo kwa miaka karibu 40 wamesafiri kuifikia.Tendo la Yoshua la kuyapiga maji ya mto yakagawanyika na kuacha nchi kavu nao wakavuka bila shida,ndilo wanaloliona kuwa la kuwaletea ukombozi kama alivyofanya Musa pale alipoyapiga maji ya bahari ya Sham yakaacha njia wakapita kwa usalama kutoka Misri.

Kristo ndiyo WOKOVU wetu tunayepaswa kumwabudu kwani alipokuja aliamua kuanzia kazi yake ya kutuletea wokovu katika mto Yordan pale ambapo Yoshua kahitimishia kazi yake.Yoshua aliwavusha watu toka ng`ambo ya mto kuwaingiza katika nchi ya ahadi ambayo ni Kanaan ya duniani na Yesu anapokuja,kama mwokozi,anataka awatoe watu wake kutoka katika nchi ya ahadi ya kidunia,kuwapeleka katika nchi ya ahadi ya mbinguni.Kumbe Yesu ni mwokozi wetu anayetutoa kutoka katika dunia kwenda mbinguni wakati Yoshua anaitwa mwokozi kwa kuwa aliwatoa Misri akawaleta Kanaan nchi ya ahadi.Yesu na Yoshua kwa mantiki hii ni hilo jina WOKOVU kama nomino wakati kazi waliyotenda ni ya kutuokoa na kikitamkwa kama kitendo,Yesu au Yoshua,anaitwa Mwokozi.

Labda nikupeleke kidogo darasani juu ya mambo ya viambishi katika lugha ya kiswahili kwani hapa ndipo wengi wanaposhindwa kueleza kile tunachokiabudu ile Ijumaa Kuu.
Padre au Shemasi husema ,
Huu ndiyo MTI wa msalaba ambao WOKOVU wa dunia Umetundikwa juu yake, njooni tuUabudu.
Katika sarufi ya kiswali hasa tunaposema juu ya upatanisho wa kisarufi, bahati mbaya ni kwamba nomino MTI na nomino WOKOVU zote zimechukua viambishi ngeli U, ili kuwa na upatanisho wa kisarufi. Tunasema kwa mfano, mti umaanguka, wokovu umetujia. Katika sentensi hiyo anayotamka padre au shemasi, ina maneno yote mawili, yaani mti na wokovu yenye kiambishi kimoja tu U kinachotuletea shida kuwa kimaresha nini, wokovu au mti. Kiambishi U, hakirejerei mti bali kinarejea wokovu yaani Yesu.
Kwa hiyo tunaposema njooni tuuabudu, hatumaanishi tuuabudu mti la hasha! Bali tuuabudu Wokovu uliotundikwa juu ya mti wa msalaba katika akili zetu. Ndiyo kusema, ibada hii kama mtu hawezi kutoka nje ya pale na kupeleka mawazo yake kwa Yesu, aliye Wokovu wetu , bila shaka anaweza kuwa anaabudu sanamu au mti wa msalaba.

Mpendwa sista, Kristo Bwana wetu ndiye sanamu ya kwanza kabisa ya Mungu. Ndiyo maana Kristo anasema aliyemwona Yesu kamwona Baba Yn 14:8f. Kama Yesu ni sanamu,hata binadamu ni sanamu za Mungu kwa vile tumeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu.Kama mtu anaziogopa sanamu,ashakumu si matusi,aogope hata kuzaa watoto kwa vile kuzaa mtoto ni kuongeza sanamu duniani kwa kuwa licha ya kufanana na Mungu,zinafanana na mzazi mwenyewe.Kama hatuziabudu,yanini kuziogopa? Kama maandishi ni sanamu lakini hatuyaabudu,kwa nini uogope kusoma herufi? Mungu si mjinga wa kutuhukumu kwa mambo kama hayo yasiyochukua sifa yake.

Pamoja na hayo,tukumbuke kuwa sanamu huanzia kichwani mwa mtu kama nilivyokwishasema.Kama mtu akibuni kichwani kutengeneza gari nzuri sana,hatuwezi kumzuia kwa sababu atakapotengeneza kile alichonacho kichwani kikawa gari,hatakiabudu.La sivyo,hata kupanda gari ili kusafiri tuache kwani tunapanda
Ndani ya sanamu walizotengeneza watu.Ukiwa na picha zako,kwa jinsi zilivyotoka vizuri,ukafurahi na kuzibusu,haina maana kuwa unaziabudu.Au,kwa vile sasa unajua kuwa mtu ni sanamu ya Mungu,je ukienda mahali ukamsalimu mkubwa wako au anayekulea wakati unampa kitu ukampatia huku ukipiga goti, utakuwa unamwabudu?

Hatimaye, Kanisa katika sheria yake no.1159 linafundisha kuwa,sanamu ya Mungu haipo kwani tangu mwanzo Mungu baba hajawahi kuonwa na mtu isipokuwa kupitia kwa mwanae ambaye watu walimwona na waliishi naye wakamfahamu na kumbe kuchonga sanamu ya kufanana naye Isingeliwezekana.Sanamu za Yesu zafanana naye kwa vile watu walimfahamu alivyofanana lakini zimeletwa kwetu kama ukumbusho wa jinsi alivyokuwa si kwa lengo la kuziabudu. Kwa kuziona,hatuna mashaka kuwa alikuwepo kuliko kama tungekuta masimlizi tu.Hivyo hivyo kizazi kijacho kikiambiwa juu ya Nyerere kitaelewa zaidi kikioneshwa picha na sanamu zake lakini hizo picha na sanamu zake hawatasema ndo Nyerere mwenyewe labda kama ni vichaa.

HITIMISHO.
Mungu si mjinga wa kukasirikia kitu kisicho na madhara. Aliwaadhibu wote waliochonga sanamu na kusema hizo zafanana na Mungu lakini sisi hatusemi zinafanana naye bali tunajua kuwa yeye yupo na hizo zipo kama ukumbusho wa sura ya Yesu mwanae ambaye tunamfahamu kupitia waliomwona wakazitengeza. Akili zetu zinapata kutufanya tumtambue Kristo tunapoziona sanamu lakini kwa zenyewe si Kristo wala Mungu wetu
Ukiona sanamu ya B.Maria au Mtakatifu Fulani, ni uthibitisho kuwa, wapo watu waliomwona wakamchonga alivyo na sanamu yake inatukumbusha alivyokuwa nasi tunahizwa kuishi kwa mfano wake. Hakuna aliyewahi kumwona Mungu Baba hivyo hakuna awezaye kuchonga sanamu ya kufanana na Mungu, atachemka tu. Ndiyo maana waisraeli waliadhibiwa, walikuwa wanachonga ndama wanajidai eti Mungu anafanana na Ndama,hayuko hivyo wala hakuna aliyekwisha kumwona ni kutwanga maji kwenye kinu.Mwishowe umeanza kusinzia,naishia hapo pole kwa kukuchosha.

Kifupi, hapo mwanzo Mungu aliwakataza waisraeli kuchonga sanamu kwa sababu aliona imani yao kuwa ni changa wangeweza kuanza kuziabudu, baadaye aliwaruhusu akijua kuwa walikuwa wamekua kiimani kwake, hata wangechonga wasingeweza kuziabudu. Sisi tunachonga kwa sababu imani yetu kwa Mungu imekomaa na hivyo sanamu haziwezi kutufanya sisi tuanze kuziabudu. Juu ya siku ya Ijumaa kuu kinachoabudiwa ni WOKOVU ambao ni Yesu mwenyewe aliye Mungu na hivyo anapaswa kuabudiwa. Hatuabudu mti wa msalaba kwani ni kinyume na Maandiko Matakatifu na kinyume na amri ya kwanza ya Mungu.
Duh
Barikiwa sana mkuu,
 
mojawapo ya maandishi ya papa ni VICARIOUS FILII DEI,hesabu ya haya maneno no 666,hii ni chapa ya mpinga kristo.na amejaa maneno ya makufuru kwa Mungu,hili kanisa linampinga Mungu.satan is behind this church.analiendesha kwa siri mno!..na lina watu wengi kweli,ila sasa hiv wengi wanashtuka wanakimbia.
Umelishwa matango pori
 
Imeandikwab,,USIVISUJUDIE ( USIVIABUDU) WALA KUVITUMIA ,,,,,msiwe mnaishia kwenye usivisujudie ..mmalizie sentensi nzima .....neno usivitumikie lina maana gan ??? Mungu hataki hata uwekee sanam kitambaa au kuifuta vumbi ,,au kusafisha ...ndo maana ya USIVITUMIKIE.
 
Tofautisha kuomba kama sala kwa mtu na kumuomba kivingine.Kwani hao walifanya sala kwa Maria kuhusu divai?
Unamatatizo ya ufahamu,hivi sala ni nini,na kuomba ni nini,
Tunasaili kutaka ama kufanya nini km kuomba hakupo hapo,
Vua chuki ulolishwa changanua mambo kwa akili huru siyo ya kukosoa ama chuki
 
SANAMU LENYEWE LA YESU SIO YESU MWENYEWE BALI NI SANAMU LA MUIGIZAJI ALIYEIGIZA KWENYE SINEMA ZA YESU YAANI MWINGEREZA AITWAYE BRIAN. SI BORA HATA INGEKUWA NI SANAMU LA YESU MWENYEWE. SANAMU LA BIKIRA MARIA SIJUI NI MUIGIZAJI GANI YULE ALIYEIGIZA HIYO NAFASI
Mkuu nenda kaendelee kushika sheria zenu za kuvaa vipedo,huku tuachie
 
Imeandikwab,,USIVISUJUDIE ( USIVIABUDU) WALA KUVITUMIA ,,,,,msiwe mnaishia kwenye usivisujudie ..mmalizie sentensi nzima .....neno usivitumikie lina maana gan ??? Mungu hataki hata uwekee sanam kitambaa au kuifuta vumbi ,,au kusafisha ...ndo maana ya USIVITUMIKIE.
Sanamu ya Nyerere inapochakaa na ikakarabatiwa,au eneo ilipo linaposafishwa nayo si kutumikia?,inamaana nchi km nchi tunamuabudu kwa kumtumikia?maana hata kusherekea siku yake ni kutumika kwa sababu yake,sasa tunaabudu?,
Binadamu ni mfano (sanamu)ya Mungu,
Ref,tuume mtu kwa mfano wetu na sura yetu,kwa hiyo baba ako anapozeeka na ukamtumikia kumpa mahitaji na kumhudumia na ukampa chakula kwa kumpigia magoti ni kumuabudu?
Maana kutumikia kumekatazwa,
Mkuu biblia ukiimeza nzima nzima utafanya maajabu,tafakari mambo
 
Sanamu ya Nyerere inapochakaa na ikakarabatiwa,au eneo ilipo linaposafishwa nayo si kutumikia?,inamaana nchi km nchi tunamuabudu kwa kumtumikia?maana hata kusherekea siku yake ni kutumika kwa sababu yake,sasa tunaabudu?,
Binadamu ni mfano (sanamu)ya Mungu,
Ref,tuume mtu kwa mfano wetu na sura yetu,kwa hiyo baba ako anapozeeka na ukamtumikia kumpa mahitaji na kumhudumia na ukampa chakula kwa kumpigia magoti ni kumuabudu?
Maana kutumikia kumekatazwa,
Mkuu biblia ukiimeza nzima nzima utafanya maajabu,tafakari mambo
SANAM INAONGEA ??? INATEMBEA ??? INAKULA ??? INASIKIA ??? INAPUMUA ???? Nijibu haya kwanza .

Bro Acha kutafsiri maandiko utakavyon wewe,, Ikitajwa MFANO ni MFANO tuuuu ,, Naikitajwa SANAM ni SANAM tu ,, km mfano ni sanam,, kwann isngesomeka ivi * Tumfanye Mtu kama Sanamu yetu ????? Nasio mfano Wetu ???? Inamaana MTU wamfano wao ,,Ataongea ,, atapumua , n.k ......

Sanam ya nyerere ,,,Mungu anakataa SANAM ZOTE zinazotengenezwa kwa ajili ya kuabudiwa ,,yaan kuzinyenyekea ,, kuziabdu ,, nakwasababu unaziabudu ndo maana akipiga marufuku kuzitumikia ,,coz huwezi kua unakipigia magoti kitu alafu kikawa na vumbi naunajua hakiwezi kujisafisha then ukakiacha kama ilivyo !! Nilazima tu utakisafisha kwakua ndicho unachokipigia magoti ,, Sasa hii ndo Mungu hapendi ...lkn km nisanamu ya kitu kuwekwa kwa ajili tu ya kutambua mchango Wa MTU nisawa na wala sio dhambi ,, kwakua nutakitumia SIO KWA DHAMIRA YA KUKIABUDU,,,,,

kuhusu Baba kuzeeka ,,Kama Baba yako ni SANAM ACHA KUMTUMIKIA KWASABABU HAONGEI WALA HASIKII ,,WALA HAKUKUZAA,,WALA HAPUMUI ,,WALA ALI .....

ILA KWAKUA MIMI BABA YANGU NI MFANO WA MUNGU ,, NITAMTUMIKIA BABA YANGU KWAKUA ANANIKUMBUSHA UKUU WA MUNGU ,, NITATUMIKIA KTK KILA HITAJI LAKE .lkn sitomuabudu ,,kwakua WAKUABDIWA NI MMOJA TU NAYE ANAITWA BABA WA MBIGUNI ,, MWENYE WIVU ,, NA AMBAYE ANAWATAKA WANADAMU WOTE KUTOMUITA MTU MWINGINE HAPA DUNIANI CHINI " BABA ' KAMA NJIA YA KUMUABDU NA KUMHESHIMU ....BABA NI MMOJA NAYE YUPO MBIGUNI ,,, KISHA KUNA MZAZI AITWAYE BABA,, NASIO BABA WENU IYO MNAYEMWITA HOLY FATHER !![emoji12] [emoji12]
 
Huyo unayemchukia una uhakika gani kama yeye anakuhusudu...? Majibu ya kishenzi kabisa...
Hatuezi chukiana kwa sababu ya imani zetu. Itakuwa ni kushindwa kunyambua mambo. I am a catholic and naheshimu dini zote kwani dini hainipeleki mbinguni. Muislamu kwangu ni ndugu, mlokole na myahudi vili vile. usilishwe chuki na mhubiri wako. simamia unachoamini maana hata bila dini kuna kitu unaamini kuhusu Mungu. hata mpagani ana haki pia. usieneze chuki. Kubali kuishi kwa neema.
 
Wanaozitumaini sanamu watafanana Nazo....nawaonya watu wote mnaosikia jihadharini na chachu ya wakatoliki....wana mafundisho mengi potofu ambayo wameyajengea ujanja wa misitari ya Biblia ili kuwasadikisha watu upotevu huo.....Mafundisho potofu yanayoendelezwa na katoliki ni pamoja na kuombea wafu, kusali rosali, kuomba wafu(watakatifu wa zamani) kunywa pombe,kuvuta sigara, kula nyamafu,kula damu, kufamfanyia ibada Maria eti ni mama wa Mungu,kuwa na kipaimara badala ya Roho Mtakatifu, badala ya kuwa na huduma tano katika kanisa wameweka papa Mtakatifu badala ya Mungu.....inawezekana wana kiasi cha 2% tu ya ukweli wa Biblia mengine yaliyobaki ni elimu ya uongo. Jihadhari nao sana sana...mwenye hekima na ayafahamu maneno hayo.
 
Wanaozitumaini sanamu watafanana Nazo....nawaonya watu wote mnaosikia jihadharini na chachu ya wakatoliki....wana mafundisho mengi potofu ambayo wameyajengea ujanja wa misitari ya Biblia ili kuwasadikisha watu upotevu huo.....Mafundisho potofu yanayoendelezwa na katoliki ni pamoja na kuombea wafu, kusali rosali, kuomba wafu(watakatifu wa zamani) kunywa pombe,kuvuta sigara, kula nyamafu,kula damu, kufamfanyia ibada Maria eti ni mama wa Mungu,kuwa na kipaimara badala ya Roho Mtakatifu, badala ya kuwa na huduma tano katika kanisa wameweka papa Mtakatifu badala ya Mungu.....inawezekana wana kiasi cha 2% tu ya ukweli wa Biblia mengine yaliyobaki ni elimu ya uongo. Jihadhari nao sana sana...mwenye hekima na ayafahamu maneno hayo.
Off course maneno yako tyu yanaonekana kuwa wew ni mwanaharakati msabato ambao mnajiita wakristo lakini siyo huijui biblia zaid ukasuku wa mistari pasipo uelewa. Unapozungumza biblia unazungumzia ukatoliki. Hahahaaaaaaa shame on you.
 
Neema, baraka na Upendo wa MUNGU, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Ushirika wa Roho Mtakatifu viwe nanyi nyote......!!!!. Ndugu zangu kumekuwa na kelele za hapa na pale kuwa eti Wakristo Wakatoliki wanaabudu Sanamu, hoja hii SIYO YA KWELI Kabisa. Nasisitiza siyo ya Kweli,Jamani mbona mnatuwekea maneno mdomoni ???.,nasema hivi Wakatoliki hatuabudu Sanamu.Weeee !!! hebu tuliza Munkali, fuatana nami.

A:UTANGULIZI.
Katika Biblia MUNGU alikataza Ibada ya Sanamu, lkn jinsi alivyokataza, katazo hilo limewaacha Wakristo Wengi njia panda, hivyo kujikuta wakichanganyikiwa.
Kutoka 20:4-"Usijifanyie Sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu Mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia ".

Kumbukumbu la torati 5:8-"Usijifanyie Sanamu ya kuchonga, mfano wa kitu chochote kile kilicho juu Mbinguni, au kilicho chini duniani, au kilicho majini chini chini ya nchi ".

Sehemu hizi ktk Biblia zikichukuliwa jinsi zilivyo maana yake zinakuwa zimetoa katazo la kutengeneza Sanamu kitu chochote kile wala picha hata Video .Sasa Ndugu Zangu, Walioweka picha za wapendwa wao majumbani, maofisini, vyombo vya Usafiri na kwenye mabango ya Matangazo ni Wakatoliki tu ???. Hivi pesa tunazotumia si zina picha za Viongozi,Wanyama na mimea, je kwa mujibu wa Vifungu tulivyosoma si mnakosea Jamani ??, Mnaonaje km mngetuachia hayo Manoti na masarafu ya hela sisi Wakatoliki ??, Najua wako wenye Vichwa vya Panzi hao watashupaza shingo kuwa picha sio sawa na Sanamu, Nawaambia tulizeni boli, twende taratibu tuwakokote "SLOW LEARNERS ".Nakwambia hivi Kibiblia "SANAMU ni SAWA NA PICHA ni SAWA na SANAMU ".Upo hapo ???!!!. Kama unabisha soma hapa Marko 12:15-16.

15 Tumpe, tusimpe ?,naye akijua unafiki wao, Akawaambia, mbona mmenijaribu ? Nileteeni dinari niione.
16 Wakaileta. Akawaambia ,ni ya nani Sanamu hii na anwani hii ?? wakamwambia ni ya Kaisari.

-Unaona ???!!!. Picha ya Kaisari, kiongozi wa nchi ambayo ipo kwenye Fedha, hapa ktk Biblia inatajwa km Sanamu ya Kaisari na hata Yesu Mwenyewe aliitumia sarafu hiyo. Kumbe mtaona kuwa kwa kuishia ktk mstari wa "4" sura ya 20 ya Kitabu cha Kutoka na mstari wa "8" sura ya 5 ya Kitabu cha Kumbukumbu la torati, Mwenyezi MUNGU amekataza kila kitu kihusucho Sanamu na picha ,lkn ili kujua ni kwanini MUNGU aliagiza hivyo au dhamira yake nini, na kwamba lengo lake si kuzuia Sanamu km Sanamu bali Ibada kwa Sanamu, hebu sasa tusome taratibu na kwa tafakari ya kina mistari inayofuata.Kutoka 20:4-6 na Kumb. 5:8-10.

Kutoka 20:4-6.
4 Usijifanyie Sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu Mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
5 Usivisujudie wala kuvitumikia. Kwa kuwa mimi Bwana Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu :nawapatiliza wana maovu ya Baba zao,hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
6 Nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri Zangu.

Kumbukumbu la torati 5:8-10.
8 Usijifanyie Sanamu ya kuchonga, mfano wa kitu chochote kilicho juu Mbinguni, au kilicho chini duniani, au kilicho majini chini ya nchi.
9 Usivisujudie wala kuvitumikia.Kwa kuwa mimi Bwana Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, nawapatiliza wana uovu wa baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
10 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao na kuzishika amri Zangu.

Kumbe hoja ya msingi hapa ni "USIVISUJUDIE WALA KUVITUMIKIA".na Mwenyezi MUNGU ametoa sababu ya Kwanini "TUSIVISUJUDIE WALA KUVITUMIKIA ".Nayo ni kwamba -yeye ni MUNGU mwenye wivu. Kumbe anachokataza MUNGU ni kuchonga Sanamu na kisha Sanamu hizo kuanza kuabudiwa kanakwamba ni MUNGU Mwenyewe, na MUNGU anatoa katazo hilo kwasababu Waisraeli waliyafanya hayo,walichonga Sanamu na wakaziabudu. Kujua kwamba MUNGU alizuia tu Kuabudu Sanamu na si kuzitengeneza hebu tuone jinsi MUNGU Mwenyewe alivyoamuru mara kadhaa Sanamu kutengenezwa na kuwekwa Hekaluni .

B:BIBLIA TAKATIFU, INAFUNDISHA
KUWA MUNGU ALIRUHUSU SAN
AMU KUTENGENEZWA.
1.Mungu alimwamuru Musa kutengeneza Sanamu za Makerubi na kisha kuwekwa Hekaluni -Kut. 25:18-19.

18 Nawe fanya makerubi mawili ya dhahabu :uyafanye ya kazi ya kufua, katika hiyo miisho ya kiti cha rehema, huku na huku.
19 Weka kerubi Moja mwisho Mmoja, na kerubi la pili mwisho wa pili. Fanya hayo makerubi ya kitu kimoja na kiti cha rehema, mwisho huku na mwisho huku.

Mambo hayo !!!, MUNGU anamwamuru Musa kutengeneza Sanamu za makerubi, makerubi wawili hao hukaa juu ya sanduku atokeapo Bwana. Kwa hiyo Bwana amesema ktk Biblia yeye hukaa juu ya Makerubi, rejea 1Sam.4:4, 2Sam.6:2 , 2Fal.19:15 ,Zab.80:1.
Katika Kitabu hicho cha Kutoka 26:1:Mwenyezi MUNGU anaendelea kutilia msisitizo juu ya kuwekwa kwa Sanamu za makerubi ktk Hekalu .

2.MUNGU alimwamuru Musa kutengeza Sanamu ya nyoka wa Shaba -Hesabu 21:8.

8 Bwana akamwambia Musa, jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi ".

Ona sasa !, MUNGU anamimina uponyaji wake ndani ya Sanamu ya nyoka wa Shaba, kwamba mtu akiumwa na nyoka, aitazamapo Sanamu hiyo ataishi ,Hebu fikiri hapo, Kwanini asingesema kuwa labda watu wataje tu jina lake nao wataishi ? Au Musa awaguse tu nao wataishi ?. Mwinjili Yohane hueleza kuwa Sanamu hiyo ya nyoka wa Shaba ni mfano wa Kristo aliyeinuliwa msalabani. Kama vile Waisraeli walivyomtazama nyoka wa Shaba walipona, vivyo hivyo kila Mmoja anayemtazama Kristo msalabani kwa kusadiki (Jicho la IMANI) ana Uzima wa milele. rejea Yohane 3:14-15.

14 Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa,
15 Ili kila aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye.

3.Katika Kitabu cha Wafalme, Mfalme Sulemani alijenga Hekalu na Kisha kulipamba Hekalu hilo kwa Vito vya Dhahabu na SANAMU.rejea 1Wafalme 6:23-28.

23 Akafanya ndani ya chumba cha ndani makerubi mawili ya mzeituni, kwenda juu mikono Kumi.
24 Na bawa Moja la kerubi lilikuwa mikono mitano urefu wake, na bawa la pili la kerubi mikono mitano ,mikono Kumi toka mwisho wa bawa Moja hata mwisho wa bawa la pili.
25 Na kerubi la pili lilikuwa mikono Kumi :makerubi yote mawili yalikuwa ya cheo kimoja na namna Moja.
26 Kwenda juu Kwake kerubi Moja kulikuwa mikono Kumi, na kerubi la pili vivyo.
27 Akayaweka hayo makerubi katika nyumba ya ndani, na mabawa ya makerubi yakanyoshwa, bawa la moja likafika ukutani huko, na bawa la kerubi la pili likafika ukutani huko :mabawa yao yakagusana katikati ya Nyumba.
Akayafunika makerubi kwa dhahabu.

Mfalme Sulemani, hakuishia kuweka Sanamu za makerubi tu, kama tulivyoona hapo, bali aliweka hata SANAMU za Wanyama km vile Ng'ombe na Simba, rejea 1Wafalme 7:23-26,27-29.Aidha Mfalme Sulemani alilipamba Hekalu hili kwa Michoro rejea 1Wafalme 7:36.
Baada ya Ujenzi wa Hekalu kukamilika, Mwenyezi MUNGU alimtokea Mfalme Sulemani na kumwambia kuwa Nyumba hiyo, yaani Hekalu, ameitakasa na tena Macho yake MUNGU na Moyo wake utakuwapo hapo siku zote. rejea 1Wafalme 9:1-3.

1 Ikawa Sulemani alipokwisha kuijenga nyumba ya Bwana, na nyumba ya Mfalme, na mambo yote yaliyoingia moyoni mwake Sulemani, naye akataka kuyafanya,
2 basi, Bwana akamtokea Sulemani mara ya pili kama alivyomtokea huko Gibeoni.
3 Bwana akamwambia, Nimeyasikia maombi yako na dua zako, ulizotoa mbele Zangu. Nimeitakasa nyumba hii uliyoijenga ili niweke jina langu humo milele, tena macho yangu na Moyo Wangu utakuwapo hapo siku zote.

Ona sasa !!!, MUNGU anavyolitakasa na kulikubali Hekalu lililokuwa limejengwa na Mfalme Sulemani, Kama Kweli SANAMU zingekuwa ni Chukizo kwa Mungu hapo MUNGU si angelimkaripia Sulemani ??. Lkn MUNGU hakufanya hivyo kwasababu Mfalme Sulemani hakuweka Sanamu hizo kwa nia ya Kuziabudu km ambavyo Kanisa Katoliki linafanya kwa kuweka Sanamu si kwa lengo la Kuziabudu.

4.Wafilisti walipo lichukua Sanduku la Agano la Kale kwa nguvu Kutoka kwa Waisraeli na kisha kuadhibiwa na MUNGU ,Walipotaka kulirudisha waliwauliza Makuhani na Waaguzi, wafanye nini watakapokuwa wanalirudisha Sanduku hilo ili kujipatanisha na MUNGU, waliambiwa kuwa -Watoe sadaka ya kuteketezwa ya ng'ombe wawili na SANAMU TANO ZA DHAHABU ZA MAJIPU na TANO Za PANYA -Rejea 1Samweli 6:1-15.(Kutokana na urefu wa somo Naomba ujisomee Mwenyewe, maana sio vizuri kukutafunia kila kitu).

5.Katika Agano jipya, Sanamu za Viongozi wa Serikali ziliwekwa katika Fedha na kisha kutumika katika Mzunguko wa Kiuchumi. rejea Marko 12:13-17.

13 Wakatumwa Kwake baadhi ya Mafarisayo na Maherodi, ili wamnase kwa maneno.
14 Hata walipofika walimwambia, Mwalimu twajua ya kuwa wewe u mtu mkweli, wala hujali cheo cha mtu ,kwa maana hutazami sura za watu, lakini katika Kweli waifundisha njia ya Mungu. Je, ni halali kumpa kaisari kodi au siyo ?
15 Tumpe, tusimpe ? Naye, kujua unafiki wao, Akawaambia, mbona mmenijaribu ? Nileteeni dinari niione.
16 Wakaileta Akawaambia, ni ya nani Sanamu hii na anwani hii ? Wakamwambia ni ya Kaisari.
17 Yesu akajibu, Akawaambia, mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na yaliyo ya Mungu mpeni Mungu. Wakamstaajabia sana.

Mafarisayo na Maherodia wanapomjaribu Yesu juu ya kulipa kodi kwa Kaisari swali lao linajibiwa kwa kutumia sarafu yenye SANAMU ya mtawala Yaani Kaisari, Jibu la Yesu linakuwa "Mpeni Kaisari yaliyo yake Kaisari, na Mpeni MUNGU yaliyo ya MUNGU ".Fikiri hapo !, Mbona Yesu hasemi msitumie hii Dinari kwasababu ina Sanamu ya Kaisari maana kadiri ya Kumb.5:8 na Kut. 20:4,ni kosa. Lkn Yesu hawakatazi kwasababu anajua kuwa Mungu hachukii Sanamu km Sanamu, bali anachukia Ibada ya Sanamu.

C:HITIMISHO .
Wapendwa sana wanajukwaa,Bado nina mengi ya kuwaeleza Kuhusu Sanamu, lkn nahisi nitawachosha sana lkn naamini nimetoa mwanga angalau kidogo tu. Tukumbuke kuwa hata sisi Wanadamu tuliumbwa kwa Sura na mfano wa MUNGU -rejea Mwanzo 1:26 ,hivyo hata sisi ni Sanamu, maana kitu chochote kilichoumbwa au kutengezwa kwa mfano wa kitu kingine ni Sanamu. Naendelea kukazia kuwa Wakatoliki HATUABUDU SANAMU, Sanamu hutumika tu Kanisani kwaajili ya kumrahisishia muumini kuelewa IMANI yake, sawa na wewe Unapotaka Kumuelezea Mwanao juu ya Namna Babu yake aliyefariki miaka mingi kabla ya yeye kuzaliwa kwa kutumia Picha. Hata katika Elimu Walimu huwa wanatumia mbinu mbalimbali kuhakikisha kwamba Wanafunzi wanaelewa somo lake, wapo wanatumia Picha, Michoro, Sanamu na kufanya ziara za Kimasomo. Tulipokuwa Sekondari ktk Maabara ya Biolojia kulikuwa na Sanamu kubwa ya SKELETON ya binadamu iliyotumika kujifunzia na Wanafunzi wa Dini zote tuliitumia kujifunzia lkn sikuwahi kusikia mtu yeyote akikataa au kulalamika kuwa mbona Sanamu zimekatazwa.Hivyo Kanisa Katoliki haliabudu Sanamu, Tunayemwabudu ni MUNGU Mmoja, ktk Nafsi tatu Yaani MUNGU Baba, MUNGU Mwana na MUNGU Roho Mtakatifu.
Karibuni sana, kwa maswali, dukuduku, n. K. Matusi mwiko.

C. C. Edwayne
 
Dini zote kwa sasa zinaabudu sanamu, hakuna hata wakumnyoshea kidole mwenzie.
 
IMG_20180123_191601.jpg

Noti kama hii kwa mujibu wa Kumb. 5:8 na Kut. 20:4,ni Makosa kuimiliki.
 
Hata hii nayo ni kosa kuimiliki
IMG_20180123_191553.jpg

Kwasababu ina picha ya Hayati Baba wa Taifa, ambapo kadiri ya Marko 12:13-17.ni Sanamu.
 
Mods rudisheni hiyo post [HASHTAG]#663[/HASHTAG] kama uzi.., mkiificha huku itakuwa hajatenda haki...!!!

Mods nazani mmenisoma.
 
Back
Top Bottom