Ukweli lazima usemwe, Tunahitaji Muungano wa Serikali 1 tu

Hakuna haja ya kuwa na Serikali mbili sijui 3 alafu fedha nyingi zinaishia kuhudumia hizo serikali na viongozi wake.

Tume na nchi moja na Serikali moja tu
Haitawezekana. Wazanzibar hawatakubali wafutwe. Ndio maana sheria ya marekebisho ya Katiba inataka suala la la Zanzibar kufutwa lisiwepo. Hakuna Cha serikali moja, Bali tatu.
 
Itategemea dola inataka nn na c vinginevyo,hii nchi ina mauzauza mengi yasiyo na idadi
 
Hii shida Nyerere hawezi kuikwepa. Muungano sahihi ulikuwa wa Serikali 1. Serikali mbili au Tatu zipo kimaslahi kwa wanasiasa wanaotaka vyeo na kula full stop
 
Hili jambo la Muungano Lina ukakasi kwa sababu tu ya siasa za kufuata mkumbo (kama nyumbu).
Ukifikiria kwa makini, kama ukifanyika utafiti rasmi, katika kundi la wanasiasa wetu, wenye akili nzuri na huru ni chini ya 5% na zaidi ya 95% hufuata mkumbo tu.
Ikitokea kiongozi mkuu akakosea kibinadamu, wote hufuata bila kuhoji.
Tanzania ni nchi moja, kama siyo moja itawezekanaje Rais atoke upande wowote wa Muungano?
Mheshimiwa Rais Mwinyi (junior) alikuwa mbunge Mkuranga, sasa hivi ni Rais wa Zanzibar.
Mheshimiwa Mama Samia ni mzabari, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mzee wetu, Rais mstaafu Mwinyi (senior), yeye alimaliza yote. Hizo nchi mbili ziko wapi?
Kelele za wanasiasa wenye akili zisizokuwa na akili.
 
Good
 

Nchi Ni moja ila serikali ni mbili.
 
Kwenye muungano tumenasa pabaya! Serikali 1 haiwezekani, tatu haiwezekani! Serikali 2 ni migogoro, na ndio iliyosababisha umaskini! Mnaona tulivyo nasa? Suluhisho hapa ni separation!
Na hiyo pia Wahafidhina hawataki !! Kwahiyo kweli tumenasa !!
 
Muungano wa tanganyika na zanzibar ni wa kipuuzi sana.mapungufu ya wazi yamejiinyesha baada ya urithi wa mzanzibar kuwa rais wa muungano.kwa sasa anataka ajenge daraja kwenda zanzibar kwa pesa za tanganyika.bora muungano ufe hadi tutakapokubaliana kuungana upya kwa kuziondoa hizi kero za tanganyika kunyonywa
 
Kwanza walikuwa wanalalamika wao sasa tunalalamika sisi ! Duh 🙄!
 
Rest in peace mchungaji Mtikila ni moja kati ya wanasiasa waliokuwa kifua mbele kuupigania utanganyika wetu baada ya kufariki sijaona tena mwanasiasa wa kitanganyika mwenye ujasiri wa kuupigania utanganyika wetu
Kweli kabisa ! R.I.P mchungaji Mtikila !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…