Uchaguzi 2020 Ukweli: Lissu atashinda uchaguzi wa Oktoba kwa 70%

Uchaguzi 2020 Ukweli: Lissu atashinda uchaguzi wa Oktoba kwa 70%

Sio dodoma?? Mi nimeingia leo kutoka dar ni hapa Mwenzo
Dodoma hapatoshi mkuu Dunia mzima itasimama week nzima sio shuguli ya kitoto ,kama uko Tunduma agiza Konyagi nakuja kulipa mwanaizaya.
 
Mwaka 2015 si mpipata 40% ya kura , basi toa 20%, sio maneno yangu ni ya lissu, unapoteza mda sana kuandika upuuzi apa mgombea mwenyewe anajua anaenda kufa,
 
Karibu sana huku Tunduma huku chips hakuna tunatoa kitu tunashushia cha uchungu ,mzee baba hata kura ya dawa hapati tunatoa mswaki
Poa mkuu ..naijua Tunduma vzr nimeishi hapo kwa miaka mitatu
 
Mh Lisu aliwahi kutuaminisha Lowasa ni fisadi lakini 2015, akampigia kampeni lowasa, imekaaje hiyo ?
Kama alikuaminisha,na wewe ukaamini bila ya EL kuchukuliwa hatua,na tena akaungana na wale waliokuwa wanasema "sebule" yao sasa i safi kwa kuwa mafisadi walikimbilia CHADEMA,basi wewe utakuwa una tatizo.
 
Hawezi kuwa kiongozi huyu, hana hoja za maendeleo na anajipendekeza sana kwa wazungu
 
Hoja za kijingajinga kwa maono yangu, hakuna wa kumpindua jiwe
 
Amani iwe nanyi wadau na kwa wakazi wa Dar poleni na Tetemeko

Niende kwenye mada!

Ni ukweli ulio wazi kuwa John Pombe Magufuli hawezi shinda uchaguzi wa mwaka huu na hizi ndizo sababu

1. Kuna mgawanyiko mkubwa sana ndani ya CCM
Najua CCM sasaivi wanajaribu kuwaita makada wao nguli ambao waliumizwa na magufuli Kama Kinana, Nape na Makamba wakiamini hawa wanaweza kurudisha hali ya CCM kikampeni ila ukweli ni kuwa hapana it’s too late. Kwa CCM wengi wana amini kuwa mwenyekiti wao ni mtu wa visasi na kutumia tu watu kwa faida zake hivyo wengi wanaamini kuwa hata hawa wakirudi hawatarudi kwa moyo mweupe. CCM wengi wanevunjika moyo na hawana raha na Magufuli. Suala la Kikwete kuonekana hivi karibuni akitoa tathimini ambazo zinaonekana kabisa ni tofauti na nyimbo anazoimba magufuli limewafanya watu wengi waone dhahili kuwa CCM sio moja!

Kwenye hili maneno ya Mzee Butiku kwa vyombo vya dola kuhusu uchaguzi wa mwaka huu aliyoyatoa kwenye kikao cha NCCR yananifanya ku conclude kuwa hata class ya wazee nyeti wa nchi hii wamesha endorse mabadiliko yatakayofanyika nchini hapo October kupitia sanduku la kura.

2.Lissu kutokuwa na makandokando!
CCM wanapata shida sana kutafuta hoja ya kumpigia Lissu. Hayuko kwenye ufisadi, hayuko kwenye uzembe wala hayuko kwenye ujanja ujanja. Track record ya Lissu kuwahenyesha CCM kuanzia bungeni hadi nje ya bunge inambeba sana Lissu. Mbaya zaidi ni tukio la kujaribu kumuua. Watanzania wengi wanajua ni mwenyekiti wa CCM ndiye ambaye yuko behind jaribio la mauaji la Lissu

3. Wapiga kura wa Mwaka huu 2020!
Kiuhalisia wapiga kura wengi wa mwaka huu ni vijana wa miaka ya themanini nwishoni na tisini. Alafu kuna kundi la vijana wa 2000. Haya makundi ni makundi yenye kiu ya mabadiriko, ni makundi ya kizazi cha internet ambacho kinajua mengi na kuona mengi. Mizani hiki sio loyal kwa CCM tofauti na kizazi cha 60’s na 70’s.

4. Makosa ya wazi ya magufuli- Magufuli kafanya makosa mengi ya wazi, kubambikia watu wanaompinga kesi na kuwaonea Mf viongozi wa upinzani, msanii idris, mwandishi erick kabendera na vijana mdude nyangari na kina tito magoti.

Magufuli katoa matamko yaliyosababisha maisha ya watu kuathilika kiuchumi kama tamko la kuzuia uagizwaji wa sukari jambo lililopelekea bei ya sukari kupanda maradufu

Kwa wakulima Pia Kuna maamuzi ya serikali yaliyoharibu biashara za wakulima na kuwa let was shida Mf Korosho, mbaazi na hata mahindi bila kusahau mazao mengine ya biashara

Kwa wafanyakazi ndo usiseme. Hawa hawaongei ila wote moyoni wanasema wana jambo Lao nae na hiyo itakuwa ni October 2020

Kwa wafanyabiashara hawa ndo wengi wana amini kuwa magufuli amekuja kuwatesa. Wengi wanaona kama snawadhulumu hasa wakiona wanavyofirisiwa na kufungiwa biashara na TRA.

Mwisho kabisa ni kwa vijana graduate- hawa ni kundi kubwa lililoachwa bila ajira. Sekta binafsi iliwaajiri wengi sana kipindi cha awamu ya nne ila kwa mkwamo kwenye awamu hii ya tano wengi wamepoteza kazi na wengine ndo hawajapata kabisa kazi.

kuna mengine mengi kama mafao ya wastaafu ila itoshe tu kusema kuwa Kuna uwezekano wa asilimia 98 kuwa kuna historia itakayitikisha Ardhi ya Africa Mashariki inaenda kuandikwa October mwaka huu!!

Karibu Ikulu( Magogoni na Chamwino) Tundu Antipas Lissu!
Na huo ndio ukweli wenyewe
 
Siku ya uamuzi ni October 28; kila mtu ana haki ya kuwa na matumaini na ndoto kwa sasa lakini kipenga cha mwisho ni siku hiyo.

Unfortunately mwaka huu mimi sitapiga kura tangu ile kura ya 2010 kwa sababu ukiwa nje ya nchi huruhusiwi kupiga kura; ila ninategemea kupiga kura 2025 nikiwa hai kwani nitasafiri tena kwenda kushiriki uchaguzi kama nilivyofanya 2010.
 
At lamadi leo
20200812_235311.jpg
 
Back
Top Bottom