Nourhan
JF-Expert Member
- Apr 7, 2023
- 1,196
- 3,026
Kwenye kupika huwa najiamini bila kumuomba Mwenyeezi Mungu najua nauza sababu kizuri kinajiuza huomba ridhiki kwa wingi ila sio nipate wateja biashara yangu iuzike hio siku watokee wateja.Unakuwa umemuomba jambo ambalo wewe tayari unakuwa unaweza kulifanya na lipo ndani ya uwezo wako. Kwa mfano wewe watu wanakusifu ni mpishi mzuri sana wa chakula. Mimi mwenyewe nimekupa sana biryani lako . Sasa Umepika biryani lako na maandazi yako ya kisomali na chai yako ya maziwa ya kisomali ambavyo tayari watu wanavipenda naturally. Una amka usiku kuomba dua Mungu akusaidie biashara yako itoke siku hiyo na kweli asubuhi wateja wana miminika kama kwa Mwamposa. Wewe utasema ni Mungu majibu dua yako lakini kumbe ni kwa sababu ya utaalamu wako..
Hata vitabu vya dini hizi mbili (ukristu na uislamu vimeweka wazi kabisa kwamba Mungu huwaga hajibu maombi ya watu ndio maana mnatakiwa kuwa na subra mnaambiwa kimafumbo kila mwenye subira yupo na Mungu ili msije mkahoji mbona maombi yenu hayajibiwi. Subira inayo tajwa hapo sio ile subira ya kusubiria wiki mbili hell no hiyo subira ya kusubiria wiki mbili ni kusikilizia. Subira inayo tajwa hapo ni ile ya kusubiria majibu siku ya kihama. Yani wewe tenda matendo yako mema hapa duniani omba maombi yako yote ila na lipo utalipwa siku ya kihama)
Na huwa naomba mambo mazito ambalo najua kwa kiubinadamu siwezi mfano tulikuwa na kesi ya mirathi ndugu watoto was ba mkubwa shangazi wanataka kuuza tumepambana na kesi Ile kila mtu anasema hamshindi usaliti kila kona ushirikina Sasa watu wanashauri mtauliwa nendeni kww waganga aisee nilimliaa Mungu usiku kama namuona mbele yangu na asubuhi sijaenda mahakamani nikasali rakaa 2 Allah atusimamie waongee ukweli aisee mahakamani wakageukana kwenye ushahidi mtu anasema nyumba haiwahusu wameshawishiwa na kaka Yao mkubwa watudhulumu hati na makalatasi ya mauziano tumetupa tukashinda kesi ndugu wakao mmba radhi akabaki kaka mtu akakata rufaa hakimu alikula rushwa bwana alikuwa hataki kusikia lolote mwanasheria anatuambia hakimu chipolopolo mlevi hatutoboi tutakata rufaa kila mtu hamtoboi aisee nilimlilia Mungu usiku aisee siku ya Hukumu Hakimu kafukuzwa kazi kwa kesi za Rushwa tukapewa mwingine tukashinda akakata rufaa tukashinda akaenda mahakama ya ardhi akaikimbia kesi tukashinda alishanisingizia nimtukana natoka mahakamani nimeshinda napelekwa polisi nilimuomba Mungu anistiri nisiwekwe mahabusu nikawa naandikisha maelezo akatokea mkuu wa kituo akauliza ana shida gani akaelezewa akasema msimuweke acheni ajidhamini msimuweke ndani aisee sikuamini ilikuwa nikae ndani mpaka waje watu kunidhamini akaniambia kesho njoo mapema nikaenda nikagoma kulipa pesa tumalizane wakati sijamtukana nikasema twende mahamani huku naogopa namuomba Mungu nikawa naingizwa kwenye gari na wahalifu wengine akatokea mkuu was kituo dada nenda mahakamani watakukuta msimpandishe ustadhati na wahalifu walevi nikaenda mahamani namuomba Mungu isichukue muda iishe kweli ikapangwa karibu karibu ×3 tu siku ya 1 tukasikilizwa kesho kutwa yake ushahidi kesho yake hukumu nikashinda,yaani mie mtu anielezi kitu kuhusu kuomba kwa Mwenyeezi Mungu na ushuhuda was mambo mengi aisee.