Taratibu tu utanielewa mkuu mnapoajiri hao mahousegirl, bado huwa mnataka wake zenu wawasaidie kazi wasiwaachie kila kitu maana wakiwaachia mnaanza kulalamika kwamba wake zenu wamejisahau, mwishowe mnaamua kutembea na hao mahousegirl kwa kisingizio kwamba eti wao ndio wanawafanyia kila kitu
Kutokana na kwamba mmeshajijengea ile mentality kuwa mwanamke anayekufanyia hizo shughuli za nyumbani ndiye unayetakiwa kulala naye, so point yangu ni kwamba kama tumeamua iwe 50/50 basi iwe applied kwenye majukumu yote ya mwanaume na ya mwanamke, isipokuwa yale ya kimaumbile tu
Yani isiwe applied kwenye majukumu ya mwanaume tu huku ya mwanamke yakiachwa, hiyo ndio sababu wanawake hawaikubali hiyo 50/50 mnayoitaka yenye double standard kama mkiamua kuajiri housegirl, basi acha housegirl afanye majukumu yote ya nyumbani bila kuona kama unapaswa kulala naye kisa tu ndiye anayekufanyia kila kitu