Ukweli Mchungu: Hakuna biashara Serikali inaweza kufanya kwa ufanisi

Waingie ubia na sekta binafsi, bila hivyo huduma zake hiyo reli itakuwa kama ya TAZARA au ya kati
 
Hii ni Africa sio China, Africa ina historia ya Soko huria tangu karne na karne kabla wajamaa uchwara hawajatuvuruga baada ya kupata Uhuru.

Hata Machifu wa Africa zamani hawakuwahi kujaribu kupandikiza mfumo wa ujamaa. Kila mtu alikuwa na mali zake, shamba lake, biashara zake na Chifu alikuwa anatoza ushuru tu.
 
Sawa komaeni na soko huria la batter trade litawaletea mafanikio.
 
Serikali ichukue kodi zake tu, historia ya kushindwa kufanya buashara ni ndefu tokea enzi za Nyerere.
 
Binafsi kuna meli za serikali ziwa victoria ziko vizuri kuliko hata za binafsi. Nadhani ni suala tu la kurekebishana na kuwajibishana wakiona miradi ya serikali inachezewa na waliopewa mamlaka ya kusimamia.
 
Hawezi kuekewa huyu amekariri tu alivyokaririshwa
 
Binafsi kuna meli za serikali ziwa victoria ziko vizuri kuliko hata za binafsi. Nadhani ni suala tu la kurekebishana na kuwajibishana wakiona miradi ya serikali inachezewa na waliopewa mamlaka ya kusimamia.
Zipe muda tu! Uwanja wa Taifa mchina alitujengea vizuri sana ila ulivyokabidhiwa kwetu tu hali yake iko hovyo sana hata maintanace yake tia maji tia maji
 
Nyinyi ni watu wa ajabu sana.
Sijui mnashindwa kuelewa kitu gani.

Serikali hiyo hiyo ndiyo inayofanya biashara na hao hao sekta binafsi, halafu mnageuka na kusema haiwezi kufanya biashara!

Tatizo ni moja tu ambalo huwa hamtaki kulikubali., kwamba huo msemo wenu wa "Serikali haiwezi kufanya biashara" unaishia hapo, bila ya kueleza sababu za kwa nini isiweze kufanya biashara.

Sababu ambazo nina hakika mnazijua vizuri, ila humtaki ukweli wake, kwamba majizi toka sekta binafsi ndiyo husababisha kuikwamisha serikali kwa rushwa na wizi wa waziwazi wa mali za umma.

Sasa kwa nini lawama iwe ya upande mmoja?

Mahali ambapo hao hao watoa rushwa na majizi hudhibitiwa, mashirika ya serikali hushamiri na kufanya shughuli zake vizuri, mfano ukiwa China.
Huko majizi na watoa rushwa wanajuwa yatokanayo na kufanya upuuzi huo wa kukwamisha shughuli za serikali..
 
... alipoingia Jiwe muharibifu aliwaondoa Max Malipo na mwisho kukawa hakuna tofauti kati ya daladala na mabasi ya mwendokasi.
Mimi nipo kutetea pasipotetewa.

Hapa nakupinga, kwanza umesema ulikuwa unapanda train ya serikali hukusema nani alivuruga, haya pili ukapanda ndege za serikali hukusema nani kaharibu simu unayopiga, (huku ndege hizo hizo unazopanda hazikuwepo now unaponda 🙄!.

Haya umekuja kwa mwendo kasi umesema ilikuwa inafanana na ulaya hapo ndipo ukamtaja muzee baba Jiwe kuwa kaharibu, ujue umeandika unafiki wa hali ya juu sana!.
 
Hawezi kuekewa huyu amekariri tu alivyokaririshwa


Jifunzeni kwa walio fanikiwa na ninyi mfanikiwe kama wao.

N.b: Asiye sikia la mkuu huvunjika guu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…