Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Waingie ubia na sekta binafsi, bila hivyo huduma zake hiyo reli itakuwa kama ya TAZARA au ya kati
Kwa namna serikali inavyohangaika na huu mradi wa SGR, hiyo siku utakapokamilika naamini itakuwa ni sherehe, sidhani kama watakuja kuuchezea huko mbele ya safari.
Muhimu ni kujipanga tu, ufuatiliaji wa reli na mabehewa yake uwe wa karibu, pawepo na vituo vya ukaguzi kila baada ya mwendo fulani, 24 hrs, ikibidi waajiriwe watu wa kufuatilia reli na vifaa vyake, ili kuifanya idumu.
Wasiwasi wangu sekta binafsi kupewa huo mradi wanaweza kuweka viwango vikubwa vya nauli, ambavyo mtanzania wa kawaida atashindwa kuvimudu, matokeo yake hiyo reli itakuwa ya wachache wanaojimudu kiuchumi, hivyo kutotimiza lengo la kuanzishwa kwake.
Binafsi ningependa viwango vya nauli viwe vya kati, sio juu sana au chini sana, vinavyoeleweka kwa wengi, ili kutimiza lengo la kupunguza adha ya usafiri kwa wale wanaoenda mikoa ya mbali hasa Mwanza na Kagera.