Ukweli Mchungu: Hakuna biashara Serikali inaweza kufanya kwa ufanisi

Ukweli Mchungu: Hakuna biashara Serikali inaweza kufanya kwa ufanisi

Waingie ubia na sekta binafsi, bila hivyo huduma zake hiyo reli itakuwa kama ya TAZARA au ya kati
Kwa namna serikali inavyohangaika na huu mradi wa SGR, hiyo siku utakapokamilika naamini itakuwa ni sherehe, sidhani kama watakuja kuuchezea huko mbele ya safari.

Muhimu ni kujipanga tu, ufuatiliaji wa reli na mabehewa yake uwe wa karibu, pawepo na vituo vya ukaguzi kila baada ya mwendo fulani, 24 hrs, ikibidi waajiriwe watu wa kufuatilia reli na vifaa vyake, ili kuifanya idumu.

Wasiwasi wangu sekta binafsi kupewa huo mradi wanaweza kuweka viwango vikubwa vya nauli, ambavyo mtanzania wa kawaida atashindwa kuvimudu, matokeo yake hiyo reli itakuwa ya wachache wanaojimudu kiuchumi, hivyo kutotimiza lengo la kuanzishwa kwake.

Binafsi ningependa viwango vya nauli viwe vya kati, sio juu sana au chini sana, vinavyoeleweka kwa wengi, ili kutimiza lengo la kupunguza adha ya usafiri kwa wale wanaoenda mikoa ya mbali hasa Mwanza na Kagera.
 
Hii ni Africa sio China, Africa ina historia ya Soko huria tangu karne na karne kabla wajamaa uchwara hawajatuvuruga baada ya kupata Uhuru.

Hata Machifu wa Africa zamani hawakuwahi kujaribu kupandikiza mfumo wa ujamaa. Kila mtu alikuwa na mali zake, shamba lake, biashara zake na Chifu alikuwa anatoza ushuru tu.
Wataalamu wa kuendesha STATE OWNERSHIP/ STATE OWNED ENTERPRISES / STATE COMPANIES hapa duniani ni CHINA asilimia 60%-70% ya makampuni ya China ni ya serikali na yanafanya vizuri ndani ya China na duniani kote.

Tanzania tukajifunze China kuendesha haya mashirika katika ubora au tuajiri wataalamu kutoka China watuendeshee haya mashirika yetu kwa miaka 10+
 
Hii ni Africa sio China, Africa ina historia ya Soko huria tangu karne na karne kabla wajamaa uchwara hawajatuvuruga baada ya kupata Uhuru.

Hata Machifu wa Africa zamani hawakuwahi kujaribu kupandikiza mfumo wa ujamaa. Kila mtu alikuwa na mali zake, shamba lake, biashara zake na Chifu alikuwa anatoza ushuru tu.
Sawa komaeni na soko huria la batter trade litawaletea mafanikio.
 
Serikali ichukue kodi zake tu, historia ya kushindwa kufanya buashara ni ndefu tokea enzi za Nyerere.
 
Yale yale.
Kuwa Serikali za Waafrika haziwezi kufanya biashara.

...Mabeberu wamo Kazini. Wanataka turudi kuuule, yaani Serikali zinapewa mikopo, wanawezeshwa, wanatumia nguvu za dola, kama vile kuwahamisha watu bila malipo stahiki na kutunga sheria zinazoipa nguvu "Shirika"....

Uwongo unatengenezwa, kuwa mashirika yanashindwa kuleta faida na hivyo basi yauzwe kwa mabeberu-kumbuka kuna kishinikizo cha kulipa deni ambalo riba yake inaendelea kupanda na kufanya deni liwe gumu kulipa.

...kinafuatia na kuuzWa Shirika kwa bei ya chini kwa kigezo kuwa wao "mabeberu" wanarithi deni, pamoja na kutaka/kuomba msamaha wa kodi/tozo n.k kwa miaka ambayo wanakuwa wanalipa deni au mpaka pale wakianza kupata faida. Wakati huo wanachagua wapi wanaweza kupata faida, kwa mfano wanaweza sema wao watakuwa wanakatisha tiketi, wanalisha wasafiri n.k watauza majengo n.k huku Serikali ikiendelea kuyatengeneza/maintanance vifaa hapa kama mabehewa na reli

...yaani ni mchezo mchafu. Kwa mgongo wa mwananchi.

Ni Uwongo mtupu kuwa Serikali, hususani za Waafrika haziwezi kufanya biashara kifanisi.

Tutapinga uwongo kama huu. Nani kasema vita ya uchumi viliisha baada Jiwe kuondoka!!!

ALUTA CONTINUA
Binafsi kuna meli za serikali ziwa victoria ziko vizuri kuliko hata za binafsi. Nadhani ni suala tu la kurekebishana na kuwajibishana wakiona miradi ya serikali inachezewa na waliopewa mamlaka ya kusimamia.
 
Hii ni Africa sio China, Africa ina historia ya Soko huria tangu karne na karne kabla wajamaa uchwara hawajatuvuruga baada ya kupata Uhuru.

Hata Machifu wa Africa zamani hawakuwahi kujaribu kupandikiza mfumo wa ujamaa. Kila mtu alikuwa na mali zake, shamba lake, biashara zake na Chifu alikuwa anatoza ushuru tu.
Hawezi kuekewa huyu amekariri tu alivyokaririshwa
 
Zipe muda tu! Uwanja wa Taifa mchina alitujengea vizuri sana ila ulivyokabidhiwa kwetu tu hali yake iko hovyo sana hata maintanace yake tia maji tia maji
 
Nyinyi ni watu wa ajabu sana.
Sijui mnashindwa kuelewa kitu gani.

Serikali hiyo hiyo ndiyo inayofanya biashara na hao hao sekta binafsi, halafu mnageuka na kusema haiwezi kufanya biashara!

Tatizo ni moja tu ambalo huwa hamtaki kulikubali., kwamba huo msemo wenu wa "Serikali haiwezi kufanya biashara" unaishia hapo, bila ya kueleza sababu za kwa nini isiweze kufanya biashara.

Sababu ambazo nina hakika mnazijua vizuri, ila humtaki ukweli wake, kwamba majizi toka sekta binafsi ndiyo husababisha kuikwamisha serikali kwa rushwa na wizi wa waziwazi wa mali za umma.

Sasa kwa nini lawama iwe ya upande mmoja?

Mahali ambapo hao hao watoa rushwa na majizi hudhibitiwa, mashirika ya serikali hushamiri na kufanya shughuli zake vizuri, mfano ukiwa China.
Huko majizi na watoa rushwa wanajuwa yatokanayo na kufanya upuuzi huo wa kukwamisha shughuli za serikali..
 
... alipoingia Jiwe muharibifu aliwaondoa Max Malipo na mwisho kukawa hakuna tofauti kati ya daladala na mabasi ya mwendokasi.
Mimi nipo kutetea pasipotetewa.

Hapa nakupinga, kwanza umesema ulikuwa unapanda train ya serikali hukusema nani alivuruga, haya pili ukapanda ndege za serikali hukusema nani kaharibu simu unayopiga, (huku ndege hizo hizo unazopanda hazikuwepo now unaponda 🙄!.

Haya umekuja kwa mwendo kasi umesema ilikuwa inafanana na ulaya hapo ndipo ukamtaja muzee baba Jiwe kuwa kaharibu, ujue umeandika unafiki wa hali ya juu sana!.
 
Hawezi kuekewa huyu amekariri tu alivyokaririshwa
Hii ni Africa sio China, Africa ina historia ya Soko huria tangu karne na karne kabla wajamaa uchwara hawajatuvuruga baada ya kupata Uhuru.

Hata Machifu wa Africa zamani hawakuwahi kujaribu kupandikiza mfumo wa ujamaa. Kila mtu alikuwa na mali zake, shamba lake, biashara zake na Chifu alikuwa anatoza ushuru tu.
55d072bb92f3421d804a011002a67b88.jpeg
Screenshot_20220912-235215.jpg
Screenshot_20220912-235240~2.jpg
Screenshot_20220912-235253.jpg
Screenshot_20220913-001217.jpg
Screenshot_20220913-001248.jpg
Screenshot_20220913-001309.jpg
Screenshot_20220913-001331.jpg

6a3giuvrl0f71.png

Jifunzeni kwa walio fanikiwa na ninyi mfanikiwe kama wao.

N.b: Asiye sikia la mkuu huvunjika guu.
 
Back
Top Bottom