Ukweli mchungu: Kikwete family ni Royal Family watatutawala milele

Ukweli mchungu: Kikwete family ni Royal Family watatutawala milele

Ngoja nipate hela,hizo familia nitazisambaratisha hamtaamini.
Kwenye account tayari nina milioni 2 wajiandae
Hiyo hela mtoto wa January makamba ni mdogo sana yuko grade 6 anayo, alipewa ya kutumia... anaitwa "Jamal Makamba" anasoma HOPAC int.

Alikuja nayo pale Oasis (Mbezi beach) mwaka jana siku ya michezo akawa anatanulia na marafiki zake.

Ndo ukashindane na babu zake... hehehe!

#TAFAKARI
 
yule mzee Msoga ni nguli kwenye siasa.

wakati Amani Karume anamaliza muda wake, zanzibar ilitaka kupasuka,yaliibuka makundi matatu makubwa yanayotaka kila mmoja mtu wao awe Rais wa Zanzibar.
moja la Shamsi Vuai Nahodha.
lingine la Dr.Ghalib Bilal.
lingine la wapemba wa CCM nao wamechachamaa kwanini Pemba aijawai kutoa Rais Zanzibar?
wakati huo Maalim yuko moto anawalia timing wapasuke apite kati.

Mzee Msoga akawachezeshea draft moja matata sana.
Dr.Shein(mpemba)akapelekwa kugombea Urais Zanzibar,alafu Dr.Gharib akachukua nafasi ya umakamo wa Rais bara.Shamsi Vuai akasuburi Shein awe Rais ili ateuliwe waziri kiongozi Zanzibar hapo kwisha habari,mzee Msoga akawaweza wote na wakatulia.
Unafikiri ni yeye ndio aliamua!!?

Kama ni yeye ndio aliamua angeamua na huku 2015,huo mchezo wa state yeye akiratibu maelekezo kama KWA Lowasa alivochomolewa 2015!
 
Kikwete ana kitu ambacho wanasiasa Wengi Sana hawana...Labda Kidogo Nyerere....Ana gift moja very unique..
"Anapenda watu genuinely"..
Kikwete anapenda watu na anapendwa na watu..

Lowassa anapendwa na watu pengine kuliko JK lakini Lowassa "hapendi "watu kama JK...

Kikwete anakumbuka watu majina hata kama ni mkulima Tu au bodaboda....
Kipaji hiko cha Kikwete anacho Bill Clinton.... Tanzania sijaona mwenye kipaji hiko mwingine...hao kina Riziwan na January hawana hiko kipaji...
Kingine Kikwete anajua Sana nini cha kuongea....mtoto wa mjini halisi...
Huwezi sikia karopoka kitu bahati mbaya...anajua exactly nini aongee na nini asiongee hiki ndo kipaji alichokosa JPM...

Katika Marais wa Tz..Hadi sasa Kikwete ndo kawa "natural president"..
Bila kuhitaji vyombo vya dola ...anaheshimika na kusikilizwa ndani na nje bila kuwa "official president"..
Tujiulize mbona Mkapa hakuweza?Mwinyi mbona hakuweza?

Kikwete mtoto wa mjini ...the most successful one politically...ever
Ndio umesema ukweli mzee kwenye kumbukumbu na kupenda watu yuko njema sana.
Kikwete alipotezana na rafiki yake wakiwa vijana wadogo,Kikwete alipokua anatoka kwenye ghafla flani uwanja wa CCM Kirumba Mwanza kipindi akiwa Rais,akamuona rafiki yake wa kitambo sana kwa jina akifahamika kama Comred M.Bisanga akiwa na raia wengine wamesimama pembezoni mwa barabara kushangaa msafara wa Rais.

mzee Msoga akamuona rafiki yake bwana Bisanga anayeelekea uzee.alisimamisha msafara akashuka na kwenda kumsalimia rafiki yake,Comred Bisanga anamuuliza Kikwete umewezaje kunikumbuka!?
 
Unafikiri ni yeye ndio aliamua!!?

Kama ni yeye ndio aliamua angeamua na huku 2015,huo mchezo wa state yeye akiratibu maelekezo kama KWA Lowasa alivochomolewa 2015!
Bado alichanga karata zake vizuri kumuweka magufuli,unadhani angemuweka nani,lowassa alikuwa amechafuka,Membe ingekuwa ngumu kumnadi walishasema ni ndugu yake,JPM ilikuwa chaguo sahihi kwa muda ule
 
Unafikiri ni yeye ndio aliamua!!?

Kama ni yeye ndio aliamua angeamua na huku 2015,huo mchezo wa state yeye akiratibu maelekezo kama KWA Lowasa alivochomolewa 2015!
vyovyote itakavyokua lakini yeye ndo alikua mwenyekiti wa chama na Rais,yani mkuu wa nchi.nguvu za hao wazanzibari wenye makundi kwa Kikwete walikua wepesi kama karatasi ndo maana aliweza kufanya na wakatulia.

issue ya 2015 iliwahusu boyz Ii men wote walikua deep state,nguvu sawa za ushawishi ndani ya serikali na chama.
ndio maana upande wa mzee mamvi walipoona mzee wao kautupwa nje nao wakamchinja jasusi mbobezi chaguo la mwenyekiti.
 
Mkuu somesha watoto na wajukuu acha kulalama na kulia wivu, ndio suluhisho la kumkomboa mtu kutoka katika umaskini.
Kauli ya kijima nq kijinga sana hii. Unataka kusema nchi nzima hii waliosoma ni watoto wa hizi familia pekee?

Mleta mada ana hoja, basi mjibu kwa hoja. Acha kurusha maneno hewani kama mvua ya mawe.
 
Huo ni uoga wako tu,mtoto mmoja wa kikwete kuwa mwanasiasa haimaanishi ndo kututawala milele,ni kawaida mtoto kuvutiwa na kazi ya babaake.wakina George bush au Akina Adam Jones kuwa Marais wa marekani baba na mtoto sio kwamba ndo kuitawala Marekani milele.clinton na mkewe hawajaitawala USA milele.Hata mwinyi na mwanae vipindi vyao vitapita watakuja wengine.Kusema watoto wengine ni marubani,madaktari etc ni fikra potofu kwanza Kuna familia nyingi za kawaida zenye watu wenye hzo professional sembuse familia ya Rais.
Wewe Hata hujui dunia inavyozunguka kabisa,,wewe na Mimi tuendelee kulimia mahindi tu
 
Hawa wameshakuwa mfumo, si rahisi kuendesha kampuni bila wao. Only person angeweza kuwarudisha kwenye mstari ni EL ambaye nae vurugu zao ndio zimemdhoofisha.

Hawa hata wapinzani wetu wapo mfukoni mwao achilia mbali tawala. Kazi sana

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Wanalolitaka katika ulingo wa siasa linakua,huwezi kushindana nao
 
1670465969871.jpg
 
Sidhani kama JAMUHURI imeamua hatma ya nchi itegemee hao PEKEE!

Jamuhuri ni complex individual haizoeleki!

Leo itakutumia vizuri kufanikisha operation fulani kesho itasema inatosha Sasa, infulence YAKO KWA kampuni ni kubwa Sana hatutaki jina lako liimbwe Sana kuliko jamuhuri!

Ni hatari Sana jina likavuma kuliko JAMUHURI, jamuhuri haipendi kudogoshwa kama KIPINDI kile, ndio maana hayati Mkapa alimwambia jpm kuwa tunataka kusikia serikali imefanya hivi na vile sio jina lako!!!

Jamhuri haidogoshwi KWA umaarufu wa majina FULANI ndio maana vijana wa NYERERE hawana majina hadi leo!hata Hawa wanaovuma sidhani kama JAMUHURI itavumilia majina yao kwenye hatma ya NCHI YETU!

"NIMEJIFUNZA HAYO,I STAND TO BE CORRECTED"
101 % truth
 
vyovyote itakavyokua lakini yeye ndo alikua mwenyekiti wa chama na Rais,yani mkuu wa nchi.nguvu za hao wazanzibari wenye makundi kwa Kikwete walikua wepesi kama karatasi ndo maana aliweza kufanya na wakatulia.

issue ya 2015 iliwahusu boyz Ii men wote walikua deep state,nguvu sawa za ushawishi ndani ya serikali na chama.
ndio maana upande wa mzee mamvi walipoona mzee wao kautupwa nje nao wakamchinja jasusi mbobezi chaguo la mwenyekiti.
Ndivyo ilivyokuwa !!
 
Kauli ya kijima nq kijinga sana hii. Unataka kusema nchi nzima hii waliosoma ni watoto wa hizi familia pekee?

Mleta mada ana hoja, basi mjibu kwa hoja. Acha kurusha maneno hewani kama mvua ya mawe.
Punguza povu kaka, hao kina Kikwete wamejaa dunia nzima. Hakuna nchi unayoweza kwenda ukawakosa.

Ni familia maarufu na damu huwa nzito kuliko maji, Baba akiwa rais anajiona ana deni kama mwanae hawezi kuwa na cheo fulani, haya ni mambo ya kawaida kabisa.

Kina Kennedy na kina Rockefeller Marekani. Hakuna nchi utakwenda usikutane na familia za aina hii..

Ni kumkumbusha tu mleta mada atafute cha kwake wa jasho, hakuna anachoweza kufanya kuzuia neema ya hao kina JK.
 
Babu yake alikuwa Akida sijui Liwali kwenye serikali ya kikoloni.

Baba yake akawa DC kwenye serikali ya Nyerere.

Mtoto mtu akawa Rais,na bado ana ushawishi.

Mke wake ni mbunge.

Mtoto ni naibu waziri na bado umri wake ni mdogo unamruhusu kupambana.

Bado anawatoto wengine wanakua, wengine ni madaktari wengine marubani nk. Ridhwani angeweza kufanya kazi BOT au State Atorneys Office ila akaamua kuongia kwenye siasa ili atutawale.

Ili kufanikisha hili kuna familia tano zimejiunga pamoja,Kikwete Family,Makamba Family,Nnauye Family,Kinana Family,chini ya master mind Rostam Aziz.bila kusahau familia ya mzee Mwinyi. Hakuna kikundi au mtu mmoja mmoja anayeweza kuwashinda hawa ex soldiers

Bila Mzee Nnauye, Makamba angekuwa anauza mapeasi Lushoto, January Makamba angekuwa anaendesha Fuso.

Bila JK, Nape angekuwa anaendesha bodaboda.

Bila mzee Ruksa JK angekuwa analima mananasi Bagamoyo

Hii ni Family moja tusipoteze muda kushindana nayo bali tuishi nao kwa akili .

Kwani we hupendi asali

Basi tulia ulambe asali kimyakimya
Aiseee
 
Mwanangu kweli we ni mdukizi haswaaa umenifumbua akili kwa kuongezea nyama kidogo ni hivi sio tu family hizo ongeza kuwa CCM yote nayo ni Jakaya family hata tuneng'eneke vipi kuitoa madarakani sisi watz ni kibarua kugumu hatutaweza labda Mungu aingilie kati maana wao ndo wnajua nchi ilivyo tamu na kwa kifahamu hilo wamejiwekea mtandao wao kote angalia hawa viongozi wakubwa wa kuteuliwa na rais kama vile wakuu wa mikoa, wilaya, wakurugenzi wa halmashauri na manispaa mpka majiji, makatibu wakuu na manaibu, hawa wote ukichunguza ni makada lialia na kindakindaki wa ccm kama sio mwanaccm hupati teuzi hizi

kwaiyo jmn tujiandae kisaikolojia kutawaliwa na hawa kijani milele mi hamna kitu kinanikatisha tamaa kama vyama vingine vya nchi jirani vingi vilivyo kuwa vinaongoza nchi zao kabla ya kupata uhuru wao mpka sasa vilishatolewa madarakani na wapinzani ila kwa ccm ni tofauti tena vinakuja na kujifunza mbinu ovu na chafu za kuendelea kubaki madarakani ama kuingia tena madarakani sasa we fikiria kama tu vyama vingine vya nchi zingine vina kuja kujifunza yaani kupata mbinu ya kutawala nchi zao unadhani ccm itakuwa lahisi kuing'oa madarakani!??

Ndio maana katiba mpya hamna mtu kati ya ccm mwenye shida nayo maana kwanza hawaitaki kwa kuwa inakuja kuwanyima baadhi ya fursa ma mamlaka kama rais kuounguziwa mamlaka hasa ya kuteua teua na kushutakiwa kwa makosa aliyayafanya akiwa madarakani yaani akiwa anatawala ama kuongoza nk.

Kama tutatulia tu hata miaka mingine 100 itaisha bila katiba mpya hata ikipatikana hawataifuata wataivunja tu kama hii iliyopo tena waliyotunga wao ccm wenyewe siku izi wanaivunja mfano wa mambo waliyowahi kuvunja katiba ni kukataza mkutano ya vyama vua siasa katiba inaruhusu hiyo mikutano ila wao walikataza ni nani alibisha wanamuelewa!?? Ikija mpya ndo kabisaa maana itawabana na kuwanyima uhuru walio uzoea.. Mazoea hujenga tabia na tabia ni kama ngozi huwezi ibadili kirahisi hivo.. Ngoja niishiw hapa nisijw kuwavuruga bure wakat hapo mlipo mumeshavurugwa na January [emoji848][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom