Ni hivi watu wengi wanaandika bila kuujua ukweli.
Ukweli ni kwamba kabla ya mradi wowote mkubwa kutekelezwa lazima kifanyike kitu kinachoitwa Environment Impact Assessment.
Ukweli ni kwamba serikali iliunda team iliyojumuisha maprofesa nguli kufanya Environment Impact Assessment ambapo serikali yetu iliwalipa fedha kufanya kazi hiyo.
Ukweli ni kwamba team hiyo ilifanya kazi hiyo na kuandika ripoti yake ambayo ilieleza kwamba madhara ya kwnye mazingira kama mradi huu ukitekelezwa yatakuwa makubwa sana hivyo wakashauri mradi huu usitekelezwe na wakashauri serikali ijikite kwenye kuzalisha umeme kwa kutumia gesi ambayo inapatikana mtwara kwani uzalishaji wa umeme kwa kutumia umeme hautakuwa na madhara kwenye mazingira kama mradi wa stiglers gorge.
Sasa bana ripoti hii iliwasilishwa kwanza wizara inayohusika na mazingira ya bwana January.
Waziri akakubaliana na ripoti naye akaifoadi ikulu.
Bwana kolichotokea almanusura huyu jamaa apoteze kazi, .
Ukweli ni kwamba jiwe alimuita akamtukana sana kwanini amekubaliana na ushauri wa hao maprofesa na kisha akamtupia ripoti yake .
Isingekuwa aibu ya jiwe akifahamu jinsi January alivyomfanyia figisufigisu ya kutengeneza matokeo yaliyomsaidia kumuweka madarakani pale mlimani city huyu january alikuwa afukuziwe mbali.
Sasa twende kwenye hoja, kwa nini serikali yetu inakataa repoti ya timu ya iliyoiunda na kuilipa ifanye kazi na wao wakafanya na wakashauri.
Mbona Serikali hiii hii haitoi vibali vya kuendeleza miradi ambayo environment impact assessment zimeshauri kwamb arhari za mradi ni hasi.
Kuna msemo wa kiingereza unaoheshimika sana unaosema "no research no right to speak"
Research imefanyika imeeleza mradi ni mbaya kwenye mazingira watu bila hata kufanya research nyingine wanakurupuka kuukataa ushauri wa wataalamu.
Tusiwalaumu sijui bunge la ujerumani , mimi binafsi siungi mkono kupangiwa mambo yetu na hao wajerunani.
Ukweli ni kwamba mradi huu ulikataliwa kwanza na timu yetu sisi wenyewe watanzania iliyohusisha maprofesa wataalamu ambao mwisho wa siku kama kawaida ya jiwe ukitoa mapendekezo tofauti na mtazamo wake unaitwa sio mzalendo au sijui umetumwa na mabepari.
Aina hii ya uongozi ya kukataa mapendekezo ya wataalamu ni mojawapo ya element za utawala wa kidikteta.
Mkuu naona unatwaga maji kwenye kinu,Hilo bwawa la umeme litajengwa hakuna wa kulizuia.
Hivi mkuu kama kweli uliiona shule ya ukweli yenye mashiko,nakuuliza umeme utokanao na Stigler Gorge ni faida ya nani?Kwanini tunapenda kudhohofisha juhudi za kupata umeme rahisi?
Miaka ya mwanzoni ya 80, nchi rafiki za Scandinavia Sweden na Norway baada ya kufanya utafiti wa kina kwa muda mrefu iliojulikana kama RUBADA walitoa financial plan namna ya kuzalisha umeme kutoka Stiglers Gorge.Wakimtaka Mwl.Nyerere ajenge bwawa la kufua umeme mara mmoja kwenye mto Rufiji.
Mwalimu Nyerere ilibidi kuhalisha mradi huo kwa sababu za ukwasi.Tanzania ilikuwa imetoka kupigana na Uganda katika vita vya Kagera.Wakati huo Mwalimu alikuwa amaishafanikiwa kujenga mabwawa ya kufua umeme ya Kidatu, na baadae Mtera, na Kihansi.
Je tafiti zilizofanywa na hao Scandinavia wenye uzoefu na utaalamu Hydro electric power plants hazina maana tena?
Mkuu hakuna mradi utakuwa 100% kulinda enviroment.Hata hiyo gesi asilia ni mbaya zaidi kwa mazingira kuliko umeme wa hydro
Katika kuchimba hiyo gesi zipo sintafahamu nyingi zinazoharibu mazingira.
Mkuu umesahau majanga makubwa (oil spill)yaliotokea huko gulf of Mexico Apri 2010 Macondo field, katika Deep Water Horizon rig mradi wa BP na kusababisha kuvuja kwa mafuta ghafi zaidi ya miezi 4 baharini kabla ya kufauru kuziba kisima?Yalivuja mapipa 4.9 milioni baharini,kusabisha vifo vya watu 17,na zaidi viumbe 8000.uharibifu mkubwa wa beach.
Labda una apetite ya kuona tunatumia gesi asilia katika kufua umeme,lakini kwa mtaji gani,wakati hao watawala wameishauzia vitalo vya gesi kwa wageni?Hatuna chetu,ni gharama kubwa kwetu kununua hiyo gesi.
Open your eyes mkuu,wanaotaka tutumie gesi katika mazingira haya,ni hatari kama IPTL,na Songas.