Mimi nimeosoma ripoti ya WWF kuhusu mradi huu, kama katiba tuu imeweza kukanyangwa na tuko ok kabisa, what is EIA compared?.
Kwenye hili mimi naungana na serikali yetu kuwa Tanzania is a sovereign state, tutaamua mambo yetu wenyewe bila kuingiliwa au kupangiwa na mataifa ya nje.
Natolea mfano wa mradi wa Kamba Samaki, shrimp farming kwenye Rufiji Delta, ulipitishwa vizuri tuu, lakini kabla ya utekelezaji, mashirika ya kimataifa ya mazingira yakaja na EIA nyingine, tukapigwa stop mradi ukafa. Hoja ya wanamazingira ni kilimo kile kingeathiri uoto wa asili wa mikoko.
Ukiangalia cost benefits na value benefits za mradi na faida za mikoko, mikoko are nothing compared.
Kama ulifuatilia issue ya Kihansi Hydro Electric Project, mradi ulichelewa sana kwa hoja ya vyura wa Kihansi hadi Marekani walipokubali kuwa relocate wakahamishwa, mradi ulipokamilika wakarudishwa. Ukiangalia faida za nchi inayohitaji umeme na faida ya vyura ni nothing compared.
Sasa kwenye Stieglers ni vile vile wanataka kutupangia, kule nyuma waliweza kwa sababu fedha walikuwa wanatoa wao. Kwa Stieglers, watakwama kwa sababu this time around fedha ni zetu.
Hili jambo niliisha lizungumza sana humu
Uzalendo wa kweli wa nchi yako ni pamoja na kusupport mipango kamambe
ya maendeleo ya nchi yako hata kama mipango hiyo itasababisha maumivu kwa walio wengi as long as itakuwa na faida kubwa kitaifa huko baadae.P
Kwahiyo Pascal unaamini kabisa ecomical impact ya mradi wa umeme kupitia Stiegler's Gorge ni kubwa zaidi kuliko mradi wa umeme kupitia gas ambayo tayari taifa limeshaingia gharama ya karibu shilingi tyrilioni moja kujenga bomba ambalo completely lipo underutilized?
Na hapa napenda nirudie tena hapa kama nilivyosema jana na kuku-tag! Kuwa Sovereign State hakumaanishi kuwa na mamlaka ya kufanya hata irrational decision!! KWA MAKUSUDI!! Huwezi kufanya jambo ambalo kitaalamu linaonesha lina madhara halafu ukajificha kwenye hoja ya kwamba, you're soverign state!!
Halafu unapenda sana kutolea mfano wa mradi wa kamba wa Delta ya Mto Rufiji! Hivi ni kweli Pasco hufahamu madhara ya kuivuruga delta?! Hivi ni kweli hufahamu umuhimu wa mikoko kwa mtu kama wewe uliyekulia Dar es salaam?! Halafu hivi una habari ule mradi ulikuwa within Reserved Marine Parks?!
Serious?! Yaani unaamini ilikuwa sawa tu kufyeka mikoko kwa ajili ya mashamba ya kuzalisha kamba; mradi ambao ungefanyika kwenye 19,000 hectares, na kui-expose nchi kavu na bahari?
Hebu soma hii taarifa:
Around half of 279,000 ha of Philippine mangroves lost from 1951-1988 were developed into aquaculture ponds, with 95% of Philippine brackish water ponds in 1952-1987 being derived from mangroves (Primavera 1995).
Baada ya kuharibu sana mikoko kwa muda wote huo na kuanza kutandikwa na vimbunga vya baharini visivyoisha, soma tena
hapa:
The Philippines said Sunday it will plant more mangrove areas to prevent a repeat of the deadly storm surges that claimed hundreds of lives during Super Typhoon Haiyan earlier this month.
Mikoko ambayo waliiharibu wenyewe, baadae wanakuja kusumbua
Umoja wa Mataifa,
Aid agencies, led by the UN, are helping to diversify incomes, as well as highlighting how sustainability can help alleviate natural disaster. Progress has been made, for example, on the restoration of coastal mangroves that will, come the next big typhoon, act as a crucial buffer.
Kuna mahali hapo juu unadai mikoko ambayo ingefyekwa pale Rufiji ingekuwa ni nothing compared na mihela ambayo tungeipata kwenye mradi ule... SERIOUS?! Hivi pesa ambazo Ufilipino imeingiza kwenye hiyo miradi zinafika hata robo ya madhara wanayopata almost kila mwaka?!
Nchi za Asia na South East Asia ziliharibu sana mikoko, na moja ya sababu zilizochangia uharibifu wa mikoko ni kilimo cha kamba! Matokeo yake, leo hii ndo wanashituka na ukanda mzima wa South East Asia wameanzisha the so called
Mangrove For Future (MFF)! What's MFF?!
Background yao wanasema:
The devastation caused by the Indian Ocean tsunami of December 2004 laid bare the vital link between coastal ecosystems and human livelihoods. It was United States President Bill Clinton’s vision that rebuilding in tsunami-hit areas should improve natural infrastructure and strengthen resilience against future natural disasters. In response to this vision, IUCN (International Union for Conservation of Nature) and the United Nations Development Programme (UNDP) developed Mangroves for the Future in 2006. Since then, MFF has grown to include eight institutional partners, plus a growing number of countries. At the launch of the Tsunami Legacy report* at the United Nations in New York in April 2009, Bill Clinton acclaimed MFF as one of the most positive and forward-looking developments of the post-tsunami period.
Hiyo ndiyo mikoko ambayo wewe unaona "mabeberu" waliingilia sovereignty yetu na kutuzuia tusifanye mchezo na mikoko!
Tena basi Bonde la Mto Rufiji linatumika sana kwa kilimo! Fanya assignment mwenyewe uone ni namna gani mashamba ya uzalishaji wa kamba yanavyotumia antibiotics na ma-chemical!
Sasa umeshawahi kujiuliza udongo kwenye Bonde la Mto Rufiji ungekuwa na hali gani na wakulima wangekuwa na hali gani?!
Anyway, wawekezaji wa ule mradi wa Rufiji Delta walituambia mradi ungezalisha USD 500 Million in terms of export!!! Je, leo hii watetezi wao wanaweza kutuambia mradi kama huo kule Jimbo, Mafia ulio chini ya Alphakrust unazalisha mabilioni mangapi?!