omunatta
JF-Expert Member
- Jun 11, 2015
- 236
- 139
Naungana na mtoa mada inawezekana kabisa ni kweli, nakumbuka siku tunazindua mfugale bridge pale tazara rais alisema tena kwa hasira kabisa kuna watu wanajiita wasomi wamekuja na mapendekezo ya hovyo. I remember this statement
Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona hujaweka ukweli mkuu, hiyo ripoti ulishaiona wewe au unasikiasikia tu kama hao wasiojua? Nimesoma bandiko lote, lakini hata wewe naona unasikiasikia tu kuhusu hiyo ripoti.
Sikubaliani na Magufuli kama kaamua tu yeye mwenyewe kama kawaida yake ya kutumia mabavu. Lakini hata kama hiyo ripoti ipo kweli na hao wataalam waliona madhara ya mradi huo, lingekuwa jambo zuri kuitoa hiyo ripoti watu waisome na kuijadili. Bado Magufuli angekuwa na uwezo wa kushawishi ripoti iwekwe pembeni kwa sababu anazoona ni za lazima mradi ufanyike kwa manufaa ya taifa. Na mimi ningekuwa mmojawapo wa kuunga mkono hatua hiyo, kwa sababu naamini mradi huo una manufaa makubwa kwa taifa, na hizo sababu za uharibifu wa mazingira athiri yake ingeweza kupunguzwa katika 'design' ya mrada wenyewe.
Kwa hiyo taarifa yako hapa bado ni 'hearsay', na hasa ukifikiria Magufuli kaingia 2015, hiyo 'study' ya wataalam hao iliteuliwa na nani, lini na ilifanya kazi kwa muda gani. Je hata magazeti hayakuweza kutoa habari yoyote juu ya utafiti huo ukatuwekea hapa tusome? Hata majina tu ya waliohusika katika utafiti huo.
Ni akina nani hawa maprofesa, una jina hata la mmoja wao? Ni nani aliyewateua na lini?
Kamati na ripoti unayoiandika hapa iliteuliwa na kufanya utafiti wake" baada ya Magufuli kutaka bwawa lijengwe" au kamati hiyo iliteuliwa kabla na kuandika ripoti yake kabla ya kutangazwa na Magufuli kuhitaji mradi huo ufanyike?
Mimi sioni kumbukumbu za uteuzi wa kamati wakati Magufuli alipotangaza nia ya ujenzi wa mradi huo. Kama wewe unazo kumbukumbu hizo tuwekee hapa tuzione.
Sent using Jamii Forums mobile app