Ukweli mchungu kuhusiana na mradi wa Stiegler's Gorge

Naunga mkono msimamo wa Serikali. Moja, gesi itaisha baada ya muda. Maji hupungua tu kutokana na ukame. Lakini baada ya muda hurudi kwenye kiwango chake.
Mbili, kuwepo kwa bwawa hilo kutasababisha ajira nyingi tu. Samaki watakaokuwepo humo watavuliwa na watu watauza na kujiingizia kipato kama ilivyo kwa bwawa la Mtera.
Wanaowaunga mkono wazungu wakumbuke kuwa akina Trump wamekataa kusaini mkataba wa kutunza mazingira ili kupunguza hewa ya ukaa kwa sababu tu ya kulinda viwanda vyao. Mbona hao wazungu hawawaazimii watu kama akina Trump.
 
Kumbuka msukuma hana kitu kinachoitwa kutunza mazingira. Miti na uoto asili sio issue kwake.
Labda kutunza ng'ombe.

Mimi ndukiiiiii....

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawa wazungu wachelewi kusema.waafrica wa wasizaliane tena wanaharibu mzngr na baba kashawawahi amekataa u,azi wa mpangl safari hii lawashika.kila kona
 
Unaambiwa wale partners wa arab-contractors baada ya kusaini mkataba wachukua wameweka mkataba ( guarantee) bank wamekopa hela kwa ajili ya miradi mingine ya pembeni
 

BWANA mdogo ebu sikia. siku nyingine unavyokuja na scientific based thread come with both theoretical and empirical evidence. sisi wengine hatupendi kuongelea vitu toka hewani.

kwa UELEWA wako kati ya umeme wa gesi (CEP) na maji (HEP) ipi ina madhara makubwa kwa mazingira ya eneo husika na dunia kwa ujumla??

kajipange uje tena.
 
Nawao wapunguze viwanda vyao kwanza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jaribuni kuwashauri nawao wafunge viwanda pia wapunguze kutengeneza magari kwakuwa vinachafua mazingira pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaambiwa wale partners wa arab-contractors baada ya kusaini mkataba wachukua wameweka mkataba ( guarantee) bank wamekopa hela kwa ajili ya miradi mingine ya pembeni

hizo sasa ni stori za vijiwe vya gahawa. wewe unajua what's a project finance?
yaani utumie contract (commercial closure) ya project hii kuingia contract (financial closure) ya ku finance project nyingine?

acheni kuzusha UJINGA. kuna benki or financier kweli atakubali negligence hiyo yenye very high potential financial risk.
 
Hii ni JF dogo hapa hakuna taarifa ya kizushi, IPO siku utaujua ukweli
 
Kupanga ni kuchagua. Kwa sasa tunahitaji umeme sana kutokana na sera za viwanda umeme wa maji ni cheap kuliko wa gas.

..anayetegemea umeme wa maji wakati mwingine hana tofauti na mkulima anayetegemea mvua.

..kwa miaka mingi Tz tumekuwa tukitegemea umeme wa maji na nadhani unajua madhara ya utegemezi huo.

..mito yetu ina changamoto nyingi. Kuna uharibifu ktk vyanzo vya mito. Kuna changamoto ya mabonde ya mito kuelemewa na shughuli za kilimo na ufugaji.

..hoja kwamba umeme wa maji ni wa bei rahisi kuliko wa gesi wakati mwingine haizingatii uhalisia wa eneo husika.

..tusikilize hoja za pande zote bila kuitana majina, halafu ndiyo tufanye maamuzi.
 
Mkuu naona unatwaga maji kwenye kinu,Hilo bwawa la umeme litajengwa hakuna wa kulizuia.
Hivi mkuu kama kweli uliiona shule ya ukweli yenye mashiko,nakuuliza umeme utokanao na Stigler Gorge ni faida ya nani?Kwanini tunapenda kudhohofisha juhudi za kupata umeme rahisi?

Miaka ya mwanzoni ya 80, nchi rafiki za Scandinavia Sweden na Norway baada ya kufanya utafiti wa kina kwa muda mrefu iliojulikana kama RUBADA walitoa financial plan namna ya kuzalisha umeme kutoka Stiglers Gorge.Wakimtaka Mwl.Nyerere ajenge bwawa la kufua umeme mara mmoja kwenye mto Rufiji.
Mwalimu Nyerere ilibidi kuhalisha mradi huo kwa sababu za ukwasi.Tanzania ilikuwa imetoka kupigana na Uganda katika vita vya Kagera.Wakati huo Mwalimu alikuwa amaishafanikiwa kujenga mabwawa ya kufua umeme ya Kidatu, na baadae Mtera, na Kihansi.

Je tafiti zilizofanywa na hao Scandinavia wenye uzoefu na utaalamu Hydro electric power plants hazina maana tena?
Mkuu hakuna mradi utakuwa 100% kulinda enviroment.Hata hiyo gesi asilia ni mbaya zaidi kwa mazingira kuliko umeme wa hydro
Katika kuchimba hiyo gesi zipo sintafahamu nyingi zinazoharibu mazingira.
Mkuu umesahau majanga makubwa (oil spill)yaliotokea huko gulf of Mexico Apri 2010 Macondo field, katika Deep Water Horizon rig mradi wa BP na kusababisha kuvuja kwa mafuta ghafi zaidi ya miezi 4 baharini kabla ya kufauru kuziba kisima?Yalivuja mapipa 4.9 milioni baharini,kusabisha vifo vya watu 17,na zaidi viumbe 8000.uharibifu mkubwa wa beach.

Labda una apetite ya kuona tunatumia gesi asilia katika kufua umeme,lakini kwa mtaji gani,wakati hao watawala wameishauzia vitalo vya gesi kwa wageni?Hatuna chetu,ni gharama kubwa kwetu kununua hiyo gesi.
Open your eyes mkuu,wanaotaka tutumie gesi katika mazingira haya,ni hatari kama IPTL,na Songas.
 
kwani ile.mradi wa gesi, kinyerezi phase I, Phase II na Phase III, tuliambiwa ni mwarobaini wa tatizo la umeme umefia wapi??

tuliambiwa utazalisha megawati zaidi ya 10,000 na umeme wa ziada tutauzia Rwanda na Uganda.

ccm wapuuzi sana.
 
Report ipo na serikali imegoma kuiweka public. Alichosema jamaa ni kweli kabisa. Hoja ya kwamba Magu kaingia 2015, unahisi EIA inafanyika miaka mingapi?? Inventory za hifadhi zilishafanyika miaka mingi tu, kwa hiyo EIA haiwezi chukua muda mrefu, mwaka mmoja unatosha kabisa kwasababu hayo maeneo sio mapya, taarifa za maeneo hayo zipo nyingi mno. Kinachofanyika ni kulinganisha kinachofanywa na impact yake kwa vilivyopo. Chakubishana hapa ni nini faida na hasara za mradi? Kama faida ni kubwa it's well and good.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Faida ingekuwa ni kubwa, ninahakika hiyo report ingewekwa wazi na serikali.
 
Well said...
 
Sasa faida ipo wapi kuunda timu ya kufanya tafiti na kulipwa pesa pia lakini bado utafiti wao hauchukiliwi maanani, serikali mnatuma timu kumbe kichwani mnamajibu yenu, hili taifa haliwapi wasomi fursa hakuna ushauri unaotumika wapo maprofesa wenye elimu ya juu na utalamu mwingi sana lakini hawatumiki vilivyo, pamoja na elimu tunayoipata huwa tunaipata katika mazingara magumu bado inakua ni sawa sawa na bure

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hudhani kama yatakosekana, si uyaweke wazi? acheni kushangilia ujinga wa wazungu, msidhani wanawapenda sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu,
Aisee umenikumbusha Mali sana kwenye ule mradi was Shrimp farming na kapteni wetu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…