Ukweli Mchungu: Marekani ni nchi ya dunia ya tatu

USA haiwezi kuwa third world country.

North Korea hakuna uhuru wa mwananchi. China yenyewe Ina limited freedom.

Marekani sasahivi ndo nchi pekee duniani ambayo imeivuka kizingiti cha recession, ajira kama zote ( kutokana na ripoti kibao zilizotoka kama NFP, Unemployed claims n.k) na inflation rate imeshuka 3%. Na pia production rate ya kuridhisha .

Tanzania hii kuna amani tele ila umaskini wa ajabu, biashara zimekuwa ngumu, money circulation imehamia kwenye real estate na huku mtaani hakuna money circulation ya uhakika mtaani, pia tunasuffer from inflation.
 
Bro!! Uwanda wako wa kujua Mambo ni mdogo sana, ni kweli USA, kuna watu kuuana sana kwa silaha, na huku Afrika, hususani TZ, kuna watu kuchunwa ngozi, mauji ya albino, nk.
Kampuni moja ya Apple ina pesa nyingi, mapato kuliko mapato yote ya TZ!
Ukwasi wa mtu mmoja USA ni mara Mia ya mtu wa Afrika, hii internet system unayotumia ilianzia ndani ya jeshi LA USA.
Niliwahi kufanya kazi tassisi moja kubwa ya Mambo ya ukimwi, unakuta unalipwa Milioni 4+, we unaona ni mpunga mreeefu! K wao ni pesa, ya kawaida sana!
Nchi yenye tekunolojia kubwa, ya anga, siraha, kilimo, ulinzi, ina makambi ya jeshi kila Kona ya dunia, unasemaje ni nchi ya ulimwengu wa tatu! Unailinganisha na bongo yenye uhaba wa madakitari na waalimu lakini haiwezi kuwaajili kwa sababu pesa na mapato hayatoshi?
Kuhusu usalama! Pita kawe usiku stend ya daladala! Au katiza eneo LA feza school,! Kituo cha police kipo km 1 tu! Utaomba ardhi ipasuke! Nilikoswa koswa, kupigwa nondo ya kichwa!
Jiwe likanipata usoni,uzuri nipo athletic, nilikimbia damu inavuja! Kufika polisi wananiuliza du bro pole sana! Hiyo ndio kawe!
 
Siasa za CCM zimeharibu akili ya watanzania wengi. Utasikia jeshi letu ni la sita kwa ubora duniani, jengo jipya la posta (Arusha) ni la sita pia kwa ubora duniani. Sasa nashangaa kusikia Marekani ni third world country na haina teknolojia[emoji16]

Sent from my M2006C3MG using JamiiForums mobile app
 

Ni vituko kaka huku hapo anaomba apate visa afike kiwanja 🤣
 
Nakuhakikishia siku ukipelekwa Moscow, Beijing, Tehran, Riyadh au Pyongyang ukapewa kazi nzuri ya Ofisini unayolipwa mshahara mara mbili wa huo wa kubeba box bado utalilia urudishwe States tu uendelee kubeba box.

Kwa mashoga
 

Ni vile hujawahi kuishi nchi za kiarabu n.k, nenda Emirates au oman, kwanza hutatamani kwenda nchi zinazokubali ushoga
 
Bila shaka wewe ni mvaa kobazi.........hata waarabu wenyewe huwa wanachomekea kanzu ili kwenda kujiachia kwenye nchi ileee

Ni nafsi ya mtu, ni kama wewe uchague kuishi nchi zinazounga mkono ushoga basi na waarabu kwenda kutembea kule
 
Haina noma, ila ndiyo Marekani sasa, ulitaka hao watu wa level ya dunia ya tatu wafukuzwe, waache wawemo ni kwa watu wa levels zote wala siyo ukweli mchungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…