LOTH HEMA
JF-Expert Member
- Dec 6, 2015
- 18,611
- 27,615
Sasa mbowe akiachia umiliki wa Chadema, mwanaJF Erythrocyte ataishi vipi au ndo itakuwa talaka hiyo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sasa mbowe akiachia umiliki wa Chadema, mwanaJF Erythrocyte ataishi vipi au ndo itakuwa talaka hiyo
tunataka mabadilikoYeyote atakaechaguliwa kihalali kwenye box la kura. Anaejua na kuamua nani anafaa ni mpiga kura.
acha upuuzi we dadaWewe.
Mabadiliko ndo muda wa kuyapambania..... Hamuwezi kuhubiri demokrasia na mkataka mambo nje ya debe..... Lissu aingie kwenye debe dhidi ya Mbowe.tunataka mabadiliko
Kwa kazi kubwa aliyoifanya ni wakati wake sahihi kuondoka.Huu ndio ukweli mchungu na pia mtakosa uhalali wa kumpinga. Samia au Mtawala mwingine yoyotw ataeamua kubadili katiba ili ajiongezee muda wa kubaki madarakani.
Mtapoteza uhalali wa kuhoji katiba hii mbovu tuliyonayo na hata madai ys tume huru nayo yatakuwa yamekufa kifo cha mende kwasababu ni lazima muwe mfano tena kwa vitendo wa kile ambacho kwa miaka mingi mmkekuwa mkikihubiri majukwaani.
Na pia iwapo uchaguzi ukifanywa kwa mizengwe, mtapoteza na uhalali wa kuhoji matokeo ya uchaguzi wowote zikiwemo chaguzi zilizopita na hata chaguzi zijazo ukiwemo uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Madhara yatakuwa ni mengi, mfano, mkiitisha maandamano, hata wale watu wachache waliokuwa wanajitokeza, hamtwaona tena na mengine mengi ikiwemo heshima ya viongozi wa chama kushuka katika jamiii na hata mbele ya watu wa mataifa mengine.
Busara ni Mbowe apumzike au uchaguzi ufanyike kwa haki na Lissu akuballi matokeo na aendelee kukitumikia chama. Tofauti na hapo, CHADEMA mtapoteza ushawishi kwa kiwango kikubwa mno na chama kitafifia kama CUF ya Lipumba.
Soma Pia:
Jambo lingine litalowamaliza ni endapo mtaendesha kampeni za chuki badala ya kampeni za hoja hasa zitazoonyesha wagombea wana mikakati gani ya kuleta mabadiliko yatayosaidia kuiondoa CCM madarakani na za kujisahihisha kwa mliokosea siki za nyuma.
- Tundu Lissu: Nimewasilisha kusudio la kugombea nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA
- Ratiba Kamili Ya Uchaguzi Wa CHADEMA Taifa
Mheshimiwa Mbowe, usipkuwa makini, kazi ulioifanya kwa miaka 20 na heshima uliyojijengea kwa moaka 20, vyote utaviharibu kwa uchaguzi wa siku moja tu.
Mheshimiwa Mbowe, ubaki kama mlezi wa CHADEMA na kama ni lazima hicho cheo kitambulike katika katiba ya chama, basi hii iwe ni agenda ya Lissu kwenye uchaguzi(kuingiza hiko kipengele kwenye katiba), agenda ambayo naamini pia italeta umoja zaidi katika chama. kipindi hiki chaguzi.
Nimemaliza, msiponielewa, ulimwengu utawafundisha na wakati huo mtakuwa teyari mmechelewa.
Na ni makamu mwenyekiti wa chama, Viongozi na wanachama waelekezwe umuhimu wa kutumia lugha za kuijenga chama na umoja kuliko kubomoa.Jamaa amesema kuwa lissu hafai, Elewa maana ya neno hafai. Tofautisha mtu hafai na simkubali.
Sasa kama hafai kwann yupo kwenye orodha ya wagombea?
Uko sahihi tunayashuhudia Rwanda kwa kagame, Uganda kwa museveni nkMadikteta huwa SIfa yao kuu nikutoamini hakuna mbadala wakushika nyadhifa zao, kama alivyo Mbowe.
Na akishinda?Mbowe hawezi kuwa Tena mwenyekiti chadema ilo analijua pia