Ukweli Mchungu: Rais Samia hupendwi na Wananchi wengi

Ukweli Mchungu: Rais Samia hupendwi na Wananchi wengi

Magufuli 05

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2023
Posts
1,433
Reaction score
2,791
Kuna sehemu wananchi umewakosea. Tafakari!

Toka uanze kazi ni mikoa 2 tu sijatembelea nayo ni Kagera na Kigoma. Mikoa mingine yote nimefika na kujaribu kufanya utafiti wa kawaida.

Hali ni mbaya, Siandiki kwa ubaya lakini ndiyo Hali halisi. Wengi wanakuongelea kwenye mtazamo hasi. Hata kwenye mikutano yako ya hadhara, wasaidizi wako wanatumia nguvu kubwa Sana kushawishi watu wajitokeze. Hii si ishara nzuri kwa kiongozi hasa wa level yako.

Niandikaye hapa ni mmoja wa watu tunaopita vijiweni Hadi vijijini. Tunakutana na watu wa kila aina na makundi tofauti na tunabadilishana mawazo. Na huwa hatuachi kuzungumzia viongozi wetu na msitakabali wa nchi yetu. Kwani Tanzania ndiyo mama yetu wa uraia.

Hali ni mbaya. Hali ni mbayaaaa!
Ndugu zetu walio vijijini wengine hata kisomo ni cha Chini lakini kila tukizungumza kwenye simu wanatuuliza " eti tunasikia hata bandari imeenda alijojo" 😭 huwa nasikitika wakiniuliza hivi lakini najiuliza Hadi huko wanajua? Nagundua teknolojia imerahisisha usambaaji wa taarifa.

Sasa wale wanakuzunguka always watakuambia unakubalika lakini kamwe usiwaamini. Wanatumia nguvu kubwa kuwa corrupt mind lakini pamoja na hilo wakitoka wanakuponda mno wananchi.

Sasa hivi waziri mmoja wa afya ametangaza kuanza kwa clinic binafsi katika hospitali za umma. Mapokeo ya hili ni hasi kwa wananchi na joto la jiwe wameanza kulionja. Wanakwenda hospital wanacheleweshwa makusudi ili ifike saa 10 huduma binafsi zianze. Hali ni mbaya.

Kwenye hotuba zako, tofauti na mtangulizi wako, wewe siku hizi hata ukiwa una schedule ya kuhutubia wananchi wengi hawajiandai kusubiri kwa hamu hotuba ya kiongozi wao na hata kujazana kwenye kumbi za starehe kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wako. Nimejaribu kuandika kile nakiona mtaani lakini.

Muda Bado upo kidogo kuelekea 2025 ukiamua kubadilika unaweza, ukiamua kupuuza haya ni Sawa tu.
Lakini kama Hali itakwenda hivi Hadi 2025 mtaleta machafuko baada ya uchaguzi. Hatupendi hayo.

Jamhuri ya muungano wa Tanzania🇹🇿
"Raslimali za nchi ziheshimiwe kwa manufaa ya wote"
 
Kwa hiyo sisi tunaempenda sio wananchi wengi?

Hizo takwimu zako umezitoa kwa mizimu gani?
Samia ameharibu hakuna mtanganyika mwenye akili timamu mwenye kutamani kumuona, achilia mbali hata kumsikia..

Ni wajinga wachache kama wewe ndio wanaomuona shujaa wao, kwasababu ndie amewageuza watumwa ndani ya mipaka ya nchi yenu.

Jana tu jioni, nimekaa na jamaa zangu wanaendesha carry, gari ndogo za kusafirisha mizigo, sikuamini maneno waliyokuwa wakiyatoa pale kijiweni kwao..

Ikabidi niwatazame mara mbili mbili, maneno makali waliyokuwa wakiyatoa dhidi ya huyo mwanamke siwezi kuyaandika hapa, chawa amini nakwambia, watanganyika wote unaowaona hawana tena imani na Samia..
 
Hii ni opinion siyo utafiti. Ni muhimu uandike baadhi ya watu kwani hakuna binadamu anayependwa kwa asilimia 100. Kwa mfano, mimi na ninao kutana nao tunamtii na kumkubali Mhe. Rais.

Mengine ya rasilimali naamini zinalindwa. Kuhusu vijijini nakubaliana na wewe watu wana taarifa nyingi, sikuhizi miji na vijiji imeunganishwa na teknolojia. Tusiwapuuze watu wa vijijini lakini pia tusiwalishe taarifa za uongo na taharuki kama hili la bandari kutoka mijini. 🙏🙏🙏
 
Kuna tofauti kubwa sana kati ya kupendwa na kuwa na wasiwasi naye.

SSH anapendwa ila watu wana wasiwasi kuwa anaingizwa Mkenge. Yeye ni bendera fata upepo. Mamlaka yanaonekana pale ambapo unakaa kwenye nafasi yako kwa uimara na uthabiti.
 
Mama hapendwi na wananchi wengi kwa sababu:

1. Kuteua waziri ambaye hajui lolote juu ya uchumi zaidi ya kubuni tozo za kuwanyang'anya wananchi hata kile kidogo walichonacho. Ref. Tozo kwenye miala ya simu, benki, atm; kupandisha kodi ya jengo kwa zaidi ya 60%; tozo kwenye mafuta etc

2. Kugawa rasilimali za nchi kwa waarabu. E.g. bandari

3. Kutowachukulia hatua wafanyakazi wanaofisadi rasilimali/fedha za umma.

4. Yeye kutokujua ni nini malengo yake kwa wananchi na nchi akiwa kama Rais

5. Kuteua watumishi ambao hawafai kwa nafasi wanazopewa

6. Kuondoa wamasai kwenye maeneo yao ya asili.

7. Kuteua waziri wa kilimo ambaye anasababisha bei za mazao kuongezeka kwa zaidi ya 300%, kwa maamuzi yake ya kuruhusu wakulima kuuza mazao yao nje ya nchi bila utaratibu
 
Chawa hawapendi taarifa kama hizi. Watakushukia kama mwewe!!

Kimsingi hali imekuwa mbaya mno kuliko wakati wowote. Sasa hivi hata kwenye TV watu hawataki kabisa kusikia hotuba ya mama.

Kwangu mimi Rais Samia ni kiongozi mzuri sana na ninampenda. Tumeona mengi anatenda vizuri. Lakini uungwana ni pamoja na kuujua ukweli na kuufanyia kazi.

Chawa wamesababisha fedheha kwa kiongozi wetu. Njia pekee na muhimu mama awapige chini hawa chawa na wasaidizi wanaomzubaisha ili waibe
 
.
JamiiForums-2066617636_111746.jpg
 
Kuna sehemu wananchi umewakosea. Tafakari!

Toka uanze kazi ni mikoa 2 tu sijatembelea nayo ni Kagera na Kigoma. Mikoa mingine yote nimefika na kujaribu kufanya utafiti wa kawaida.

Hali ni mbaya, Siandiki kwa ubaya lakini ndiyo Hali halisi. Wengi wanakuongelea kwenye mtazamo hasi. Hata kwenye mikutano yako ya hadhara, wasaidizi wako wanatumia nguvu kubwa Sana kushawishi watu wajitokeze. Hii si ishara nzuri kwa kiongozi hasa wa level yako.

Niandikaye hapa ni mmoja wa watu tunaopita vijiweni Hadi vijijini. Tunakutana na watu wa kila aina na makundi tofauti na tunabadilishana mawazo. Na huwa hatuachi kuzungumzia viongozi wetu na msitakabali wa nchi yetu. Kwani Tanzania ndiyo mama yetu wa uraia.

Hali ni mbaya. Hali ni mbayaaaa!
Ndugu zetu walio vijijini wengine hata kisomo ni cha Chini lakini kila tukizungumza kwenye simu wanatuuliza " eti tunasikia hata bandari imeenda alijojo" 😭 huwa nasikitika wakiniuliza hivi lakini najiuliza Hadi huko wanajua? Nagundua teknolojia imerahisisha usambaaji wa taarifa.

Sasa wale wanakuzunguka always watakuambia unakubalika lakini kamwe usiwaamini. Wanatumia nguvu kubwa kuwa corrupt mind lakini pamoja na hilo wakitoka wanakuponda mno wananchi.
Sasa hivi waziri mmoja wa afya ametangaza kuanza kwa clinic binafsi katika hospitali za umma. Mapokeo ya hili ni hasi kwa wananchi na joto la jiwe wameanza kulionja. Wanakwenda hospital wanacheleweshwa makusudi ili ifike saa 10 huduma binafsi zianze. Hali ni mbaya.

Kwenye hotuba zako, tofauti na mtangulizi wako, wewe siku hizi hata ukiwa una schedule ya kuhutubia wananchi wengi hawajiandai kusubiri kwa hamu hotuba ya kiongozi wao na hata kujazana kwenye kumbi za starehe kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wako. Nimejaribu kuandika kile nakiona mtaani lakini.

Muda Bado upo kidogo kuelekea 2025 ukiamua kubadilika unaweza, ukiamua kupuuza haya ni Sawa tu.
Lakini kama Hali itakwenda hivi Hadi 2025 mtaleta machafuko baada ya uchaguzi. Hatupendi hayo.

Jamhuri ya muungano wa Tanzania🇹🇿
"Raslimali za nchi ziheshimiwe kwa manufaa ya wote"
Una data boss au ndio umeshashiba vitumbua una anza kuota Samia wakati umeshiba?
 
Mimi namkubali sana,ila kwenye suala la bandari katia doa,Ila Lile bunge ndio kabisaaa natamani hata lisiwepo.
 
Back
Top Bottom