Ukweli Mchungu: Rais Samia hupendwi na Wananchi wengi

Ukweli Mchungu: Rais Samia hupendwi na Wananchi wengi

Kuna sehemu wananchi umewakosea. Tafakari!

Toka uanze kazi ni mikoa 2 tu sijatembelea nayo ni Kagera na Kigoma. Mikoa mingine yote nimefika na kujaribu kufanya utafiti wa kawaida.

Hali ni mbaya, Siandiki kwa ubaya lakini ndiyo Hali halisi. Wengi wanakuongelea kwenye mtazamo hasi. Hata kwenye mikutano yako ya hadhara, wasaidizi wako wanatumia nguvu kubwa Sana kushawishi watu wajitokeze. Hii si ishara nzuri kwa kiongozi hasa wa level yako.

Niandikaye hapa ni mmoja wa watu tunaopita vijiweni Hadi vijijini. Tunakutana na watu wa kila aina na makundi tofauti na tunabadilishana mawazo. Na huwa hatuachi kuzungumzia viongozi wetu na msitakabali wa nchi yetu. Kwani Tanzania ndiyo mama yetu wa uraia.

Hali ni mbaya. Hali ni mbayaaaa!
Ndugu zetu walio vijijini wengine hata kisomo ni cha Chini lakini kila tukizungumza kwenye simu wanatuuliza " eti tunasikia hata bandari imeenda alijojo" 😭 huwa nasikitika wakiniuliza hivi lakini najiuliza Hadi huko wanajua? Nagundua teknolojia imerahisisha usambaaji wa taarifa.

Sasa wale wanakuzunguka always watakuambia unakubalika lakini kamwe usiwaamini. Wanatumia nguvu kubwa kuwa corrupt mind lakini pamoja na hilo wakitoka wanakuponda mno wananchi.
Sasa hivi waziri mmoja wa afya ametangaza kuanza kwa clinic binafsi katika hospitali za umma. Mapokeo ya hili ni hasi kwa wananchi na joto la jiwe wameanza kulionja. Wanakwenda hospital wanacheleweshwa makusudi ili ifike saa 10 huduma binafsi zianze. Hali ni mbaya.

Kwenye hotuba zako, tofauti na mtangulizi wako, wewe siku hizi hata ukiwa una schedule ya kuhutubia wananchi wengi hawajiandai kusubiri kwa hamu hotuba ya kiongozi wao na hata kujazana kwenye kumbi za starehe kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wako. Nimejaribu kuandika kile nakiona mtaani lakini.

Muda Bado upo kidogo kuelekea 2025 ukiamua kubadilika unaweza, ukiamua kupuuza haya ni Sawa tu.
Lakini kama Hali itakwenda hivi Hadi 2025 mtaleta machafuko baada ya uchaguzi. Hatupendi hayo.

Jamhuri ya muungano wa Tanzania🇹🇿
"Raslimali za nchi ziheshimiwe kwa manufaa ya wote"
Utafitti wako haujaonesha TAKWIMU (i.e. njia uliyotumia kukusanya Data, kipindi/muda wa utafiti, Mahali au eneo la utafiti, Methods of research and data analysis na References) manake ni kwamba, huo uliouweka hapa sio Utafiti bali ni aina ya masimulizi tu au mtizamo wako binafsi. Hakuna msomi atakayekubali kwamba eti huo ni Urafiti (Research). Labda kama ulimaanisha Mkusanyo wa maoni.......
BTW; Elewa kwamba Utafiti i.e. Research ina utaratibu wake (vigezo na masharti)ambao unapaswa (lazima) kuzingatiwa.
Ni hayo tu.
 
Ukweli mtupu. Ni tofauti kabisa na Mzee Baba, JPM.
Ilikuwa ukisikia JPM atakuja siku fulani, hata kama mtu alikuwa na safari fulani anaahirisha hiyo safari ili kwanza amsikilize JPM.

Hata Hotuba tu za JPM zilikuwa na mvuto sana kwa Watanzania asilimia kubwa ikilinganishwa na Hotuba za Mama.

Mimi nadhani, Mama ajitahidi tu kufanya Mambo yenye manufaa zaidi kwa Wananchi na ajitahidi sana kufuata nyayo za JPM.
 
Back
Top Bottom