Ukweli Mchungu: Rais Samia hupendwi na Wananchi wengi

Ukweli Mchungu: Rais Samia hupendwi na Wananchi wengi

Mnasema hapendwi lakini utashangaa 2025 kuna watu kibao watampa kura zao kwa kuwa na mahaba na chama bila kuangalia utendaji wake pia kuna ambao hawatampa kura pengine hawa wanaweza kuwa wengi lakini kwa kuwa haya ma CCM ni majizi mazoefu ya kura utashangaa amepata kura za kutosha lakini za mchongo
 
sisi tunampenda mnooo. kafanya mengi ndani ya mda mfupi wafanyakazi wengi tunampenda katutoa kwenye minyororo ya ukandamizwaji ya magufuli
Huku niliko pia tunampenda sana tu, tena saaaaaanaaa!
Akichukiwa na nyumbu wachache kuna shisa gani kwani?!!!

Mama analeta mabadiliko makubwa ya kiuchumi........hayo lazima kuna kuna walinda legacy kadhaa hawapendi kuyaona wala kuyasikia; kutoka kwao, lazima tutasikia kila aina ya uongo kama huu
 
Toka pande za R.CHUGA namkubali Mama kinoma noma
Kairudisha Arusha kwenye kiti chake cha ufalme baada ccm ya kina siambiliki kuondoka.
 
Uenda hakuwekwa na wananchi,raisi akifia madarakani Kama Sio miezi 6 kuelekea uchaguzi mkuu.
Uchaguzi ufanyike wananchi waweke chaguo lao.
Uraia Sio zawadi ya kupewa apewae hana uchungu.
 
Mnasema hapendwi lakini utashangaa 2025 kuna watu kibao watampa kura zao kwa kuwa na mahaba na chama bila kuangalia utendaji wake pia kuna ambao hawatampa kura pengine hawa wanaweza kuwa wengi lakini kwa kuwa haya ma CCM ni majizi mazoefu ya kura utashangaa amepata kura za kutosha lakini za mchongo
Kwani lini kura za halali ziliwahi kupigwa nchi hii?
 
Huku niliko pia tunampenda sana tu, tena saaaaaanaaa!
Akichukiwa na nyumbu wachache kuna shisa gani kwani?!!!

Mama analeta mabadiliko makubwa ya kiuchumi........hayo lazima kuna kuna walinda legacy kadhaa hawapendi kuyaona wala kuyasikia; kutoka kwao, lazima tutasikia kila aina ya uongo kama huu
Wafanyakazi wengi wa bandarini na maagent wa mizigo hawampendi anataka kuondoka na ulaji wao.
 
Huo ni mtazamo wako....suala la mkataba wa bandari kuwa wazi ni Moja ya sifa kuu ya kiongozi anayeshirikisha wananchi wake.

Ulitaka mkataba uwe wa Siri kama ule wa kununua ndege? Tena kipengele Cha usiri tuliweka sisi! Ukiondoa hizo ndege kupigwa double price pia tumeshalipa fedha nyingi za fidia kutokana na maamuzi ya hovyo ya kuvunja mikataba
 
Nikimpenda amimi inatosha mkuu

Muache Mama
Ukiona watu wanamzungumzia Rais wewe unazungumzia Mama tayari ujue tayari mnazungumzia watu wawili tofauti.
Huyu anazungumzia kiongozi wa nchi ambaye anachaguliwa, anafukuzwa pia, anapingwa, anapinduliwa kwa nguvu na mengine mengi lakini Mama hachaguliwi, hapingwi na hafukuzwi umama wake.
We baki na mama yako sisi acha tumkosoe Rais
 
KAMA NI HIVYO BORA KUINGIA GHARAMA ZA KUMCHAGUA RAISI TENA PUNDE MUNGU AMPENDAPO ZAIDI MLIYEMCHAGUA KULIKO MTU KURITHI URAIS MAANA MRITHI HUWA HANA UCHUNGU KULINDA MALI NA WATU ALIZORITHI/ ALIOWARITHI NA HUWA HAJALI.
 
Kuna sehemu wananchi umewakosea. Tafakari!

Toka uanze kazi ni mikoa 2 tu sijatembelea nayo ni Kagera na Kigoma. Mikoa mingine yote nimefika na kujaribu kufanya utafiti wa kawaida.

Hali ni mbaya, Siandiki kwa ubaya lakini ndiyo Hali halisi. Wengi wanakuongelea kwenye mtazamo hasi. Hata kwenye mikutano yako ya hadhara, wasaidizi wako wanatumia nguvu kubwa Sana kushawishi watu wajitokeze. Hii si ishara nzuri kwa kiongozi hasa wa level yako.

Niandikaye hapa ni mmoja wa watu tunaopita vijiweni Hadi vijijini. Tunakutana na watu wa kila aina na makundi tofauti na tunabadilishana mawazo. Na huwa hatuachi kuzungumzia viongozi wetu na msitakabali wa nchi yetu. Kwani Tanzania ndiyo mama yetu wa uraia.

Hali ni mbaya. Hali ni mbayaaaa!
Ndugu zetu walio vijijini wengine hata kisomo ni cha Chini lakini kila tukizungumza kwenye simu wanatuuliza " eti tunasikia hata bandari imeenda alijojo" [emoji24] huwa nasikitika wakiniuliza hivi lakini najiuliza Hadi huko wanajua? Nagundua teknolojia imerahisisha usambaaji wa taarifa.

Sasa wale wanakuzunguka always watakuambia unakubalika lakini kamwe usiwaamini. Wanatumia nguvu kubwa kuwa corrupt mind lakini pamoja na hilo wakitoka wanakuponda mno wananchi.
Sasa hivi waziri mmoja wa afya ametangaza kuanza kwa clinic binafsi katika hospitali za umma. Mapokeo ya hili ni hasi kwa wananchi na joto la jiwe wameanza kulionja. Wanakwenda hospital wanacheleweshwa makusudi ili ifike saa 10 huduma binafsi zianze. Hali ni mbaya.

Kwenye hotuba zako, tofauti na mtangulizi wako, wewe siku hizi hata ukiwa una schedule ya kuhutubia wananchi wengi hawajiandai kusubiri kwa hamu hotuba ya kiongozi wao na hata kujazana kwenye kumbi za starehe kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wako. Nimejaribu kuandika kile nakiona mtaani lakini.

Muda Bado upo kidogo kuelekea 2025 ukiamua kubadilika unaweza, ukiamua kupuuza haya ni Sawa tu.
Lakini kama Hali itakwenda hivi Hadi 2025 mtaleta machafuko baada ya uchaguzi. Hatupendi hayo.

Jamhuri ya muungano wa Tanzania[emoji1241]
"Raslimali za nchi ziheshimiwe kwa manufaa ya wote"
Sawa hapendwi, kwa hiyo.....
 
Back
Top Bottom