Ukweli Mchungu: Rais Samia hupendwi na Wananchi wengi

Utafitti wako haujaonesha TAKWIMU (i.e. njia uliyotumia kukusanya Data, kipindi/muda wa utafiti, Mahali au eneo la utafiti, Methods of research and data analysis na References) manake ni kwamba, huo uliouweka hapa sio Utafiti bali ni aina ya masimulizi tu au mtizamo wako binafsi. Hakuna msomi atakayekubali kwamba eti huo ni Urafiti (Research). Labda kama ulimaanisha Mkusanyo wa maoni.......
BTW; Elewa kwamba Utafiti i.e. Research ina utaratibu wake (vigezo na masharti)ambao unapaswa (lazima) kuzingatiwa.
Ni hayo tu.
 
Ukweli mtupu. Ni tofauti kabisa na Mzee Baba, JPM.
Ilikuwa ukisikia JPM atakuja siku fulani, hata kama mtu alikuwa na safari fulani anaahirisha hiyo safari ili kwanza amsikilize JPM.

Hata Hotuba tu za JPM zilikuwa na mvuto sana kwa Watanzania asilimia kubwa ikilinganishwa na Hotuba za Mama.

Mimi nadhani, Mama ajitahidi tu kufanya Mambo yenye manufaa zaidi kwa Wananchi na ajitahidi sana kufuata nyayo za JPM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…