Tofautisha kati ya raha na furaha.Utakataa na kufyonza pengine hata kuniporomoshea matusi, ila huu ndio ukweli mchungu kwa baadhi ya wanawake walio ndani ya ndoa zao ambao hawataki kuusikia abadani.
Nina siku ya 4 leo tangu nimetoka vacation Dubai, haijalishi nimetumikaje au nani kanitumia nikiwa huko, ila kiukweli nimeridhika na haya maisha ninayoishi.
Najua wanawake wengi sana wanatamani maisha tunayoishi sisi.
Sijasema msiolewe, nyie kama mmechagua kuolewa ni ninyi.
Kila mtu abaki na amani ya moyo wake.
Ila kiufupi ni kuwa sisi tuna maisha mazuri na yenye furaha kuliko ninyi.
Nimejenga
Nina biashara huria
Nina usafiri wa kutembelea
Kwanini nisijisifu?
Muhimu tujali afya zetu tu.
Raha inanunuliwa kama ulivyoenda kuinunua Dubai,nyumba magari na vitu vya kifahari haviwezi kuwa sababu ya furaha,bali vinaleta raha.
Furaha ni bure na watu wachache wa aina yako wanayo.
Kuna watu wako vijijini huku wana furaha ya kweli na hawawazi hata tu kununua paso.
Huna furaha wala amani hapo ulipo na nina uhakika ni suala la muda tu utarudusha majeshi kwa Mwamposa.
Utakuja kutana na matajiri wenye maagano ya utata ndipo utajua faida na hasara ya raha za muda katika kazi unayoipigia upatu.
Kiroho sio wewe unayeongea hapa,ila ni shetani anaongea kupitia were.Shetani yuko kazini na umemruhusu akutumie.