UKWELI MCHUNGU: Wazazi wengi hawana upendo wa kweli

Naomba kujua tofauti kati ya wazazi na baba
Umemtaja mwanaume kama mtu mwenye upendo wa kweli anayehudumia mkewe, watoto na pia kuwasomesha na kila kitu kwa upendo tu
Lakini umewashutumu wazazi kufanya hivyo kwa ku expect matokeo
Swali: huyu mwanaume anasimama kama nani sasa

Kama Mume.

Nimeshasema wengi wanasomesha watoto sio Kwa sababu ya upendo Bali Kwa sababu ya uwekezaji wa baadaye ili wasaidiwe. Tofautisha uwekezaji na Upendo.

Hilo utaliona kwenye matamshi Yao. Utajua huyo Mzazi alikusomesha Kwa upendo au Kwa kutaka faida ya baadaye.

Tuache tabia hizi
 
umepiga kwenye mshono basi tegemea povu

bottom line ni kwamba hakuna yeyote anayekupenda unconditionally

upendo wowote ule ni wa faida(maslahi), kama siyo pesa, materiali basi ngono

huko ndoani ndiyo kabisa

Na hiyo ni kutokana na watu kuingiza biashara ndani ya Ndoa.

Ila uhakika ni kuwa Wanaume wengi tunaupendo wa dhati Kwa Wake zetu bila kutegemea kurudishiwa kitu
 
Ukitaka kila siku uonekane unaandika madini ndio matokeo yake haya.....Punguza ujuaji

Naungana na jamaa juu pale umepuyanga parefu
Ungetoa hoja kupinga hoja yangu ningekuona unachochote cha maana lakini ulichofanya ni kuonyesha akili yako haitofautiani na hao wazazi niliowataja hapo. Ni hasara.

Kuja na hoja kuonyesha kuwa nimepuyanga, alafu onyesha watu kipi ni sahihi. Sio ulete mihemko yako kama mtoto aliyepewa Peremende
 
Kaka umenijibu maswali yangu mengi sana natamani huu ujumbe umfikie baba yangu aliyenitenga nikiwa sina kitu na kuwajali watoto wengine waliokuwa wakimtumia fedha na zawadi mimi kapuku hata kuulizwa uhali gani ilikuwa mtihani ila Mungu mkubwa amenifanikisha nipo nchi ya ahadi alivyopata taarifa naishi nje ndio akaanza kunitafuta kwa juhudi kutaka yaishe ila najua kabisa upendo hana na mimi ila amenitafuta kwasababu anataka pesa zangu hili andiko lako limenigusa na kunibariki sana .. kiuhalisia wazazi wengi wa wenye roho za kimaskini wapo hivyo na wamefanikiwa kuvuruga watoto wao sana.. nilichojifunza kwenye maisha haya ni kwamba upendo ni utu sio vitu. Mungu akutunze kamanda karibu sana canada.

Pole Sana Mkuu.
"..nilichojifunza kwenye maisha haya ni kwamba upendo ni utu sio vitu" ~ Mcanada.

Na wengi WA wazazi tupo hivyo.
Hatupendi watoto wetu Kwa moyo wote isipokuwa tunawapenda Kwa sababu ya vitu walivyonavyo au vile wanavyoonekana.
 
Kaka umenijibu maswali yangu mengi sana natamani huu ujumbe umfikie baba yangu aliyenitenga nikiwa sina kitu na kuwajali watoto wengine waliokuwa wakimtumia fedha na zawadi mimi kapuku hata kuulizwa uhali gani ilikuwa mtihani ila Mungu mkubwa amenifanikisha nipo nchi ya ahadi alivyopata taarifa naishi nje ndio akaanza kunitafuta kwa juhudi kutaka yaishe ila najua kabisa upendo hana na mimi ila amenitafuta kwasababu anataka pesa zangu hili andiko lako limenigusa na kunibariki sana .. kiuhalisia wazazi wengi wa wenye roho za kimaskini wapo hivyo na wamefanikiwa kuvuruga watoto wao sana.. nilichojifunza kwenye maisha haya ni kwamba upendo ni utu sio vitu. Mungu akutunze kamanda karibu sana canada.

Yaani watu hawajui baadhi ya wazazi ni watu wa maslahi kuliko Upendo,Mimi hiki nimekishuhudia hata kwa baadhi ya wazazi WA ndugu zangu
 
Hii ni kwaajiri ya wazazi masikini ambao hawakujijenga wao kimaisha,mwisho wa siku wanaweka nguvu kuwekeza kwa watoto zao ili waje wawasaidie baadae lakini mzazi mwenye akiri anabalance vyote yeye ajiimalishe kiuchumi akizeeka asipate shida yoyote na huku akimtengenezea mtoto wake njia za kujitegemea kiuchumi vile vile asipate shida kimaisha,hapo kwenye mtoto kumsaidia mzazi panakua sio pa lazima labda kwa upendo tuu
 
Hio asilimia ya wazazi kutopenda watoto umeipata wapi? Umefanya utafiti gani? Kama wewe hupendwi na wazazi wako usidhani ni wazazi wote wako hivyo.

Mbona kwenye harusi tunawapa watoto wetu zawadi za viwanja au magari? Unaweza kusema mzazi anayempa mtoto zawadi ya thamani kiasi hicho hampendi?

Kifupi, umeandika PUMBA kwa sababu umetoa takwimu bila utafiti. Ni kweli wapo wazàzi wanataka pesa kwa watoto wao, lakini sio wengi sana.

Wazazi wako wanaweza kuwa wameamua kukudao pesa kwa nguvu kwa sababu wamepata ushahidi kwamba pesa zako unakula na malaya tu wao huwakumbuki
 
Nilichoeleza ndio uhalisia.
Mambo ya unafiki Mimi huwaga sinaga.

Nimesema wazazi wengi. Sio wote. Elewa kilichoandikwa.

Ukweli upo katika familia nyingi. Hata kama wewe ukibisha. Huo ndio Ukweli.

Hapa wakisema watu watoe ushuhuda sio ajabu 80% ya watu wataungana na andiko hili.
 
Hii ni kwaajiri ya wazazi masikini ambao hawakujijenga wao kimaisha,mwisho wa siku wanaweka nguvu kuwekeza kwa watoto zao ili waje wawasaidie baadae lakini mzazi mwenye akiri anabalance vyote yeye ajiimalishe kiuchumi akizeeka asipate shida yoyote na huku akimtengenezea mtoto wake njia za kujitegemea kiuchumi vile vile asipate shida kimaisha,hapo kwenye mtoto kumsaidia mzazi panakua sio pa lazima labda kwa upendo tuu

Ni kweli kabisa
 
Back
Top Bottom