Joannah
JF-Expert Member
- May 8, 2020
- 20,921
- 49,014
Kuna haja ya kubadilika.Mzazi WA hivyo hawezi kumfundisha mtoto Upendo.
Watu wanasema siku hizi hakuna upendo kumbe ndivyo tulivyolelewa.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuna haja ya kubadilika.Mzazi WA hivyo hawezi kumfundisha mtoto Upendo.
Watu wanasema siku hizi hakuna upendo kumbe ndivyo tulivyolelewa.
Kweli kabisa hapo ni mwendo wa kunafikana tu maana wazazi wenyewe wanaonyesha mfano mbaya.😂😂😂😂😂
Na watoto wakigundua tabia za namna hii Kwa wazazi upendo wao Kwa mzazi unapungua. Pia wao wanapunguza kupendana na kushirikiana.
Wanaishi kinafiki nafiki. Kisa walizaliwa tumbo moja.
Yaani watu hawajui baadhi ya wazazi ni watu wa maslahi kuliko Upendo,Mimi hiki nimekishuhudia hata kwa baadhi ya wazazi WA ndugu zangu
But wewe hapa umejenga hoja kwa jambo lingine. Mleta uzi hajasema kuwa wazazi wote hawapendi watoto wao ile ya dhati ya moyo. Ila ameweka bayana kuwa wengi wao huwa wanaishi na watoto kijamaa kuwa nikusaidia sasa ili unisaidie baadae. So bidii yote ya kuwekeza pesa kusomesha au kupambania mtoto afanikiwe ni aina ya uwekezaji.Subiri uzae ndiyo uje na hili andiko, kwa sasa liko obsolete.
Yani oa, kisha mpate mtoto, umshuhudie since akiwa tumboni anavyomvuruga mama yake, siku anazaliwa, akiwa na wiki, mwezi, mwaka, miaka nk. Hii kitu inajenga upendo wa ajabu mnoo kati ya mzazi na mtoto.
Hata kama wewe wazazi wako walikuneglect ila wanao hautaweza kufanya ivo unless itokee a very strong bond breaker...
Asilimia kubwa wanazo japo kwa viwango tofauti.Unataka kusema Watu wote wanamali za kuwaridhisha watoto wao?
Upendo ni zaidi ya Urithi
Pole Sana Mkuu.
Endelea tuu kuwaheshimu Sana wazazi wako.
Ila kimsingi suala la upendo Kama huna lolote ni nadra Sana.
Mtoto mwenye kipato akifariki utasikia mama analia MUNGU UMENIWEZAAAA KWA NINI UMEMCHUKUA JIMMY,MBONA UMENIKOMOA MIMI.....,sasa wengine inabidi mstop kulia muangaliane sasa huyu mama alitaka achukuliwe nani?
Umeongea ukweli kabisa wazazi wa siku hizi wanapenda sana mtoto mwenye uwezo,hata wajukuu wakikutana likizo kale ka mwenye hela kanatreatiwa kama ka princess..tupambane tu kutafuta hela
Kweli kabisa,unaweza wewe jibana ukampa kahela yeye anakaficha anakuja kumpa mpenzi wa moyo wake.Na wazazi wengi wakiwa na watoto wengi hawawez balance upendo kwa sababu nao ni binadam mfano mama yangu kuna watoto anawapenda kabisa ile realy ila wengine ni kwa vile unampa hiki na kile
Kweli kabisa,unaweza wewe jibana ukampa kahela yeye anakaficha anakuja kumpa mpenzi wa moyo wake.
Kuna watu wameumbwa kuishi kwa kufuata mkumbo tu ila sio kuelewa mambo yanakwenda vipi. Kama huyu kasoma ameona hajaelewa badala ya kuuliza maswali apewe ufafanuzi anatapika mashudu na buni inayotengeza kahawa.
Unanikumbusha hekaheka za wazazi na wazee wa ukoo wa kichaga
Yaani we acha tu,,,,ni msala😂😂😂😂
Noma Sana hiyo.
Alafu huyo anayempa anaenda kunywea pombe hapo ndio utajua hujui
Huyu jamaa hajui anachosema,tangu lini wazazi wote wakawa na Mali za kuwarithisha watoto zaidi hata ya wawili? Kuna wazazi ni maskini,na hawa mara nyingi ndio unakuta Wana hasira na watoto wao,Unataka kusema Watu wote wanamali za kuwaridhisha watoto wao?
Upendo ni zaidi ya Urithi
I Disapprove of What You Say, But I Will Defend to the Death Your Right to Say It
Umepuyanga hadi umepuyanga tena. Unasema mme anaempenda mke ndo mwenye upendo wa kweli? Mume huyu huyu ambae anakuletea mchepuko na ana uwezo wa kukufukuza akipata mali?
Wewe endelea kuamini unachoamini ila kwa sisi wazazi tunaelewa. Personally mzazi wangu pamoja na kwamba leo hii niko kwangu na ndoa yangu ananiona nastahili msaada wake. Hata akiona umetoa kitu kusaidia ndugu ambao ni wanae wa damu anakutumia hela unamuuliza ya nini anasema aah najua tu maisha magumu unatamani umwambie hii sio sawa hawa ni jukumu langu.
Na mimi kama mzazi, niko napambana usiku na mchana wanangu nawaanadalia mazingira hata siku nikidondoka leo niwaachie knowledge na mali. Ile
Dhana ya kwamba acha mtoto aje ajitaftie ni kama kukomoa. Basi usizae. Kama una uwezo ya nini kutupa mali wakati kuna viumbe umetengeneza? Mtoto muelekeze
Njia njema na hata akiwa anakua asijue kwamba kuna mali zake zinamsubiri anaweza kubweteka. Ila ajue yeye ni kijana wako unaetegemea aje kuwa mfano katika jamii.
Sasa we usisemee wazazi wako kwenye general rule mkuu. Usijenge chuki ndani ya mioyo ya watu waanze kuwaona wazazi wao kama takataka. Maana kuna watu wana akili za kushikiwa wanabeba bandiko lako wanalihamishia kichwani kama mataaira.
Mzazi atabaki kuwa mzazi hata maandiko yamesema.
Mungu wabariki wazazi wetu waliotulea kwa shida..
Ila kwa kuwa umesema ni baadhi ya wazazi basi nyie wenye wazazi wa hivyo Mungu awape tumaini la milele huku mkijikumbushia na waefeso 6:2-3. Na ile amri ya Kuheshimu Baba na mama ndo amri yenye ahadi. Hata mzazi akutese vipi. Baraka na laana vipo katika kurudisha kwako. Kama mzazi anakutesa bora ukae mbali kuliko kumvunjia heshima. Tunawaona wazazi wanaonyang’ana vitu vya watoto wao kwa nguvu kwasababu ni mzazi inatesa haswa lakini kwakuwa ni mzazi unabaki unaugulia moyoni.
Wewe kama mzazi. Unategemea nini kwa mtoto wako? Unataka mtoto wako akikua aje kuwa mtu wa namna gani?
Yaani we acha tu,,,,ni msala
Huyu jamaa hajui anachosema,tangu lini wazazi wote wakawa na Mali za kuwarithisha watoto zaidi hata ya wawili? Kuna wazazi ni maskini,na hawa mara nyingi ndio unakuta Wana hasira na watoto wao,
"Hata mzazi akutese vipi" hiyo kauli iandike tu,alafu iache humu ndugu. Mzazi anayemtesa mtoto wake huyo ni mhuni,na hafai kuwa mzazi,mzazi anatakiwa awe faraja kwa mwanae,nakwambia hakuna maumivu mabaya kama ya kuumizwa na mzazi,Bora uumizwe na mtu Mwingine aise,kumbuka mzazi wako ndio msiri wako,ndio Alfa na omega,yaani yy ndio alikuleta dunia hii,ndio anajua uzuri wako na mafhaifu yako,ikitokea anakutesa alafu eti uvumulie,Hilo umetudanya mchana kaka. Alafu,kama hukupitia machungu ya kulelewa ndivyo sivyo,hutaelewa.
Walishawahi kumcharaza mtoto wa father mdogo viboko na faini ya mbuzi wawili na debe za mbege juu kisa ni kutohudhuria misiba ya ukoo na kugoma kutoa michango ya ugonjwa, misiba na sherehe mbalimbali za wanaukoo kwa miaka minne mfululizo.Walikufanya nini Mkuu?
Mkuu uko sahihi Biblia imetabiri kuwa kuna siku upendo utapoa na kila mtu atapenda pesa. So hapo unaona dhahiri ya kuwa mtoto mwenye pesa ndio atapendwa. Pesa itareplace upendo.