Ninachompendea
ROBERT HERIEL anaongea kitu na kama ni muhanga wa hiyo kitu basi unagundua anagusa mulemule.... Imagine mimi Baba yangu mzazi alishawahi kuniropokea kwamba "Kuanzia leo wewe sio mwanangu, nahesabia sina mtoto tu, maana huna msaada wowote kwangu sasa wewe wa nini kwangu" ilikuwa tunaongea kwenye cm kisa aliniomba hela nikamuambia hali haipo sawa ile kitu iliniuma kinoma ukizingatia nipo kwenye situation ngumu sana kimaisha maana hata nilipokuwa naishi palikuwa kwa mwana tu alinihifadhi so, akili ilikuwa inawaza nikusanye vijiehela ninavyopata kwenye vibarua na mimi nihamie gheto kwangu kumbuka mimi nipo Dar mzee yupo Moshi nilichomjibu ni kwamba "haina tatizo mzee me pia naanza kuhesabu sina baba na wala usiwe na wasiwasi sitokutafuta tena" kweli zikapita weeks hatujawasiliana siku moja akapiga anajichekesha... Me nikawa nishaelewa hapa hamna upendo wa kweli wala nini watu wanajali pesa tu so, acha tuishi kinafiki na mzee nikipata vielfu kumi namtumia till now tunaishi tu.
Baada ya hapo nikawa nikihisi pengine wamama ndo wana upendo kweli kuliko wababa maana wao ndo walituzaa.... Mwaka jana mama pia akani-disappoint mno kwa maneno yake.... Dah yeye ndo aliniongelea vibaya mpaka nikajikuta nimekata cm.... Kumbuka hata hawajanisomesha nikafika levels za juu no, Wala hawajui huku Dar najishughulisha na nini wao hujua kujifanya wana upendo na mimi pale wanapoona messages za Transactions ndo utaona mara "Oooh lini utakuja kutusalimia, Oooh ni muda sasa mimi baba, mama sinakuona sio vizuri"
Dah! oya wanangu Rafiki wa kweli kwa sisi wanaume ni Mungu na Hela tu wakuu... Usiamini upendo wowote mbali na hapo labda kama umezaliwa kwenye familia yenye misingi mizuri ya kipato.
Umasikini ni laana.