UKWELI MCHUNGU: Wazazi wengi hawana upendo wa kweli

UKWELI MCHUNGU: Wazazi wengi hawana upendo wa kweli

Mimi huwa nawashangaa watu wanaowatukuza na kuwaabudu mama zao eti hakuna kama mama(Mungu je?) Hawajui kwamba hiyo ni kutokana na ubinafsi wa wao ili watoto wasahau na kuwadharau Baba zao. Nachoamini Mimi wazazi wote ni Sawa,Ila,ukiingia kwenye kumi nane ya mwanamke (mama) utaniona hii dunia chungu, yaani watu hawajui tu.
Acha kabisa
 
Anaeweza elewa mada kama hizi nj mtu aliyepitia haya, na hata hua ukifanikiwa ukisema unamsaidia huyo mzazi unafanya tu kwa ajili unatafta radhi za mola.wako lkn kama sivyo hushighuliki nae.kwa lolote. Uzi huu umenikumbusha maisha yangu, yan wengin hata uumwe ufe kwake anaona sawa tu lkn.mwanae mwingine akiugua anafanya kupata wazimu.
Niliwahi kuomba pesa ya matumizi nikiwa chuo baada ya bibi kushindwa kunisaidia pesa ya chakula alichonijibu mama yangu " kwa sasa sina pesa ya kukupa kwani nimeagiza gari nashughulika na mambo makubwa " imagine kwa wakti ule nilitamani anipe hata 5000 niweze kula kwenye mikoa ya watu lkn hayo ndo yalikua majibu yake.ki ukwel watu wakisema nani kama mama mimi najisemea hakuna kama bibi. mungu atusaidie
Mama mzazi huyo? Duuh

Mi nisingemsaidia
 
Mwana fasihi umeeandika upumbavu...kumsaidia mzazi ni wajibu wako kama ilivyo mzazi kulea na kukusomesha ili uwe na maisha Bora
 
Mama mzazi huyo? Duuh

Mi nisingemsaidia
Wala hata hahitaji msaada anajiweza vema, shida inakua kwako ukikwama ukiwaza nan anakusaidia ndo unapagawa maana hata ukitafuta msaada kwa wengine wanajua mzazi wako hashindwi kukusaidia maana pesa ipo.
Ni kujikaza tu kutoa salamu na kutimiza Mungu anachotaka lkn rohoni hayupo hata kidogo. Mungu azidi kumueka bibi yangu ingawaje umri wake umekimbia mno
 
Wala hata hahitaji msaada anajiweza vema, shida inakua kwako ukikwama ukiwaza nan anakusaidia ndo unapagawa maana hata ukitafuta msaada kwa wengine wanajua mzazi wako hashindwi kukusaidia maana pesa ipo.
Ni kujikaza tu kutoa salamu na kutimiza Mungu anachotaka lkn rohoni hayupo hata kidogo. Mungu azidi kumueka bibi yangu ingawaje umri wake umekimbia mno
Duuh inaumiza sana
 
Umeandika madini ya thamani sana mkuu....kiufupi Iko hvyo anayebisha ajaribu kucompare na kujibu swali Hilo; kwny familia kwann mtoto mwenye kipato (fedha) anapendwa kuliko wengne?
Mr ukweli ndiyo huo
Nakumbuka kunasiku nilihisi mama yangu hanipendi kabisaaa na hana uchungu na nnayo yapitia yeye anachotaka NI pesa

Haijalishi nalala lake nakulaje navaaje anacho taka yeye nihera
Mpaka leo hiii nikiiona namba yake maongezi yake nihera tuuu japo atazungukaa Ila mwisho wa siku pesa tuu

Kiukweli NI biashara sio upendo
 

I Disapprove of What You Say, But I Will Defend to the Death Your Right to Say It​


Umepuyanga hadi umepuyanga tena. Unasema mme anaempenda mke ndo mwenye upendo wa kweli? Mume huyu huyu ambae anakuletea mchepuko na ana uwezo wa kukufukuza akipata mali?

Wewe endelea kuamini unachoamini ila kwa sisi wazazi tunaelewa. Personally mzazi wangu pamoja na kwamba leo hii niko kwangu na ndoa yangu ananiona nastahili msaada wake. Hata akiona umetoa kitu kusaidia ndugu ambao ni wanae wa damu anakutumia hela unamuuliza ya nini anasema aah najua tu maisha magumu unatamani umwambie hii sio sawa hawa ni jukumu langu.

Na mimi kama mzazi, niko napambana usiku na mchana wanangu nawaanadalia mazingira hata siku nikidondoka leo niwaachie knowledge na mali. Ile
Dhana ya kwamba acha mtoto aje ajitaftie ni kama kukomoa. Basi usizae. Kama una uwezo ya nini kutupa mali wakati kuna viumbe umetengeneza? Mtoto muelekeze
Njia njema na hata akiwa anakua asijue kwamba kuna mali zake zinamsubiri anaweza kubweteka. Ila ajue yeye ni kijana wako unaetegemea aje kuwa mfano katika jamii.

Sasa we usisemee wazazi wako kwenye general rule mkuu. Usijenge chuki ndani ya mioyo ya watu waanze kuwaona wazazi wao kama takataka. Maana kuna watu wana akili za kushikiwa wanabeba bandiko lako wanalihamishia kichwani kama mataaira.

Mzazi atabaki kuwa mzazi hata maandiko yamesema.
Mungu wabariki wazazi wetu waliotulea kwa shida..

Ila kwa kuwa umesema ni baadhi ya wazazi basi nyie wenye wazazi wa hivyo Mungu awape tumaini la milele huku mkijikumbushia na waefeso 6:2-3. Na ile amri ya Kuheshimu Baba na mama ndo amri yenye ahadi. Hata mzazi akutese vipi. Baraka na laana vipo katika kurudisha kwako. Kama mzazi anakutesa bora ukae mbali kuliko kumvunjia heshima. Tunawaona wazazi wanaonyang’ana vitu vya watoto wao kwa nguvu kwasababu ni mzazi inatesa haswa lakini kwakuwa ni mzazi unabaki unaugulia moyoni.

Wewe kama mzazi. Unategemea nini kwa mtoto wako? Unataka mtoto wako akikua aje kuwa mtu wa namna gani?
umeandika sana wakati hata huajelewa, punguza mihemko tumia sense
 
Anaandika, Robert Heriel

Wazazi msiwape watoto wenu mzigo wa kununua upendo wenu kwa kuhangaika ili kuwapa pesa na mali. Upendo haununuliwi. Tabia ya kudai malipo kisa mliwasomesha au kuwazaa na kuwatunza huo ni uhuni. Kuwapenda watoto wenye vipato au wanaowapa vijizawadi ni dalili moja wapo inayoharibu ile dhana kuwa wazazi mnaupendo wa kweli kwa watoto wenu. Itaonekana kama propaganda tuu lakini uhalisia ni kinyume.

Kuna wale wenzangu na miye wanaokwambia hakuna upendo wa kweli kama upendo wa mama. Hakuna kitu kama hicho. Wanaosema hivyo ni wale wanaoongozwa na mihemko.
Taikon kama nitaulizwa katika huu ulimwengu nani mwenye upendo wa kweli basi karata yangu itadondokea kwa wanaume waliooa.

Yaani mume akimpenda mke. Huo ndiyo upendo wa kweli. Hizo nyingine ni drama. Kumpenda mtu ambaye hauna uhusiano naye, undugu naye na pengine humfahamu kabisa, huo ndiyo upendo halisi. Yaani upendo unaokuja naturally siyo upendo wa wajibu. Najua kuna watu watabisha hapa. Lakini huo ndiyo ukweli.

Upendo wa wazazi waliyowengi ni upendo wa faida. Wengi tumezaa watoto ili baadaye waje watusaidie. Hatuzai kwa sababu tunawapenda watoto bali tunazaa kwa sababu ya manufaa yetu ya baadaye. Mzazi anakusomesha siyo kwa sababu anakupenda, siyo kwa sababu ati uwe na maisha mazuri, wengi wanasomesha ili baadaye uwasaidie. Yaani kwa kifupi unaitwa uwekezaji au biashara.

Yaani mzazi wako alivyokuwa anakusomesha ni kama mfanyabiashara anayefanya biashara ya kupanda miti ya mbao. Anategemea siku moja atapata return ya uwekezaji wake. Huo hauitwi upendo, hiyo inaitwa biashara!

Kadiri unavyokua mkubwa ndivyo utakavyoona kuwa hata wazazi wenyewe hawana upendo wa kweli. Uhakika uliyokuwepo ni kuwa upendo wa kweli upo baina ya mume na mke/yaani baba na mama. Ila upendo wa wazazi na watoto au watoto na wazazi huo hauitwi upendo bali wajibu[emoji4][emoji4].

Mume kumpenda mke siyo wajibu wala siyo jukumu lake bali hiyo inatokana na silika/hulka ambayo huja automatically/naturally. Na huo ndiyo upendo wa kweli.

Ni kama vile mtu kuwa na njaa. Huo siyo wajibu bali ni silika/hulka ya mwanadamu. Huwezi sema unaowajibu wa kusikia njaa. Hiyo haipo. Ndivyo ilivyo kwenye upendo. Upendo wenye wajibu siyo wa asili. Upendo wa kweli ni ule wa mke na mume. Yaani huo unakuja automatically/naturally.

Unaweza kujitahidi kuuzuia lakini ndani yako unaumia, ni kama kuizuia njaa, lazima uumie. Huwezi fundishwa kumpenda mke au mume hiyo haipo kwa sababu inakuja naturally. Lakini watu hufundishwa kupenda watoto wao, au kupenda wazazi wao huko makanisani na misikitini. Na jambo lolote la kufundishwa huwezi liita la asili.

Upendo ni maamuzi ya uchaguzi yanayokuja automatically/naturally kutoka moyoni na kujikuta unampenda na kuvutiwa na mwanamke au mwanaume fulani. Lakini yote hayo hufanyika kutokana na utashi na vile mtu apendavyo mtu atakayempenda aweje.

Mzazi hakujua atakuzaa wewe. Pengine alitamani kuzaa mtoto wa aina fulani mwenye maumbile fulani, au mwenye akili fulani, lakini hiyo huwa siri ya mzazi mwenyewe. Hata hivyo zile sifa mbaya ulizonazo mara nyingi mzazi mmoja hupenda kuzihusisha na upande wa mzazi mwingine.

Halikadhalika, mtoto hukutegemea kama ungezaliwa na baba au mama uliyenaye. Watoto huweza kuwa walitamani kuwa wangekuwa na wazazi wa namna fulani, wenye maumbile au hali fulani ya maisha. Hizo ni siri za watoto.

Ndiyo maana kuna kanuni na sheria isemayo, "Waheshimu wazazi wako." Sheria haijasema wapendeni wazazi wenu. Kwani inajua kuwa upendo unahusu uchaguzi na siyo amri/siyo lazima. Kwani haukuamua wala kuchagua huyu awe baba au mama yako, wala yeye hakuchagua, ila imetokea tuu.

Hii ni tofauti na upendo wa mume na mke. Hawa wao walichaguana, waliamua wakiwa na akili timamu. Hivyo kwao kupendana kwao ni amri/lazima. Yaani nature itawalazimisha kufanya hivyo automatically.

Sisi wanaume ndiyo wenye upendo wa kweli hasa kwa wake zetu. Kwani ndiyo tunauwezo wa kuonyesha mapenzi yetu kwao pasipokutegemea malipo hasa ya vitu/pesa au mali. Sisi tunachohitaji ni heshima na utiifu.

Sisi wanaume tunaweza kutunza mke na watoto kwa furaha kubwa miaka nenda rudi pasipo kudai malipo ya fedha au mali. Hiyo ni mpaka tunakufa. Tunachohitaji ni heshima na utiifu tuu ambapo hayo hayapo kwenye mambo ya biashara.

Lakini ni wazazi wachache sana ambao wanaupendo wa namna hiyo. Narudia wazazi wachache Sana. Yaani kwenye wazazi 100 basi mzazi mmoja ndiye mwenye upendo wa kweli. Hao 99 waliobaki ni wafanyabiashara wanaotaka malipo ya fedha au mali au kitu chochote kinachoshikika (materials).

Siyo ajabu ukipata tuu kazi, badala ya kufurahia kazi yako unaweza kujikuta kwenye mtihani mzito sana. Kwani baadhi ya wazazi huweza kukuletea shida mpaka ukajuta. Ni kama walikukopesha sasa unatakiwa kurudisha marejesho.

Shida inakuwa kubwa zaidi kijana wao wa kiume mwenye kazi akipata mke, hapo ndiyo mambo huweza kuwa mabaya zaidi. Wengine hufikia hatua ya kuwaloga watoto wao. Wengine kuwavurugia nyumba za vijana wao.

Nina uhakika mzazi wako akiambiwa achague mtu mmoja ambaye anampenda katika maisha yake yote hawezi kukuchagua wewe. Tena mkiwa watoto wengi ndiyo Kabisa.

Wazazi wa siku hizi wengi ukiona anakupenda ujue ni kwasababu kuna kitu unampatia, na kitu hicho ni materials aidha iwe pesa au zawadi ndogondogo, na huo hauitwi upendo bali ni biashara.

Hata hivyo wazazi wetu wengi wapo hivyo au tupo hivyo kwa sababu ya umasikini. Ingawaje wapo wazazi matajiri lakini bado wanatabia ya kutokupenda watoto wao.

Upendo wa wazazi mara nyingi unafanana na upendo wa mke Kwa mume wake. Yaani kama hutoi materials basi uwezekano wa kupendwa unakuwa ni mdogo sana. Lakini kamwe hautofikia upendo wa mume kwa mkewe.

Sisi kama wazazi tunaowajibu wa kuwapenda watoto wetu pasipo kutarajia malipo ya fedha na mali. Wao kutuheshimu na kututii kama wazazi wao inatosha.

Tuwekeze kwenye miradi, tuweke akiba ili uzee ukitukuta utukute tukiwa tumejiandaa vyema. Watoto wetu watupe vitu kwa mioyo yao kadiri wanavyowiwa na sisi tusiwe na kinyongo kuwa mbona hawatupi vingi kama sisi tulivyotoa kwao. Huo hauitwi upendo bali ni biashara.

Tuwapende watoto wote bila kujali hadhi na hali zao. Wote ni watoto wetu. Hii itamfanya nao wapendane. Kwani ninyi mtaonyesha mnaupendo wa dhati bila kujali hali zao za vipato. Mbona sisi wanaume tunawapenda wake zetu kwa mioyo yetu yote bila kujali hali zao za vipato?

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
Hapa duniani hakuna upendo wa kweli ,
At least upendo ambao uko close na truth ni WA mama

Yaani upendo wa huku duniani basically ni transaction,
Ni mchezo wa nipe nikupe,
Ukipendwa jua aliyekupenda anameona kitu unaweza kuoffer.
 
Hapa duniani hakuna upendo wa kweli ,
At least upendo ambao uko close na truth ni WA mama

Yaani upendo wa huku duniani basically ni transaction,
Ni mchezo wa nipe nikupe,
Ukipendwa jua aliyekupenda anameona kitu unaweza kuoffer.

Upendo wa kweli ni ule wa mume Kwa Mke.
Mechanism ya kumpenda mtu ambaye hamfahamiani, hamjuani na kumuonea uchungu ni zaidi ya Upendo WA Mama Kwa Mtoto.

Wamama wanatabia kuonyesha upendo wa kuendeshwa na mihemko na sio Upendo halisi. Hasa mtoto ukishakuwa mkubwa.
 
Umepuyanga.
Hajapuyanga. Sababu kuu inayofanya waafrika wazae watoto wengi ni kudhani kuwa wanawekeza. Wanazaa watoto ili watoto waje watunze wazazi, na wala siyo ili wazazi watunze watoto.

Hiyo ni kinyume. Ndiyo maaana utakuta mzazi kama ana mtoto wa kike, yuko tayari kumtuma hata afanye ukahaba ili mradi alete pesa, Huo ni ukatili, roho mbaya na ushetani uliopitiliza.

Wazazi wengi Afrika hawajui wajibu wao, ni washenzi, wapuuzi na wapumbavu.
 
Back
Top Bottom