Wakati nikiwa sekondari niliupenda ualimu. Baada ya kwenda high schoo niliuchukia. Chuo kikuu sikuchukuwa ualimu, lakini baadaye nilijikuta nimekuwa mwalimu, na hadi leo sijatamani kazi nyingine zaidi ya kufundisha, ndiyo maana nimefundisha zaidi ya miaka 40.
Ni kweli kuwa ualimu, hasa siku hizi hauheshimiwi kama kazi nyingione. Waalimu wengi hasa shule za msingi na sekondari za kata wanafanya kazi katika mazingira magumu. Lakini kudai kuwa hiyo kazi ni mbaya kuliko kuendesha bodaboda ni kuidhalalisha hiyo fani. Yeyote anayesema hii fani ni mbaya basi akumbuke kuna fani nyingi ambazo ziko chini ya hizo. Kuna watu wanaitwa clerical officer, messenger, typist, n.k. huwe kulinganisha na ualimu.
Watu wengi wanadhani ualimu ndiyo wenye kipato cha chini. Kwa taarifa yako kuna waalimu wa shule za msingi wenye mishahara mikubwa kuliko wakubwa wao makao makuu. Ualimu unaa ngazi na wengi hupanda na kufikia mishara inayoweza kuwakaribia makatibu wakuu, mameneja wa kati, n.k. Bodaboda anaweza kupata kipato kikubwa na kujiendeleza na kuwa na pesa nyingi (tajiri) kuliko hata engineer, daktari, n.k. Hiyo hutokea katika kada zote. Mimi nimeshuhudumia wahudumu ofisi waklifanikiwa na kutajirika, lakini hii haina maana wahudumu ofisi kazi yao/maisha yao ni bora kuliko maofisa wao. Ni mtu mmoja mmoja. Hii ndiyo maana tuna watu wana masters/Ph.D. lakini bado kati ya hao hali zao zinaweza kuwa duni kuliko wachache wa darasa la saba au la 12.
Mimi nakubaliana na wewe uwezekano wa bodaboda kumzidi mwalimu upo, lakini huwezi kumlinganisha au kuwalinganisha walimu na bodaboda. Mimi nimefanikiwa kwenye ualimu na hata siku mopja sitajilinganisha na bodaboda na bodaboda hawanikaribii kwa vyovyote vile (generally). Lakini nakubali kuna bodaboda mmoja mmoja ambao inawezekana kufanikiwa kuliko mimi. Pia huenda kuna wahudumu offisi weamepata kufanikiwa kuliko mimi. Na hao ni wale waliyopata pesa na kufanya investment zenye kulipa. Walimu nao wapo waliyotumia vipato vyao na kuytajirika!