Ukweli ni kwamba kama Nchi tunahitaji watu kama Tundu Lissu na Hayati Magufuli walioboreshwa

Kama ni wa kufuata sheria, sioni ni jinsi gani unaweza kuwa u-dikteta.

Lakini hata tukiupa jina la udikteta; udikteta huu ni mzuri sana kwa mazingira kama yaliyopo Tanzania. Watu hapa wanapenda kusukumwa ndipo waweke bidii kwenye maisha yao. Maofisini, hivyo hivyo.

Unajuwa, pamoja na kuwa na kinachoitwa 'Democracy' katika baadhi ya nchi, lakini viongozi wa nchi hizo walionekana kufanya udikteta ilipohitajika kuwa hivyo ili kuleta mabadilko ya haraka katika nchi zao. Korea Kusini ni mfano mzuri sana wa hali hii.

Tanzania sasa hivi tunataka sana kiongozi asiyechezea mali za umma kwa njia yoyote. Tunahitaji kila hicho kidogo kusukuma mbele maendeleo ya nchi hii.
Kuchekacheka kwa akina Kikwete/Samia, hakutupeleki kokote.
 

Bado naamini TL ni presidential material aandaliwa .
Your browser is not able to display this video.
Yaliyosemwa hapa hata TL angekuwa CCM kwa nafasi ya JPM yasingekuwa na Tofauti .​
Huko unakokusema "kuandaliwa" ndiko "kuharibiwa," kama hujui.

Tundu Lissu hana hulka za kishetani shetani alizokuwa nazo Magufuli. Kwa upande huo kuna tofauti bayana.
 
Yaliyosemwa hapa hata TL angekuwa CCM kwa nafasi ya JPM yasingekuwa na Tofauti .
Dah, nilikuwa sijaisikiliza hii hotuba ya Magufuli.
Sasa nimeisikiliza na mara moja swali likaniijia kichwani: Hivi Samia alishawahi kuisikia hotuba hii?

Inawezekana sana alikwisha isikiliza na yeye akahitimisha, kama alivyofanya Magufuli, kwamba "aliyofanya Magufuli ni ya Magufuli, yeye Samia atafanya yake"

Lakini kuna tofauti kidogo. Samia hajawahi kusimama na kuomba uongozi kwa waTanzania ili akipewa fursa hiyo, afanye anayotaka kufanya yeye, na siyo yale Magufuli aliyochaguliwa ayafanye. Samia amefanya makosa, kutoendeleza yale yaliyokuwa yakifanywa na mwenye serikali yake, Magufuli; Samia akiwa msaidizi tu!
 
Uko sawa kabisa mkuu, atakayebisha ameamua kubisha tu!
 
Lissu akiingia madarakani hata hizo sheria hawezi fuata
 
Lissu akiingia madarakani hata hizo sheria hawezi fuata
Sawa. Huenda unamfahamu zaidi. Sijui.

Mimi nilivyomuona miaka mingi ni kuwa Lissu anaogopwa sana kuwa “hana ustaarabu” sheria zinapovunjwa au kupindishwa. Hasiti kumuita hata Rais “mwizi” au “fisadi”. Fikiri mtu wa aina hiyo akiingia madarakani patashika itakayotokea.

Kama ulikuwepo utaikumbuka orodha ya mafisadi (List of Shame) iliyosomwa Mwembechai 2007 na Dr Slaa. Unajua ilivyovyoandaliwa? Pia unajua kuelekea uchaguzi wa 2010 Rais JK alisema “heri ya Dr Slaa kuwa Rais kuliko Lissu kuwa mbunge”. Unajua kwa nini?
 
Huwezi fuata sheria na still ukaweza leta maendeleo na kusimamia haki ,ndio maana nchi kama China ,Russia hawasaini mikataba ya kimataifa ya haki za Binadamu .
 
Naunga hoja mkono nanina uhakika kwa sasa hakuna anayeweza kuirudisha nchi kwenye mstari tofauti na lisu ili hata ccm wenyewe ukiwauliza watakueleza kwa lisu ndio mbadala wa jpm
 
Naunga hoja mkono nanina uhakika kwa sasa hakuna anayeweza kuirudisha nchi kwenye mstari tofauti na lisu ili hata ccm wenyewe ukiwauliza watakueleza kwa lisu ndio mbadala wa jpm
Usije ukawa ndio TL mwenyewe
 
Magufuli na Lissu wote ni watu wapgania haki Wazalendo na hawapendi kuburuzwa ila JPM hana mfano kwa hawa waliopo he was something else, special and very unique person.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…