Kama ni wa kufuata sheria, sioni ni jinsi gani unaweza kuwa u-dikteta.Tofauti: Lissu kwake utawala wa sheria ndio kila kitu. Hakuna aliye juu ya sheria na hakuna huruma katika kutekeleza sheria. Hakuna mtu kusamehewa hata kama kakosea kwa “nia njema”. No flexibility, no leniency, no double standards. Ni adhabu tu. Hapo ndipo ulipo udikteta wa Tundu Lissu.
Lakini hata tukiupa jina la udikteta; udikteta huu ni mzuri sana kwa mazingira kama yaliyopo Tanzania. Watu hapa wanapenda kusukumwa ndipo waweke bidii kwenye maisha yao. Maofisini, hivyo hivyo.
Unajuwa, pamoja na kuwa na kinachoitwa 'Democracy' katika baadhi ya nchi, lakini viongozi wa nchi hizo walionekana kufanya udikteta ilipohitajika kuwa hivyo ili kuleta mabadilko ya haraka katika nchi zao. Korea Kusini ni mfano mzuri sana wa hali hii.
Tanzania sasa hivi tunataka sana kiongozi asiyechezea mali za umma kwa njia yoyote. Tunahitaji kila hicho kidogo kusukuma mbele maendeleo ya nchi hii.
Kuchekacheka kwa akina Kikwete/Samia, hakutupeleki kokote.