Ukweli ni kwamba Mbagala ina ardhi nzuri kuliko Bunju, Tegeta na Msasani

Bei ya Viwanja huko Tegeta, Bunju na Boko ni kubwa mno ukilinganisha na Mbagala, lakini linapokuja suala la Mvua Mbagala haina mafuriko kabisa kulinganisha na Tegeta, Bunju na Boko.

Sasa kinachowafanya wengi kukimbilia huko ni nini?
Hao wa Tegeta wanaamini Mbagala ndo kajamba nani korido of laifu
 
Tatizo la mbagala ni hapa nyuma mbele jalala🎶🎶
alieimba mwimbo huo, kipindi hicho akiishi tandale kwa mtogole, aliamua kutetea kwao kwa kuwasakizia maeneo ya wenzake. Uhalisia kwa Mtogole kuko ovyo ndio mana amepakimbia
 
Kisarawe haina maendeleo kwa sababu hiyo watu wanaoweza kuishi pale ni Waha kutoka Kigoma wengi wanapakimbia...
 
Kufuata mkumbo tu, hakuna cha zaidi, nataka niende vikindu nikanunue eneo la kutosha, nimechoka na dhahama za Bunju.
Mwaka 2022 nilinunua huko Vikindu. Ilibidi niuze tu.

Maeneo yanapimwa kwa futi, viwanja ni vidogo na vimesongamana; usafiri ni shida kutokea pande zote za Dar.

Labda ukaishi huko na ukienda Dar uishie Mbagala Zakhem.

Viwanja vya kusini ni changamoto kwa mtu anayependa ustaarabu wa Kizungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…