Mkuu
britanicca , they are competent, ila ajali ni ajali.
Poleni kwa ajali ya ndege Bukoba!. Bukoba sijui vipi?, Tangu Vita vya Kagera, ndio vita iliyoua watu wengi Tanzania kuliko vita nyingine yoyote nchini Tanzania. Ukaja ugonjwa wa Ukimwi, ukiitwa Juliana, Bukoba ndio the most hit kabla ya kusambaa kungine kote!. Ikaja ajali ya MV Bukoba ni Bukoba, hii ndio ajali kubwa ya meli iliyouwa watu wengi kuliko ajali nyingine yoyote ya meli Tanzania!. Likaja Tetemeko la Ardhi Bukoba, ndilo tetemeko kubwa kuliko matetemeko yote Tanzania, na sasa hii ajali ya ndege ya Precision Air Bukoba, ndio ajali kubwa ya ndege iliyo ua watu wengi kuliko ajali zote za ndege nchini Tanzania, imetokea ni Bukoba!.
Pamoja na majanga haya, pia kuna mambo mazuri ya Bukoba. Ingefanywa sensa ya wasomi wa kiwango cha Ph.D unaweza kukuta watu wa Bukoba ndio wanao ongoza kwa idadi ya Ph.D na ma profesa,
Chakula kinachoongoza kwa protein ni senene akifuatiwa na kumbikumbi wanapatikana Kagera.
Kuna fani fulani ambayo Baganda women wanaongoza bara la Africa, baada ya Baganda wa pili ni Bahaya!.
Pia kwenye tiba asili Bukoba wanaongoza kwa most effective tiba asili wakifuatiwa na Wamasai na pia Bukoba ndio wanao ongoza kwa utaalamu wa mambo fulani, hivyo vitu kama shuntama na limbwata is real na sii mchezo bila kusahau kile kijiji cha ile siku ya Gulio ya kwenye kitabu cha Kiswahili Darasa la 4 la zamani!.
Poleni sana ndugu zetu wa Bukoba.
P