Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?

Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?

eti mtu kaenda exile mtu wanadai kumvua mchango wake kwa nchi hii na kumwita coward, fraud, hana balls na kadhalika. madai yanaendelea kwamba alikimbia "moto jikoni". sasa tizameni hoja
hii hapa chini ambayo mtu huyo huyo anayewakadia watu "waliokimbia moto jikoni" ameitoa sehemu nyingine

"Most of us knew his name by reading his articles and opinions in Mzalendo, Daily News and Uhuru; He was one of the leading nationalists of his time and indeed a patriot of Africa, a true son of our beloved motherland..." tukuitaje mwenzetu? http://mwanakijiji.podomatic.com/entry/2007-11-23T10_20_20-08_00

kama nilivyosema hapo awali mtu kuondoka nchini kwake hakuondoi uzalendo wake au uchungu kwa nchi yake. mifano wa wanamapinduzi wa aina hii wapo wengi na michango yao naiheshimu sana.
 
amiri jeshi kajificha sio tatizo anashambuliwa waziri aliyejitokeza. sasa huko mafichoni amiri jeshi alikuwa
na mawasiliano na waziri wake? hamjiulizi hilo!
 
Marehemu Sekou Ture alifanya mazungumzo na Rais Nyerere kuhusu kurudi nyumbani kwa Oscar Kambona na Kassim Hanga na Mwalimu alitoa msamaha ili viongozi hao warejee nchini.alitangulia Kassim Hanga lakini Mwalimu alimdhalilisha katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mnazi mmoja kwa kumtukana matusi makubwa na kisha kumrudisha Zanzibar ambako alipotea na hata mwili wake haujaonekana hadi leo.Mwenzake Kambona kuona hivyo akaamua kubaki Uk.
Kassim na Kambona wote wanastahili kuandikwa katika historia kama mashujaa waliopokonywa utu wao na utawala wa kidikteta wa Mwalimu.Ulizeni madingi wa enzi zile.

mzee, unadhani hili litazungumziwa? we acha tu
 
Heshima kwa wote waliochangia madaa hii.

Nimesoma hii mada nimeamua kutoa mchango wangu mdogo. Kambona alikuwa na mabaya na mazuri yake. Amefanya mengi mazuri katika kipindi kifupi alichokuwa kiongozi. Mchango wake mkubwa ni kwenye harakati za kupigania uhuru wa Tanzania na katika ukombozi wa nchi za Afrika ya kusini. Alitoa mchango kwenye harakati za TANU; hapo mchango wake sio mdogo. Na pia alikuwa ni mmoja wa viongozi wa kwanza baada ya uhuru kujaribu kujenga nchi.

Kwa upande mwingine, Kambona alitoa mchango mkubwa kwenye mapambano ya uhuru katika nchi za Afrika ya Kusini. Alikuwa na power sana katika kushughulikia vyama mbali mbali vinavyopigania uhuru vilivyokua na ofisi Tanzania au wale waliokuwa wanajaribu kufungua ofisi. Kwa mfano, baadhi ya viongozi wa FRELIMO walitegemea sana support yake. Pia kikundi cha wakina Mugabe na wenzaki waliotoka ZAPU na kuunda ZANU wasingeweza kupata support ya Tanzania na nchi za Kiafrika kama Kambona asingewalinda. PAC na vyama vingine walimtegemea sana Kambona katika jitihada zao za kupokelewa na Tanzania na nchi nyingine. Mchango wake katika ukombozi wa Africa ya Kusini ni mkubwa sana kama Chairman wa ALC.

Yeye alikuwa mmoja wa watu walioshiriki kusaidia mapinduzi ya Zanzibar. Ni kweli pia kwamba bila Kambona ile army mutiny ya 1964 ingeweza kuwa na matokeo mabaya. Yeye alienda kuongea na wanajeshi waliochoshwa kuona mabadiliko kati yao na wazungu yalikuwa yanaenda polepole sana, moja kati ya sababu walizotoa. Nyerere na Kawawa walikuwa wemejificha wakati Kambona amejitolea kusuluhisha hilo tatizo.

Kuna mengine mengi mazuri aliyofanya. Na kwa kiasi fulani baadhi ya vitu alivyokataa kuhusu sera za Kijamaa alikuwa sawa. Lakini tukumbuke kwamba Kambona pia alikuwa na mtatizo yake.

Kuna ripoti nilipata ambazo nyingine bado sijaweza ku-confirm ambazo sio nzuri sana. Nilisoma mahali kwamba alifeli mtihani wa sheria huko London. Alikuwa na nafasi ya kurudia huo mtihani, lakini akaamua kurudi nyumbani. Sijaweza kucheki kama ni kweli au laa.

Kambona pia alifanya blandaa kadhaa. Kwa mfano wakati wa scandal ya Frank Carluchi, Kambona alihamaki akaongea na vyombo vya habari bila kujadili na wakubwa wengine. Matokeo yake kukawa na major diplomatic scandal. Jamaa wa usalama walikuwa wanasikiliza simu kati ya maofisi wa ubalozi wa Marekani (Dar na Zanzibar) wakasema kwamba walikuwa wanapanga mpango wa kupindua nchi. Nyerere alikasirishwa sana na jinsi Kambona alivyo deal na hiyo ishu publicly.

Kwa kweli sioni sababu ya Nyerere kumuonea wivu Kambona. Nyerere alikuwa mbali sana ya wenzake. Uwezekano wa Kambona kuchukua power kutoka kwa Nyerere ulikuwa mdogo. Ila nimeona kulikuwa na msukumano kati ya Kambona na Kawawa. Hawa wawili walikuwa wanashindani.

Baadhi ya ripoti za Waingereza na Wamarekani kuhusu wakati huo zinachekesha. Kuna moja inasema Kambona alikuwa anapata matatizo ya akili katika hicho kipindi kigumu. Huo ulikuwa uzushi tuu. Kuna ripoti nyingine ya Wamarekani inasema waliambiwa kwamba Kambona amediposit dola 10,000 kwanye Barclays bank pale Dar. Wanasema alipewa na Wachina. Hiyo ripoti inaweza kuwa na ukweli. Katika kipindi cha Cold War, Wamarekani, Wachina, Warusi, na Waingereza walikuwa wanatoa mapesa kwa viongozi ili kupata influence. Kambona alikuwa katika nafasi nyeti sana kwenye mambo ya serikali na ALC na jamaa walikuwa wanamuandama na mapesa.

Nina mengi mazuri niliyosoma kuhusu kipindi alichokuwa kiongozi kulingana na mabaya. Tatizo langu kubwa ni pale alipoondoka. Alianza kampeni kubwa ya kujaribu kupindua nchi. Alikuwa anapata wapi pesa bado sijaweza kujua kwa uhakika. Ile ripoti moja inasema alienda Portugal akapewa pesa na serikali ya Salaazar. Hilo lilikuwa jambo hatari sana kwa kipindi hicho. Akaleta ndege ndogo zikaangusha makaratasi ya propaganda. Tukumbuke hicho ni kipindi Makaburu walikuwa wanatishia kushambulia nchi. Na ni kweli kwamba baadaye, Makaruburu wilipiga mabomu Dar, moja ya hilo bomu lililipuka Salender bridge. Na pia nimeona barua Kambona alimwandikia Kwame Nkrumah baada ya kupinduliwa. Nkrumah alikuwa anasapoti mipango ya Kambona. Alikuwa anaenda Guinea kuongea na Nkrumah na kukutana na Leballo na wengine.

Cha pili nisichopenda ni alipojaribu kutumia wapigania uhuru wa nchi za Afrika ya kusini waliopo Tanzania kujaribu kupindua nchi 1969/70. Alijaribu kuwashawishi watu kama Oliver Tambo na P.K. Leballo wampe wanajeshi wao waliopo Tanzania kupindua nchi. Tambo akakaa kimya, Leballo akashtua serikali. Matokeo yake ni ANC wakafukuzwa Tanzania.

Nikiangalia kile kipindi alichokuwa mmoja wa viongozi wa Tanzania, naona kwamba Kambona alitoa mchango mkubwa na ningependa kuona historia ya hawa wazee inaandikwa. Nasikitika sana kuona hawa wazee wanatutoka tuu bila kutuachia vitabuu tujue ubaya na uzuri wa historia ya nchi yetu.
 
Jukwaa la Historia

Kurasa hazijafungwa bado

...Kuna mtu anaweza kutuambia kuhusu Kambona, mtu huyo bado yupo hai na aliwahi kuwa msaidizi wa karibu wa Mwalimu Nyerere na Kambona; mtu huyo aliwahi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kama Mwalimu alikuwa na nafasi yoyote ya kumlipa Kambona na kumpa Urais hata wa heshima ni kumchagua mmoja wa wasaidizi wake Kambona na kumpa nafasi kubwa. Mwalimu alitoa nafasi hiyo kwa mmoja wa wasaidizi wake Kambona kuwa Rais wa Tanzania, msaidizi huyo wa Kambona ambaye alikuwa ni mwandishi wake wa hotuba na baadaye mhariri wa magazeti na msaidizi wa Rais ... yes you guessed it!! it is him.

mzee hapa imebidi nicheke tu, kwi, kwi, kwi. kweli apendaye chongo huita kengeza. wengine wakisema effect za siasa za mwalimu unasema miaka zaidi ya ishirini imepita tangu mwalimu aachie uongozi (hoja ambayo sina tatizo nayo). lakini mzee ben kuwa mwandishi wa kambona huoni suala la muda kupita. halafu zaidi kwa kulinganisha muda influence ya mwalimu kwa ben ni ya karibu zaidi kuliko ya kambona hilo hulioni. jee utasemaje kuhusu mwalimu kuwa alikuwa anakwenda likizo bagamoyo na kufikia nyumbani kwa mzazi wa muungwana?
 
mzee, unadhani hili litazungumziwa? we acha tu

Kafara mbona unalialia kama mtoto?

Unategemea nani akuzungumzie kile unachotaka kizungumzwe? Kwa nini unataka kulazimisha watu wazungumze kile unachotaka wewe?

Yote uliyonayo unaweza kuyazungumza hapa na umekuwa tu ukiyazungumza hapa all the weekend. Hii topic imekuwa hapa for all these days na sijaona hata mtu mmoja akikuzungumzia kusema kuwa Kambona alikuwa hero.

Tatizo ni kuwa ukisikia opinion nyingine kwenye hili unaanza oohh watu hawasemi chochote cha Kambona. Sema tu hawasemi unachopenda!

Kambona kwangu ni coward na ballzless guy. Nimesema hapa na unaweza kuniua ukipenda ila that is my opinion. Nawewe sema ya kwako na uyasimamie si kuanza kulialia kama Kambona!
 
Hii topic ukiisoma vizuri mwanzoni wakati watu mkianza kujisifia sijui ubaharia, ukaribu na watoto wa wakubwa, na personal story kibao hapo ndipo ilibadilika ikawa kibweka.

Mimi sihamishi thread na hata hivyo I care less kama hii iko hapa kwani kama mtu unataka kuendeleza story zako kuwa ulikuwa wapi wakati wengine hapa hatujazaliwa itakuwa ni vyema ukiziweka hapa kwenye vibweka!

La sivyo inabidi uende:

nimechukiakwasababunimeshindwakuongeastoryzangukwenyevibweka.co.?
 
mkuu maswali, karibu. shukurani kwa mchango wako ambao binafsi naona ni balanced. sidhani kama kuna hoja kwamba kambona alilingana na mwalimu, la hasha. na wala sidhani kama dhana ni kutaka kambona kumpiku mwalimu.

hoja ni kwamba pamoja na makosa ya kisiasa aliyoyafanya kambona pia alikuwa na mema mengi tuu aliyoyafanya kwa nchi hii na anastahili nafasi yake katika historia ya nchi hii.

matusi ambayo mzee huyu alitukanwa na hata watoto wadogo haikuonekana kosa kumuita malaya na kadhalika nadhani yalipita kiasi. nchi ilisahau hata tamaduni kwamba mtoto hatukani mkubwa tena kwa nyimbo na vigerere. nadhani hiyo ilikuwa adahabu tosha na sasa umefika wakati wa kuweka mambo sawa.

kukosa kambona alikosa kama ambavyo viongozi wengine walivyokosa. kuna mahali mkjj kaita makosa yaliyofanyika wakati wa "operation villagization" yalikuwa "criminal" swali nani aliwajibishwa? watu hawakufa? walilipwa fidia? yapo mengi tuu ambayo watu wakitazama nyuma wengine wanatoa machozi. lakini jee makosa hayo ndiyo yafanye historia ikatae michango mema ya viongozi wetu? la hasha.

tuwaenzi viongozi wetu kwa michango yao.
 
Hii topic ukiisoma vizuri mwanzoni wakati watu mkianza kujisifia sijui ubaharia, ukaribu na watoto wa wakubwa, na personal story kibao hapo ndipo ilibadilika ikawa kibweka.

Mimi sihamishi thread na hata hivyo I care less kama hii iko hapa kwani kama mtu unataka kuendeleza story zako kuwa ulikuwa wapi wakati wengine hapa hatujazaliwa itakuwa ni vyema ukiziweka hapa kwenye vibweka!

La sivyo inabidi uende:

nimechukiakwasababunimeshindwakuongeastoryzangukwenyevibweka.co.?

binafsi sikuchukiikabisakwauamuziwakohatakamahaunifurahishi.co

lakini mbona ziko thread nyingi tuu kwenye siasa ambapo watu wamefika mahali wakachombeza vituko na kisha hoja zikaendelea?

mwk nadhani hii hoja umeionea kwa vile tayari unao msimamo wako kuhusu muhusika mkuu, msimamo ambao nauheshimu sana tu.

hata hivyo nimekusikiakwasautikubwatuu.co
 
Kafara mbona unalialia kama mtoto?

Unategemea nani akuzungumzie kile unachotaka kizungumzwe? Kwa nini unataka kulazimisha watu wazungumze kile unachotaka wewe?

Yote uliyonayo unaweza kuyazungumza hapa na umekuwa tu ukiyazungumza hapa all the weekend. Hii topic imekuwa hapa for all these days na sijaona hata mtu mmoja akikuzungumzia kusema kuwa Kambona alikuwa hero.

Tatizo ni kuwa ukisikia opinion nyingine kwenye hili unaanza oohh watu hawasemi chochote cha Kambona. Sema tu hawasemi unachopenda!

Kambona kwangu ni coward na ballzless guy. Nimesema hapa na unaweza kuniua ukipenda ila that is my opinion. Nawewe sema ya kwako na uyasimamie si kuanza kulialia kama Kambona!

naona unanitafuta. tafadhali sana naomba uishie hapo hapo! stop!
umejaribu kuchombeza vijineno vyako nimekustahi lakini naona sasa
unakoenda siko. binti wa kike aste aste. we unapenda sana kushutumu wenzio wanalialia kama watoto, wewe wakati unalia mbona huji kutangaza hapa. kila thread mtu akitofautiana na weye unaaza za kuleta "ooh usilielie" unadhani unavyolia wewe kila mtu analia!
 
Hii pia ilikuwa ni trick ya Nyerere, kufanya hoja za wenzake zionekana za kiendawazimu na vituko....urithi mzuri, halafu wewe(unajijua) unashanga pale JMK anaposema kelele za wapinzani hazimnyimi usingizi. Kimsingi ni kwamba mnatumia "same play book" na mwalimu wenu ni Nyerere!!. Mie sishangai kwa MKJJ na boo wake (jina kapuni) kushabikia hii kuwa udaku/kibweka, hayo ni matusi ya bei ya dezo na aibu nyingi ziwafikie. Kwa mawazo yao wao, wanadhani kwamba hapa watu wanashindana kupata mshindi kati ya Kambona na Mchonga......ukweli ni kuwa hatushindani, ni jaribio tu la kuweka historia sawa na kila mtu apate haki yake kwa mchango alotoa kwa Tanzania.

Binafsi, vyovyote itakavyokuwa, ila nimefurahi kupata fursa ya kutoa na kuona madukuduku ya wengine juu ya marhumu Julius. Bottomline hapa ni kuwa yupo xposed ki-legacy than ever. Kama nyie mtatangaza ushindi, that's fine, ila mkae mkijua hakuna free ride tena ya kupotosha ukweli na WE WILL BE BACK (ina accent kama ya Governator wa Cali).!!
 
Kafara,
Huyo ndio alivyo, ndio ANN COULTIER wetu wa JF. MKJJ ni Rush Limbaugh with some brain. Usishangae sana kwa tabia hiyo walionayo..........kwani kumshabikia Nyerere hapa, na kuzima hoja za wengine kwa matumizi ya lugha za kejeli ndio ilikuwa tabia ya BWANA WAO MTUKUFU. Wewe huwezi kuwa na "fikra sahihi" kama wao, kwasababu tu hukubaliani nao(hiyo ilikuwa tabia ya Nyerere).......what a shame ktk karne na generation hii!!. Yametumika maneno hapa kama stupid, sijui huna ballz na utoto mwingine mwingi, yote ktk juhudi za ku-discredit wengine...........Ann Coultier tuliza boli na punguza masifa, katabia kako kanaanza kuboa wengi humu ndani.!!!!
 
bwana we, labda Kambona hazungumzwi.. inakuwa ni siasa anapozungumzwa Mwalimu na "vibweka" anapozungumzwa Kambona. On the other hand, labda ma MoD walipoona mambo ya Maboli na Magololi basi wakaona vimekwisha nadhani irudishwe tu kule na heading ibadilishwe kidogo iwe "Kambona: Shujaa Aliyesahauliwa?"

Nadhani kuna conspiracy imepikwa na mtu hapa ili kuipa nguvu hoja yake. Kuna mtu alisema eti topiki iligeuka kuwa kibweka pale watu walipoonesha uhalisia wa Kambona...na ndio maana topiki ikahamishwa.....mmmhhhhhh!!!!! It makes me wonder
 
Kafara mbona unalialia kama mtoto?

Unategemea nani akuzungumzie kile unachotaka kizungumzwe? Kwa nini unataka kulazimisha watu wazungumze kile unachotaka wewe?

Yote uliyonayo unaweza kuyazungumza hapa na umekuwa tu ukiyazungumza hapa all the weekend. Hii topic imekuwa hapa for all these days na sijaona hata mtu mmoja akikuzungumzia kusema kuwa Kambona alikuwa hero.

Tatizo ni kuwa ukisikia opinion nyingine kwenye hili unaanza oohh watu hawasemi chochote cha Kambona. Sema tu hawasemi unachopenda!

Kambona kwangu ni coward na ballzless guy. Nimesema hapa na unaweza kuniua ukipenda ila that is my opinion. Nawewe sema ya kwako na uyasimamie si kuanza kulialia kama Kambona!

Wewe kila mtu unasema analia lia kama mtoto wakati wewe mwenyewe kila kukicha unalia lia kuhusu Kikwete. Watu wengine bana....halafu nikikuita kinanihino unanikasirikia...
 
naona unanitafuta. tafadhali sana naomba uishie hapo hapo! stop!
umejaribu kuchombeza vijineno vyako nimekustahi lakini naona sasa
unakoenda siko. binti wa kike aste aste. we unapenda sana kushutumu wenzio wanalialia kama watoto, wewe wakati unalia mbona huji kutangaza hapa. kila thread mtu akitofautiana na weye unaaza za kuleta "ooh usilielie" unadhani unavyolia wewe kila mtu analia!

Nadhani kile kidubwana kimeanza kumtekenya au kuwasha....kwikwikwiiiii....
 
Mkishindwa hoja sasa mnaleta vioja kwa kushambulia watu.

a. Binafsi sijasema hii mada ni ya vibweka nimesema ilihamishwa huku baada ya mimi kumexpose Kambona a hero who turned into a political fraud. Hapo ndipo ilipohamishwa. Lakini sikulilia irudishwe kwenye siasa kwani sijali sana mada ziko wapi, najua pa kuzifuata.

b. Pili, tofauti na wengine ambao wanajifanya wanamuenzi Nyerere lakini ndani yao wamejawa na chuki (angalia mada hii ilivyoanza) utaona kuwa watu walitaka tukubaliane tu kiurahisi kuwa Kambona was a hero that Tanzania never had na Mwalimu ndiye mtu mbaya, watu wamemuita na wanaendelea kumuita Nyerere Dikteta. Sasa watu walidhani watu hawamfahamu Kambona na aliyoyafanya alipotoka hapa. Tumeyaweka wazi na sasa badala ya hoja kujibiwa kwa hoja tunaanza kuletewa vioja. Mnakaribishwa.

c. Maneno yangu nayapima vizuri sana na kila neno ninalichagua vizuri. Hakuna mahali hata pamoja ambapo nimekataa mchango wa Kambona au nafasi yake katika historia yetu. Hakuna mahali ambapo nimesema Kambona asienziwe hakuna hata mtafute vipi. Nilichoonesha ni kuwa Kambona baada ya kukimbia nchi he turned into a political fraud, yes he did. Ushujaa wake wote ulikuwa kabla hajaondoka nchini na kama kuna sababu yoyote ya kumuenzi ni sababu ya kilichofanyika kabla hajatimka. Tukukibaliana hilo, tutatendelea kufuatilia tumuenzije?

d. Wale ambao hawataki Kambona achumbuliwe wasingempa ushujaa wa chee! Kuna mengi ya Kambona ambayo hatukuambiwa na sasa yanaanza kutoka. Aliyoyasema kujaribu kuleta ghasia nchini n.k Kambona simply was a hero who never was!

Sasa wale wanaotaka kushambulia watu go ahead we have been there before lakini ukweli utakuwa ukweli.
 
Phillemon, hakuna alichofanya Kambona kwenye Maasi ambacho was extraordinary! Alichofanya ni kile ambacho alitakiwa kufanya na RAis wake na kilikuwa ndani ya majukumu yake kama Waziri wa Mambo ya Nje, na pia kama Waziri wa Ulinzi. Why is that so heroic?

ipo siku watu watamfukua wamzike upya kwa itifaki
.
sidhani kama kutakuwa na tatizo hilo isipokuwa kama itatokana na mchango wake wakati wa uhuru na miaka ya mwanzo ya jamhuri. Zaidi ya hapo sioni sababu ya kumfukua!

changamoto tulionayo sasa ni tofauti..tunao uwazi na haki na uelewa zaidi..marais wa sasa hawawezi tena kumaliza upinzani wa ndani au nje kwa njia hizi ...wanazo njia nyingine kama mnazoziona..lakini ni muendelezo ule ule!!!!!

well said..
 
amiri jeshi kajificha sio tatizo anashambuliwa waziri aliyejitokeza. sasa huko mafichoni amiri jeshi alikuwa
na mawasiliano na waziri wake? hamjiulizi hilo!

Kafara hivi umeangalia nilichosema? Maasi yalichukua siku tano! sasa ulifikiri hakuwa na mawasiliano na Kambona akajiendea kwa mandate yake na kutoa dili kwa wanajeshi ambayo hakuwa nayo? duh.. nadhani wewe ndio ujiulize, aliweza kuwatuliza askari kwa ahadi gani ambayo alikuwa na nguvu ya kuitekeleza kama Mwalimu hakuibariki.. duh??
 
Mkishindwa hoja sasa mnaleta vioja kwa kushambulia watu.

a. Binafsi sijasema hii mada ni ya vibweka nimesema ilihamishwa huku baada ya mimi kumexpose Kambona a hero who turned into a political fraud. Hapo ndipo ilipohamishwa. Lakini sikulilia irudishwe kwenye siasa kwani sijali sana mada ziko wapi, najua pa kuzifuata.

b. Pili, tofauti na wengine ambao wanajifanya wanamuenzi Nyerere lakini ndani yao wamejawa na chuki (angalia mada hii ilivyoanza) utaona kuwa watu walitaka tukubaliane tu kiurahisi kuwa Kambona was a hero that Tanzania never had na Mwalimu ndiye mtu mbaya, watu wamemuita na wanaendelea kumuita Nyerere Dikteta. Sasa watu walidhani watu hawamfahamu Kambona na aliyoyafanya alipotoka hapa. Tumeyaweka wazi na sasa badala ya hoja kujibiwa kwa hoja tunaanza kuletewa vioja. Mnakaribishwa.

c. Maneno yangu nayapima vizuri sana na kila neno ninalichagua vizuri. Hakuna mahali hata pamoja ambapo nimekataa mchango wa Kambona au nafasi yake katika historia yetu. Hakuna mahali ambapo nimesema Kambona asienziwe hakuna hata mtafute vipi. Nilichoonesha ni kuwa Kambona baada ya kukimbia nchi he turned into a political fraud, yes he did. Ushujaa wake wote ulikuwa kabla hajaondoka nchini na kama kuna sababu yoyote ya kumuenzi ni sababu ya kilichofanyika kabla hajatimka. Tukukibaliana hilo, tutatendelea kufuatilia tumuenzije?

d. Wale ambao hawataki Kambona achumbuliwe wasingempa ushujaa wa chee! Kuna mengi ya Kambona ambayo hatukuambiwa na sasa yanaanza kutoka. Aliyoyasema kujaribu kuleta ghasia nchini n.k Kambona simply was a hero who never was!

Sasa wale wanaotaka kushambulia watu go ahead we have been there before lakini ukweli utakuwa ukweli.

Ekzaktli! Kuhamisha mada ya kisiasa na kuiweka kwenye vibweka ni mfano hai wa kushindwa hoja na kuanza viroja ili kuvipa viroja nguvu ya hoja.

Yaani unataka kutuambia wewe (kwa mabandiko yako) ndio umesababisha mada ihamishwe? Kwa nini hao ma Mods hawakuuliza watu au kutoa warning kabla hawajafanya hivyo.
Sasa imehamishwa ndio mnajifanya hoja zenu zimeshinda. Kama ndio hivyo basi mmeshinda.
 
sikusema hivyo nadhani labda ni kwa mabandiko yako ndio maana ikahamishwa. Miye nikaamua kujianzisha mada yangu "Kambona: A Hero that Never Was" ikaunganishwa ni hii na ikahamishwa sasa you tell me if there is no cause and effect here. Sasa tumewashinda kwa hoja na hakuna kigeni cha Kambona ambacho hakijulikani he was a hero before independence and a hero few years after the independence but after he ran away he turned into a political fraud. Kambona had a chance to prove what he was made of and he blew it; he had time to prove to the world that Nyerere was that benevolent dictator he never did. Kambona died a miserable man which was indeed very sad. But history, will remember him rightly, a Hero who never became!

mchango wangu wa mwisho katika mada hii unless kuna mtu ataleta information nyingine ambayo hatujaijua.
 
Back
Top Bottom