Mabadiliko ya siasa nchini Tanzania kuanzia mwaka 1967 ndiyo yalisababisha kusimama kwa uchumi wa taifa.
Hili si kweli hata kidogo. Matatizo ya Kiuchumi ya Tanzania hayakutokana na kutangazwa Azimio la Arusha bali hali ya kiuchumi duniani na ukweli sisi tulifanya vizuri ukilinganisha na nchi nyingine. Kwa upande wa Tanzania mambo matatu yalitusumbua sana; Ongezeko la bei ya mafuta la 1970 lilikuwa ni pigo kubwa sana kwenye uchumi wetu na uchumi wa nchi nyingi. Kwa taifa changa hilo lilianza kutuingiza kwenye madeni makubwa. Ukame wa 1974 ukaumiza sana kilimo chetu na kabla hatujatulia tukawa na Vita ya Kagera mwishoni mwa miaka ya sabini na baada ya hapo tukiwa tumeanza kujiandaa, ukaja ukame wa 1984. Ingekuwa sisi Ethiopia tungeimbiwa wimbo wa "We are the World". But we did a lot better as a nation than most countries. Ethiopia (while united with Eritrea), Somalia, Uganda n.k did worse than us na Mwalimu hakuwa Rais wao. So kusema kwa haraka kuwa matatizo yalianzia 1967 (kwa Azimio la Arusha) is a mediocre attempt in trivilializing of history. Matatizo ya kiuchumi ya Tanzania yalikuwa na msingi mkubwa zaidi na Azimio la Arusha was the instrument used to check it, it could have been worse.
Operesheni vijiji vya ujamaa ilisababisha watu kuondolewa kwa nguvu kutoka kwenye makazi yao na mashamba yao, walikusanywa kwenye maeneo mapya yenye wanyama wakali bila nyumba wala chakula. Watanzania hawa walianza maisha mapya kwa kuanza kujenga nyumba kufyeka na kusafisha mapori na kuanza kulima, hali hii ilichukuwa miaka mingi na kipindi hiki ndicho ambacho tatitizo la ukosefu wa chakula lilianza.Wakulima walitoka vijijini kutafuta chakula mijini.
Mojawapo ya ukosoaji halali wa Mwalimu na watendaji wake ulikuwa ni utekelezaji wa zoezi la "Operesheni Vijiji vya Ujamaa" ambayo Kawawa alikuwa msimamizi mkuu. Ni kweli kabisa kuwa dhana yake ilikuwa nzuri lakini utekelezaji wake bordered criminal activities. Hilo Mwalimu pia aliliona na mojawapo ya vitu ambavyo alikiri baadaye kuwa didn't go they way he envinsioned them. Badala ya kuisukuma nchi nzima kwenda vijiji vya ujamaa kungekuwa na vijiji vya mazoezi au vya mfano ambavyo vingetumika kushawishi. Hata hivyo, leo hii vijiji vingi vilivyopo vimetokana na zoezi hilo na vinaendelea kufana which vindicates Mwalimu's vision. Leo hii, miradi na mipango mingi inajengwa kutoka vijijini (vilivyoundwa wakati wa operesheni) na imerahisisha upatikanaji wa huduma nyingi muhimu. Utekelezaji was botched? Absolutely, was it a good idea to bring all these Tanzanians in an organized form of living to bring them services and unite them at the basic social level? you betcha!
Tatizo la pili lilikuwa ni kutaifisha mabenki, bima, viwanda nyumba na mashamba ya walioitwa mabwenyenye, makabaila n.k. kutaifisha maana yake ni kuchukua mali ya mtu kwa nguvu bila ya ridhaa yake na bila kumlipa kitu chochote. Matokeo yake mashamba ya mkonge yaligeuka mapori, kwa sababu bei ya mkonge ambao ndio wakati huo ulikuwa ukiingiza fedha nyingi za kigeni iliporomoka. Magonjwa ya ajabu ajabu alianza kushambulia kahawa, nayo mavuno yakapungua kwa kiwango cha kutisha.
Ukosoaji huu una msingi lakini pia una makosa ya kihistoria na kiukweli. Je kulikuwa na ulazima wa kutaifisha njia kuu za uchumi? Mwanzoni lilionekana wazo zuri lakini kwenye utekelezaji it went far than it was necessary. Hilo nalo Mwalimu aliliona na hasa kwenye utaifishaji wa mashamba ya mazao ya biashara. Hatukuwa na uwezo na utaalamu wa kuendesha vyombo hivyo; lakini kwenye makampuni fulani muhimu Mwalimu was absolutely right. Katika Tanzania baada ya Uhuru watu wachache walikuwa na access na ownership ya njia za uchumi na kuacha kikundi cha watu wachache kumilika njia za uchumi wakati wachache ndio wanakuwa omba omba halikuweza kuvumilika.
Leo hii nchi kama Zimbabwe, Namibia, Botswana na Afrika ya Kusini zote zinatambua kwa kiasi kikubwa haja ya kuhakikisha kuwa wale wananchi wa asili wa nchi zao na wenyewe wanapata nafasi katika kumiliki njia za uchumi, nafasi za kibiashara n.k Anayedhania kuwa Waasia na Wazungu waliokuwa wanamiliki makampuni makubwa na ardhi kubwa wangekuwa na ukarimu wa kutoa nafasi kwa watu weusi mtu huyo hajajifunza historia. Watanzania wengi wangeendelea kuwa wahamiaji kwenye ardhi yao huku wakifanya kazi za kubangaiza na kufurahia kile ambacho mabwana wao wanawagaiya.
Leo hii tena Mwalimu anakuwa vindicated na historia. Tumeona jinsi gani ukiuachia ubepari ufanye utakalo inavyosababisha kutoridhika kwa wananchi. Wale wanaokumbuka political economic theories watakumbuka kuwa ubepari huundwa kwanza kabisa na kile tunachosema ni "Ukusanyaji wa Kijima wa Mtaji" (Primitive Accumulation of Capital). Leo wananchi wanapolilia kuona ardhi yao inagawanywa na madini yake yanachotowa kama maji kisimani wanamrudia Mwalimu; wanapoona mabenki yaliyokuwa "yao"yanapewa wageni tena kwa bei chee wanamkumbuka Mwalimu; hata kelele zunazopiga humu kuhusu watawala wetu ni kwa sababu tunatambua kuwa kuna vitu haviendi vinavyopaswa. Watu wasichofahamu ni kila ambacho Mwalimu alikuwa anakisema mwishoni mwa maisha yake "ubepari hauna macho".
Leo hii tunaogopa kutumia neno "ulanguzi" kwa sababu linasikika vibaya, wakati watu wanajua kabisa kuna ulanguzi wa bidhaa mbalimbali nchini. Tunaogopa kuingilia kati uwekezejai kwa sababu 'wawekezaji watakimbia' lakini hadi pale yale ya Delta Nigeria yatakapoanza kutokea Tanzania ndipo tutakapojua Mwalimu siyo tu aliona mbali, bali aliombea pia kuwa siku moja kuna kizazi cha Watanzania ambacho kitakuja na ubunifu wa kuwianisha haki za mtu binafsi na haki za jamii nzima; nafasi sawa kwa wote na uhuru sawa kwa wote. Kwa vile wameacha zile dhana muhimu za Mwalimu, watawala wetu hawana cha kusimamia.
Serikali ilifika wakati ikaliona tatizo lakini ilishindwa kusema ukweli kwa wale wote ambao mali zao zilichukuliwa. Badala yake serikali ilianza kuwaalika kama wawekezaji na siyo tena mabwenyenye.
Bahati mbaya wamebadilisha jina tu; waliorudi ni wale wale na tunatambua kwa matunda ya kazi zao. Kabaila ni nani? Ni mtu yule ambaye anamiliki ardhi kubwa ambayo anatumia kuzalisha mali kwa kuajiri vibarua na kutengeneza pesa kwa kutumia ardhi hiyo. Kina Sinclair siyo mabepari tu, ni makabaila pia! Na sasa hivi tunaogopa kusema hivyo, kwa sababu makabaila kama kina Mkapa ni watanzania wenzetu! Chupa ni tofauti, mvinyo ni ule ule.
Tunaogopa kutumia neno "unyonyaji" wakati wote tunafahamu vizuri ni nini kinaendelea. Watu wanashindwa kuelewa kuwa ubepari asili yake ni manufaa ya watu wachache na adha kwa watu wengi. Leo hii kuna mabepari wakupindukia nchini hadi Bungeni wamelundikana. Msingi wa maisha yao ni faida na faida kwa namna yoyote; kazi yao ni kuchuma wasipopanda, na kucheua wasichotafuna. Madaktari walipotaka nyongeza ya senti chache wakapigwa mkwara wa nguvu lakini mabepari wetu serikali walipojiongezea kipato wakapigiwa makofi! Sasa hivi tunaogopa kuwaita wanyonyaji kwa sababu huko nyuma wanyonyaji walikuwa weupe, sasa hawa weusi wanapotunyonya tena kwa mirija saba saba na kutuacha vimbavu mbavu huku wakiturishia nguo nzuri, Radio nzuri, luninga, na tu barabara kama twa Mwenge, tunajisikia vizuri!
Tukumbuke kuwa kosa lolote baya likifanyika kinachofuata ni kujitakasa kwa toba kwa wale wote ambao serikali iliwapora mali zao. Ni kweli wawekezaji walianza kuja nchini, tunakumbuka walivyochukua benki ya NBC watanzania tulipiga kelele nyingi jinsi walivyoichukua kwa bei ya kutupa. Lakini jambo moja la msingi ni kuwa kibaka akipora mkufu wa dhahabu atauza kwa bei yoyote atakayokuja nayo mnunuzi. Hizi benki hazikuwa zetu tulipora mali za watu na kinachofanyika sasa hivi tunauza kwa staili ile ile ya vibaka. Raisi wetu kila siku ni kiguu na njia akizungukia dunia kutafuta wawekezaji, sawa tunaowapata ndio kama akina buswagi. Bila toba kwa dhambi iliyofanywa na awamu ya kwanza, kwa kukaa na wale wote walioporwa mali zao na kukubali kosa na kuomba msamaha na kukubali kulipa fidia angalau kidogo ni hakika hatasimama kiongozi yeyote katika taifa hili akabadilisha maisha ya watanzania, bila ya kuondoa hii dhuluma taifa la Tanzania lililowafanyia mabwenyenye na makabaila.
Ndugu yangu kuna sheria katika Tanzania na kama kuna mtu anahisi amedhulumiwa afungue kesi. Lakini hata hivyo, kiongozi mzuri ni yule ambaye anakubali makosa ya kihistoria na ambaye haogopi historia yake. Ningekuwa mimi wao, nafahamu kabisa kuwa kuna watu hawakutendewa haki wakati wa utaifishaji; kuna vitu ambavyo inabidi kutengenezwa; lakini katika kutengeneza huko hatutaacha wananchi wetu wawe ombaomba kwenye Taifa leo, au wazamiaji kwenye ardhi yao. Tungetengeneza mpaka pale tu ambapo tunakubaliana na waliodhulumiwa kuwa "ni haki kwa wote". Tungewakaribisha nyumbani Watanzania waliokimbia; tungerudisha makampuni au mashamba ambayo kwa hakika hayakustahili kuwa mikononi mwa serikali, na kwa hakika tungetengeneza kwa kiasi kikubwa pale palipoharibiwa.
Kufanya hivyo kunahitaji uongozi wa kijasiri; siyo ujasiri wa maneno bali ujasiri unaotokana na uthabiti wa vitendo. Bado naamini kabisa kuwa nia ya mwalimu ilikuwa nzuri, naamini maono yake yalikuwa ni mazuri; na ninakubali pia utekelezaji wa baadhi ya maono haya haukuwa sahihi.
Ndugu zangu, sisi tuko kama Marekani. Dhana iliyounda Taifa la Marekani ilianza kwa kutangazaia dunia kuwa "We hold these truths to be self evident; that all people are created equal and endowed by their creator with certain unalieanable rights; among these ar life, liberty and the pursuit of happiness". Wakati wanaandika hilo, Marekani ilikuwa na watumwa kwa mamilioni, wanawake walikuwa hawapigi kura, na wahindi waliishi kama wageni kwenye ardhi yao! Hata hivyo ukweli wa kauli hiyo hapo juu haukundoa ukweli halisi ardhini.
Tangu wakati huo Marekani imejaribu kutengeneza kilichoharibiwa kwa kupigania umoja wa nchi hiyo katika vita vya wenyewe 1860s na baadaye katika kuondoa sheria za kibaguzi na kuwapa wanawake haki ya kupiga kura ya 1920s; kuondoa sheria za Jim Crow miaka ya 1950s na baadaye kupitisha sheria ya Haki za Kiraia ya Mwaka 1964. Hata leo hii Amerika imekuwa ni wazo ambalo linatamaniwa na linaloendelea kuwa halisia. Marekani haijafikia kuwa "mji ung'arao juu ya mlima".
Lakini haiondoi ukweli kuwa wamepiga hatua katika haki za wananchi na raia na licha ya manung'uniko ya hapa na pale Marekani haitarudia utumwa, ubaguzi n.k
Sisi nasi vivyo hivyo, tunaitwa na historia kuwa mji ung'arao pembezoni mwa Afrika. Mji ambao uliweka mwenge juu ya mlima Kilimanjaro kuleta "matumaini pasipo matumaini, upendo penye chuki, na heshima palipojaa dharau". Bahati mbaya mwali wa mwenge ule unazidi kufifia siku kwa siku huku kwa nguvu zetu zote tukiacha misingi ile iliyotuunda kama Taifa na kubakia kuwa waigizaji wa demokrasia!
Siku moja hata hivyo inshallah, atasimama kiongozi katika Taifa letu ambaye atakuwa na ujasiri wa kutengeneza palipobomoka; kujenga pasipojengwa na kulinda vilivyokwishajengwa. Kiongozi huyo yupo na siku moja atakuja. Yawezekana ikawa katika kizazi chetu au kizazi kingine. Tusikate tamaa kwa Taifa letu na tusirudi nyuma kwa aibu! Tusonge mbele enyi wana na mabinti wa Tanzania, tusimame wa moja licha ya tofauti zetu, na pamoja tuongeze juhudi za kuhakikisha kuwa "Taifa huru, la watu sawa, na lenye utu ambalo ni la watu, limetoka kwa watu na ni kwa ajili ya watu litaendelea kuwepo na halitaondoshwa kwenye uso wa dunia!"