Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?

Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?

Je NASA ni ujamaa wa kuzalisha mali au ujamaa wa matumizi ya umma. Ukitumia kodi, pesa, au nguvu za wananchi kufanya uzalishaji wa kitu chochote (iwe kwa faida au sio kwa faida) kwa manufaa ya jumuiya hiyo, basi hiyo ni social production - au uzalishaji wa kijamaa (emphasis on social (jamii)).

Sipingani nawe katika hili!

Si kweli, nchi nyingi za kimagharibi zinatumia pia ujamaa kuzalisha mali - kumbuka kuwa public transportation katika nchi zote za magharibi mara nyingi inagharimiwa na serikali. Transportation pia ni part ya uzalishaji na kama inagharimiwa na serikali au public au walipa kodi basi hiyo inakuwa social production (ujamaa).

Hilo fungu la kulipia gharama kama linatokana na pesa za kodi au michango ya wananchi kama jumuiya basi huo ndio ujamaa wenyewe. Waulize hata mabepari wenyewe wa kimarekani watakuambia kuwa AMTRAK inaendesha kijamaa na conservative wengi wanataka serikali iache kujiingiza kwenye biashara na uzalishaji. Kumbuka kuwa uzalishaji ni vyote - bidhaa na huduma (goods and services)

Kumbuka pia kuwa hiyo research and development ni part ya uzalishaji (production) na bila hiyo basi hakuna cha kuzalishwa. Kama NASA kazi yake ni research basi ujue kuwa NASA inajihusisha na uzalishaji kwa kutumia pesa za jamii (social production)kitu ambacho kinafanya kazi za NASA ziwe part ya uzalishaji wa kijamaa

Hicho kipindi lazima kiwe kirefu au kifupi kwa kiasi gani? miaka 5, 20, au 100?

Labda usome tena maana ya ubepari. Ukisoma utajua kuwa hata kutumia kodi ya watu wengine kwa kufanyia uzalishaji wako basi umekiuka misingi ya ubepari. Waroma walitumia utumwa (nilikisema hiki kule juu) kujenga himaya yao - huu sio ubepari.

Sheria ya waroma ilimpa nguvu mfalme wa nchi kuliko raia wa nchi katika mipango yote ya kiuchumi na kijamii (kinyume na misingi ya kibepari). Mambo mengi ya Roma yalifanywa kwanza kwa faida ya mfalme na ufalme kabla ya faida binafsi (hii ni moja ya forms za kijamaa).

Mabepari wenyewe duniani wanapinga kuwa hakuna mfumo kamili wa kibepari kama vile wanauchumi walivyokubali kuwa hakuna pure or perfect competition market. Nakushangaa kuwa bado unabishia hili!

Kwa mawazo unayotoa hapa naona ni afadhari wakoloni warudi tu watutawale. Uhuru tulipata mapema.

Na jinsi navyosoma posti zako, naanza kupata imani kubwa kuwa nyinyi mnaomfuata Nyerere kwa sehemu kubwa ni MAMBUMBU na hamjuhi alikuwa anasema nini?

KAMA MNGEJUA NYERERE ANASEMA NINI, mzee wa watu hasingeacha nchi katika hali mbaya ya kiuchumi.

Unachoeleza kuhusu ROMA ni UTUMBO MTUPU.

Sijaeleza UJAMAA NA UBEPARI KWA KUTUMIA ANALOGY YA BINARY NUMBER (TRUE, FALSE). Natumia ANALOGY YA FUZZY LOGIC. Nchi ni ya kibepari iwapo zaidi ya 70% ya miundo mbinu yake ni ya kibepari.

Nyerere alimwita Kenyatta pure capitalist lakini serikali ya Kenyatta ilikuwa na makampuni ya kiserikali. Hayo makampuni hayafanyi serikali ya Kenya kuwa ya KIBEPARI-UJAMAA.

Nyerere pia alikuwa pure mjamaa, lakini aliwaachia watu kufanya biashara na kumiliki. Lakini haitafanya serikali yake kuwa UJAMAA-KIBEPARI.

Serikali ya mkoloni ilikuwa inamiliki shirika la reli, ndege, meli n.k, lakini itaendelea kuitwa serikali ya kikoloni kwa sababu vitu hivyo vilikuwepo ku-support ukoloni. Hatuwezi kusema tulikuwa na UKOLONI-UJAMAA.
 
Mwafrika, sidhani watu wako tayari kuangalia comprehensive factors za kwanini tulishindwa, kwao tatizo ni nyerere na sera tu. Unapopanua swali lako hilo na kujiuliza je nchi zote ambazo hazikuwa na Azimio la Arusha (Zimbabwe), Kenya, Uganda n.k zilifanikiwa zaidi kuliko sisi? Hivi miaka 46 baadaye nchi ambazo zilikuwa na watu walioukumbatia ubepari kama Zaire zimekuwa na mafanikio zaidi kuliko sisi.

Kila nikiangalia, naona we really faired better than; na hakuna anayeweza kusema kuwa kama tungefuata sera za kibepari tungekuwa mbali sana. Yawezekana tungekuwa mbali kama Ghana, Ivory Coast, Sierra Leone, Liberia au Ghana...

Good point,

Inaonekana hapa issue ni kupondea tu kila alichofanya Nyerere (the same way waliompondea Kambona hapa) bila kuweka perspective ya mambo yote. Inafurahisha kuona kuwa wewe umeamua kuchukua yale mazuri ya Nyerere na kuacha mabaya.

Wakati wamarekani wanaanzisha social securiy Administration, ilikuwa vigumu sana kutumia neno social maana hili lilikuwa linaenda moja kwa moja kwenye socialism (ujamaa). Kuna mtu alitaka waiite individual capital security administration ili iendane na capitalism ila wakajiona kuwa watakuwa wanaongopa.

In the end, wakaiita social security administration (they should have anyway) na wakasema hicho anachosema Bin Maryam kuwa ohhhh huu ni ugawanaji tu wa kijamaaa na wala sio uzalishaji wa kijamaa.

Bottom line hakuna nchi iliyofanikiwa kwa ujamaa au ubepari peke bila kuchanganya vingine. Matatizo ya Tanzania yaliletwa na vitu zaidi ya kujiita ujamaa peke yake ingawa inawezeka pia sense ya ujamaa ndiyo ilisukuma kutumia rasilimali za Tanzania kusaidia nchi za kusini kupata uhuru.
 
Kwa mawazo unayotoa hapa naona ni afadhari wakoloni warudi tu watutawale. Uhuru tulipata mapema.

Sikutegemea kuwa ulielekea huku!

Na jinsi navyosoma posti zako, naanza kupata imani kubwa kuwa nyinyi mnaomfuata Nyerere kwa sehemu kubwa ni MAMBUMBU na hamjuhi alikuwa anasema nini?

yoooooo, mbona majina tena ndugu yangu?

Tafuta post moja niliyomfuata Mwalimu na ninakuahidi kuwa nitajiita Mbumbumbu mwenyewe from today on...

KAMA MNGEJUA NYERERE ANASEMA NINI, mzee wa watu hasingeacha nchi katika hali mbaya ya kiuchumi.

Sidhani kama nimekupinga kuwa Nyerere akuacha nchi katika hali mbaya kiuchumi. Nilichosema ni kuwa hali mbaya ilisababishwa na mambo mengi zaidi tu ya term ujamaa.

Unachoeleza kuhusu ROMA ni UTUMBO MTUPU.

Ni vizuri kuona kuwa unaweza kuona hoja zangu kama utumbo mtupu badala ya kuacha wasomaji wakaamua wenyewe.

Sijaeleza UJAMAA NA UBEPARI KWA KUTUMIA ANALOGY YA BINARY NUMBER (TRUE, FALSE). Natumia ANALOGY YA FUZZY LOGIC. Nchi ni ya kibepari iwapo zaidi ya 70% ya miundo mbinu yake ni ya kibepari.

Haijalishi utakuja na namba gani au jina gani la kihesabu ila in the end umeshindwa kutoa mfano hata wa nchi moja ambayo imetumia ubepari peke yake kufanikiwa.

Nyerere alimwita Kenyatta pure capitalist lakini serikali ya Kenyatta ilikuwa na makampuni ya kiserikali. Hayo makampuni hayafanyi serikali ya Kenya kuwa ya KIBEPARI-UJAMAA.

Nyerere pia alikuwa pure mjamaa, lakini aliwaachia watu kufanya biashara na kumiliki. Lakini haitafanya serikali yake kuwa UJAMAA-KIBEPARI.

Hapa sasa ndipo unarudi kwenye point kuwa hakuna pure ujamaa au pure ubepari. Watu walijiita majina tu lakini ukisoma tafsiri ya neno ujamaa na ubepari utakubali kuwa hakuna nchi yoyote imetumia kimojawapo peke yake na kufanikiwa.

Asante sana kwa kutafuta common ground

Serikali ya mkoloni ilikuwa inamiliki shirika la reli, ndege, meli n.k, lakini itaendelea kuitwa serikali ya kikoloni kwa sababu vitu hivyo vilikuwepo ku-support ukoloni. Hatuwezi kusema tulikuwa na UKOLONI-UJAMAA.

Sijui hili linahusiana vipi na mada hii ila naona tu unazidi kukubali kuwa hakuna nchi yoyote duniani iliyotumia ubepari pekee kujipatia maendeleo. Colonial masters (nchi za kimagharibi) ndio waliendesha hizo reli, ndege nk na kisha faida ikatumika kujenga uchumi kwenye nchi zao - huu si upepari hata kidogo.
 
MKJJ,

..kwanini tunakuwa na hii hali ya kukata tamaa? why should we compare ourselves with failures in africa--mobutu and the likes?

..nisaidie ndugu yangu. mimi naona we had all the reasons[unity,patriotism,...] to succeed under nyerere, yet we failed.

Mwafrika,

..i am not really concerned about political ideologies. i am interested with economic performance, and results of the policies that were being implemented.

..wewe mwenyewe umeelekeza kwamba hakuna nchi ambayo ni 100% capitalist au socialist.

..ninavyoelewa mimi a well managed factory will efficiently produce regardless of whether it in a communist or capitalist country. the same applies to an entire economy.
 
Mwafrika, sidhani watu wako tayari kuangalia comprehensive factors za kwanini tulishindwa, kwao tatizo ni nyerere na sera tu. Unapopanua swali lako hilo na kujiuliza je nchi zote ambazo hazikuwa na Azimio la Arusha (Zimbabwe), Kenya, Uganda n.k zilifanikiwa zaidi kuliko sisi? Hivi miaka 46 baadaye nchi ambazo zilikuwa na watu walioukumbatia ubepari kama Zaire zimekuwa na mafanikio zaidi kuliko sisi.

Kila nikiangalia, naona we really faired better than; na hakuna anayeweza kusema kuwa kama tungefuata sera za kibepari tungekuwa mbali sana. Yawezekana tungekuwa mbali kama Ghana, Ivory Coast, Sierra Leone, Liberia au Ghana...

Mwanakijiji:

Kudidimia kwa nchi za kiafrika kunatokana zaidi na phenomena inayoitwa Dutch Bonanza.

Inaonyesha kabisa kuwa nchi za Asia ambazo Natural Resource sio msingi wa maendeleo, zimeendelea.

Na nchi za kiafrika au Kiarabu ambazo pato lake limetegemea sana Natural Resource (Dutch Bonanza) zinadidimia au kuwa kwenye matatizo ya kijamii.

Mobutu akipata pesa za almasi anakwenda kujirusha Brussels akitegemea kuwa mgodi wa almasi utaingiza tena pesa. Hajui kuwa soko la dunia linabadilika na mitambo ya kuchimba almasi inachakaa.

Nyerere na Kwame watataifisha mashamba ya katani na kakao kupata hela za kusomesha wanafunzi na kutoa huduma za afya. Lakini walichosahau kuwa matumizi ya katani yatapungua na wazalishaji wa kakao wataongezeka. Na vilevile wanasahau kuwa wafanyakazi wa mashamba hayo nao wanahitaji maslahi na uongozi mzuri katika mashamba.

Ivory Cost wao wanatumia pesa ya kakao kuifanya Abdajan kuwa Paris kimajengo.

Kulikuwepo na Naivette katika masuala ya financials karibu katika nchi zote za Kiafrika.
 
MKJJ,

..kwanini tunakuwa na hii hali ya kukata tamaa? why should we compare ourselves with failures in africa--mobutu and the likes?

..nisaidie ndugu yangu. mimi naona we had all the reasons[unity,patriotism,...] to succeed under nyerere, yet we failed.

Mkuu Joka kuu,

Ukiona kuwa tumeshindwa hata kama tulikuwa na all reasons basi ujue kuwa inawezekana tatizo liko/lilikuwa zaidi kwetu as people na sio sera za ujamaa na Nyerere peke yake. Inaonyesha pia kuwa kuna factors zaidi zimechangia na sie wote tumekuwa responsible kwa failures zetu na ndio maana tunatafuta suluhisho hapa.

Mwafrika,

..i am not really concerned about political ideologies. i am interested with economic performance, and results of the policies that were being implemented.

..wewe mwenyewe umeelekeza kwamba hakuna nchi ambayo ni 100% capitalist au socialist.

..ninavyoelewa mimi a well managed factory will efficiently produce regardless of whether it in a communist or capitalist country. the same applies to an entire economy.

Amina mkuuu,

Afadhali nawewe pia umeona hili ila nakuhakikishia ukiendelea kusema hivi kuna watu hapa watakuita mfuasi wa Nyerere. Kuna ukweli kuwa maendeleo ni zaidi ya ideology au majina. Unajua Kenya sasa hivi kuna chama kinajiita kuwa chama cha muungano wa kitaifa lakini ukweli unabaki kuwa hicho chama ni cha kikabila kuliko kinavyodai. Bush alianzisha sera ya no child left behind lakini imeonekana kuwa hiyo sera ndiyo imeacha alot of children behind. Hoja sio jina gani unatumia kuelezea unachofanya, hoja ni namna gani hicho kitu kimefanyika.

Muda mwingine majina haya yanatupoteza bure. Inasikitisha kuona watu wakitaka kufuata ubepari kwa asilimia mia kama vile wengine walivyojaribu kufuata ujamaa kwa asilimia mia bila kukumbuka kuwa hizi sera mbili ni majina tu na haziwezi kamwe kusimama peke yake.

Ninaamini kuwa kushindwa kwa uchumi wa Tanzania kulichangiwa na vitu vingi ikiwemo subotage toka kwa nchi za kimagharibi na ule msimamo wa Nyerere dhidi ya waingereza katika issue ya Rhodesia zote mbili.

Katika hili naona migongano kuliko hali ya uongozi kama chanzo cha matatizo. The same thing/argument ambayo huwa inatolewa na republicans hapa USA kutetea deficit na madeni kwenye serikali zao ni hii hii ambayo naona ilimkumba Nyerere.
 
Mwanakijiji:

Kudidimia kwa nchi za kiafrika kunatokana zaidi na phenomena inayoitwa Dutch Bonanza.

Inaonyesha kabisa kuwa nchi za Asia ambazo Natural Resource sio msingi wa maendeleo, zimeendelea.

Na nchi za kiafrika au Kiarabu ambazo pato lake limetegemea sana Natural Resource (Dutch Bonanza) zinadidimia au kuwa kwenye matatizo ya kijamii.

Mobutu akipata pesa za almasi anakwenda kujirusha Brussels akitegemea kuwa mgodi wa almasi utaingiza tena pesa. Hajui kuwa soko la dunia linabadilika na mitambo ya kuchimba almasi inachakaa.

Nyerere na Kwame watataifisha mashamba ya katani na kakao kupata hela za kusomesha wanafunzi na kutoa huduma za afya. Lakini walichosahau kuwa matumizi ya katani yatapungua na wazalishaji wa kakao wataongezeka. Na vilevile wanasahau kuwa wafanyakazi wa mashamba hayo nao wanahitaji maslahi na uongozi mzuri katika mashamba.

Ivory Cost wao wanatumia pesa ya kakao kuifanya Abdajan kuwa Paris kimajengo.

Kulikuwepo na Naivette katika masuala ya financials karibu katika nchi zote za Kiafrika
.

Agree with you,

Asante kwa vile sasa kuna common ground hapa inazidi kupatikana na nimefaidika sana na shule hasa hiyo ya dutch bonanza.

Post yako mkuu hapa imethibitisha hoja sasa kuwa kushindwa kwa Tanzania na nchi nyingi za Afrika haikuwa kwa sababu ya ujamaa au ubepari peke yake. Kuna sababu nyingi sana na kadri mjadala huu unavyoendelea nina imani tutajifunza mengi maana naona hakuna matusi au kashfa ila shule tu wakuu.

Haya mambo yakitazamwa kwa mtizamo wa kitaifa yanatoa shule zaidi kuliko yakitazamwa kwa msingi wa kudunisha mtu (iwe Nyerere, Mwinyi, au Kambona).
 
Mwanakijiji:

Nyerere hakutoa nafasi kwa mtu yoyote kupinga mawazo yake. Sababu ya Tanzania kuwa na magazeti ya uhuru, mzalendo, daily news na Sunday news tu katika kipindi cha nyuma ni kunyima uhuru wa wengine kusema.

Unaweza kuelezea sababu ya Rosie kuandamwa na conservative talk radios in America hadi kufikia hatua ya kutolewa kwenye the view ya abc? Au unaweza kutoa sababu iliyotumika kufuta kipindi cha liberal actress Whoopi Goldberg? Sensor zipo hadi America, tena America ya karne ya 21? Sijui huu nao ni ujamaa au ni Nyerere yuko all over the world!

Angekuwepo madarakani leo na siasa zake za ujamaa Tanzania ingekuwa haina internet. Na vi-blog vyenu visingekuwepo.

BBC world Service kila siku inatangaza bei ya bidhaa duniani. Lakini Nyerere akafanya watanzania kuwa matahira. Anasikiliza BBC world Service na baadaye anato-hotuba za bei za mazao zinavyoshuka duniani na watu wanafikiri Nyerere ana uwezo wa kutabiri bei za mazao.

Kuna mengi sana yamesemwa kuhusu Nyerere lakini hili sijui hata kama mtoto wa miaka mitano anaweza kuamini! Nyerere kuwafanya watanzania matahira? Inahitaji nguvu kubwa sana kufanikiwa hilo unless huyu Nyerere alikuwa na nguvu za kimungu au mganga wake wa Bagamoyo alikuwa ni shetani mwenyewe.

China, Cuba na Vietnam wako mbali kwa sababu walikuwa mbali sana zaidi yetu kabla ujamaa na kabla ya kutawaliwa. Zaidi ya miaka mia tano iliyopita wakati Maco Polo anatembelea China alikuta tayari wanatumia noti kama pesa. Miaka 2000 iliyopita wachina tayari walikuwa na pump za kuvuta maji zenye muundo sawa na pump zinazotumika kuvuta mafuta au gesi sasa.

Yaani ujamaa hautambui matumizi ya pesa? Ujamaa pia unapinga matumizi ya pump?

Vietnama ilikuwa koloni la China hivyo hakuna la kuongeza. Ukienda Cuba, sehemu kubwa ya nchi hiyo imejengwa kabla Castro hajaingia madarakani.

Nchi za Nordic ambao wakazi wake ni Viking walitawala sehemu kubwa ya ulaya ya kaskazini ikiwemo United Kingdom na kuvumbua Marekani kabla ya Columbus. Watu kama hao wenye miundo wa kiserikali yenye uzoefu na muda mrefu, wenye technologia ya kujitegemea na mitaji ya uhakika wanaweza kuchagua mfumo wowote wa uchumi na wakianguka wanaelewa wapi pa kuanzia.

Hii haiondoi au kujenga dhana kuwa ni mfumo wa kibepari tu au kijamaa tu ndio ulifanya haya. Soma vizuri historia ndugu yangu.

Ukirudi kwetu, miaka 120 sehemu kubwa ya nchi ilikuwa bado iko primitive. Ata makabila yaliosoma yalikuwa hajui kuvaa nguo katika kipindi hicho. Hivyo kuchukua mifano ya nchi nyingi kuonyesha mafanikio ya ujamaa IS PURE CRAP.

Mada hii inahusu Kambona. Kambona aliona Ujamaa haufai. Na bila ya watu kama Kambona Nyerere asingepata hiyo nafasi ya kuleta Ujamaa. Nyerere alipoambia kuchagua ualimu au siasa. Nyerere alichagua ualimu. Ni kina Kambona waliomwambia wako tayari kumlipia gharama za maisha akiacha ualimu. Leo hii historia yako inasema ni kwa mapenzi ya wananchi Baba wa taifa aliachia kazi ya ualimu na kuendelea kupigania uhuru. Ukweli ni kuwa mzee mzima alibwaga manyanga na hiyo ni fact.

Kwa hili, inaonekana hakuna chochote kile chema Nyerere aliwahi kufanya kwa Tanzania. Kama Afrika nzima ilikuwa na dutch bonanza kama ulivyosema, sijui mafanikio ya Kambona yangekuwa tofauti kwa vipi na ya Nyerere, Mobutu and the like.
 
Mkuu Joka kuu,

Muda mwingine majina haya yanatupoteza bure. Inasikitisha kuona watu wakitaka kufuata ubepari kwa asilimia mia kama vile wengine walivyojaribu kufuata ujamaa kwa asilimia mia bila kukumbuka kuwa hizi sera mbili ni majina tu na haziwezi kamwe kusimama peke yake.

Ninaamini kuwa kushindwa kwa uchumi wa Tanzania kulichangiwa na vitu vingi ikiwemo subotage toka kwa nchi za kimagharibi na ule msimamo wa Nyerere dhidi ya waingereza katika issue ya Rhodesia zote mbili.

Katika hili naona migongano kuliko hali ya uongozi kama chanzo cha matatizo. The same thing/argument ambayo huwa inatolewa na republicans hapa USA kutetea deficit na madeni kwenye serikali zao ni hii hii ambayo naona ilimkumba Nyerere.

Ulichosema ni kweli.

Watu wengi wanashindwa kuweka hivi vitu in context. Matatizo ya Tanzania hayakuwa pekee. Inabidi tuangalie sehemu nyingine zilikuwa vipi kwenye hicho kipindi. Moja ya sababu uchumi wa Tanzania ulishindwa ni subotage kwasababu ya siasa zetu za nchi za Afrika ya Kusini. Nchi za magharibi zilifanya kila hila kuhakikisha uchumi huendelei. Historia itakuja kutufundisha hilo somo. Bado nasubiri wanahistoria watuandikie.

Pili nchi ambazo zilikubali kuwa watumwa wa nchi za magharibi kama Brazzaville group/Union of Afro Malagasy States (UAM) walipewa misaada. Ndio maana wakina Felix Houphouet-Boigny wa Ivory Coast aliweza kuwa na uchumi mzuri. France subsidized uchumi wao. Waliotaka uhuru kama Sekou Toure wa Guinea, France wakatoa kila kitu, mpaka mabomba ya maji kwenye ofisi za serikali.

Between Freedom and perpetual slavery, I am for Freedom. Development will come with determination and hard work. We have to learn from our failure and success and device new plan to move forward. Kambona and Nyerere did many things I am proud of.
 
Kwa hili, inaonekana hakuna chochote kile chema Nyerere aliwahi kufanya kwa Tanzania. Kama Afrika nzima ilikuwa na dutch bonanza kama ulivyosema, sijui mafanikio ya Kambona yangekuwa tofauti kwa vipi na ya Nyerere, Mobutu and the like.

Ninakujibu kipande cha hiki tu. Vipande vingine naona bado unaboronga.

Nampa Nyerere heshima kwanza kupigania uhuru wa nchi yake na za wengine. Uhuru kwanza uchumi baadaye. Kizazi chao kilikuwa cha wapigania uhuru. Kama ningekuwa kwenye kamati ya NOBEL PRIZE ya amani, ningepigania apewa na kama wanakamati wengine hawataki, ningejitoa na kuachia ngazi.

Nabii Mussa aliwakomboa wana-Israel kutoka Utumwani lakini hakukanyaga Nchi ya ahadi. Ilibidi Joshua awaongoze kwenye nchi ya ahadi.

Nyerere, Karume, Kambona, Mwinyi na viongozi wengine waliopigania uhuru wako katika kundi la Mussa - Ukombozi.

Kwa kizazi chetu kinachotapatapa jangwani kutafuta riziki, tunamtafuta Joshua wa kutupeleka katika nchi ya maziwa na asali.
 
Ninakujibu kipande cha hiki tu. Vipande vingine naona bado unaboronga.

Haya ni maoni yako binafsi. Inawezekana kabisa hata wewe unachoandika unaboronga lakini mwamuzi ni msomaji na mimi sina uwezo wa kuamua maandishi yako kama ni point au utumbo.

Nampa Nyerere heshima kwanza kupigania uhuru wa nchi yake na za wengine. Uhuru kwanza uchumi baadaye. Kizazi chao kilikuwa cha wapigania uhuru. Kama ningekuwa kwenye kamati ya NOBEL PRIZE ya amani, ningepigania apewa na kama wanakamati wengine hawataki, ningejitoa na kuachia ngazi.

Nabii Mussa aliwakomboa wana-Israel kutoka Utumwani lakini hakukanyaga Nchi ya ahadi. Ilibidi Joshua awaongoze kwenye nchi ya ahadi.

Nyerere, Karume, Kambona, Mwinyi na viongozi wengine waliopigania uhuru wako katika kundi la Mussa - Ukombozi.

Kwa kizazi chetu kinachotapatapa jangwani kutafuta riziki, tunamtafuta Joshua wa kutupeleka katika nchi ya maziwa na asali.

Nikikupinga katika hili itabidi nipelekwe group home na kufungiwa huko kwa miaka 40 ijayo. Mimi sina uwezo wa kuamua nafasi ya Nyerere au Kambona katika historia, hata hivyo bado ni vizuri pia kusoma maneno na mtizamo wako kuhusu hawa viongozi.
 
Ulichosema ni kweli.

Watu wengi wanashindwa kuweka hivi vitu in context. Matatizo ya Tanzania hayakuwa pekee. Inabidi tuangalie sehemu nyingine zilikuwa vipi kwenye hicho kipindi. Moja ya sababu uchumi wa Tanzania ulishindwa ni subotage kwasababu ya siasa zetu za nchi za Afrika ya Kusini. Nchi za magharibi zilifanya kila hila kuhakikisha uchumi huendelei. Historia itakuja kutufundisha hilo somo. Bado nasubiri wanahistoria watuandikie.

Pili nchi ambazo zilikubali kuwa watumwa wa nchi za magharibi kama Brazzaville group/Union of Afro Malagasy States (UAM) walipewa misaada. Ndio maana wakina Felix Houphouet-Boigny wa Ivory Coast aliweza kuwa na uchumi mzuri. France subsidized uchumi wao. Waliotaka uhuru kama Sekou Toure wa Guinea, France wakatoa kila kitu, mpaka mabomba ya maji kwenye ofisi za serikali.

Between Freedom and perpetual slavery, I am for Freedom. Development will come with determination and hard work. We have to learn from our failure and success and device new plan to move forward. Kambona and Nyerere did many things I am proud of.

Kila nchi ya ki-Afrika ilijipanga na wafadhiri wake. Wakati ufaransa inasaidia nchi kama Ivory-Cost, Tanzania ilimwagiwa misaada kibao na nchi za Nordic. Misaada hiyo haikwenda Kenya au Zaire, ilikuja Tanzania kwa sababu tunafuata siasa zao. Na hiyo misaasa ikawa kama DUTCH BONANZA.

Kwa zaidi ya miaka 30, bajeti ya Tanzania inategemea misaada kwa zaidi ya 50%. Na hii imefanya viongozi wetu wasiwe wabunifu. Kitu kidogo kikifanyika, balozi wa Denmark atasema wataondoa misaada yao kwa asimilia fulani.
 
Inaonekana matatizo ya Tanzania ni zaidi ya Nyerere vs Kambona au ujamaa vs ubepari. Muda kwenye hii thread umefundisha mengi
 
Huwezi kulinganisha msaada Tanzania uliopewa na nchi za Nordic na system ya Wafaransi na nchi walizotawala kule Afrika magharibi. Hata baada ya uhuru, Boigny alikuwa memba wa serikali ya France; budget yake kubwa ilikuwa inatoka Paris.

Zaidi ya hapo, nakubaliana na wewe kwamba kutegemea misaada kumefanya viongozi wetu wasiwe wabunifu.
 
Mwana wa Maryamu, ni kwa kiasi gani matatizo ya kiuchumi ya mwanzoni mwa 60s, yale ya 70s, vita ya Kagera na njaa ya 80s na siasa za Vita baridi vilichangia kudumaza uchumi wetu? Unafikiri sera ya Kijamaa ilikuda na athari kubwa kuliko matatizo ambayo yameshainishwa hapo juu? au sera hizo ndizo zilitusaidia kwa kiasi kikubwa kuyapitia bila kugeuka Taifa lililovunjika?

Mkuu MMJ,

Heshima mbele mkuu, haya matatizo uliyoyasema mkuu huoni kuwa ya;likuwa ni kujitakia kuliko ya natural?

Mkuu MWK,

Nimeskusikia mkuu, ila it is nice for once wewe na Mkuu MMJ, kuwa kwenye defense, I am enjoying it, ingawa in the process ninajifunza cha kumtetea Mwalimu mbele ya foregners, unajua hii ni sisi kwa sisi tu yaani nigger kuita nigger mwenziwe nigger, lakini sio mzungu, Na mimi pia mkuu siwezi mponda Mwalimu, mbele wageni au nikakubali akapondwa na wageni wasiokuwa wabongo, atakufa mtu ndio maana ninasema tunachota arguments hapa,

Ila Respect kwenu wote mnaoshiriki kwamba finally, inatolewa elimu na that is all tunachoomba!
 
Hata mimi pia siwezi mponda mchonga mbele ya wageni/mtu asiye mtanzania ingawaje nipo strongly against huyu jamaa......kamjadala katamu, ingawaje at times watu wana-lose tamper!!! well ndio domo-cracy hiyo.....
 
Inaonekana matatizo ya Tanzania ni zaidi ya Nyerere vs Kambona au ujamaa vs ubepari. Muda kwenye hii thread umefundisha mengi

Matatizo ni mengi lakini katika safu za umasikini miaka ya 60, nchi za Asia tiger pia zilikuwepo.

Nchi za kiasia zilizofuata ujamaa zipo juu kuliko nchi za kiafrika zilizofuata ujamaa. Nchi za ki-asia zilifuata mabepari wako juu kuliko nchi za kiafrika zilizofuata ubepari.

Bangladesh ilikuwa ndio kipimo cha umasikini duniani, sasa inaonekana inajaribu kuliko nchi nyingi za kiafrika.

Tukiulizana kwanini tunaboronga, tunatoa visingizio kibao ambavyo havitoi makosa yetu wenyewe na mifumo ya utawala tuliochangua baada ya uhuru.

Ukitaka kuendelea jilinganishe na wanaofanya vizuri hata kama watakuwa ASIA. Haya mambo ya kujilinganisha na nchi zingine za ki-afrika hayana mpango.

Kama wa-Ghana wataacha kutumia vyoo na kuanza kutumia mapori, je na sisi tuwafuate kwa sababu ni waafrika wenzetu?
 
Huwezi kulinganisha msaada Tanzania uliopewa na nchi za Nordic na system ya Wafaransi na nchi walizotawala kule Afrika magharibi. Hata baada ya uhuru, Boigny alikuwa memba wa serikali ya France; budget yake kubwa ilikuwa inatoka Paris.

Zaidi ya hapo, nakubaliana na wewe kwamba kutegemea misaada kumefanya viongozi wetu wasiwe wabunifu.

Hey hey. Hakuna free lunch. Misaada ilikuwa direct proportional na invenstment ya nchi inayokusaidia.

Baada ya kutaifisha invenstments zao, ulitaka watusaidie?
 
Mwana wa Maryamu, ni kwa kiasi gani matatizo ya kiuchumi ya mwanzoni mwa 60s, yale ya 70s, vita ya Kagera na njaa ya 80s na siasa za Vita baridi vilichangia kudumaza uchumi wetu? Unafikiri sera ya Kijamaa ilikuda na athari kubwa kuliko matatizo ambayo yameshainishwa hapo juu? au sera hizo ndizo zilitusaidia kwa kiasi kikubwa kuyapitia bila kugeuka Taifa lililovunjika?

Matatizo yalioangusha Tanzania kiuchumi yalitokea miaka ya 70 na sehemu kubwa ni UJAMAA.
 
Matatizo yalioangusha Tanzania kiuchumi yalitokea miaka ya 70 na sehemu kubwa ni UJAMAA.

Nakuunga mkono ndugu yangu, mfano mzuri ni huo hapo chini toka ktk article flani hivi.......... hiyo ni pick ya paragraph mbili tu ambazo zina dissect Tanzania, ukweli ni kwamba li-ujamaa la Nyerere ndio limeua "timu". James Carville angesema' "it's ujamaa stupid."!!!! Well, mtu anaweza ku-spin atakavyo...............

In fact, ujamaa villages were generally failures as satisfactory human communities and, above all, as units of production. What the high-modernist planners of the Tanzanian state failed to realize was that the prior dispersion and movement of the population was a finely-tuned and long-practiced response to a very stingy semi-arid environment. Similarly, the complex forms of poly-cropping they practiced were generally quite productive and ecologically sound, despite having been judged, partly on aesthetic grounds, to be "backward" by agricultural planners. The mono-cropping mandated in its place typically failed. As the failures of the ujamaa became more manifest and the fiscal capacity of the regime to subsidize them weakened, communal production was abandoned and many of the villages broke up altogether. Where the new villages persisted it was due more to the improvisational skills and kinship networks of those resettled than to the logic of the planners' design.

Like the Soviet state, the Tanzanian state had replaced an independent, migratory, and illegible rural population with a regimented, fixed peasantry. In the process it damaged, if not destroyed, a preexisting human capital of working knowledge and social connective tissue. By making an abstraction of the peasant farmer and insisting on a vastly simplified, mono-cropping regimen, its own scheme proved a recipe for failure.

There u go!!!!.
 
Back
Top Bottom