Bin Maryam
JF-Expert Member
- Oct 22, 2007
- 685
- 13
Je NASA ni ujamaa wa kuzalisha mali au ujamaa wa matumizi ya umma. Ukitumia kodi, pesa, au nguvu za wananchi kufanya uzalishaji wa kitu chochote (iwe kwa faida au sio kwa faida) kwa manufaa ya jumuiya hiyo, basi hiyo ni social production - au uzalishaji wa kijamaa (emphasis on social (jamii)).
Sipingani nawe katika hili!
Si kweli, nchi nyingi za kimagharibi zinatumia pia ujamaa kuzalisha mali - kumbuka kuwa public transportation katika nchi zote za magharibi mara nyingi inagharimiwa na serikali. Transportation pia ni part ya uzalishaji na kama inagharimiwa na serikali au public au walipa kodi basi hiyo inakuwa social production (ujamaa).
Hilo fungu la kulipia gharama kama linatokana na pesa za kodi au michango ya wananchi kama jumuiya basi huo ndio ujamaa wenyewe. Waulize hata mabepari wenyewe wa kimarekani watakuambia kuwa AMTRAK inaendesha kijamaa na conservative wengi wanataka serikali iache kujiingiza kwenye biashara na uzalishaji. Kumbuka kuwa uzalishaji ni vyote - bidhaa na huduma (goods and services)
Kumbuka pia kuwa hiyo research and development ni part ya uzalishaji (production) na bila hiyo basi hakuna cha kuzalishwa. Kama NASA kazi yake ni research basi ujue kuwa NASA inajihusisha na uzalishaji kwa kutumia pesa za jamii (social production)kitu ambacho kinafanya kazi za NASA ziwe part ya uzalishaji wa kijamaa
Hicho kipindi lazima kiwe kirefu au kifupi kwa kiasi gani? miaka 5, 20, au 100?
Labda usome tena maana ya ubepari. Ukisoma utajua kuwa hata kutumia kodi ya watu wengine kwa kufanyia uzalishaji wako basi umekiuka misingi ya ubepari. Waroma walitumia utumwa (nilikisema hiki kule juu) kujenga himaya yao - huu sio ubepari.
Sheria ya waroma ilimpa nguvu mfalme wa nchi kuliko raia wa nchi katika mipango yote ya kiuchumi na kijamii (kinyume na misingi ya kibepari). Mambo mengi ya Roma yalifanywa kwanza kwa faida ya mfalme na ufalme kabla ya faida binafsi (hii ni moja ya forms za kijamaa).
Mabepari wenyewe duniani wanapinga kuwa hakuna mfumo kamili wa kibepari kama vile wanauchumi walivyokubali kuwa hakuna pure or perfect competition market. Nakushangaa kuwa bado unabishia hili!
Kwa mawazo unayotoa hapa naona ni afadhari wakoloni warudi tu watutawale. Uhuru tulipata mapema.
Na jinsi navyosoma posti zako, naanza kupata imani kubwa kuwa nyinyi mnaomfuata Nyerere kwa sehemu kubwa ni MAMBUMBU na hamjuhi alikuwa anasema nini?
KAMA MNGEJUA NYERERE ANASEMA NINI, mzee wa watu hasingeacha nchi katika hali mbaya ya kiuchumi.
Unachoeleza kuhusu ROMA ni UTUMBO MTUPU.
Sijaeleza UJAMAA NA UBEPARI KWA KUTUMIA ANALOGY YA BINARY NUMBER (TRUE, FALSE). Natumia ANALOGY YA FUZZY LOGIC. Nchi ni ya kibepari iwapo zaidi ya 70% ya miundo mbinu yake ni ya kibepari.
Nyerere alimwita Kenyatta pure capitalist lakini serikali ya Kenyatta ilikuwa na makampuni ya kiserikali. Hayo makampuni hayafanyi serikali ya Kenya kuwa ya KIBEPARI-UJAMAA.
Nyerere pia alikuwa pure mjamaa, lakini aliwaachia watu kufanya biashara na kumiliki. Lakini haitafanya serikali yake kuwa UJAMAA-KIBEPARI.
Serikali ya mkoloni ilikuwa inamiliki shirika la reli, ndege, meli n.k, lakini itaendelea kuitwa serikali ya kikoloni kwa sababu vitu hivyo vilikuwepo ku-support ukoloni. Hatuwezi kusema tulikuwa na UKOLONI-UJAMAA.