Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?

Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?

- Kambona alitaka majaribisho kwanza kabla ya kuingia full scale!

William.

Prof Abrahaman Babu alichukia sana kuwafanyia experiment wanadamu. Aliwahi kusema ujamaa should be experimented into rats first before people. Sidhani kama alikuwa ana maana ya panya kweli, naona kama alikubaliana na Kambona kuliko Nyerere. Kwa mfano Botswana wamechukua princile ya ujamaa vilage, baadaye wakatoa ujamaa wakabaki na vilage. Sasa nenda ukaangalie vilage zao, they are superb. Kambona alikuwa right kwa hilo.
 
Malecela Sr almost became a PM in 1983 when Sokoine resigned...........do you know why this never happened? The same person who made Nyerere and Kambona at loggerheads!
 
Tulipokowa tunamuimba kambona, na hata wakati kumbeza mzee mtei, Zilikuwa ni dirty propaganda.

Kimsingi unapotaka kufanya kitu chochota ili kupata ufanisi mkubwa unatakiwa kufanya yafuatayo (Mtaongezea)

1. Get smart leaders
2. Establish a complete master plan
3. Come with a project charter for review and approval (Stake holders should participate, umma) Hapa hata debate zinatakiwa kuruhusiwa (Wakati ule subutu)
4. Develop a detailed physical (Business) case for approval
5. Come with the implementation plan (including number of analysis, you can outsource if you don't have internal competence)
6. Review the plan (Malimbano ya hoja nk)
7. Fanyia kazi
8. Pima utekelezaji. Ni lazima uwe na upimaji yakinifu (Sio hizi report za kiinteligensia za kujikomba)
9. Panua wigo wa utekelezaji
10. Sasa unakuwa na model ya ujamaa na kujimetea.

Kimsingi kilichotia dosari katika dhamira nzuri ya Mwalimu kutofurahia baadhi ya majina kama haambiliki. Angelikubali hili jina na kujinasua angekuwa na akina kambona hadi mwisho. Na leo Singapore wasingetamba mbele yetu.
 
Heshima mbele sana wakuu wote JF;-

- Unajua ukiangalia sana matatizo ya Taifa letu kwa sasa ya kisiasa, kiuchumi na hasa kisheria one thing comes in mind, the FOUNDATION ya taifa letu, kule unakuta Baba wa Taifa na Ideas zake kwa Taifa, lakini pia utamkuta Kambona, his one time trusted right hand man, lakini wakafikia mahali wakaenda njia panda kwa kutokubaliana kuhusu Muelekeo unaoweza kulipeleka hili taifa kunakofaa!

-Swali langu kwa wasomi, wananchi wa kawaida na wengine wote, nani kati yao was right in policies, hasa ukiangalia wakati mgumu tulionao sasa hivi hili taifa?

MUCH RESPECT PEOPLE!

William.

Willie, ashakum si matusi.Wajua ngedere angekuwa na uwezo kujitazama nyuma angetafuta nguo ya kujisitiri, lakini Mungu kamnyima uwezo huo, na hivyo haoni kama hali ile inatukera wengine.
 
Tatizo la Tanzania sio Sera bali ni utekelezaji wake! Hata tuje na Sera ipi tutaendelea kupiga maktaimu endapo kutaendelea kulea mafisadi, tutaendelea kununua/kurithishana uongozi, kutokutoa maamuzi, nk
 
Tatizo la Tanzania sio Sera bali ni utekelezaji wake! Hata tuje na Sera ipi tutaendelea kupiga maktaimu endapo kutaendelea kulea mafisadi, tutaendelea kununua/kurithishana uongozi, kutokutoa maamuzi, nk
kwenye blue nakubaliana na wewe, kwenye red nakataa, tatizo ni wanaoongoza huo utekelezaji, wamejaa tamaa za kujilimbikizia mali, ufisadi umetamalaki nafsini mwao, wanasababisha utekeleaji kushindwa.
 
Akiwa miongoni mwa watanganyika wachache waliobahatika kupata elimu wakati wa ukoloni, oscar kambona, mzaliwa wa kijiji cha kwembe wilaya mpya ya nyasa(ilikua sehemu ya wilaya ya mbinga) alifanya kazi bega kwa bega na wpigania uhuru wengine watanganyika akiwamo nyerere.kuna wakati alikua katibu mkuu wa TANU na waziri wa ulinzi wa Tanganyika.

Mwaka 1964 kambona ambaye alikuwa kiongozi wa pili kwa umaarufu na mvuto wa kisiasa nyuma ya nyerere, alifanikiwa kuzungumza na wanajeshi walioasi na alimudu kuutuliza uasi huo huku nyerere na kawawa wakitokomea kusikojulikana. mwaka 1967 mara baada ya kutangazwa kwa azimio la arusha, kambona alilazimika kuondoka tz akiwa na familiya yake kwenye gari lake hadi nairobi kenya then uingereza.

kilichomkimbiza tz ni kutozikubali sera za nyerere zilizotokana na azimio la arusha. kambona alipendekeza viteuliwe vijiji kadhaa vya mfano wa namna gani vijiji vya ujamaa vingekuwa,then ufanyike utafiti ni kwa namna gani sera itafanikiwa au laa, kabla ya kutekeleza sera hiyo kwa nchi yote.
ujasiri na uwezo wake wa ku-argue against nyerere ulimtofautisha kambona na kawawa as well as viongozi wengine ambao hawakuthubutu kubishana na nyerere, hii ni sababu nyingine iliyopelekea nyerere kuanza kumuwinda kambona ili akamatwe kwa tuhuma za uhujumu ambazo hadi leo hazijathibitishwa.


mnaweza kuendelea kwa mnayoyajua kwa hon kambona(nakaribisha ukosoaji na marekebisho)
 
Soma hii kuhusu: Oscar Kambona: Shujaa,
Adui wa Taifa lake BY WAVUTI.COM - WAVUTI ON FEBRUARY 2, 2013 WIKI iliyopita niliwaletea makala ya
muasisi wa chama cha TAA, TANU na
baadaye CCM ambaye alikuwa
mpigania uhuru wa Tanganyika
iliyozaa Tanzania, marehemu Lawi
Nangwanda Sijaona. Makala ile imeleta hoja nyingi kutoka
kwa wasomaji ambao wameomba
kuandikwa kwa Watanzania wengine
waliolitumikia taifa kwa uaminifu na
kuwa mashuhuri katika nyanja
kadhaa za siasa, michezo, utamaduni na utawala lakini wamesahaulika. Hivyo kwa nia ya kutimiza matakwa
yao na kuendeleza makala hii, leo
ninawaletea historia ya mwanasiasa
Oscar Kambona. Oscar Kambona ni miongoni mwa
viongozi mahiri na shupavu waliowahi
kuwa gumzo ndani na nje ya
Tanzania, kutokana na uongozi wake,
hekima na busara. Ndiye Mtanzania wa kwanza kuwa
waziri aliyeongoza wizara mbili kwa
wakati mmoja. Ndiye Mtanzania pekee
anayeaminika kusimama kidete na
kufanikiwa kulidhibiti jeshi lililoasi
mwaka 1964. Hata hivyo, pamoja na umahiri huo,
lakini kubwa zaidi kutokuwa na
tamaa ya kutumia nafasi ya uasi wa
jeshi kushika madaraka ya nchi. Pamoja na hayo mchango wake
hauthaminiwi kabisa. Tofauti na
viongozi wengine wa siasa au hata
utamaduni, mpaka sasa hakuna
barabara yenye ukumbusho wa jina la
mwanasiasa huyu aliyefariki akiwa katika matibabu mjini London, Juni
1997 na mwili wake kurudishwa
Tanzania kwa mazishi. Oscar Kambona alizaliwa mwaka
1925, katika kijiji cha Kwambe
kilichoko mwambao mwa Ziwa Nyasa,
karibu na Mbamba-Bay, wilaya ya Mbinga,
mkoani wa Ruvuma. Alikuwa ni mtoto wa Kasisi David
Kambona ambaye alikuwa miongoni
mwa Waafrika wa kwanza kupata
upadri katika kanisa la Anglikana la
Tanganyika, na kwa mama Miriam
Kambona. Akiwa mdogo, baba yake alikuwa
akimweleza kuhusu ndoto zake juu ya
uhuru wa nchi yake, hivyo kumfanya
Oscar kujawa na hamu ya kuitumikia
nchi yake. Msingi wa elimu yake aliupata
nyumbani kwao, chini ya mwembe
(ambao bado uko mpaka sasa), katika
kijiji cha Kwambe, kwa kuwatumia
wazazi wake wote wawili na mjomba
wake, ambao wote walikuwa walimu. Alipelekwa shule ya kati ya Mt.
Barnabas, Liuli na baadaye Shule ya
Sekondari ya Alliance (sasa Shule ya
Sekondari Mazengo), ambako alilipiwa
ada na askofu Mzungu wa Anglikana
kwa vile baba yake hakuweza kumudu kulipa ada ya pauni 30 kwa
mwaka. Inasimuliwa kuwa
kilichomvutia Mzungu huyo kukubali
kumlipia Oscar ada ni baada ya kusali
sala ya Baba Yetu Uliye Mbinguni kwa
Kizungu. Alichaguliwa kwenda ‘Tabora Boys
Senior Government School ambako
ndiko alikokutana na Mwalimu Julius
Nyerere kwa mara ya kwanza. Wakati
huo Nyerere alikuwa anafundisha
katika shule ya Kikatoliki ya St Marys. Kukutana tena na Nyerere Ilikuwa mwaka 1954, kwenye
mkutano wa kitaifa wa walimu, ndipo
Oscar Kambona ambaye naye alikuwa
amemaliza shule na kufundisha katika
shule ya Alliance, alikutana tena na
Nyerere na kujadili mambo mbalimbali ikiwemo harakati za chama cha TANU. Oscar alishawishika kuitumikia TANU
ambayo ilikuwa imeanzishwa muda si
mrefu, bila malipo baada ya Mwalimu
Nyerere kumweleza kuwa asingeweza
kuajiriwa ndani ya chama kwa vile
haikuwa na fedha. Huo ulikuwa uamuzi mzito na mgumu
mno, hasa kwa mtu kukubali kuachia
nafasi ya ualimu ambayo alikuwa
akilipwa vizuri na kufanya kazi bila
malipo tena za chama ambacho ndiyo
kwanza kilikuwa kikianza harakati za ukombozi. Kwa miezi takriban sita, Oscar
Kambona alifanya kazi ngumu ya
kuzunguka sehemu mbalimbali za
nchi na kuonana na machifu na wazee
wa vijiji ili kusajili wanachama. Kwa kipindi hicho huku akitumia
fedha kidogo alizokuwa amejiwekea
akiba yake, alifanikiwa kusajili
wanachama 10,000 na haikuwa ajabu
kuwa baada ya mwaka mmoja
alikuwa amepata wanachama hai 100,000. Ili kutunza fedha za chama, Kambona
alifungua akaunti ya kwanza ya TANU
na kisha kwenda Butiama
kumshawishi Mwalimu Nyerere
achukue uongozi wa chama moja kwa
moja kama mtendaji mkuu. Mwaka 1957, Kambona alikwenda
kusomea sheria katika Chuo cha
Middle Temple, nchini Uingereza kwa
ufadhili wa Gavana. Akiwa London Kambona alikuwa
kiongozi wa chama cha wanafunzi wa
Tanganyika na mwenyekiti wa tawi la
TANU la London. Kukutana na watu mashuhuri Mwaka 1958, Kambona alipata fursa
ya kukutana kwa mara ya kwanza na
watu mashuhuri akiwemo George
Padmore, mwanaharakati wa umoja
wa wa Waafrika duniani, ambaye
alimshawishi ahudhurie mkutano wa Waafrika wote (All Africa’s Peoples
Conference), uliofanyika nchini Ghana
muda mfupi baada ya kupata Uhuru. Kambona alisafiri mpaka Ghana,
wakati huo akiwa bado anaendelea
na masomo yake nchini Uingereza na
huko alipata nafasi ya kukutana na
mwanaharakati mwingine maarufu
wa siasa za Afrika, Kwame Nkrumah. Utangazaji wake BBC Kambona ndiye Mwafrika wa kwanza
kutangaza taarifa ya habari kwa lugha
ya Kiswahili, katika Idhaa ya Kiswahili
ya BBC, ambayo sasa inajulikana kama
(BBC Swahili). Inadaiwa kuwa alikuwa akipenda
sana uandishi wa habari kwenye
vyombo vya kimataifa. Katika kuhakikisha anapigania uhuru
na mafanikio ya TANU, Kambona
akiwa anaendelea na masomo yake
nchini Uingereza, alikutana na
Mwalimu Nyerere kila alipoenda nchini
humo na kupanga mikakati ya kudai uhuru. Kambona alifunga ndoa na Flora
Moriyo na harusi ilifungwa katika
kanisa la Mt. Paul, London, na Nyerere
ndiye alikuwa msimamizi. Kurudi Tanganyika Mwaka 1959, Kambona alirudi
Tanganyika na kuendeleza harakati za
kudai uhuru kupitia TANU, huku
wakiweka bayana madai ya kupewa
serikali ya madaraka. Kambona kwa kushirikiana na
wenzake akiwamo Nyerere, waliweka
mikakati mbalimbali huku wakiwa
tayari kuanzisha mapambano kama
ilivyokuwa kwa Mau Mau ya Kenya. Katika uchaguzi wa kwanza TANU
ilishinda viti vyote isipokuwa kimoja
na kuunda Serikali ya Mambo ya Ndani
chini ya Mwalimu Nyerere ambaye
alikuwa Waziri Kiongozi wa kwanza. Kambona aliteuliwa kuwa Waziri wa
Elimu na baadaye alishika nyadhifa za
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mambo ya
Nchi za Nje na Ulinzi na Tawala za
Mikoa. Katika nyadhifa hizo, Kambona pia
alikuwa mwenyekiti wa kwanza wa
Kamati ya Ukombozi ya Umoja wa Nchi
Huru za Afrika na Mwenyekiti wa
Utayarishaji wa OAU ambayo sasa ni
AU. Kuunganisha bara na visiwani Mwaka 1964, Kambona alifanya kazi
kubwa katika kuunganisha Zanzibar
na Tanganyika, akiwa pamoja na Rais
Nyerere na Karume. Hii ilikuwa ni
baada ya Mapinduzi ya Zanzibar. Januari 20, 1964, wanajeshi wa kikosi
cha Calito waliasi. Kambona akiwa
waziri wa Ulinzi, alisimama kidete
kusuluhisha na msemaji mkuu
upande wa serikali huku viongozi
wakuu Mwalimu Nyerere na makamu wake, Rashid Kawawa, ikisemekana
wakiwa wamekimbilia mafichoni
Kigamboni walikokaa kwa siku tatu za
majadiliano mazito mpaka machafuko
yalipoisha. Moja ya nukuu za Kambona katika
mahojiano na gazeti la Daily Telegraph
la London, alisema, “Baada ya
kuwatuliza wanajeshi nilikwenda
kuwatafuta viongozi wengine na
kuwarudisha mjini kwa kutumia Land Rover yangu.” Kambona alisifiwa sana na Mwalimu
Nyerere kwa hekima na busara yake
hadi kufanikiwa kumaliza uasi huo
kwa kutumia nafasi yake ya uwaziri
wa ulinzi. Wapo walioanza kuvumisha
kuwa huenda kwa uaminifu wake, angeshika nafasi ya urais baada ya
Nyerere kumaliza muda wake. Ilikuwaje akawa adui wa serikali?
Endelea toleo lijalo… ---
Imeandikwa na Andrew Chale/ TANZANIA DAIMA Share this on:by WAVUTI.COM
www.wavuti.com/uploads/3/0/7/6/3076464/2074549.png?420
 
02/02/2013


2074549.png


WIKI iliyopita niliwaletea makala ya muasisi wa chama cha TAA, TANU na baadaye CCM ambaye alikuwa mpigania uhuru wa Tanganyika iliyozaa Tanzania, marehemu Lawi Nangwanda Sijaona.

Makala ile imeleta hoja nyingi kutoka kwa wasomaji ambao wameomba kuandikwa kwa Watanzania wengine waliolitumikia taifa kwa uaminifu na kuwa mashuhuri katika nyanja kadhaa za siasa, michezo, utamaduni na utawala lakini wamesahaulika.

Hivyo kwa nia ya kutimiza matakwa yao na kuendeleza makala hii, leo ninawaletea historia ya mwanasiasa Oscar Kambona.

Oscar Kambona ni miongoni mwa viongozi mahiri na shupavu waliowahi kuwa gumzo ndani na nje ya Tanzania, kutokana na uongozi wake, hekima na busara.

Ndiye Mtanzania wa kwanza kuwa waziri aliyeongoza wizara mbili kwa wakati mmoja. Ndiye Mtanzania pekee anayeaminika kusimama kidete na kufanikiwa kulidhibiti jeshi lililoasi mwaka 1964.

Hata hivyo, pamoja na umahiri huo, lakini kubwa zaidi kutokuwa na tamaa ya kutumia nafasi ya uasi wa jeshi kushika madaraka ya nchi.

Pamoja na hayo mchango wake hauthaminiwi kabisa. Tofauti na viongozi wengine wa siasa au hata utamaduni, mpaka sasa hakuna barabara yenye ukumbusho wa jina la mwanasiasa huyu aliyefariki akiwa katika matibabu mjini London, Juni 1997 na mwili wake kurudishwa Tanzania kwa mazishi.

Oscar Kambona alizaliwa mwaka 1925, katika kijiji cha Kwambe kilichoko mwambao mwa Ziwa Nyasa, karibu na




Mbamba-Bay, wilaya ya Mbinga, mkoani wa Ruvuma.

Alikuwa ni mtoto wa Kasisi David Kambona ambaye alikuwa miongoni mwa Waafrika wa kwanza kupata upadri katika kanisa la Anglikana la Tanganyika, na kwa mama Miriam Kambona.

Akiwa mdogo, baba yake alikuwa akimweleza kuhusu ndoto zake juu ya uhuru wa nchi yake, hivyo kumfanya Oscar kujawa na hamu ya kuitumikia nchi yake.

Msingi wa elimu yake aliupata nyumbani kwao, chini ya mwembe (ambao bado uko mpaka sasa), katika kijiji cha Kwambe, kwa kuwatumia wazazi wake wote wawili na mjomba wake, ambao wote walikuwa walimu.

Alipelekwa shule ya kati ya Mt. Barnabas, Liuli na baadaye Shule ya Sekondari ya Alliance (sasa Shule ya Sekondari Mazengo), ambako alilipiwa ada na askofu Mzungu wa Anglikana kwa vile baba yake hakuweza kumudu kulipa ada ya pauni 30 kwa mwaka. Inasimuliwa kuwa kilichomvutia Mzungu huyo kukubali kumlipia Oscar ada ni baada ya kusali sala ya Baba Yetu Uliye Mbinguni kwa Kizungu.

Alichaguliwa kwenda ‘Tabora Boys Senior Government School ambako ndiko alikokutana na Mwalimu Julius Nyerere kwa mara ya kwanza. Wakati huo Nyerere alikuwa anafundisha katika shule ya Kikatoliki ya St Marys.

Kukutana tena na Nyerere

Ilikuwa mwaka 1954, kwenye mkutano wa kitaifa wa walimu, ndipo Oscar Kambona ambaye naye alikuwa amemaliza shule na kufundisha katika shule ya Alliance, alikutana tena na Nyerere na kujadili mambo mbalimbali ikiwemo harakati za chama cha TANU.

Oscar alishawishika kuitumikia TANU ambayo ilikuwa imeanzishwa muda si mrefu, bila malipo baada ya Mwalimu Nyerere kumweleza kuwa asingeweza kuajiriwa ndani ya chama kwa vile haikuwa na fedha.

Huo ulikuwa uamuzi mzito na mgumu mno, hasa kwa mtu kukubali kuachia nafasi ya ualimu ambayo alikuwa akilipwa vizuri na kufanya kazi bila malipo tena za chama ambacho ndiyo kwanza kilikuwa kikianza harakati za ukombozi.

Kwa miezi takriban sita, Oscar Kambona alifanya kazi ngumu ya kuzunguka sehemu mbalimbali za nchi na kuonana na machifu na wazee wa vijiji ili kusajili wanachama.

Kwa kipindi hicho huku akitumia fedha kidogo alizokuwa amejiwekea akiba yake, alifanikiwa kusajili wanachama 10,000 na haikuwa ajabu kuwa baada ya mwaka mmoja alikuwa amepata wanachama hai 100,000.

Ili kutunza fedha za chama, Kambona alifungua akaunti ya kwanza ya TANU na kisha kwenda Butiama kumshawishi Mwalimu Nyerere achukue uongozi wa chama moja kwa moja kama mtendaji mkuu.

Mwaka 1957, Kambona alikwenda kusomea sheria katika Chuo cha Middle Temple, nchini Uingereza kwa ufadhili wa Gavana.

Akiwa London Kambona alikuwa kiongozi wa chama cha wanafunzi wa Tanganyika na mwenyekiti wa tawi la TANU la London.

Kukutana na watu mashuhuri

Mwaka 1958, Kambona alipata fursa ya kukutana kwa mara ya kwanza na watu mashuhuri akiwemo George Padmore, mwanaharakati wa umoja wa wa Waafrika duniani, ambaye alimshawishi ahudhurie mkutano wa Waafrika wote (All Africa's Peoples Conference), uliofanyika nchini Ghana muda mfupi baada ya kupata Uhuru.

Kambona alisafiri mpaka Ghana, wakati huo akiwa bado anaendelea na masomo yake nchini Uingereza na huko alipata nafasi ya kukutana na mwanaharakati mwingine maarufu wa siasa za Afrika, Kwame Nkrumah.

Utangazaji wake BBC

Kambona ndiye Mwafrika wa kwanza kutangaza taarifa ya habari kwa lugha ya Kiswahili, katika Idhaa ya Kiswahili ya BBC, ambayo sasa inajulikana kama (BBC Swahili).

Inadaiwa kuwa alikuwa akipenda sana uandishi wa habari kwenye vyombo vya kimataifa.

Katika kuhakikisha anapigania uhuru na mafanikio ya TANU, Kambona akiwa anaendelea na masomo yake nchini Uingereza, alikutana na Mwalimu Nyerere kila alipoenda nchini humo na kupanga mikakati ya kudai uhuru.

Kambona alifunga ndoa na Flora Moriyo na harusi ilifungwa katika kanisa la Mt. Paul, London, na Nyerere ndiye alikuwa msimamizi.

Kurudi Tanganyika

Mwaka 1959, Kambona alirudi Tanganyika na kuendeleza harakati za kudai uhuru kupitia TANU, huku wakiweka bayana madai ya kupewa serikali ya madaraka.

Kambona kwa kushirikiana na wenzake akiwamo Nyerere, waliweka mikakati mbalimbali huku wakiwa tayari kuanzisha mapambano kama ilivyokuwa kwa Mau Mau ya Kenya.

Katika uchaguzi wa kwanza TANU ilishinda viti vyote isipokuwa kimoja na kuunda Serikali ya Mambo ya Ndani chini ya Mwalimu Nyerere ambaye alikuwa Waziri Kiongozi wa kwanza.

Kambona aliteuliwa kuwa Waziri wa Elimu na baadaye alishika nyadhifa za Waziri wa Mambo ya Ndani, Mambo ya Nchi za Nje na Ulinzi na Tawala za Mikoa.

Katika nyadhifa hizo, Kambona pia alikuwa mwenyekiti wa kwanza wa Kamati ya Ukombozi ya Umoja wa Nchi Huru za Afrika na Mwenyekiti wa Utayarishaji wa OAU ambayo sasa ni AU.

Kuunganisha bara na visiwani

Mwaka 1964, Kambona alifanya kazi kubwa katika kuunganisha Zanzibar na Tanganyika, akiwa pamoja na Rais Nyerere na Karume. Hii ilikuwa ni baada ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Januari 20, 1964, wanajeshi wa kikosi cha Calito waliasi. Kambona akiwa waziri wa Ulinzi, alisimama kidete kusuluhisha na msemaji mkuu upande wa serikali huku viongozi wakuu Mwalimu Nyerere na makamu wake, Rashid Kawawa, ikisemekana wakiwa wamekimbilia mafichoni Kigamboni walikokaa kwa siku tatu za majadiliano mazito mpaka machafuko yalipoisha.

Moja ya nukuu za Kambona katika mahojiano na gazeti la Daily Telegraph la London, alisema, "Baada ya kuwatuliza wanajeshi nilikwenda kuwatafuta viongozi wengine na kuwarudisha mjini kwa kutumia Land Rover yangu."

Kambona alisifiwa sana na Mwalimu Nyerere kwa hekima na busara yake hadi kufanikiwa kumaliza uasi huo kwa kutumia nafasi yake ya uwaziri wa ulinzi. Wapo walioanza kuvumisha kuwa huenda kwa uaminifu wake, angeshika nafasi ya urais baada ya Nyerere kumaliza muda wake.

Ilikuwaje akawa adui wa serikali? Endelea toleo lijalo…

---
Imeandikwa na Andrew Chale/
TANZANIA DAIMA





 
Oscar kambona anabaki kuwa shujaa wangu kwa baadhi ya mambo.Najuta na kulaani walioniimbisha nyimbo primary school za kumkashfu
 
Asante sana Andrew; napenda makala zinazofufua historia yetu na kukweza mashujaa wetu. Na ni haki yao kutambulika na vizazi vya leo na kesho katika nchi hii.
 
Retrieved from Tanzania Daima 2/2/2013 and 9/2/2013

Oscar Kambona ni miongoni mwa viongozi mahiri na shupavu waliowahi kuwa gumzo ndani na nje ya Tanzania, kutokana na uongozi wake, hekima na busara.

Ndiye Mtanzania wa kwanza kuwa waziri aliyeongoza wizara mbili kwa wakati mmoja. Ndiye Mtanzania pekee anayeaminika kusimama kidete na kufanikiwa kulidhibiti jeshi lililoasi mwaka 1964.Hata hivyo, pamoja na umahiri huo, lakini kubwa zaidi kutokuwa na tamaa ya kutumia nafasi ya uasi wa jeshi kushika madaraka ya nchi.

Pamoja na hayo mchango wake hauthaminiwi kabisa. Tofauti na viongozi wengine wa siasa au hata utamaduni, mpaka sasa hakuna barabara yenye ukumbusho wa jina la mwanasiasa huyu aliyefariki akiwa katika matibabu mjini London, Juni 1997 na mwili wake kurudishwa Tanzania kwa mazishi.

Oscar Kambona alizaliwa mwaka 1925, katika kijiji cha Kwambe kilichoko mwambao mwa Ziwa Nyasa, karibu na Mbamba-Bay, wilaya ya Mbinga, mkoani wa Ruvuma.
Alikuwa ni mtoto wa Kasisi David Kambona ambaye alikuwa miongoni mwa Waafrika wa kwanza kupata upadri katika kanisa la Anglikana la Tanganyika, na kwa mama Miriam Kambona.

Akiwa mdogo, baba yake alikuwa akimweleza kuhusu ndoto zake juu ya uhuru wa nchi yake, hivyo kumfanya Oscar kujawa na hamu ya kuitumikia nchi yake. Msingi wa elimu yake aliupata nyumbani kwao, chini ya mwembe (ambao bado uko mpaka sasa), katika kijiji cha Kwambe, kwa kuwatumia wazazi wake wote wawili na mjomba wake, ambao wote walikuwa walimu.

Alipelekwa shule ya kati ya Mt. Barnabas, Liuli na baadaye Shule ya Sekondari ya Alliance (sasa Shule ya Sekondari Mazengo), ambako alilipiwa ada na askofu Mzungu wa Anglikana kwa vile baba yake hakuweza kumudu kulipa ada ya pauni 30 kwa mwaka. Inasimuliwa kuwa kilichomvutia Mzungu huyo kukubali kumlipia Oscar ada ni baada ya kusali sala ya Baba Yetu Uliye Mbinguni kwa Kizungu. Alichaguliwa kwenda ‘Tabora Boys Senior Government School ambako ndiko alikokutana na Mwalimu Julius Nyerere kwa mara ya kwanza. Wakati huo Nyerere alikuwa anafundisha katika shule ya Kikatoliki ya St Marys.

Kukutana tena na Nyerere

Ilikuwa mwaka 1954, kwenye mkutano wa kitaifa wa walimu, ndipo Oscar Kambona ambaye naye alikuwa amemaliza shule na kufundisha katika shule ya Alliance, alikutana tena na Nyerere na kujadili mambo mbalimbali ikiwemo harakati za chama cha TANU. Oscar alishawishika kuitumikia TANU ambayo ilikuwa imeanzishwa muda si mrefu, bila malipo baada ya Mwalimu Nyerere kumweleza kuwa asingeweza kuajiriwa ndani ya chama kwa vile haikuwa na fedha.

Huo ulikuwa uamuzi mzito na mgumu mno, hasa kwa mtu kukubali kuachia nafasi ya ualimu ambayo alikuwa akilipwa vizuri na kufanya kazi bila malipo tena za chama ambacho ndiyo kwanza kilikuwa kikianza harakati za ukombozi. Kwa miezi takriban sita, Oscar Kambona alifanya kazi ngumu ya kuzunguka sehemu mbalimbali za nchi na kuonana na machifu na wazee wa vijiji ili kusajili wanachama.

Kwa kipindi hicho huku akitumia fedha kidogo alizokuwa amejiwekea akiba yake, alifanikiwa kusajili wanachama 10,000 na haikuwa ajabu kuwa baada ya mwaka mmoja alikuwa amepata wanachama hai 100,000. Ili kutunza fedha za chama, Kambona alifungua akaunti ya kwanza ya TANU na kisha kwenda Butiama kumshawishi Mwalimu Nyerere achukue uongozi wa chama moja kwa moja kama mtendaji mkuu.

Mwaka 1957, Kambona alikwenda kusomea sheria katika Chuo cha Middle Temple, nchini Uingereza kwa ufadhili wa Gavana. Akiwa London Kambona alikuwa kiongozi wa chama cha wanafunzi wa Tanganyika na mwenyekiti wa tawi la TANU la London.

Kukutana na watu mashuhuri

Mwaka 1958, Kambona alipata fursa ya kukutana kwa mara ya kwanza na watu mashuhuri akiwemo George Padmore, mwanaharakati wa umoja wa wa Waafrika duniani, ambaye alimshawishi ahudhurie mkutano wa Waafrika wote (All Africa’s Peoples Conference), uliofanyika nchini Ghana muda mfupi baada ya kupata Uhuru. Kambona alisafiri mpaka Ghana, wakati huo akiwa bado anaendelea na masomo yake nchini Uingereza na huko alipata nafasi ya kukutana na mwanaharakati mwingine maarufu wa siasa za Afrika, Kwame Nkrumah.

Utangazaji wake BBC

Kambona ndiye Mwafrika wa kwanza kutangaza taarifa ya habari kwa lugha ya Kiswahili, katika Idhaa ya Kiswahili ya BBC, ambayo sasa inajulikana kama (BBC Swahili). Inadaiwa kuwa alikuwa akipenda sana uandishi wa habari kwenye vyombo vya kimataifa. Katika kuhakikisha anapigania uhuru na mafanikio ya TANU, Kambona akiwa anaendelea na masomo yake nchini Uingereza, alikutana na Mwalimu Nyerere kila alipoenda nchini humo na kupanga mikakati ya kudai uhuru. Kambona alifunga ndoa na Flora Moriyo na harusi ilifungwa katika kanisa la Mt. Paul, London, na Nyerere ndiye alikuwa msimamizi.

Kurudi Tanganyika

Mwaka 1959, Kambona alirudi Tanganyika na kuendeleza harakati za kudai uhuru kupitia TANU, huku wakiweka bayana madai ya kupewa serikali ya madaraka. Kambona kwa kushirikiana na wenzake akiwamo Nyerere, waliweka mikakati mbalimbali huku wakiwa tayari kuanzisha mapambano kama ilivyokuwa kwa Mau Mau ya Kenya. Katika uchaguzi wa kwanza TANU ilishinda viti vyote isipokuwa kimoja na kuunda Serikali ya Mambo ya Ndani chini ya Mwalimu Nyerere ambaye alikuwa Waziri Kiongozi wa kwanza. Kambona aliteuliwa kuwa Waziri wa Elimu na baadaye alishika nyadhifa za Waziri wa Mambo ya Ndani, Mambo ya Nchi za Nje na Ulinzi na Tawala za Mikoa. Katika nyadhifa hizo, Kambona pia alikuwa mwenyekiti wa kwanza wa Kamati ya Ukombozi ya Umoja wa Nchi Huru za Afrika na Mwenyekiti wa Utayarishaji wa OAU ambayo sasa ni AU.

Kuunganisha bara na visiwani

Mwaka 1964, Kambona alifanya kazi kubwa katika kuunganisha Zanzibar na Tanganyika, akiwa pamoja na Rais Nyerere na Karume. Hii ilikuwa ni baada ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Januari 20, 1964, wanajeshi wa kikosi cha Calito waliasi. Kambona akiwa waziri wa Ulinzi, alisimama kidete kusuluhisha na msemaji mkuu upande wa serikali huku viongozi wakuu Mwalimu Nyerere na makamu wake, Rashid Kawawa, ikisemekana wakiwa wamekimbilia mafichoni Kigamboni walikokaa kwa siku tatu za majadiliano mazito mpaka machafuko yalipoisha.

Moja ya nukuu za Kambona katika mahojiano na gazeti la Daily Telegraph la London, alisema, “Baada ya kuwatuliza wanajeshi nilikwenda kuwatafuta viongozi wengine na kuwarudisha mjini kwa kutumia Land Rover yangu.” Kambona alisifiwa sana na Mwalimu Nyerere kwa hekima na busara yake hadi kufanikiwa kumaliza uasi huo kwa kutumia nafasi yake ya uwaziri wa ulinzi. Wapo walioanza kuvumisha kuwa huenda kwa uaminifu wake, angeshika nafasi ya urais baada ya Nyerere kumaliza muda wake.
Ilikuwaje akawa adui wa serikali?

Ugomvi wa Nyerere, Kambona
Vyanzo mbalimbali vya habari hadi sasa vinashindwa kueleza ukweli juu ya hasa kile kilichosababisha kuzuka kwa tofauti kati ya Mwalimu Nyerere na Kambona. Kila mtu amekuwa akijaribu kueleza ugomvi wa wawili hawa kadiri ajuavyo. Kuna madai kwamba viongozi hawa wawili ambao kwa sasa wote ni marehemu, walianza kutofautiana baada ya maasi ya wanajeshi.

Inadaiwa kuwa Nyerere alitaka kuanzisha mfumo wa chama kimoja nchini ili kuimarisha usalama na Kambona alipinga hoja hiyo kwa maelezo kwamba mfumo huo ungezorotesha uhuru na maendeleo ya demokrasia. Hoja hiyo ikafikishwa bungeni kwa maamuzi na kwa bahati mbaya kwa Kambona akashindwa lakini akagoma kusaini muswada huo.

Katika safari ya China ya Mwalimu ya mwaka 1965, alipendezwa na mfumo wa kikomonisti wa Mao, na akataka kuanzisha mfumo kama huo kwa jina la ‘Ujamaa’ hapa nchini.

Dhana ya msingi ya mfumo wa Ujamaa ilikuwa ni kuwahamishia watu katika vijiji vya ujamaa na kutaifisha viwanda na vitegauchumi vilivyokuwa vikimilikiwa na watu binafsi ili kuwa chini ya wananchi, hatua iliyopingwa vikali na Kambona kwa maelezo kwamba ungeongeza umaskini na udhibiti wa serikali kwa watu.

Inadaiwa kuwa kulikuwa na msuguano mkali, kiasi kwamba ilimlazimu Kambona alijiuzulu nyadhifa zake ndani ya serikali na chama na hatimaye yeye na familia yake wakakimbilia Nairobi, Kenya na kisha Uingereza ambako walipatiwa hifadhi ya kisiasa.
Mara baada ya kukimbia nchi, mali za Kambona zilichukuliwa na serikali, huku ndugu zake wawili, wakiwekwa kizuizini bila ya kufikishwa mahakamani na kufungwa kwa zaidi ya miaka kumi. Inaaminika kuwa wazo la Kambona lilikubaliwa na baadhi ya viongozi wa chama na serikali.

Hii inatokana na kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake, Bibi Titi Mohammed, Michael Kamaliza ambaye alikuwa mwanaharakati wa chama cha wafanyakazi, mwanachama wa TANU na waziri, pamoja na Gray Mattaka, Eliya Chipaka na Prisca Chiombola kwa tuhuma za uhaini. Viongozi hao walihukumiwa pamoja na Kambona licha ya kuwa alikimbilia London lakini walikata rufaa katika Mahakama Kuu ya Afrika Mashariki na wakaachiwa huru. Hata pamoja na kuachiwa huru,walikamatwa na serikali na kufungwa tena.

Tuhuma kubwa ya Kambona ni kwamba aliiba pesa nyingi za umma, na kukamatwa nazo alipopekuliwa katika uwanja wa Embakasi, mjini Nairobi jambo ambalo alilipinga kwa miaka mingi na kuliweka wazi katika taarifa yake kwa waandishi wa habari Septemba 6, 1967 huko London. Kambona alikwenda mbali zaidi akaitaka serikali ya Tanzania kuiomba Kenya kutoa ukweli juu ya jambo hilo, jambo ambalo halikufanyika hadi kifo chake.

Inaaminika kuwa maisha ya Kambona jijini London yalikuwa ya shida na dhiki. Mwaka 1982, baadhi ya ndugu wa Kambona waliachiwa toka kizuizini baada ya juhudi za Waziri Mkuu wa New Zealand, Robert Muldoon. Mwaka 1990, Kambona akiwa na matumaini makubwa ya mabadiliko ya kisiasa katika Tanzania, aliunda chama kiitwacho Tanzania Democratic Alliance, akiwa bado uhamishoni.

Kurudi Tanzania

Mwaka 1992, wakati mfumo wa vyama vingi ulipoanzishwa Tanzania, Kambona aliomba kurudi nchini. Hata hivyo, serikali ya Tanzania ilimkatalia katakata. Kuona hivyo, Kambona aliiomba serikali ya Uingereza kumpa pasi ya kusafiria kurudi Tanzania, lakini pia akakumbana na tishio la kukamatwa na kuwekwa ndani pindi angelitua.

Septemba 5, 1992, bila woga wa kukamatwa, Kambona alitua katika ardhi ya Tanzania na hakushikwa, badala yake alipewa miezi mitatu awe amekamilisha utata wa uraia wake. Nia yake ya kushiriki kwa nguvu katika harakati za siasa ilitiwa doa na kudorora kwa afya yake akisumbuliwa na shinikizo la damu.

Afya yake ilizidi kuwa mbaya, na hivyo akalazimika kurudishwa tena London Uingereza kwa matibabu. Hata hivyo, Juni,1997, Kambona alifariki akipishana kwa siku chache tu na mdogo wake Otini Kambona ambaye pia alikuwa nchini humo kwa matibabu ya moyo.

Katika namna ambayo yaweza kuelezwa kuwa ni tendo pekee la kumuenzi mwanasiasa huyo mashuhuri, serikali ilikubali kusafirisha mwili wake na wa Otini na pia shughuli zote za mazishi. Kambona ameacha mke na watoto wawili, akiwemo Neema Kambona ambaye hivi karibuni alijiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) tawi la London. Mtoto wa kwanza, Mosi Kambona aliuawa miaka si mingi sana iliyopita mjini London katika mazingira ya kutatanisha.

Kambona ameondoka, lakini pamoja na kuwepo kwa dosari hiyo ya kusigana katika siasa, alifanya makubwa mengi. Ni kiongozi pekee ambaye askari wa jeshi walipoasi na kuwalazimu Mwalimu Nyerere na Rashid Kawawa kukimbia, angeweza kutwaa madaraka ya nchi baada ya kufanya mazungumzo yaliyowalainisha wanajeshi hao.

Bila tamaa Kambona, alikwenda Kigamboni kuwachukua Mwalimu Nyerere na Kawawa waliokuwa mafichoni, na kubaki mwaminifu kwa nafasi yake ya uwaziri aliyokuwa nayo. Kambona kasahaulika pamoja na uaminifu huo na mema yote kiasi kwamba hakuna hata sehemu ya kumbukumbu inayomwelezea kwa mazuri yake. Ameingizwa katika kapu la waliosahaulika!

My Take
Pamoja na sifa nyingi tunazompa Nyerere, ukisoma stori hii unatambua kwamba Nyerere hakuwa mtu mzuri kama tunavyomuelezea. Alikuwa na ubabe wa kijinga. Naweza sema Nyerere amekuwa chanzo cha umasikini mkubwa tunaokabiliana nao nchini.
 
Siyo unasikia kitu kimoja tu unaconclude mkubwa. Vile vile tafuta upande wa pili. Kwa nini huyu jamaa alikimbilia Uingereza na wala siyo China?
 
Ngoja Mzee Mwanakijiji and c.o wakusikiae.

CC. zomba,

Mkuu Ritz najua huwa unamkubali sana Oscer Kambona safahamu kama watoto wake hawajihusishi na siasa but kuna kipindi nkiwa mdogo kiasi nliwahi kumsikia.. Nadhan anaitwa Neema akisema one day ataendeleza what his dad fought for sijajua yuko wapi.
 
Last edited by a moderator:
Nimesoma maandiko mengi sana yanayomuhusu kambona hata katika nadharia nyingi kuhusiana na Vita Ya Biafra kule Nigeria.Kweli katika jambo ambalo najutia na ninalichukia kupita kiasi ni kuimbishwa nyimbo za kumkashfu na kumtukana kambona nikiwa Nursery school.


Halafu kuna tawala nyingine ni za ajabu kweli kweli.hivi makosa ya ndugu inakuaje wakamatwe ndugu halafu wafungwe mika 10 na wengine waendelee kukamatwa na kufungwa hata baada ya mahakma kutoa hukumu ya kuwaachia huru?

Kwangu serikali ya Tanzani hadi leo imeonyesha Usaliti wa hali ya juu kutomuenzi Oscar kambona.Kwangu huyu ni shujaa hata kama nitamuona hivyo peke yangu kama ninavyoamini kwenye Ushujaa wa Kasim Hanga,Abdulrahaman Babu,Muammar Ghaddafi na Robert Mugabe
 
Mkuu Ritz najua huwa unamkubali sana Oscer Kambona safahamu kama watoto wake hawajihusishi na siasa but kuna kipindi nkiwa mdogo kiasi nliwahi kumsikia.. Nadhan anaitwa Neema akisema one day ataendeleza what his dad fought for sijajua yuko wapi.
Neema yupo London na amejiunga na CHADEMA tawi la London siku za hivi karibuni.
 
Hivi huyu Kambona hayuko kwenye lile kundi la wazee wa Gerezani.Ni wazi kabisa tofauti zake na Mwl Nyerere zilimsababishia mateso makubwa ikiwemo kuishi uhamishoni kwa miaka 27.Mzee wa ngano za Gerezani sijui kama kamtia kwenye kile kitabu chake au kwakuwa ni mgalatia anaweza kumsahau.
 
Back
Top Bottom