Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?

Ukweli ni upi kuhusu Oscar Kambona?

Hata Nyerere mwenyewe alishakiri kuwa aliwahi kufanya makosa wakati wake.Tena aliwashutumu wanaoiga makosa yake badala ya kufanya mazuri (ya kuboresha). Jambo moja, aliwaogopa watu wenye upeo wa kumzidi na hivyo alifanya kila awezalo kuwadhoofisha au vinginevyo.Wakati huo usalama wa taifa hawakuwa tiss ila kidogo zaidi ya tiss. Sasa haisaidii kumlaumu bali inapasa tujiulize na sisi tunafanya nini kwa wenzetu na nchi yetu? Nyerere asingependa uongozi kama wa Makinda na Ndugai bali kama wa Mbowe au Mnyika. Tafakari, chukua hatua.
 
Kifo cha sokoine nyerere alihusika asilimia 100 . Huyu mzee hakutaka mtu wa kutofautiana naye chochote . Alikuwa dikteta mmbaya sana.

Hayati Sokoine alimtia ndani Butiku kwa ajili ya kosa la Uhujumu uchumi. Nyerere alimtoa Butiku na akamtetea sana tena kwa hali iliyokuwa inamdhalilisha Sokoine. Haikupita mda Sokoine akatolewa roho yake. Huyu Nyerere hafai hata kupewa jina la kumbukumbu la mtaa uliopo Manzese kwa Mfuga Mbwa.
 
Hata Nyerere mwenyewe alishakiri kuwa aliwahi kufanya makosa wakati wake.Tena aliwashutumu wanaoiga makosa yake badala ya kufanya mazuri (ya kuboresha). Jambo moja, aliwaogopa watu wenye upeo wa kumzidi na hivyo alifanya kila awezalo kuwadhoofisha au vinginevyo.Wakati huo usalama wa taifa hawakuwa tiss ila kidogo zaidi ya tiss. Sasa haisaidii kumlaumu bali inapasa tujiulize na sisi tunafanya nini kwa wenzetu na nchi yetu? Nyerere asingependa uongozi kama wa Makinda na Ndugai bali kama wa Mbowe au Mnyika. Tafakari, chukua hatua.

Kusema tu una makosa bila kuyataja ni makosa gani uliyoyafanya ni unafiki. Kwa nini asiyataje makosa yake aliyoyafanya ili Watanzania wasiyarudie? Maneno mengi yanayotumika kumnukuu Nyerere ni yale aliyoyazungumza baada ya kustaafu. Mtu mwenye akili timamu ukiyasikiliza unaona kabisa yanapingana na imani yake na matendo yake. Alipanga kuacha rekodi ya kisanii ya kuhubiri vitu ambavyo hakuvitenda. Na Watanzania wanaitumia kumsifia Nyerere kama mazuzu.
 
Retrieved from Tanzania Daima 2/2/2013 and 9/2/2013

Oscar Kambona ni miongoni mwa viongozi mahiri na shupavu waliowahi kuwa gumzo ndani na nje ya Tanzania, kutokana na uongozi wake, hekima na busara.

Ndiye Mtanzania wa kwanza kuwa waziri aliyeongoza wizara mbili kwa wakati mmoja. Ndiye Mtanzania pekee anayeaminika kusimama kidete na kufanikiwa kulidhibiti jeshi lililoasi mwaka 1964.Hata hivyo, pamoja na umahiri huo, lakini kubwa zaidi kutokuwa na tamaa ya kutumia nafasi ya uasi wa jeshi kushika madaraka ya nchi.

Pamoja na hayo mchango wake hauthaminiwi kabisa. Tofauti na viongozi wengine wa siasa au hata utamaduni, mpaka sasa hakuna barabara yenye ukumbusho wa jina la mwanasiasa huyu aliyefariki akiwa katika matibabu mjini London, Juni 1997 na mwili wake kurudishwa Tanzania kwa mazishi.

Oscar Kambona alizaliwa mwaka 1925, katika kijiji cha Kwambe kilichoko mwambao mwa Ziwa Nyasa, karibu na Mbamba-Bay, wilaya ya Mbinga, mkoani wa Ruvuma.
Alikuwa ni mtoto wa Kasisi David Kambona ambaye alikuwa miongoni mwa Waafrika wa kwanza kupata upadri katika kanisa la Anglikana la Tanganyika, na kwa mama Miriam Kambona.

Akiwa mdogo, baba yake alikuwa akimweleza kuhusu ndoto zake juu ya uhuru wa nchi yake, hivyo kumfanya Oscar kujawa na hamu ya kuitumikia nchi yake. Msingi wa elimu yake aliupata nyumbani kwao, chini ya mwembe (ambao bado uko mpaka sasa), katika kijiji cha Kwambe, kwa kuwatumia wazazi wake wote wawili na mjomba wake, ambao wote walikuwa walimu.

Alipelekwa shule ya kati ya Mt. Barnabas, Liuli na baadaye Shule ya Sekondari ya Alliance (sasa Shule ya Sekondari Mazengo), ambako alilipiwa ada na askofu Mzungu wa Anglikana kwa vile baba yake hakuweza kumudu kulipa ada ya pauni 30 kwa mwaka. Inasimuliwa kuwa kilichomvutia Mzungu huyo kukubali kumlipia Oscar ada ni baada ya kusali sala ya Baba Yetu Uliye Mbinguni kwa Kizungu. Alichaguliwa kwenda ‘Tabora Boys Senior Government School ambako ndiko alikokutana na Mwalimu Julius Nyerere kwa mara ya kwanza. Wakati huo Nyerere alikuwa anafundisha katika shule ya Kikatoliki ya St Marys.

Kukutana tena na Nyerere

Ilikuwa mwaka 1954, kwenye mkutano wa kitaifa wa walimu, ndipo Oscar Kambona ambaye naye alikuwa amemaliza shule na kufundisha katika shule ya Alliance, alikutana tena na Nyerere na kujadili mambo mbalimbali ikiwemo harakati za chama cha TANU. Oscar alishawishika kuitumikia TANU ambayo ilikuwa imeanzishwa muda si mrefu, bila malipo baada ya Mwalimu Nyerere kumweleza kuwa asingeweza kuajiriwa ndani ya chama kwa vile haikuwa na fedha.

Huo ulikuwa uamuzi mzito na mgumu mno, hasa kwa mtu kukubali kuachia nafasi ya ualimu ambayo alikuwa akilipwa vizuri na kufanya kazi bila malipo tena za chama ambacho ndiyo kwanza kilikuwa kikianza harakati za ukombozi. Kwa miezi takriban sita, Oscar Kambona alifanya kazi ngumu ya kuzunguka sehemu mbalimbali za nchi na kuonana na machifu na wazee wa vijiji ili kusajili wanachama.

Kwa kipindi hicho huku akitumia fedha kidogo alizokuwa amejiwekea akiba yake, alifanikiwa kusajili wanachama 10,000 na haikuwa ajabu kuwa baada ya mwaka mmoja alikuwa amepata wanachama hai 100,000. Ili kutunza fedha za chama, Kambona alifungua akaunti ya kwanza ya TANU na kisha kwenda Butiama kumshawishi Mwalimu Nyerere achukue uongozi wa chama moja kwa moja kama mtendaji mkuu.

Mwaka 1957, Kambona alikwenda kusomea sheria katika Chuo cha Middle Temple, nchini Uingereza kwa ufadhili wa Gavana. Akiwa London Kambona alikuwa kiongozi wa chama cha wanafunzi wa Tanganyika na mwenyekiti wa tawi la TANU la London.

Kukutana na watu mashuhuri

Mwaka 1958, Kambona alipata fursa ya kukutana kwa mara ya kwanza na watu mashuhuri akiwemo George Padmore, mwanaharakati wa umoja wa wa Waafrika duniani, ambaye alimshawishi ahudhurie mkutano wa Waafrika wote (All Africa’s Peoples Conference), uliofanyika nchini Ghana muda mfupi baada ya kupata Uhuru. Kambona alisafiri mpaka Ghana, wakati huo akiwa bado anaendelea na masomo yake nchini Uingereza na huko alipata nafasi ya kukutana na mwanaharakati mwingine maarufu wa siasa za Afrika, Kwame Nkrumah.

Utangazaji wake BBC

Kambona ndiye Mwafrika wa kwanza kutangaza taarifa ya habari kwa lugha ya Kiswahili, katika Idhaa ya Kiswahili ya BBC, ambayo sasa inajulikana kama (BBC Swahili). Inadaiwa kuwa alikuwa akipenda sana uandishi wa habari kwenye vyombo vya kimataifa. Katika kuhakikisha anapigania uhuru na mafanikio ya TANU, Kambona akiwa anaendelea na masomo yake nchini Uingereza, alikutana na Mwalimu Nyerere kila alipoenda nchini humo na kupanga mikakati ya kudai uhuru. Kambona alifunga ndoa na Flora Moriyo na harusi ilifungwa katika kanisa la Mt. Paul, London, na Nyerere ndiye alikuwa msimamizi.

Kurudi Tanganyika

Mwaka 1959, Kambona alirudi Tanganyika na kuendeleza harakati za kudai uhuru kupitia TANU, huku wakiweka bayana madai ya kupewa serikali ya madaraka. Kambona kwa kushirikiana na wenzake akiwamo Nyerere, waliweka mikakati mbalimbali huku wakiwa tayari kuanzisha mapambano kama ilivyokuwa kwa Mau Mau ya Kenya. Katika uchaguzi wa kwanza TANU ilishinda viti vyote isipokuwa kimoja na kuunda Serikali ya Mambo ya Ndani chini ya Mwalimu Nyerere ambaye alikuwa Waziri Kiongozi wa kwanza. Kambona aliteuliwa kuwa Waziri wa Elimu na baadaye alishika nyadhifa za Waziri wa Mambo ya Ndani, Mambo ya Nchi za Nje na Ulinzi na Tawala za Mikoa. Katika nyadhifa hizo, Kambona pia alikuwa mwenyekiti wa kwanza wa Kamati ya Ukombozi ya Umoja wa Nchi Huru za Afrika na Mwenyekiti wa Utayarishaji wa OAU ambayo sasa ni AU.

Kuunganisha bara na visiwani

Mwaka 1964, Kambona alifanya kazi kubwa katika kuunganisha Zanzibar na Tanganyika, akiwa pamoja na Rais Nyerere na Karume. Hii ilikuwa ni baada ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Januari 20, 1964, wanajeshi wa kikosi cha Calito waliasi. Kambona akiwa waziri wa Ulinzi, alisimama kidete kusuluhisha na msemaji mkuu upande wa serikali huku viongozi wakuu Mwalimu Nyerere na makamu wake, Rashid Kawawa, ikisemekana wakiwa wamekimbilia mafichoni Kigamboni walikokaa kwa siku tatu za majadiliano mazito mpaka machafuko yalipoisha.

Moja ya nukuu za Kambona katika mahojiano na gazeti la Daily Telegraph la London, alisema, “Baada ya kuwatuliza wanajeshi nilikwenda kuwatafuta viongozi wengine na kuwarudisha mjini kwa kutumia Land Rover yangu.” Kambona alisifiwa sana na Mwalimu Nyerere kwa hekima na busara yake hadi kufanikiwa kumaliza uasi huo kwa kutumia nafasi yake ya uwaziri wa ulinzi. Wapo walioanza kuvumisha kuwa huenda kwa uaminifu wake, angeshika nafasi ya urais baada ya Nyerere kumaliza muda wake.
Ilikuwaje akawa adui wa serikali?

Ugomvi wa Nyerere, Kambona
Vyanzo mbalimbali vya habari hadi sasa vinashindwa kueleza ukweli juu ya hasa kile kilichosababisha kuzuka kwa tofauti kati ya Mwalimu Nyerere na Kambona. Kila mtu amekuwa akijaribu kueleza ugomvi wa wawili hawa kadiri ajuavyo. Kuna madai kwamba viongozi hawa wawili ambao kwa sasa wote ni marehemu, walianza kutofautiana baada ya maasi ya wanajeshi.

Inadaiwa kuwa Nyerere alitaka kuanzisha mfumo wa chama kimoja nchini ili kuimarisha usalama na Kambona alipinga hoja hiyo kwa maelezo kwamba mfumo huo ungezorotesha uhuru na maendeleo ya demokrasia. Hoja hiyo ikafikishwa bungeni kwa maamuzi na kwa bahati mbaya kwa Kambona akashindwa lakini akagoma kusaini muswada huo.

Katika safari ya China ya Mwalimu ya mwaka 1965, alipendezwa na mfumo wa kikomonisti wa Mao, na akataka kuanzisha mfumo kama huo kwa jina la ‘Ujamaa’ hapa nchini.

Dhana ya msingi ya mfumo wa Ujamaa ilikuwa ni kuwahamishia watu katika vijiji vya ujamaa na kutaifisha viwanda na vitegauchumi vilivyokuwa vikimilikiwa na watu binafsi ili kuwa chini ya wananchi, hatua iliyopingwa vikali na Kambona kwa maelezo kwamba ungeongeza umaskini na udhibiti wa serikali kwa watu.

Inadaiwa kuwa kulikuwa na msuguano mkali, kiasi kwamba ilimlazimu Kambona alijiuzulu nyadhifa zake ndani ya serikali na chama na hatimaye yeye na familia yake wakakimbilia Nairobi, Kenya na kisha Uingereza ambako walipatiwa hifadhi ya kisiasa.
Mara baada ya kukimbia nchi, mali za Kambona zilichukuliwa na serikali, huku ndugu zake wawili, wakiwekwa kizuizini bila ya kufikishwa mahakamani na kufungwa kwa zaidi ya miaka kumi. Inaaminika kuwa wazo la Kambona lilikubaliwa na baadhi ya viongozi wa chama na serikali.

Hii inatokana na kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake, Bibi Titi Mohammed, Michael Kamaliza ambaye alikuwa mwanaharakati wa chama cha wafanyakazi, mwanachama wa TANU na waziri, pamoja na Gray Mattaka, Eliya Chipaka na Prisca Chiombola kwa tuhuma za uhaini. Viongozi hao walihukumiwa pamoja na Kambona licha ya kuwa alikimbilia London lakini walikata rufaa katika Mahakama Kuu ya Afrika Mashariki na wakaachiwa huru. Hata pamoja na kuachiwa huru,walikamatwa na serikali na kufungwa tena.

Tuhuma kubwa ya Kambona ni kwamba aliiba pesa nyingi za umma, na kukamatwa nazo alipopekuliwa katika uwanja wa Embakasi, mjini Nairobi jambo ambalo alilipinga kwa miaka mingi na kuliweka wazi katika taarifa yake kwa waandishi wa habari Septemba 6, 1967 huko London. Kambona alikwenda mbali zaidi akaitaka serikali ya Tanzania kuiomba Kenya kutoa ukweli juu ya jambo hilo, jambo ambalo halikufanyika hadi kifo chake.

Inaaminika kuwa maisha ya Kambona jijini London yalikuwa ya shida na dhiki. Mwaka 1982, baadhi ya ndugu wa Kambona waliachiwa toka kizuizini baada ya juhudi za Waziri Mkuu wa New Zealand, Robert Muldoon. Mwaka 1990, Kambona akiwa na matumaini makubwa ya mabadiliko ya kisiasa katika Tanzania, aliunda chama kiitwacho Tanzania Democratic Alliance, akiwa bado uhamishoni.

Kurudi Tanzania

Mwaka 1992, wakati mfumo wa vyama vingi ulipoanzishwa Tanzania, Kambona aliomba kurudi nchini. Hata hivyo, serikali ya Tanzania ilimkatalia katakata. Kuona hivyo, Kambona aliiomba serikali ya Uingereza kumpa pasi ya kusafiria kurudi Tanzania, lakini pia akakumbana na tishio la kukamatwa na kuwekwa ndani pindi angelitua.

Septemba 5, 1992, bila woga wa kukamatwa, Kambona alitua katika ardhi ya Tanzania na hakushikwa, badala yake alipewa miezi mitatu awe amekamilisha utata wa uraia wake. Nia yake ya kushiriki kwa nguvu katika harakati za siasa ilitiwa doa na kudorora kwa afya yake akisumbuliwa na shinikizo la damu.

Afya yake ilizidi kuwa mbaya, na hivyo akalazimika kurudishwa tena London Uingereza kwa matibabu. Hata hivyo, Juni,1997, Kambona alifariki akipishana kwa siku chache tu na mdogo wake Otini Kambona ambaye pia alikuwa nchini humo kwa matibabu ya moyo.

Katika namna ambayo yaweza kuelezwa kuwa ni tendo pekee la kumuenzi mwanasiasa huyo mashuhuri, serikali ilikubali kusafirisha mwili wake na wa Otini na pia shughuli zote za mazishi. Kambona ameacha mke na watoto wawili, akiwemo Neema Kambona ambaye hivi karibuni alijiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) tawi la London. Mtoto wa kwanza, Mosi Kambona aliuawa miaka si mingi sana iliyopita mjini London katika mazingira ya kutatanisha.

Kambona ameondoka, lakini pamoja na kuwepo kwa dosari hiyo ya kusigana katika siasa, alifanya makubwa mengi. Ni kiongozi pekee ambaye askari wa jeshi walipoasi na kuwalazimu Mwalimu Nyerere na Rashid Kawawa kukimbia, angeweza kutwaa madaraka ya nchi baada ya kufanya mazungumzo yaliyowalainisha wanajeshi hao.

Bila tamaa Kambona, alikwenda Kigamboni kuwachukua Mwalimu Nyerere na Kawawa waliokuwa mafichoni, na kubaki mwaminifu kwa nafasi yake ya uwaziri aliyokuwa nayo. Kambona kasahaulika pamoja na uaminifu huo na mema yote kiasi kwamba hakuna hata sehemu ya kumbukumbu inayomwelezea kwa mazuri yake. Ameingizwa katika kapu la waliosahaulika!

My Take
Pamoja na sifa nyingi tunazompa Nyerere, ukisoma stori hii unatambua kwamba Nyerere hakuwa mtu mzuri kama tunavyomuelezea. Alikuwa na ubabe wa kijinga. Naweza sema Nyerere amekuwa chanzo cha umasikini mkubwa tunaokabiliana nao nchini.



Kweli nimeamini Marehemu alikua na kaElement cha Uditekta flani hiv,,,unamuweka mtu kizuizini miaka 10?
Mkuu tupe na history ya Mwanaharakati Babu nae nasikia aliwekwa kizuizin:shut-mouth::shut-mouth:
 
Kweli nimeamini Marehemu alikua na kaElement cha Uditekta flani hiv,,,unamuweka mtu kizuizini miaka 10?
Mkuu tupe na history ya Mwanaharakati Babu nae nasikia aliwekwa kizuizin:shut-mouth::shut-mouth:
Ngoja niitafute hiyo! Soon itakuwa hapa jamvini

Nimetafuta kila namna ya ku - upoload article kuhusu Abdulahman Mohammed Babu nimeshindwa. So ninawawekea tu link, muisome. Kama Mods wataona ina umhimu basi wanaweza kuiupload hapa.

http://www.jpanafrican.com/docs/vol1no9/AbdulRahmanMohamedBabu.pdf
 
"A campaign by the
government was started to
vilify him again. First was the
claim that he was not a citizen
of Tanzania and had never been one even though
he had served as the country's
minister of home affairs,
minister of defence, and
minister of foreign
affairs, and even led the struggle for independence
with Nyerere in the 1950s. Yet
nothing was said in all those
years that he was not a citizen
of Tanganyika. It was only
decades later, in the 1990s, that the government said he
was not a Tanzanian but a
Malawian. Others said he was
a Mozambican.
The government even
withdrew his passport on the same grounds that he was not
a Tanzanian citizen.He could
not even travel
outside the country after his
passport was withdrawn. The
vilification campaign against him by the Tanzanian
government made the
government look bad and it
finally relented and gave the
passport back to him.
Kambona himself had his own "revelations"concerning the
national identities of other
Tanzanian leaders including
President Nyerere himself.
He said Nyerere's father was a
Tutsi from Rwanda who was a porter for the Germans and
settled in Tanganyika and that
he could prove it. He also said
Vice President Rashid Kawawa
came from Mozambique, and
John Malecela - who once served as Tanzania's foreign
affairs minister, prime minister
and vice president among
other posts at different times -
came from Congo where his
grandparents were captured as slaves before they settled
in Dodoma, central Tanzania.
But few people took any of
those claims seriously any
more than they did the claim
that Kambona himself was not a Tanzanian citizen but a
Malawian, from Likoma Island,
or a Mozambican"

Source:
en.m.wikipedia.org/wiki/
Oscar_Kambona/


NB:nimeirudisha hii mada kama ilivyo kutokana na modes kuiunganisha na uzi mwingine...tena content isiyo na uhusiano..
Ombi:Tafadhali kuweni makini na content na sio majina ya wahusika
 
Duu! Jasusi, sijui yupo wapi.
 
Last edited by a moderator:
nimewahi kusoma humuhumu kuwa eti asili ya ututsi ya nyerere ndo ilisababisha tz kuwabeba zaidi watutsi dhidi ya wahutu.
 
bora mtutsi aliyekuwa hatuibii. bora mtutsi aliyejitahidi kutuweka pamoja kwa kadri alivyoweza. bora mtutsi aliyejitahidi kutuwezesha tujitegemee wenyewe. ushahidi upo. rip kambona. rip nyerere. both were great men.
 
bora mtutsi aliyekuwa hatuibii. bora mtutsi aliyejitahidi kutuweka pamoja kwa kadri alivyoweza. bora mtutsi aliyejitahidi kutuwezesha tujitegemee wenyewe. ushahidi upo. rip kambona. rip nyerere. both were great men.

haya ni mawazo positive mkuu
 
safi sana ndugu,sema inabidi tujifunze mengi kutoka kwa viongozi wa miaka hiyobb
 
Kifo cha sokoine nyerere alihusika asilimia 100 . Huyu mzee hakutaka mtu wa kutofautiana naye chochote . Alikuwa dikteta mmbaya sana.

Labda unaweza kutuarifu kitu kimoja tu ambacho Nyerere alitofautiana na Sokoine.
 
Kusema tu una makosa bila kuyataja ni makosa gani uliyoyafanya ni unafiki. Kwa nini asiyataje makosa yake aliyoyafanya ili Watanzania wasiyarudie? Maneno mengi yanayotumika kumnukuu Nyerere ni yale aliyoyazungumza baada ya kustaafu. Mtu mwenye akili timamu ukiyasikiliza unaona kabisa yanapingana na imani yake na matendo yake. Alipanga kuacha rekodi ya kisanii ya kuhubiri vitu ambavyo hakuvitenda. Na Watanzania wanaitumia kumsifia Nyerere kama mazuzu.

Na waliomfuata ndio wameendekeza usanii kuliko alioufanya Nyerere. Ukiangalia yanayoendelea leo,bila wasiwasi yanathibitisha ukweli huo. Leo hii baba akiwa Rais na familia nzima imepata cheo hiko. Wizi wa mali ya umma,deal za upendeleo na za matumizi mabaya ya madaraka ndio kigezo cha kuongoza. Tuwe na uhakika tunapotoa hoja zetu. Nyerere had his problems so as the rest
 
yaKuna wtu ukimsema nyrere hata salamu hawakupi maana kwao bwana huyu hna makosa.Lkn nawambia na kuwashauri kuruhsu akili kufanya kazi ktk kuchambua mswala ya siasa ili kuelimisha wale wenye kufuata upepo.JMANI makosa ni sehemu kujifunza ili kutorudia makosa.Tukubali kukosolewa ili tujenge nchi yetu.
 
Kuna mtu hapa ananidokeza kua uhuru wa Tanganyika ulipiganiwa na watu wengi sana ila kwa bahati mbaya historia zao zilifunikwa makusudi na muheshimiwa mwalimu.
Jamani wenye data mtumwagie.

Mkuu ni kweli kabisa, waliopigania Uhuru wa Tanganyika ni wengi na hawatajwi popote. Nilipata bahati ya kuongea na Marehemu Bhoke Munanka akaniambia kuwa miongoni mwa watu walijitolea sana kufanikisha uhuru wa Tanganiyka alikuwapo Mzee mmoja wa Rufiji jina silikumbuki ambaye alikuwa anakuja Dar kwa baskeli kuchukua kadi za TANU na kwenda kuhamasisha wananchi wajiunge na pia kusaidia TANU kupata fedha za kujiendesha. Watu hawa hawatajwi popote.
 
Watu wenye akil timamu hatuwezi kuwaelewa kwa kutuambia "akakwaruzana na mwalimu,akajiuzuru,akakimbia",ebu wewe mjuzi wa mambo tuambie alikwaruzana nae nin.?ndio tutakuelewa..
Vinginevo mpo hapa kumponda mwalmu tu..
Mfano:-kuna watu wanadai vita ya uganda iliandaliwa na nyerere kwa nia ya kumrudsha obote madarakani,na kwakua amin n muislamu,lakin GT tunakumbuka kua mwaka 72 amin alirusha bomu mwanza lakin nyerere alitulia tu,angekua anataka vita c angelianzisha..
Mnapotaka kutuaminsha kua kambona alikua mtakatifu,pia twawakumbusha kua mbna alirud hapa na kutuambia anakuja kutuonesha mabilioni ya pesa yaliyofchwa na nyerere lakin hatukuyaona..

"Upumbavu ni kipaji,kuna watu wanazaliwa nacho"..Mwalimu Nyerere..

Cc.. Lukolo Zali la Mentali
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom