Ukweli tuuweke hapa kuhusu Kassim Mganga!

Ukweli tuuweke hapa kuhusu Kassim Mganga!

Aaah Awena sasa

Niliapa ukiondoka mpenzi, ntaondoka nawe
Sikuahidi kukufuta machozi, bali ntalia nawe
Ina maana hata kugeuka kunitazama hutaki Awena
Basi kama nakosa kwako nililofanya, nieleze Awena
Chozi langu la thamani unaliacha lianguke eeeh
Mti nilopanda zamani ina maana si chochote...........

Maneno matamu ulonipa chumbani, huku kichwa chako umelaza kifuani
Machozi yakikutiririka mashavuni
Kwamba hutoniacha mimi labda nitoweke duniani. ........
Kassim anajua sana ..tunaopenda mziki mzuri tunajua hilo
 
Kwenye hiyo list Barnaba hayupo kweli?
Heahima kwako mkuu...barnaba bado sana...asubiri hawa mabwana watoke duniani au waache kazi ya muziki...
mpaka hawa wamefika hapo ni baada ya mzee gurumo na banza stone kuondoka...ila wangekuwapo bado wasingeeleweka kabisa kwenye ulimwengu wa watunzi mahiri wa muziki.
wafuatilie vizuri tokea enzi za mzimuni family utaelewa kwann chilla ni balaa...pia anapita kuanzia rege tags2 ridim mpaka mnanda ....jamaa ni balaa.
 
Aaaaaaah jamani, kwenye utunzi napo barnaba naye si mtu wa mchezo mchezo kabisa
 
Sikiza sweet nikuelezeee yamoyoni nikutoe wasiwasiiii
Sikiliza kipenzi mwenye sura ya upoleee nibembelezee ili nisiwe na wasi
sikiliza kisuraa mwenye sifa ya upolee mwenye mapenzi hi hiii ya kweli kwangu
Kama shida mamy bas vumilia shida wewe
Kama njaa wote tutashinda mamaa
Amini wewe ndiwe wa pekee
Niamini basi mimi
Niamini basi mimi
Niamini basi
Usije niacha mpweke
Nikaikosa nafasi kwako
Nikaikosa nafasi
Basi twende kwetu chumpana
Wakakuone wazazi nyumbani
Nivumilie mamii tabu zitakwisha baby

Tabu zitakwisha sijachoka kutafuta
 
Kwel huyu jamaa huwa ana mziki fulani mzuri........tatzo wabongo hatujuagi mziki mzuri,
 
Habari zenu wakuu!

Nimefikiria kitu kuhusu huyu jamaa, katika tasnia ya mziki hapa Tanzania! Huyu jamaa yupo vizuri, ukisikiliza nyimbo zake kuna tungo nzuri kwa lugha yetu ya kiswahili fasaha pasipo kuchanganya lugha za kigeni, pia ana mashairi yaliyotulia pasipo kuwa na matusi au misamiati ya kipuuzi!

Hakika jamaa anatisha sana kuliko hata hawa 'waramba midomo' wa sasa.

Ongeza ulichoona kutoka kwa huyu jamaa!
Ulichokosea ni hiyo R kwenye WALAMBA MIDOMO
 
Aaaaaaah jamani, kwenye utunzi napo barnaba naye si mtu wa mchezo mchezo kabisa
Ni kweli mamaa ila ni lazima jua lizame ili nyota zionekaneee.

Ndio nikakuambia hata Q chilla na kassim nimewapa heshima ya kuwa watunzi mahiri Tanzania ni baada ya jua kuzama nikimaanisha kuondoka kwa mzee gurumo na ramadhan masanja banzastone.
 
Ooh nimekuelewa
 
Dah! na mimi kwenye kuhesabiwa nimo.
Fan wa Kassim Mganga toka kitambo.
 
Back
Top Bottom